CHIMBUKO YA KISWAHILI NA WASWAHILI

 

CHIMBUKO YA KISWAHILI NA WASWAHILI

CHIMBUKO LA KISWAHILI
NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU CHIMBUKO LA KISWAHILI
Kiswahili ni lugha ya kiarabu.waasisi wa nadharia ni kama vile stignd,Reusch na Knappert wanaodai kwamba Kiswahili ni mojawapo wa kati ya lahaja ya kiarabu.vile vile wanasema kuwa utamaduni wa waswahili ni utanzu wa waharabu

USHAIDI UNAOTOLEWA
1.      Wanasema kwamba lugha ya Kiswahili imekopa maneno mengi ya kiarabu kama vile
a.buibui
b.daima-milele
c.fahamu-elewa
d.katibu-mwandishi
       2.lugha ya Kiswahili imefungamana na mafunzo ya dini ya kiislamu.wao hutumia majina                                                mengi ya kiislamu kama vile
                Mohamed
                Rajab
                Mwanaidi
   Baadhi ya maneno ya Kiswahili yaliyokopwa kutoka kwa kiarabu yanahusiana na masaa ya waisilamu ya kuswali.kwa mfano, alfajiri,adhuhuri,ramashari,alasiri
      3.wanadai nyimbo za taarabu ziliteuliwa kuimbwa kwa kiarabu ndipo zikaanza kuimbwa kwa mashairi ya Kiswahili
 OHLY anadai kwamba waswahili walilazimika kutunga nakuimba mashairi ya Kiswahili yaliyoitwa mangazi ili  waepuke kufanywa watumwa na waarabu.
4.ustaarabu wa uswahilini umebuniwa na kuimarishwa na wageni waliotoka nchi za magharibi uarabuni,uajemi nauturuki. Ustaarabu huo ni pamoja na mavazi kama vile buibui,mtandio,kanzu,kikoi na kofia ya kiislamu na vyakula kama vile papuru na papai.



UPUNGUFU WA NADHARIA HII
1.Watafiti wa lugha ya uarabuni wanasema kuwa Kiswahili si mojawapo ya lugha ambazo zinapatikana uarabuni na hamna lahaja yoyote ya kiswahilui.
2.kukopa maneno kutoka lugha moja hadi nyingine ni jambo la kawaida.si Kiswahili tu kimekopa manena kutoka kwa lugha ya kiarabu. Lugha nyingine kama kiausa,kihindu bara hindi na kimalay huzungumzwa maleyzimekopa maneno ya kiarabu
3.kiswahili hakijakopa maneno kutoka kwa lugha ya kiarabu bali kutoka kwa lugha nyingine. Kwa mfano hospitali, daktari na kalenda ni kiageni, mnara,bandari,nanga klutoka lugha ya kireno mvinyo,bendera padre parafundu
4.miji ya uswahilini kama vile pate ,lamu na kilwa ilikuwa imestawi kabla ya waarabu kuja pwani. Madai kwamba wageni ndio walikuja na kustawi miji ya uswahilini ni madai ya wazungu kwa kuwa miji hii ilinyakuliwa na waarabu na wageni wengineo nah ii si sababu tosha ya kufanya kubunuwa na wao. Haya ni madai yao tu.
Kulingana na Mbaabu kuna aina tatu za waswahili.
(1)waswahili wenye asili ya kibantu ambao walijulikana kama wangozi na waswahili wamegawanyika katika makabila madogo madogo kwa mfano wabarawa wanaoishi Somali. Nchini Kenya makabila hayo nikama lamu wapate,waunya,wasinyu,wamalindi, wakilifi,wamvita,wamtang`ata,wakiingili,wanjovu na wavanga
Nchini Tanzania kuna weamafia na watumbatu
(2)kuna waswahili waliozaliwa kutokana na ndoa kati ya waarabu na waswahili asili.
(3)kuna waswahili waliotoka katika makabila mengine ya waafrika. Hawa ni watu walioishi na waswahili kwa muda mrefu na kuacha mila zao na kufuata za waswahili. Walijifanya wenyeji wa waswahili  baada ya wenyeji kukutana na kusema kuwa watoe ada iliyoitwa  ada ya mji na wanati. Baadhi yao walikuwa watumwa na wengine waliotoka bara na kuhama.

