MIILI YA WATU WALIOKUFA CONGO YAIBUKA KIGOMA WENGI WASHANGAA





 
JUMLA ya maiti 14 zimezikwa baada ya makubaliano baina ya serekali ya Tanzania na serekali ya Demokrasia ya Congo(DRC)ambapo katika mazishi hayo serekali ya Congo iliwakilishwa na Balozi wa Congo kutoka ubalozi mdogo wa DRC Mkoani Kigoma.

Akizungumza muda mfupi baada ya mazishi ya raia hao Balozi mdogo wa DRC nchini kutoka Ubaozi mdogo Mkoani hapa,Mh. Riki Moleme alisema.

Mh. Maleme alisema kuwa amefarijika sana kwa namna serekali ya Tanzania ilivyochukulia kwa umuhimu mkubwa swala la maafa hayo ya Raia wa Congo na namna ilivyojitoa kushughulikia mazishi ya miili hiyo
Naye Mhifadhi wa mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Herman Batiho alisema alianza kuona miili ya watu majira ya jioni ya Desemba 20 Mwaka huu na ndipo walipoamua kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali ambapo waliwasiliana na uongozi wa kijiji cha kalilani ambapo uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wanachi walianza kazi ya uopoji wa miili.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani,Songoro Saidi alisema kuwa waliona moja ya mili wa maiti hizo asubuhi ya Desemba 21 ukiwa umeibuka juu,pia walipata kuwepo kwa miili mingine ikiibuka na kuelea ndani ya Hifadhi ya Mahale na ndipo waliposhirikiana kuipoa miili hiyo na hadi kufanikisha mchakato wa mazishi.
Desemba 12 mwaka huu ya watu 128 walifariki dunia na wengine 250 waliokolewa kufuatia meli waliyokuwa wakisafiria kutoka Mobaa kuelekea Kalemii kuzama katika mwambao mwa ziwa Tanganyika katika Mkoa wa Kalemii nchini DRC
Powered by Blogger.