Kitendawili cha Escrow: Chadema yaongeza orodha
Dar es Salaam. Masikio ya Watanzania leo yameelekezwa kwa Rais
Jakaya Kikwete watakapokuwa wakisikiliza hotuba yake kwa Taifa
inayotarajiwa kujibu maswali yapatayo 10 ambayo yanatarajiwa kutegua
kitendawili cha kashfa ya uchotaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya
Tegeta Escrow.
Maswali hayo yanatokana na maazimio ya Bunge
ambayo yalionekana kuvuta hisia za wananchi katika kona mbalimbali za
nchi ambako walikuwa wanafuatilia moja kwa moja mjadala wa Bunge hadi
kupitishwa maazimio hayo.
Hotuba hiyo inayotarajiwa kutolewa wakati Rais
atakapozungumza na wazee wa Dar es Salaam, ikiwa ni siku nne baada ya
Kampuni za IPTL na Pan Africa Power Solutions (PAP) kukimbilia
mahakamani kuzuia utekelezwaji wa maazimio ya Bunge.
Baadhi ya wasomi nchini wamesema hatua ya kuzuia
utekelezaji wa maazimio hayo pamoja na kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuwa akijiuzulu Rais
atamshangaa, ni mambo yanayofanya hotuba ya Rais kusubiriwa kwa hamu.
Swali la kwanza ambalo wananchi wanasubiri jibu
lake ni iwapo Rais Kikwete atatuliza kiu yao kuhusu kashfa hiyo ambayo
imekuwa gumzo nchi nzima na hivyo kulegeza msimamo wa wahisani wa
kuinyima nchi misaada.
Pili, wananchi wanasubiri kusikia iwapo Rais
Kikwete ataagiza uchunguzi zaidi wa Takukuru, Polisi na vyombo vingine
kama ambavyo azimio la kwanza la Bunge linavyotaka wahusika wachukuliwe
hatua za kisheria kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na
miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Tatu, wanasubiri kwa hamu kuona hatua ambayo Rais
Kikwete atachukua dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi pamoja na Profesa
Tibaijuka kutokana na kutajwa katika maazimio hayo ya Bunge.
Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamekaririwa
wakisema kuwa hawahusiki na kashfa hiyo. Mbali ya Profesa Tibaijuka
kujitokeza kujitetea mwenyewe, baadhi ya wananchi wamejitokeza kuwatetea
na kuwasafisha viongozi hao katika vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii.
Nne, Je, atatengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Umeme (Tanesco) ambayo pia ilitakiwa kuwajibishwa ikiwa
chini ya Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma.
Tano, ili kuwachukulia hatua majaji waliotajwa,
Aloysius Mujulizi na Profesa Eudes Ruhangisa, Rais Kikwete anatakiwa
aunde Tume ya Kijaji ya kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili
zinazowakabili, kinachosubiriwa kwa hamu ni kuona endapo ataunda tume
hiyo.
Swali la sita linalohitaji jibu linahusu kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa
mwananchi