TAFSIRI NA UKALIMANI NI TAALUMA MUHIMU SANA ULIMWENGUNI

 DHANA  YA  TAFSIRI
Kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake (2006) wanaeleza kuwa tafsiri ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine. Woa wanatilia mkazo katika zoezi la uhawilishaji na kinachohawilishwa ni mawazo katika maandishi.
Pia Catford (1965) anaeleza kuwa, kutafsiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha mmoja yaani lugha chanzi na kuweka badala yake mawazo yanayolingana kutoka katika lugha nyingine yaani lugha lengwa. Hapa msisitizo upo katika matini zilizoandikwa na kuzingatia zaidi ujumbe au wazo lililopo katika matini chanzi lijitokeze vile vile katika matini lengwa. Mawazo haya hayawezi kuwa sawa kabisa na ya matini chanzi bali ni mawazo yanayolingana toka matini chanzi na matini lengwa, hii ni kutokana na sababu tofauti kama vile utamaduni, historia, kiisimu na mazingira.
Naye Newmark (1982) anaeleza kuwa tafsiri ni mchakato wa uhawilishaji wa maneno kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa.
Pia Nida na Taber (1969) wanaeleza kuwa tafsiri hujumuisha kuzalisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutumia visawe vya asili vya lugha lengwa vinavyo karibiana zaidi na lugha chanzi kimaana na kimtindo. Wao wanatilia mkazo uzalishaji upya wa kwa kutumia visawe asili vinavyokaribiana na matini chanzi kimaana na kimtindo. Kutokana na maana hizi tunaweza kusema kuwa tafsiri hufanywa katika ujumbe uliopo katika maandishi, ni jaribio la kiuhawilishaji na wazo linalatafsiriwa huwa na visawe vinavyokaribiana na sio sawa kutokana na tofauti za kiisimu, kihistoria, kiutamaduni na mazingira.
Kwa  ujumla  tunaweza  kusema
Tafsiri  ni  taaluma  inayohusika  na  uhaulishaji  wa   mawazo  kutoka  lugha  chanzi  kwenda  lugha  lengwa   kwa  maandishi  bila  ya  kupoteza , kupotosha  na  kubadili  maaana .mawazo  yanayoshugulikiwa  katika  taaluma  ya  tafsiri  sharti  yawe  kwenye  maandishi  na  yalingane  kati  ya  lugha  lugha  asilia  na  lugha  lengwa.
AINA  ZA  TAFSIRI
Tafsiri  ya  neno   kwa  neno ,  Hii  ni  tafsiri  amboyo  mofimu  na  maneno  mengine  hufasiriwa  yakawa  pwekepweke  kwa  kuzingatia  maana  zake  za  msingi  bila  kujali  muktadha. Mpangilio  wa  mofimu  na  lugha  chanzi  hubaki  vilivile , maneno  yanayofungamana  na  utamaduni   hufasiliwa  kisisisi .matini  ya  tafsiri (matini  lengwa)  huwandikwa  chini  ya  matini  ya  lugha  chanzi
Mfano  (1) Kiswahili        : a – li – lala – hadi –asubuhi
                 Kiingereza        : she /past /sleep/  until / morning
             (ii) kiwahili           : a  -likwenda / nyumbani / kwke
                Kiingereza          : he / past  / until /at /house /his.
Ø  Ubora  wa  tafsiri  neno  kwa  neno
Tafsiri  ya  aina  hii  humsaidia  kumsaidia  kuelewa  jinsi  lugha inavyofanya  kazi  katika  kuanisha  muundo
Ø  Udhaifu  wa  tafsiri  ya moja  kwa  moja
Upungufu  wa  tafsiri  ya  neno  kwa  neno  ni  kwamba  mara  nyingi  haitoi   kwa  uangavu  maana  inayokusudiwa  kwa  sababu  nahau  na  misemo  inayohusika  na  utamaduni  hufasiliwa  kisisisi.
sababu  nahau  na  misemo  inayohusika  na  utamaduni  hufasiliwa  kisisisi.
