AINA ZA USHAIRI (BAHARI)
AINA ZA USHAIRI (BAHARI)
Bahari;
hii
ni aina mahususi ya ushairi yenye sifa
fulani kiumbo na pengine hata kimaudhui na kimatumizi na zinazoipambanua na
aina nyingine ya ushairi.
S.A Kibao (2003)
anasema, ushairi wa Kiswahili umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo
ni: shairi, utenzi na ngonjeara. Anaendelea kusema, aina zote hizi kanuni zake
ni za pamoja isipokuwa utenzi ambao una mpangilio wa namna ya pekee.
S. Robert na Amri Abeid (1954) wanasema zipo bahari tatu tu za ushairi nazo
ni:wimbo, shairi na utenzi.
A.S. Nabhany na wenzake wameainisha bahari 13 za
ushairi na kusema kuwa utungo wowote lazima uingie katika bahari mojawapo.
Bahari hizo ni hizi zifuatazo:
1.
Ushairi;
Ni utenzi wenye mishororo minne na vipande
viwili kila msitari. Kila mstari una mizani 16 na kila kipande kina
mizani 8. Maudhui yake yanatokana na jambo lolote lile analoliona mtunzi.
2.
Wimbo;
Ni
utungo wenye mishororo mitatu kila ubeti na kila mshororo una vipande viwili.
Nyimbo nyingi huongelea mapenzi.
3.
Tenzi;
Ni
utungo wenye vipande vine katika kila ubeti na vina hubadilika kila ubeti
isipokuwa kipande cha mwisho. Tenzi nyingi zina mizani nane kila mshororo na
nyingine zina mizani 11 na zingine 10.
4.
Inkshafi/Duramandhuma;
Imepata
jina lake kutokana na utenzi wa Aliinkshafi. Tenzi hizi zina maadili ya kidini
japokuwa maudhui yake yanaweza kutumika katika maadili ya kidunia. