Meseji za Mapenzi za Kajala na Bwana Aliyekuwa na Wema Sepetu Zanaswa
BAADA ya taarifa za mwigizaji Kajala Masanja kudaiwa kumuibia bwana
aliyekuwa shosti yake, Wema Sepetu kudumu kwa muda mrefu na kukosa
ushahidi wa moja kwa moja, hatimaye ushahidi wa SMS za mapenzi za Kajala
na bwana huyo wa Wema ambaye ni kigogo zimenaswa, Amani linakumegea
mchongo kamili
Chanzo makini kilichokuwa karibu na Kajala na kigogo huyo, kilipenyeza habari kuwa kimefanikiwa kuzinasa meseji za Kajala kupitia kwenye simu ya kigogo huyo ambaye alidumu katika penzi na Wema kisha kumwagana baada ya Kajala kuingilia kati.
“Nimetumia ujanja wa hali ya juu hadi nikafanikiwa kupata SMS za Kajala na yule kigogo wa Wema, kama vipi niwatumie,” kilisema chanzo chetu.Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, SMS hizo zilionesha namna Kajala alivyokuwa akiitana baby na kigogo huyo, huku wakiwa ‘dip kimalovee’ kiasi cha kigogo huyo kuwagharamia wazazi wa Kajala mahitaji mbalimbali.
“Jamaa walikuwa wanapika na kupakua, kigogo alikuwa akigharamia kila kitu, kuanzia misosi ya nyumbani, usafiri wa location na hata kwa wazazi wa Kajala, alikuwa anatuma fedha,” kilisema chanzo hicho.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuzinasa SMS hizo na kujionea zikiwa na majibizano ya muda mrefu huku zikitaja pia marafiki wa Kajala anaofanya nao kazi kwa muda mrefu.
Baada ya paparazi wetu kumwagiwa SMS hizo, alimvutia waya Kajala ambaye alizikana SMS hizo na kuomba atumiwe ndipo atoe jibu ambapo mwandishi wetu alifanya hivyo lakini hakujibu chochote na hata alipopigiwa tena, hakupokea.
GPL