JK amteua Dk Kusikuka kuwa Kamishna wa Ardhi


















 







Dar es Salaam. Rais wa Jakaya Kikwete amemteua Dk Moses Kusiluka (42) kuwa Kamishna Ardhi nchini.Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, uteuzi huo ulianza Desemba 23.
Kabla ya uteuzi wake, Dk Kusiluka alikuwa Mkuu wa Idara ya Real Estate Finance and Investment katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar Es Salaam, ambako amekuwa mhadhiri kwa miaka minane iliyopita, tangu 2006.
Dk Kusiluka ana Shahada ya Kwanza ya BSC (Land Management and Valuation) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shahada ya Uzamili ya MSC (Land Management) kutoka pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamivu (Real Estate Investment) kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.
Katika uteuzi, Rais Kikwete alisema ana matumaini makubwa kuwa ataleta nguvu mpya na mtazamo mpya katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali za umiliki na uendelezaji wa ardhi nchini.

Powered by Blogger.