Sing'atuki ng'o:Mugabe
Rais
wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake
tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza
katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo
majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini
akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.Mugabe ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi.
Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na kukifanya kama mali yake binafsi.
Bi Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu.
source;bbcswahil