Nyalandu ajitosa rasmi mbio za Urais kupitia CCM 2015
WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel
WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu, ambaye ametangaza rasmi kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Singida.WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la
Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu,ametangaza rasmi nia ya
kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwakani.
Nyalandu ametangaza nia hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilongero Jimbo la Singida kaskazini.
Alisema
baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kujikagua kwa kina,ameona anao
uwezo wa kutosha wa kuweza kupokea kijiti kutoka kwa rais anayemaliza
muda wake mwakani kwa mujibu wa katiba.
“Kujikagua huko
ni pamoja na kutafakari jinsi alivyoweza kutekeleza ilani ya uchaguzi
ya CCM katika vipindi vitatu (miaka 15) akiwa mbunge wa jimbo la Singida
kaskazini.Katika kipindi hicho cha ubunge,nimeweza kutumia zaidi ya
shilingi bilioni mbili katika kufanikisha kuchangia miradi ya maendeleo
katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya,maji na barabara”,alisema
Nyalandu.
Alisema wakati ukifika,Watanzania kutoka
sehemu mbalimbali za nchi wakiongozwa na wakazi wengi wa kutoka jimbo la
Singida kaskazini,kwenda Dodoma kuchukua fomu za kuwania urais.
“Watanzania
waliokwisha onyesha nia ya kuwania urais mwakani,nawaomba sote
tuonyeshe kazi tulizozifanya katika kuwahudumia Watanzania,ili waweze
kutupima vizuri waweze kujijengea mazingira mazuri ya kuchangua rais
atakayewafaa kwa kuwaletea maendeleo endelevu”,alisema.
Nyalandu
alisema kuwa anakishukuru Chama Cha Mapinduzi,kwa maandalizi yake
mazuri ya kuhakikisha chama kinapata mwanaCCM safi,mwadilifu na mchapa
kazi atakayepeperusha bendera ya chama katika kinyang’anyiro cha kuwania
urais mwakani.