Tafsiri  sisisi
Kwenye  aina  hii  ya  tafsiri  maneno  hufasiliwa  yakiwa  pwekepweke  kwa  kuzingatia  maana  zake  za  msingi  katika  lugha chanzi  bila  kujali  sana  muktadha . lakini  kufuatana  na  mfumo  wa  kisarufi ,hususani  sintaksia  ya  lugha  lengwa
Mfano    kiingereza      :He  was  taken  a  centrel  police  station
               kiswahili       : Alipelekwa  kwenye  kituo  cha  kati  cha  police ( badala  ya  kituo        
                                      kikuu  cha  police)
           kiingereza        :Dear  listener , lend  me  your  ears
             kiswahili          : Wasikilizaji  wapendwa , niazimeni  masikio  yenu (badala  ya naomba 
                                     mnisikilize.
Mfano   Kiingeza   : Two  heads  are  better  than one
              Kiswahili   : Mbili  vichwa  ni  bora  kuliko  moja .(badala  yake  vichwa  viwili  ni  bora 
                                  kuliko  kichwa   kimoja
              Kizaramo   : Zege dimlemelwe  fisi ,mbwa  domgela  muhe.
               Kiswahili   : Mfupa uliomshinda  fisi  mbwa  utampa  pumu
Ø  Ubora  wa  tafsiri  sisisi  :
 Tafsiri  hii  husaidia  sana  mfasiri kuwa  hakuna  maaana  ya kudumu  ya  maneno , bali  maana  halisi .Kutokana  na  matumizi  yake  katika  muktadha  maalumu  aidha  aina  hii  ya  tafsiri  hutumika  sana  katika  tafsiri  ya  vichekesho  kwani  huibua  ukinzani  wa  ajabu  katika  tungo .(Mfano; My name is Dr Livingstone I come from Johanesberg
Ø  Upungufu  wa  tafsiri  sisisi  : Tafsiri  sisisi  agharabu  hutoa  tafsiri  potofu  na  kwa  hiyo  huwa  na  uwezekano  wa  kuleta     utata  na  hasara  katika  mawasiliano
Tafsiri ya  kisemantiki/maana/uwazi/(semantic trasilation)   hii ni aina ya tafsiri ambayo mfasiri huegemea zaidi kwenye kugha chanzi. Katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hufasiri kila neno katika sentensi jinsi ilivyo ila kwa kufuata sarufi hususani vipengele vya kisemantiki na kistakisia ya lugha chanzi.Katika aina hii ya tafsiri masahihisho au ya neno au jambo lolote unalodhani limekosewa haliruhusiwi isipokuwa uweza kuweka haya marekebisho hayo au ufafanuzi katika tanbihi. (mujibu wa( Catford na Nida 1965)
Mfano  :  Kizaramo    :  kihanga  cha  mkulu  kilava  nongo  ya ugimbi.
                 Kiswahili    : uso  wa  mkubwa  umetoa  mtungi  wa  pombe
                 Kizaramo     :ngwengwe  hadisolo  jake
                  Kiswahili     : dume  la  njani  huwa  na  mamlaka  zaidi  katika  eneo  lake
Ø  Ubora  wa  tafsiri  :
Ubora  wa  tafsiri  ni  kuwa  na  uwezo  mkubwa wa  kuendeleza lugha  legwa kwa  kuingiza   miundo  na  misemo  toka  lugha  asilia .
Ø  Udhaifu  wa  tafsiri  :
 tafsiri  hii  haitilii  maanani  nahau , misemo  maalumu  inayohusiana  na  utamaduni  na  lugha  inayolengwa  katika  tafsiri . Mfano  (Assaina  married  Mtillah. –kiwahili :Assaina  alimuoa  Mtillah)  badala Asha  kuolewa  na  Moses  kwani  katika Kiswahili  mwanamke  huwa  anaolewa  na  mwanaume  ndiye  anaoa  hii  huweza  kuleta  utata  katika  lugha  ya  kiwahili  kwa  mwanamke  ndiye  kuoa  na  mwanaume  kuolewa.
