Banki Moon ayatembelea mataifa ya ebola

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon yuko eneo la Afrika magharibi kama sehemu ya ziara ya siku mbili ya kuzitembelea nchi zilizoathirika na ugonjwa wa ebola.
Kituo chake cha kwanza kilikuwa nchini Liberia ambapo aliosha mikono yake na kupimwa joto muda mfupa baada ya ndege kutua zikiwa hatua mbili muhimu za kuzui kusambaa kwa ugonjwa huo.
Bwana Ban aliwashauri watu kufuata kwa makini kanuni za afya hadi ugonjwa huo uangamizwe.
Katika nchini zilizoathiirika zaidi na ugonjwa huo zikiwemo Guinea, Liberia and Sierra Leone njia za kitamaduni za kuzika maiti zimechangia kusambaa kwa ugonjwa huo.
 bbcswahil