Afungwa jela miaka 30 kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imemuhukumu kifugo cha miaka 30 jela, Stephan Moleli
Hai. Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imemuhukumu kifugo cha miaka 30 jela, Stephan Moleli mkazi wa Ngereiyani Wilayani Siha kwa kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhii wa Mahakama ya Wilaya ya Hai, Martha Mahambuga baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi wanne, kuthibitisha bila ya kuacha shaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Roymax Membe alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni, mwaka jana muda wa saa nane mchana huko Ngereaiyani wilayani Siha mkoani hapa.
Inadaiwa kuwa Molleli aliiba pikipiki moja aina ya Daz yenye thamani ya Sh,1,700,000 mali ya Shabani Hamza na simu moja aina ya Nokia 6,000 yenye thamani ya Sh100,000, kwa kutumia silaha dhidi ya Saidi Shabani kwa lengo la kujipatia vitu hivyo.
Kwa mujibu wa kifungu cha sheria 287(a) Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 marekebisho ya 2002, kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha mahakama imeridhishwa na ushahidi hivyo mshtakiwa kutumikia kifugo jela miaka 30.
Powered by Blogger.