Miongoni
mwa watu waliowasili katika kuitambua miili ya jamaa zao katika chumba
cha kitaifa cha kuhifadhia maiti Nairobi Jumatano alikuwa ni Douglas
Ondari Ochodho.
Yeye ni mwalimu wa shule
ya upili huko Mandera. Aliponea shambulio la kwanza katika eneo hilo la
Mandera wiki mbili zilizopita, ambapo watu takriban 28 waliuawa,
miongoni mwao ni mkewe.
Amezungumza na mwandishi wa BBC Maryam Abdallah kuhusu mkosi ulioikumba Safari hiyo.