KISWAHILI NI LUGHA YA KIBANTU
Wafuasi wa nadharia hii ni Greenberg, Mbaabu,Guthrie,Chimera,Chicago na Mnyampala. Hawa wanadai kwamba Kiswahili ni asili ya kibantu kwa hivyo inafanana na lugha nyingine kiganda,kinyamwezi na k
KISWAHILI NI LUGHA YA MSETO
Wafuasi ni pamoja na Taylor Broomfield,  steere Johnson hawa wanadai kwamba Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha za kiafrika na lugha za kigeni,kiarabu,kiajemi,kituni n.k.wametoa ushaidi ufuatao ili kudhibitisha.
(1)Johnson anadai waarabu walipokuja aghalabu hawakuandamana na bibi kutoka uarabuni kwa sababu hiyo kuliwako na uhaba wa wanawake.walianza kufunga ndoa na wanawake wa kibantu. Watoto wao walianza kujifunza maneno ya kiarabu kutoka kwa baba zao na maneno ya kibantu kutoka kwa mama zao kwa hivyo vizazi vilivyofuata vikawa na lugha ya Kiswahili iliyo na mchanganyiko wa lugha mbalimbali. Johnson anadai kwamba maneno ya kiarabu na kiajemi ambao watoto hawa walijifunza kutoka kwa baba zao yalihusu vita,ubaharia,usafiri na vyombo vya ufundi lakini maneno ya kibantu waliyojifunza kutoka kwa mama zao yalihusu kilimo,ufugaji,chakula na maisha ya kila siku.
(2) Broomfield anadai kwamba kulikuwa na haja ya waarabu kuwasiliana na watumwa wa kibantu kwa hivyo iliwabidi kuchanganya maneno ya kibantu na ile ya kiarabu ili waweze kuelewana wakati walipokuwa wakifanya kazi za utumwa.kutokana na mchanganyiko huu lugha ya Kiswahili ikaibuka.

Upungufu wa nadharia
(1)   Kama anvyosema mbaabu (1978) lugha mbili katika ndoa haziwezi kuzaa nyingine kwani lugha hazichanganyikani kama vile watu wa asili wanavyochanganyika.
(2)   Watafiti wa Kiswahili wamedhibitisha kwamba takriban 60% maneno yote ya Kiswahili ni asili ya kibantu, asilimi 30% ni ya asili ya kiarabu na asilimia 10% hutokana na lugha nyingine na mbalimbali za kibantu
(3)   Chimerah 1998 anasema Kiswahili sio lugha ya mseto kwa sababu sarufi haifanani na sarufi ya kiarabu wala lugha zingine za kigeni bali inakaribiana na sarufi zingine za kibantu

ikuyu
Ushaidi
1.ushaidi wa kihistoria
2.ushaidi wa kiisimu

(1)Ushaidi wa kihistoria
Haya ni maandishi ya kale ya Kiswahili.mashairi ya kale yanadhihirisha kwamba lugha ya waarabu kufika pwani mashariki. Mfano wa mashariki ya kale ni kama vile.
(a)   Utenzi wa mwana kupona
Utenzi huu una maneno mengi ya kingozi,mfano wa maneno haya ni kama vile ng`andu-dhahabu na pulika-sikiza
(b)   Utenzi wa taambuka
Uliandikwa katika lahaja za kipate

(c)    Utenzi ya liyongo na takhmisa ya liyonga
(d)   Utenzi wa mwanakupona
(e)   Habari za kiindi

HISTORIA SIMULIZI YA MIJI YA USWAHILINI
Inapatikana katika tarihi ya lamu kiiwa na pate ambazo zilipatikana karne nne zilizopatikana. Historia hii inazungumzia mambo kuhusu waswahili.
(1)   Katika tarihi ya lamu tunaelezewa kwamba makundi matatu yaloyounda koo ya lamu yaliyojulikana kwa majina ya Kiswahili ambayo ni kimanti yumbe mfumao na uungwana.
(2)   Katika tarihi yakiiwa tunaelezwa kwamba sultan wa kwanza wa kiiwa yaani iIbn Hussein alijulikana kama lakabu naye mwanawe aliyekuwa akitawala mji wa mafia alijulikana kama(mkoma watu) kwa vile haya ni maneno ya Kiswahili hii inaonyesha kwamba wenyeji wa mafia walikuwa wakitumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana
(3)   Katika tarihi ya kipate kuna maneno mengi yaliyotumika ambayo ni pamoja na yumbe –ujumbe na dhahabu-ng`andu
1(b) Wasafiri wa zamani
Wasafiri hawa ni  kama vile Al-masud,Al-idris,Ibn-buttata walipotembelea mwambao wa Afrika mashariki waliona na kuandika vitabu vingi sana kuhusu mamboa mbalimbali

