Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji
Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo
wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa
hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni
kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa
habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa
pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona
hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa
amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa
Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea
kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa
amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.
“Huu
uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi kujiuzuru kwa
kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata hili la Escrow” anasema
Profesa Anna Tibaijuka.