MSWAHILI NI NANI

 
 
 MSWAHILI NI NANI
Dhana ya "Mswahili"
Dhana ya "mswahili ni nani?" ni dhana pana na imejadiliwa na  wanataaluma mbalimbali. Uwepo wa mjadala huu umetokana dhana ya  Mswahili kuwa tata kwa "Waso- Waswahili" lakini pia na "Waswahili"
wenyewe (Massamba:2002)
 Hivyo  ikaonekana haja  ya kumfasili  Mswahili ili  kutataua mgogoro huo na kumpa uhalali wa kuwepo na kutumia lugha yake ya Kiswahili.
Kuna wanazuoni mbalimbali waliojadili dhana ya Mswahili. Wataalamu  wafuatao walijaribu kutoa maana ya Mswahili
Kwa mujibu wa  Stigand (1913), anaeleza kuwa "Mswahili" ametokana na uzao wa mmojawapo wa Waarabu, au Waarabu  na Waajemi walioishi katika upwa wa Afrika Mashariki.
Vilevile Steer (1870), anaeleza kuwa Mswahili ni mtu mwenye mchanganyiko wa  Kinegro na Kiarabu.
Nae  Prins (1967) ambaye anafafanua maelezo ya watu  wengine juu ya dhana ya Mswahili na mawazo hayo yanamnasibisha  Mswahili na Mwarabu.
Na  Ponera (2010), Mswahili ni mtu mwenye kiwango kikubwa cha umilisi wa lugha ya Kiswahili. Vilevile , ni mtu ambaye amefungamana sana na mila na desturi za jamii ya watu watumiayo lugha ya Kiswahili kiasi hata cha kumuathiri kifikira, kimtazamo na kiitikadi.
DAFINA YA KISWAHILI
INAELEZA DHANA YA MSWAHILI:
Kutokana na mtazamo hiyo na dhana na maendeleo ya lugha ya kiswahili, inaonekana wazi kuwa ni vigumu kumpata mswahili ambaye ni mmiliki wa lugha hii ya kiswahili. Inaonesha dhahili kuwa mswahili anaweza kutazamwa kwa namna tofauti kama zifuatazo;-
i).  Mswahili anaweza kuwa ni mtu mahuruti yaani ni mtu chotara ambaye ni lazima awe ametokana mwingiliano wa pande mbili ambao ni wabantu na watu wanaonasibishwa na Waarabu
ii). Mswahili anaweza kuwa ni mtu wa mjini aliyeacha dini, utamaduni, mila na desturi zake za asili na kukimbilia dini, utamaduni, mila na desturi kutoka mataifa mengine kutoka uarabuni na nchi za kimagharibi
iii). Mswahili anaweza kuwa ni mtu ambaye anazungumza vizuri lugha ya kiswahili kwa kufuata taratibu zote za kiisimu na utamaduni wa lugha ya kiswahili
iv). Mswahili anaweza kuwa ni mkazi wa ya Afrika Mashariki hususani paeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki.
v). Mswahili anaweza kuwa ni mtu anayeishi katika maeneo ya kawaida ya mjini (uswahilini)
vi). Mswahili anaweza kuwa ni mtu ambaye ni mwafrika asili, anayepatikana katika nchi za Kenya na Tanzania
v). Mswahili ni mtu mwenye maumbile na ya kiafrika, ikimaanisha kuwa ni mtu wa miraba minne. 
MAREJEO YA ZIADA
Massamba, D.P.B (1995) 'Lahaja na Mitindo katika Kiswahili Sanifu' katika
Kiango, J. (mh),Dhima ya Kamusi katika Kusanifisha Lugha. uk. 1 - 17.
 Steere, E. (1930) A handbook of the Swahili Language. East African Language
Committee
Stigand, C.H. (1915) Dialects in Swahili. Cambridge University Press
Ponera, A.S.  and Luhwango, N.  (2015), Riwaya ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Powered by Blogger.