Miili yazidi kuopolewa katika ajali ya AirAsia

Ndugu wa abiria wa AirAsia akiangua kilio na kubembelezwa na watu mara baada ya kupata habari ya kupatikana kwa miili ya abiria wa ndege iliyopotea ya AirAsia, QZ 8501.

Habari / Dunia

Maafisa wa  Indonesia wamefanikiwa kuopoa miili arobaini kutoka baharini, karibu na yalipo mabaki ya ndege ya abiria ya AirAsia iliyoanguka wakati wa hali mbaya ya hewa siku ya Jumapili.
Televisheni ya huko imeonyesha ndege za uokoaji zikitoa miili katika bahari ya Java, kilometa 160 kutoka katika ufukwe wa kisiwa cha Borneo.
Wanafamilia wa abiria wa ndege hiyo waliangua vilio baada ya kuona picha za kwanza za miili iliyovimba na ikiwa haijavaa vifaa vya kujiokoa maisha baharini.
Kabla giza kuingia, waokoaji walikuwa wameopoa robo tu ya miili ya waliopanda ndege hiyo. Hakuna abiria wala wafanyakazi wa ndege waliopatikana wakiwa hai.
Miili ilipatikana mara baada ya kugundulika kwa mabaki ya ndege, pamoja na kitu kilichoonekana kuwa ni kifaa cha kujiokoa baharini, mizigo na mlango wa dharura uliopakwa rangi nyeupe na nyekundu.
Watafutaji wa ndege hiyo wa angani pia waligundua kitu kinachoonekana kama kivuli chini ya bahari ambacho kinaaminika kuwa ni sehemu kubwa ya ndege.
Ndege aina ya Airbus A320 ilipotea siku ya Jumapili, ikiwa karibu na nusu ya safari yake ambayo ilikuwa fupi ya saa mbili, kutoka katika mji wa Indonesia, wa Surabaya, kwenda Singapore.
Tony Fernandes, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa AirAsia, amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba moyo wake umegubikwa na uchungu kwa familia za wale waliopatwa maafa, na kusema maneno pekee hayawezi kuelezea namna alivyoguswa.
 
Powered by Blogger.