Mahakama yawahukumu watu Sita kunyongwa hadi kufa
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa sita katika kesi ya mauaji
ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na
mfanyakazi wa Benki ya NMB.
Mauaji hayo ambayo yalipata umaarufu na kupewa jina la mauaji ya Ubungo Mataa yalifanyika Aprili 20,2006 jijini Dar es Salaam.
Jaji
Projest Rugazia amewataja washtakiwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa
kuwa ni Mashaka Pastory, John Mndasha, Martine Mndasha, Haji Kiweru,
Wycliff Imbora na Rashidi Abdikadir.
Jaji Rugazia
anasema aliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwahukumu kunyongwa hadi
kufa, kufuatia ushahidi ulitolewa na mashahidi 29 wa upande wa mashtaka
pamoja na vielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo na ushahidi wa
utetezi.
“Maungamo ya washtakiwa, ushahidi wa kitaalam
na utambuzi wa washtakiwa kutambuliwa eneo la tukio inaonesha wazi
walikuwa na nia ya kujaribu kupora takribani Sh 150 milioni mali ya
benki ya NMB zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda
Morogoro tawi la Wami.” Anasema Jaji Rugazia.
Anasema
siku hiyo ya huzuni ya Aprili 20,2006 majambazi hao walilivamia gari
hilo kwa lengo la kupora lakini bila ya kuwa na huruma yoyote
walilimiminia risasi na kuwaua D 6866 Konstebo Abdallah Marwa na
mfanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyonyi.
Walifanya
tukio hilo nyakati za saa 6:30 mchana, eneo la Ubungo Mataa jijini Dar
es Salaam kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.
Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Jaji Rugazia aliwaachia huru washtakiwa Rashid Lemblisi, Philipo Mushi, Yassin Juma,
Hamisi
Daud, MT 77754 Nazareth Amurike, MT 76162 Emmanuel Lameck, James
Chamangwana na Hussein Idd baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi
hiyo.
Kwa upande wa washtakiwa, Jackson Issawangu aliyekuwa mshtakiwa wa sita katika kesi hiyo na Mussa Mustafa aliyekuwa mshtakiwa wa 10 waliachiwa huru awali baada ya mahakama hiyo kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu.
Hadi wanaachiwa huru jana, washtakiwa hao walikuwa wamekwisha kaa rumande kwa muda wa zaidi ya miaka 8.
Kwa habari zaidi Usiache kusoma gazeti lako la Mwananchi kesho
mwananchi
Kwa upande wa washtakiwa, Jackson Issawangu aliyekuwa mshtakiwa wa sita katika kesi hiyo na Mussa Mustafa aliyekuwa mshtakiwa wa 10 waliachiwa huru awali baada ya mahakama hiyo kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu.
Hadi wanaachiwa huru jana, washtakiwa hao walikuwa wamekwisha kaa rumande kwa muda wa zaidi ya miaka 8.
Kwa habari zaidi Usiache kusoma gazeti lako la Mwananchi kesho
mwananchi