Ufeministi
Ufeministi
Kikosi cha Femen ni Wafeministi wenye itikadi kali.
Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile. [4]
Kati ya haki hizo za msingi, ufeministi umepigania kwa mfano zile za kupiga kura, kupata vyeo serikalini, kufanya kazi, kulipwa mshahara, kumiliki, kupata malezi, kufanya mikataba sawa na wanaume n.k.
Ufeministi umepinga pia ubakaji wa aina zote.[5]
Ufeministi ni kati ya matapo yaliyochangia zaidi mabadiliko katika jamii.
Historia
Katika historia harakati za kudai haki za wanawake zilianza katika Ulaya wakati haki za binadamu zilipoanza kutangazwa, ambazo awali zilijadiliwa kwa wanaume pekee.Harakati ya kuwapa wanawake haki za kupiga kura kwenye uchaguzi wa kisiasa ilikuwa kampeni ya awali kuanzia karne ya 19.
Mikondo tofauti ya ufeministi leo
Mgawanyiko umeanza kujitokeza kati ya wale wanaotaka wanawake wafanane kabisa na wanaume na wale wanaoona umuhimu wa kutunza upekee wa mwanamke katika uhusiano wa kukamilishana na mwanamume. Kwa mfano:- wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani hoja ya jadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa: wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki katika shughuli zote sawasawa.
- wengine hukubali kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakini tofauti hizo zisiruhusiwe kuwapa wanaume kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa, lakini wasilazimishwe kufanya hivyo, nao wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hiyo ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka waliyoitumia kwa kazi ya nyumbani.
- wengine husema jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenzi ya wanaume, hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapinduzi katika jamii.
- kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume, na ni muhimu watoe mchango wao wa pekee.