Mmiliki wa meli za mizigo Mwanza aigomea serikali Kuondoa meli zake katika bandari tatu.
Mmiliki wa meli za mizigo Mwanza aigomea serikali Kuondoa meli zake katika bandari tatu.
Licha ya kaimu mkuu wa wilaya ya Ilemela Baraka Konisaga, ambaye
pia ni mkuu wa wilaya ya Nyamagana kutumia zaidi ya saa tatu kutafuta
suluhu ya mgogoro baina ya mkurugenzi wa RS Pedersen Transport Ltd
Richard Birikaa na mmiliki wa kampuni ya Mkombozi Marine Fishing kitana
chacha kuanzia eneo la bandari namba tatu lililopo mwaloni kirumba hadi
katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya kirumba, kuhusu mwafaka wa
meli ya MV. Luxury kutumia bandari hiyo kwa ajili ya kushusha na kupakia
mizigo mbalimbali ya wafanyabiashara, Kitana Chacha amekataa katakata
kuondoa meli zake.
Kauli ya mfanyabiashara huyo Kitana Chacha imemlazimu kaimu mkuu wa wilaya ya Ilemela Baraka Konisaga kutoa msimamo wa serikali.
Mgogoro huo wa kugombea eneo la ghati ambao umedumu kwa siku nne na
kusababisha wananchi zaidi ya 300 kukosa ajira kwa muda katika bandari
hiyo, umepelekea baadhi ya wafanyabiashara kupaaza sauti zao.