Sintaksia ya kijalizo cha Kiswahili Sanifu: mtazamo wa x-baa.

                                                                                                                                                                                                         
Utafiti wetu umechanganua kijalizo cha Kiswahili kwa kutumia nadharia ya X-baa. Tumepanua tafsiri ya kijalizo cha Kiswahili sanifu na kubainisha uamilifu wake katika tungo. Tumebainisha miundo tofauti ya vijalizo na kudhihirisha sheria zinazotawala uunganishwaji wa vipashio vinavyojaliza virai tofauti katika sentensi. Sura ya kwanza inaweka wazi mada ya utafiti, sababu ya kuchagua somo, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, msingi wa kinadharia na yaliyoandikwa kuhusu mada. Katika sura ya pili tumewekea msingi kazi yetu kwa kufafanua dhana tofauti ambazo tumetumia katika kuchanganua kijalizo. Dhana hizi ni kama vile, sintaksia, vishazi, virai na kategoria amilifu za sentensi. Katika sura ya tatu tumechanganua miundo tofauti ya Kijalizo. Kijalizo kinaweza kuwa nomino au kirai nomino, kihusishi au kirai husishi, kivumishi au kirai vumishi, kitenzi au kirai tenzi. Pia tumejadili aina tofauti za kijalizo kwa msingi wa nadharia ya x-baa. Kwa mfano, kijalizo cha kitenzi, kijalizo cha nomino, kijalizo cha kivumishi kijalizo cha kihusishi na kile cha kielezi. Katika sura ya nne, tumeandika matokeo ya utafiti, mapendekezo na mwisho , hitimisho.Tuligundua kuwa dhana ya kijalizo hueleweka kwa njia nyingi kutegemea mwelekeo wa nadharia inayotumiwa. Kijalizo katika sarufi mapokeo kilichukuliwa kuwa neno au fungu la maneno linalotokea baada ya kitenzi kishirikishi. Katika utafiti wetu, tumetumia nadharia ya x-baa kufafanua kijalizo. Kijalizo katika nadharia ya x-baa ni neno au fungu la maneno linalofungamanishwa moja kwa moja na kichwa cha kirai husika (dada ya kichwa cha kirai). Kijalizo hupanua kichwa cha kirai hadi kiwango vii kingine. Kwa mfano: Funga huo mlango. Maneno kwenye mlazo  kijalizocha kitenzi ‘funga’.
Powered by Blogger.