Almasud-alipofika Afrika mashariki alisema kuwa aliona nchi ya watu weusi kuanzia Sofala hadi Mogadishu walikuwa na wafalme wao na Mungu waliyemwita Mkungulu. Alielezea kuwa chakula cha watu nao kilikuwa ndizi na mtama. Huenda neon Mkungulu ilibadilika na kuwa Mulungu kasha baadaye ilikuwa Mungu.
Al-indris-aliitembelea mwambao wa Afrika mnamo karne ya kumi na akaandika kitabu kiitwacho River aliitaja miji ya Zanzibar ilikuwa Unguja. Aliandika baadhi ya majina ya mandazi kwa mfano kisukari kikonde mkono wa tembo wa kadhalika.
Ibn batata-alizuru Afrika mashariki. Alisema kwamba aliitembelea nchi ya Swahili alieleza kwamba watu wa Mombasa walikuwa wakinunua nafaka nchi ya Swahili.
Msafiri  mgiriki
Huyu aliandika kitabu chake cha periplus of erythrean sea. Yaani kitabu cha maelezo kuhusu bahari hindi akiandikia mjini Alizandria miaka mia moja iliyopita

Matatizo yanayokumba mtafiti wa Kiswahili anayetegemea ushahidi wa kihistoria
(1)   Kuna uwezekano kuwa mambo  yaliyomulikwa yalisaulika kabla ya kuwekwa kwenye maandishi
(2)   Huenda wasafiri walionakili habari za pwani walieneza uvumi tu kama Yule mgiriki aliyesema kuwa aliandika kitabu chake akiwa huko Alizandria
(3)   Hati za kiarabu zilizotumika kuandika miswada hazikuwa na herufi za Kiswahili hali hii ilitatiza hali ya kutafsiri
(4)   Miswada iliyokuwa na ujumbe muhimu iliibiwa wakati wa vita mengine yakateketea kwa kutumia moto
(5)   Miswada mingine ilifichwa na miji ya uswahilini

Maenezi ya Kiswahili na sera ya lugha kabla ya uhuru
Kiswahili kimevuka mipaka ya kuwa lugha ya kimataifa
Je Kiswahili kilienezwa vipi kutoka bara Kenya Uganda na afrika ya kati  Tanzania
Vyombo vitatu vilichangia maenezi ya lugha ya hii ya Kiswahili. Vilichangia  kukuza na kusambaza Kiswahili kutoka pwani hadi bara
(a)misafara ya waarabu
(b)utawala wa wakoloni
(d)wameshenari na walowezi
Misafara ya waarabu
Kenya
Misafara ya biashara ilikuwa michache kulinganishwa na Tanganyika. Ilianza mwembe Taba,Lamu na malindi ikielekea bara kulingana na whitely misafara ilikuwa michache kwelikweli kwa sababu zifuatazo
(1)Wamaasai  walikuwa wakali kwa vile hawakuruhusu misafara yoyote ipitie katika eneo lao la si hivyo wangeuteka nyara
(2)Baadhi ya makabila kama vile wakikuyu na wanandi hawakuwa na moyo wa kushirikiana na waswahili. Wawanga tu ndio waliowaruhusu kufanya biashara na waswahili.
(3)Vita vya kuvizia vilivyopangwa na Wamazrui ili kupinga utawala wa seyyid said viliadhiri sana misafara hiyo
(4)Hali ya ukame iliyopatikana katika sehemu nyingi za Kenya ilikuwa pingamizi kubwa sana kama vile ukosefu wa maji na chakula
(5)Kisiwa cha unguja kilikuwa kimetawaliwa sana kibiashara ukilinganisha na visiwavya Kenya kama vile lamu
(6)Tishio la wanyama pori kama vile samba hatari na nyoka

