Mvua ya muda mfupi yaleta mafuriko jijini Dar es Salaam.
Mvua ya muda mfupi yaleta mafuriko jijini Dar es Salaam.
Mvua
zilizonyesha kwa muda mfupi katika jiji la dar es Salaam zimesababisha
mafuriko katika maeneo ya katikati ya jiji na kusababisha baadhi ya
maduka kufungwa na magari kuzimika barabarani kutokana na kuingiwa na
maji kulikotokana na tatizo sugu la miundombunu ya maji taka.
ITV imetembelea katika maeneo mbalimbali ya jiji hapo katika
makutabo ya barabara ya Morogoro na Bibi titi imeshuhudiwa idadi kubwa
ya maduka kufungwa kutokana na hofu ya kuingiliwa na maji yaliyokuwa
yamefurika barabarani ambapo baadhi ya madereva wakilazimika kusukuma
magari yao baada ya kuziba kutokana na kuingia maji huku watembea kwa
wakilazika kupita kwenye maji hali inayoweza kuhatarisha afya zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wakazi wa jiji la
Dar es Salaam wameitaka serikali kutenga fedha na kuweka mikakati
maalumu ili kuondoa kero sugu ya tatizo la miundombinu ya maji taka
katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha ITV imepita katika eneo la Jangwani na kukuta eneo maalumu ya
ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo haraka likiwa limezungu kwa
maji ambapo baadhi ya wananchi wanaoishi maeneo hayo wameitaadharisha
serikali mradi huo hautaweza kufanya kazi kama inavyokusudiwa hususani
wakati wa mvua bila kuongeza kina cha daraja la mto msimbazi ili
kuwezesha maji mengi kuelekea baharini.