Polisi yachunguza mauaji Dar

 Mtuhumiwa wa mauaji ya kijana Mahamudu Muhasi, Lucas Muhabe anashikiliwa na Jeshi la Polisi


Dar es Salaam. Mtuhumiwa wa mauaji ya kijana Mahamudu Muhasi, Lucas Muhabe anashikiliwa na Jeshi la Polisi na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Muhabe anaendelea kushikiliwa Polisi kwa tuhuma za mauaji, usiku wa kuamkia juzi eneo la Tabata Kisukulu kwa madai ya kukerwa na kelele za mkesha wa harusi.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mary Nzuki, alisema mtuhumiwa alikwenda kituoni kujihami kuwa kuna watu wanamfanyia fujo nyumbani kwake, ndipo askari walikwenda kuwakamata wafanya fujo baada ya kufika eneo la tukio wakapewa taarifa kwamba yeye ndiyo ameua.
“Askari walipokwenda kuwakamata watuhumiwa wa fujo wakakuta mtuhumiwa huyo ameua hivyo wakamuweka chini ya ulinzi, hadi uchunguzi utakapokamilika,” alisema Nzuki.
Alisema kinachofanyika sasa ni kukamilisha uchunguzi ikiwamo kupata taarifa kutoka kwa daktari anayeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Akizungumza na gazeti hili kaka wa marehemu Salim Ally alisema baada ya mwili kufanyiwa uchunguzi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, mwili huo wamekabidhiwa.
Alisema taarifa ya daktari inaonyesha kuwa marehemu alipigwa risasi moja kwenye moyo ambayo ilisababisha atoke damu nyingi kichwa na kuzua hisia kuwa alipigwa mbili.
Alisema kuwa daktari amethibitisha kifo chake kusababishwa na risasi hiyo kwa sababu alimpiga kwa karibu.
na iliingilia mbele na kutoke nyuma na wala siyo mbili kama ilivyotaarifiwa na mashuhuda hapo mwanzo.



Powered by Blogger.