Hadhi kuu zilizofanya kieneo na kukuwa barani Afrika
(1)Hati za kiarabu
Waarabu walileta hati  zinazotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu hayo mambo yote yanayohifadhiwa. Ilikuwa ni kwa lugha ya maandishi ni pamoja na fasihi ya waswahili. Kwa hivyo Kiswahili na fasihi ya waswahili. Kwa hivyo Kiswahili kiliweza kukuwa kwa vile kingeweza kuhifadhiwa katika maandishi na kusomwa wakati wowote.
(2)Biashara
Misafara ya wafanyibiashara ilikuwa ikitumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano. Hii ilifanya lugha hii ya Kiswahili kuwabora zaidi na kuenea zaidi. Matumizio ya Kiswahili yalijikita katika maeneo maalum.
(3)Ndoa
Waarabu waliofika pwani walifunga ndoa na wabantu. Hii ilisababisha kizazi kipya kutokea. Hii ni kwa sababu waliyakopa maneno mengi kutoka kwa baba na mama zao kasha lugha ya Kiswahili ikatokea.



(4)Dini ya kiislamu
Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini yao kwa undani kabisa. Kwa hivyo iliwabidi kuanzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia lugha iliyokuwa ikitumiwa ni lugha ya Kiswahili

UTAWALA WA KIKOLONI
Tanganyika(Wajerumani)
Wajerumani walisaidia kukuza Kiswahili kwa njia zifuatazo
(1)Waliwalazimisha wafanyikazi wote wa serikali kujifunza lugha hii ya Kiswahili. Yeyote ambaye hangeweza kukimundu Kiswahili hangeruhusiwa kufanya kazi katika lugha ya Kiswahili hangeruhusiwa kufanya kazi katika serikali ya ujerumani.
(2)Wafanyikazi kama vile makarani walikuwa wakihamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa hivyo ilikuwa ni lazima wajifunze Kiswahili.
(3)Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza lugha hii. Wajerumani walipotoka ujerumani walishauriwa wajifunze lugha hii kabla ya kuhamia TanganyIKA
                                       
walishauriwa kujifunza kiswahili kwao hata kabla ya kuja ya Tanganyika ambapo kiswahili UTAWALA WA KIKOLONI
TANGANYIKA
KIPINDI CHA WAJERUMANI
Watawala wa mwaka wa 1885-1916 walipokuja walikuta kwamba kiswahili kilikuwa kimeene humu nchini kutokana na msafara wa waarabu. Hata  hivyo badala ya kutambua kiswahili lugha ya utawala   . Walitumia  lugha ya kijerumani katika masomohuku wakifunza masomo yote katika shule zote walizoanzisha  lakini  shughuli hizo hazikufua dafu kwa sababu hawakuzigatia kuwa kiswahihili ndio lugha iliyokuwa imeenea tangu wakati huo.

JINSI WAJERUMANI WALISAIDIA KUENEZA NA KUKUZA KISWAHILI
1.Walilazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujivfunza kiswashili kwa sababu pasi jua kiswahilihungeajiriwa katika serekali ya mjerumani
2.Wajerumani walilazimika kujifunza kiswahili  ili waweze kutumika katika utawala huo. Walipotoka  ujerumani kilienea Sana.
3.Watawala wa  wajerumani waliwateua watu wa jumba na diwani katika sehemu mbalimbali  za nchi kuwakilisha wanao jifunza  lugha ya Kiswahili aidha ripoti walitoa kwa viongozi wao wajerumani ziliandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
4.Wafanyikazi kama vile wakalimani walikuwa wakiamishwa kutokka sehemu moja hadi nyingine na katika huamishaji Kiswahili kilitumiwa kwa vile wafanyikazi wangepelekwa sehemu yeyote bila  kujulikana wanafahamu lugha ya  Kiswahili kwa   hivyo wangefanya kazi kama majaji ama kwa ofisi.

