FASIHI SIMULIZI:




FASIHI SIMULIZI:
Hii ni sanaa itoayo maudhui yake kwa kutumia
lugha ya maneno ambayo hutamkwa au kutendwa.
Makala ya Fasihi Simulizi:
i)Lugha ndiyo itumiwayo fanani.
ii) Matumizi ya maneno kisanaa.
iii) Huonyesha hisia za binadamu.
iv) Hufunulia shughuli na kazi za watu husika.
v) Huonyesha uhusiano baina ya binadamu na
mwingine.
vi) Humtazama binadamu na mazingira yake.
vii) Huwajenga watu kitabia.
Umuhimu wa Fasihi Simulizi:
i) Hutuwezesha kuelewa utamaduni na historia
yetu vyema.
ii) Husaidia katika elimu ya jamii.
iii) Husaidia katika uga wa siasa- ulumbi
iv) Hukuza ufasaha na ustadi wa mtambaji.
v) Hufurahisha na kuburudisha.
vi) Huendeleza umoja na utangamano.
vii) Hukuza mtalaa wa lugha.
viii) Huipa jamii mwelekeo na nasaha kwa
kuonya na kushauri.
ix) Hukuza upeo wa wanafunzi.
x) Hufunza mbinu za sanaa na uchambuzi.
xi) Kupokezana utamaduni wa jamii.
xii) Kukuza maadili katika jamii.
xiii) Ni kazi kwani watu hupata malipo kutokana
na fasihi.
xiv) Huwazindua watu ili wajue haki zao.
xv) Hurekebisha tabia.
Sifa bainifu za uwasilishaji wa Fasihi Simulizi na
Fasihi Andishi:
Fasihi Simulizi Fasihi Andishi
1. Huwasilishwa kwa mdomo -
Hutegemea maandishi yasomwayo
2. Hadhira huwasiliana na mwasilishaji -Si
lazima hadhira iwasiliane na msimulizi
3. Hadhira huweza kuchangia -Hadhira
haina njia ya kuchangia usimulizi
4. Humilikiwa na jamii -Ni milki
ya mtunzi au mwandishi
5. Ina tanzu nyingi -Haina
tanzu nyingi
6. Sifa zisizo za lugha kutumika -
Hutegemea sifa za lugha isipokuwa igizo
7. Huonyesha ubunifu mpya -Hubakia
kama ilivyoandikwa na mtunzi
8. Huifadhiwa akilini kwa kukumbuka -
Huifadhiwa kwa maandishi vitabuni
9. Huweza kubadilishwa (ufaraguzi) -
Msomaji hana uhuru wa kubadilisha
10. Msamiati wa utungo kupotea -Kazi
hubakia kama ilivoandikwa
11. Kuambatanisha na utendaji -
Haiambatanishwi na utendaji ijapo’ igizo
12. Hutumia wahusika changamano -
Hutegemea sana wahusika binadamu
Muainisho wa Fasihi Simulizi:
Tanzu nne kuu za Fasihi Simulizi ni:
a) Hadithi/ Simulizi-hutumia lugha nathari
b) Maigizo-uwasilishaji mbele ya hadhira
c) Semi- ufupi wa kimuundo
d) Ushairi- uimbaji na muundo maalum
Vipera vya Tanzu hizi:
a) Hadithi/ Simulizi b) Maigizo
i) Migani/ mighani I) Michezo ya
jukwaani
ii) Hekaya ii) Mazungumzo
iii) Khurafa/ hurafa iii) Vichekesho
iv) Ngano za mazimwi iv) Ngomezi
v) Soga v) Ulumbi
vi) Ngano za mtanziko iv) Malumbano ya
utani
c) Ushairi d) Semi/ Tanzu-bainifu
i) Nyimbo I) Methali
ii) Ngonjera ii) Nahau
iii) Sifo iii) Misimu iv) Maghani iv) Misemo
v) Majigambo v) Lakabu
vi) Vitendawili
vii) Vitanza-ndimi


Powered by Blogger.