Majadiliano:Ufeministi
Ufeministi (far. féminisme) unamaanisha harakati ya ukombozi wa wanawake.
Neno hili linataja jumla ya harakati na itikadi tofautitofauti zinazolenga kufikia usawa wa haki za wanawake katika siasa, uchumi, utamaduni na jamii kote duniani. Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile. [1] Hii ni pamoja kutafuta nafasi sawa kwa wanawake katika elimu na ajira.
Kuna mikondo tofauti za ufeministi

- wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani ya hoja la kijadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa na wanaume sawa na wanawake wanapaswa kushiriki katika shughuli hizi sawa.
- wengine hukubali kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakinitofauti hizi zisiruhusiwe kuwapa wanauma kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa lakini wasilazimishwe kufanya hivyo na ya kwamba wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hii ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka walipotumia kwa kazi ya nyumbani.
- wengine husema ya kwamba jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenziy a wanaume hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapindizi katika jamii.
- kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume.