TBS yafanya ukaguzi wa kushtukiza na kufungia kiwanda cha juisi aina ya into.
Shirika la viwango nchini TBS limefanya ukaguzi wa kushtukiza na kufungia kiwanda cha Devideic Group kinachotengeneza juisi aina ya into kilichopo Kihonda manispaa ya Morogoro kwa kuuza juice zenye vimelea vya wadudu ambazo hazifai kwa matumzi ya binadamu na kuagiza juice hizo kuondolewa sokoni mara moja.
Akizungumza wakati wa kufunga kiwannda hicho afisa viwango TBS
Raurence Chenge amesema TBS limefunga kiwanda hicho baada ya kubaini
kuwa juisi inayozalishwa katika kiwanda hicho zina vimelea vya wadudu na
kiwanda hicho kinazalisha chini ya kiwango pamoja na kutumia vikoleza
ya sukari kinyume na utaratibu.
Naye afisa uhusiano wa TBS Roida Andusamile amesema sambamba na
kuzalisha chini ya kiwango kiwanda hicho hakijatenganishwa na nyumba ya
kuishi jambo ambalo ni kinyume na sheria ya viwanda ambapo amewataka
wafanyabiashara kuondoa juisi hizo sokoni maramoja na ametoa tahadhari
kwa wananchi kuacha kununua juisi aina ya into kwani hazifai kwa
matumizi ya binadamu.
Kwa upande wake meneja uzalishaji wa kiwanda cha Devideic Group
Limited Tadeus Ngonyani amesema hajakubaliana na utaratibu uliotumika
kufunga kiwanda hicho kwani ameonewa huku akilalamikia kuwa kiwanda
chake kinazalisha kwa kufuata taratibu za viwango kama viwanda vingine
vivyotengeneza juisi.