Asilimia 97 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2015
Dar es Salaam. Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohiyimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.
Idadi hiyo ni sawa an asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) kwa waandishi wa habari leo imesema ufaulu huo umeongezeka
kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.
Hata
hivyo, jumla ya wanafunzi 12, 432 waliofaulu, hawajapata nafasi ya
kuchaguliwa kuendelea na masomo ay sekondari kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo uungufu wa majengi, hali inayowalazimisha kusubiri
chaguo la pili litakalofanyika mapema mwakani.
Jumla ya
wanafunzi 808,085 walisajiliwa kufanya mtihani wa taifa mwaka 2014
lakini ni wanafunzi 792,122 tu ndio waliofanya mtihani, hiyo ikiwa ni
asilimia 98.02% ya wanafunzi wote waliosajiliwa.
Taarifa
ya Tamisemi inaongeza kuwa wavulana wanaongoza kwa kuchagaliwa zaidi ya
wasichana ambapo jumla ya wavulana 219,964 wamechaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 97.28 ya wanafunzi wote
waliochaguliwa huku wasichana wakifikia 218,996 ambayo ni sawa asilimia
97.1 ya wanafunzi waliochaguliwa.