          KIPINDI  CHA WAINGEREZA
Waliingia baada ya vita vya kwanza ulimwenguni vilivyotokea 1914-915 waingereza walisaidia kueneza kwa njia tofauti kama:
1.walitumia Kiswahili kufundishia katika shule  za misingi na kiingereza  katika shule za upili na vyuo vikuu  na hii ser
akueneza Kiswahili  hata kwa tabaka la chini.
2.watumishi wote  wa serekali  na madhehebu yote ya kidini  walilazimika kufunza na kutumia Kiswahili  kabla ya kuanza kutumia lugha za makabila tofauti pamoja na biashara na kilimo na uijilisti.
3.lugha ya Kiswahili ilitumiwa mahakamani katika kushughulikia kesi za wafrika iwapo ripoti ziliandikwa kwa kiingereza  na mwishowe kutafusiriwa kwa kiaswahili.
                                         KENYA
Misafara ya biashara ilikuwa michache kulingana Tanganyika lilianza mwembeteare lamu na malindi ikipelekea bara kulingana na Whitely misara ilikuwa michache kwa sababu ya:
1.wamasaiwalikuwa tishio kubwa kwa wafanyibiashaara  kwa kutotakamisafara katika eneo lao na mwishowe waliwadhuru wana biashara.
2.baadhi ya makabila kama vile wakalenjin na wanandi  hawakuwa na moyo wakushirikiana   na waswahili 
3.vita vya kuvizia vilivyopangwa na wamazrui ili kupiga utawala wa Seyyid Said viliadhiri sana pwani ya Mombasa na viongozi wake na kufanya  biashara kuwa hatari    kufanya  na misafara mingi kutoenda bara
4.hal iya ukame  iliyopatikana katika sehemu tofauti ya  Kenya ilikuwa pingamizi kubwa  kwa wasafiri sabau ya ukosefu wa maji na chakula
5.kisiwa cha ugunja kilikuwa kinatumiwa sana na wafanyibiashara kilitenganishwa na visiwa vya Kenya kama lamu na malindi.
6.tishio la wanyama pori  kama vile smba hatari na nyoka

                               NCHI  YA  KENYA
Kusudi la waingereza katika nchi ya Kenya ilikuwa kudidimiza kisu wakitatizamaenezi kwa njia zifuatazo:
1.walitumia kisu kuendesha shughuli za utawala  kama vilekuwekeana mikataba na wenyeji
2.wai ngereza Waliwatawala wenyeji kimabavu huku wakiitumia washauri katika kueneza Kiswahili.
3.katika elimu waingereza walisizitiza matumizi ya kiingereza huku wakipuuza kiswahili sera hii iliimarika zaidi kwa sababu waliofia wangetumia Kiswahili kuwaunganisha dhidi ya wakoloni kwa hivyo waliimiza matumizi ya lugha ya kwanza katika kufunzia shuleni

WAMISHENARI NA WALOWEZI
TANGANYIKA
Walowezi hawakuathiri na kukua kwa Kiswahili nchini Tanganyika kwa sababu walikuwa wachache. Wamishenari walikuwa wengi sana na walichangia kwa njia zifuatozo.
1.baadhi ya wamishenari walifanyia Kiswahili utafiti na kuandika   na vitabu
2.walifungua shule ambsazo zilitoa mafunzo mbalimbalibh kwa wanafunzi  wanchi hiyo 
3.walianzisha vituo ambavyo kueneza kiswahnili hii ni pale ambapo kilitumiwakatika  kutoa mashauri
4.waliweza kutafsiri vitabu  vingi katika lugha ya Kiswahili mfano wa  vitabu hivi ni kama vilebibilia
6.wamishenari waliweza kuchapisha magazeti kwa lugh ya  kiswahil  .magazeti hayani

                 MAREJELEO
    ess TUKI (1990) kamusi sanihfuya isimu and lugha .dar es salaam:TUKI. MULIKA Na.13& Na 20 Dar es  salaam.      Weber, H .(1985) A dictionary  of phonetics and linguistics .Harlow longman
     Saussure,F. (1916) Course in general linguistics.New york: macGraw-Hill
     Sapir,E.(1921) LANGUAGE .New   york : Harcourt brace
     Steere ,E.(1950) Ahardbook for swahili  language. London : The sheldon press .
     Kapinga, C (1983) sarufi Maumbo ya kiswahili sanifu .Dar es salaam :TUKI
     Hartman, R. (1972) .Dictionary of language and linguistics .London: Applied science publisher
     Bloomfield, (1933) language.New york:Harit Rinehart.
      Mdee,j .(1967) kiswahili: muundo na matumizi yake.Nairobi: intercontinental publishers ltd.
     Mgullu, RS (1988) "Uhakiki wa makala ya Dhana za Mofu,alomofu na mofimu "katika mulika na 20 .dar  es salaam.
     Martinet,A (1973) morphonemics .New york.
     Aitchison ,j.(1981) language change, progress or decay. London:Fontana paperbacks.
     Ashton, (1947) swahili grammar .London:Longman.
     Crystal ,C.( 1971) Linguistics.Middlesex:Penguin.
     Abercrombie,D.(1965) studies in phonetics and linguistics.London:oxford university pr
Powered by Blogger.