Mnyama kakakuona aonekana maeneo ya kigamboni jijini Dar es Salaam


Mnyama kakakuona aonekana maeneo ya kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mnyama kakakuona ameonekana kigamboni kisiwani kata ya Vijibweni na kutengewa vitu mbalimbali na wazee hatimae amechagua maji, unga na fedha hali inayoashiria kuwepo kwa mvua nyingi kipindi hiki.
Akioongea wakati wa kumwekea vitu hivyo, mzee Salum Abdalah amesema katika miaka iliyopita mnyama huyo uwa akionekana ni baraka katika eneo husika na nchi kwa jumla kwa kuwa utoa mwelekea wa yatakayojitokeza katika kipindi kijacho. 
 
Akizungumzia kuhusu kakakuona, mmiliki wa nyumba aliyokutwa mnyama huyo, bibi Tatu Lukatala amesema wamemkuta mnyama huyo katika maeneo ya banda ya kuku baada ya kuwepo kwa kelele nyingi za mbwa huku baadhi ya majirani wakiomba idara ya maliasili kufika katika maeneo hayo kwa ajili ya kumchukua na kumhifadhi.
Powered by Blogger.