Tafsiri  ya  kimawasiliano ,
hii  ni  aina  ya  tafsiri  ambayo  huzingatia  hadhira ya  matini  ya  lugha  lengwa   kwa  kumjali  sana  msomaji  wa  matini  hiyo . hii  ni  tafsiri  huru  kwa  sababu  mfasiri  anaweza  kuongeza  au  kupunguza  maneno  ya  matini  ya  lugha  asilia wakati  wa  kufasili  ili  mradi  ujumbe  uwafikie  kwa  namna  inayotakiwa  na  bila  kupoteza  wazo   la  matini  ya  lugha  asilia, mfasiri  ana  uhuru  wa  kutafuta  maneno  au  mafungu  ya  maneno  yanayolingana  na  nahau,misemo ,methali , utamaduni  na  mazingira  ya  lugha  lengwa
Ø  Ubora  wa  tafsiri  mawasiliano
Ubora  wa  tafsiri  hii  ya  kimawasiliano  ni  kwamba  hufuata  kanuni  taratibu  na  sheria  za  lugha  lengwa  na  kuzingatia  mweelekeo  wake  wa  kiutamadudi ,kiistoria ,kimazingira  na  kijamii  kwa  hadhira  lengwa
Mfano
Kiingereza    : Veronika  married  chris
Kiswahili       :chris  alimuoa  veronica
Ø  Udhaifu  wa  tafsiri  mawasiliano
Kutokuwa  na  uwezo  wa  kuendeleza  ,kuingiza  miundo  au  misemo  kutoka  lugha  asilia  kwenda  katika  lugha  lengwa. Hali   hii  inatokana  na  ukweli  kuwa  tafsiri  hii  haizingatii  miundo ,misemo , na  msamiati  wa  lugha  asilia  wakati  wa  kufasiri  bali  huzingatia  wazo  la  jumla  la kiutamaduni  kwa  lugha  lengwa
Udhaifu  mwingine  katika  tafsiri  ya  kimawasiliano hujitokeza  pale  mfasiri  anapoegea  sana  kwenye  mawzo , historia ,utamaduni , mazingira  na  itikadi  ya  lugha  lengwa . kwa  mfano  katika  mwaka  2002  vyombo  vya  habari  vilisikika  vikitangaza
Mfano kiingereza  : His  excellency  president  saddam  Hussein  (vyombo  vya  habari  vya
Iraq     mwaka  2002)
Kiswahili    :Gaidi  saddam  Hussein  ( vyombo  vya  habari  vya  marekani  mwaka 2002
Kutokuwa  na  uwezo  wa  kuendeleza  ,kuingiza  miundo  au  misemo  kutoka  lugha  asilia  kwenda  katika  lugha  lengwa. Hali   hii  inatokana  na  ukweli  kuwa  tafsiri  hii  haizingatii  miundo ,misemo , na  msamiati  wa  lugha  asilia  wakati  wa  kufasiri  bali  huzingatia  wazo  la  jumla  la kiutamaduni  kwa  lugha  lengwa
Udhaifu  mwingine  katika  tafsiri  ya  kimawasiliano hujitokeza  pale  mfasiri  anapoegea  sana  kwenye  mawzo , historia ,utamaduni , mazingira  na  itikadi  ya  lugha  lengwa . kwa  mfano  katika  mwaka  2002  vyombo  vya  habari  vilisikika  vikitangaza
Mfano kiingereza  : His  excellency  president  saddam  Hussein  (vyombo  vya  habari  vya
Iraq     mwaka  2002)
Kiswahili    :Gaidi  saddam  Hussein  ( vyombo  vya  habari  vya  marekani  mwaka 2002)
                                                         MAREJEREO
Catford J.C. (1965) A Linguistic theory of Translation: OUP London.
Mwansoko, H.J.M. na wenzake (2006) Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu: TUKI
                         Dar es Salaam.
Newmark, P. (1988) A Textbook of Translaton. : Prentice Hall London.
Nida, A. E. na Charles, R. T. (1969) The Theory and Practice of Translation. The United
                       Bible Societies: Netherlands.
Wanjala S. F (2011) Misingi ya ukalimani na tafsiri; Serengeti Education publisher (T)
                      L.T.D. Mwanza Tanzania
Powered by Blogger.