Kibarua cha mama kumpa mwanawe 'Bangi'

Mamake Liam anasema hana budi ina kumpa mwanawe Bangi kwani anahitaji matibabu hayo kila siku
Mama wa kijana anayeugua kifafa amekataa kumpa mwanawe wa kiume bangi kama matibabu inavyotakikana-kupitia moshi na mvuke. Mtoto huyo anapasawa kutumia Bangi kama dawa kupambana na ugonjwa wake wa Kifafa kwa maagizo ya daktari.
Liam McKnight mwenye umri wa miaka sita napenda kucheza na ndiye wa kwanza kila mara kukimbia kuelekea mlangoni.Mamake mzazi,Mandy,anasema kuwa mwanawe anapenda kujua nani anawatembelea.
Familia hiyo ya McKnight inayoishi jijini Otawa nchini Canada ina wageni wengi wanaowatembelea-kutoka kwa wanachama wa kukindi cha densi anachoshiriki binti yao,na hata wauguzi wa kutamka,wa kunyosha viungo vya mwili,wataalam wa kusikiza-wote wanaomtembelea Liam.
Liam ana ugonjwa unaojulikana kama Dravet ambayo,ni aina kali sana ya kifafa.Afya yake hudhoofika mara kwa mara lakini baada ya kufanyiwa majaribio kadha wa kdha ya matibabu ya ugonjwa huo, anglau hali yake imeimarika kidogo.
Mamake Liam humpa mafuta ya Bangi, ambayo yemtolewa kwa sehemu changa sana ya mmea huo.
Mwezi Juni mwaka huu,siku kabla Liam kuanza kutumia mafuta hjayo ya Bangi,(iliyotengezwa kutoka kwa aina ya bangi yenye ufanisi) alizirai kama mara 67. Katika siku kumi zilizofuatia alizirai tu mara moja.
Nchi nyingi duniani zinakabiliwa na changamoto za kuidhinisha matumizi ya Bangi.
Tatizo ni kuwa matibabu ya Liam ni haramu. Kutumia dawa inayotengezwa kwa Bangi inakubalika Canada lakini lazima iwe tu majani ya Bnagi yaliyokaushwa au mvuke wa majani hayo.
Kwa Mandy hilo haliwezakni kwa mwanawe kuvuta moshi wa Bangi akiwa umri huo mdogo.
Matoto mdogo anawezaje kuvuta Bangi? anauliza mamake Liam.
Mapema mwaka 2001, Canada iliruhusu wagonjwa wanaohisi uchungu mwingi kutumia Bangi kama matibabu. Lakini hakuna majaribio yaliyofanyiwa mafuta ya Bangi kujua usalama wake kwa afya ya mtu.
Liam ana umri mdogo sana lakini anaweza kutumia mvuke wa Bangi lakini mamake Liam anasema vipimo vinyovyofa akwa afya ya Liam ni vya mafuta ya Bnagi.
Mamake Liam aliwahi kuiandikia serikali Barua kuielezea kuhusu masaibu yake kuhusiana na matibabu ya Liam. Lakini waziri wa afya alimjibu kwa kusema anaelewa masaibu ya mtoto Liam wakati akikabiliana na ugonjwa wake hatari wa kifafa. Lakini alisisitiza kuwa hadi leo serikali bado haijaidhinisha matumizi ya mafuta ya Bangi wala uuzaji wa mafuta hayo nchini Canada.
Matumizi ya mafuta ya Bangi, yaliruhusiwa mjini Minnesota Marekanimwezi Mei, lakini sheria hiyo haitaanza kutumika hadi Julai mwaka 2015.
Sheria za Bangi kote duniani zinatofautiana.
Mamake Liam anafahamu kuwa anavunja sheria pamoja na kufahamu athari z akutumia mafuta ya Bangi. ''Je nahofia kuwa navunja sheria? ndio. Lakini nahofia zaidi ikiwa hatutafanya chochote hali ya afuya ya mtoto wangu itazorota.
Kwetu Mafuta ya Bangi ndio tiba anayohitaji mwanangu. Hatukuwa na mda wa kusubiri majaribio kufanywa. Kwa kila siku, Liam hula kijiko kimoja cha Bangi ikiwa imechanganywa na mafuta ya nazi.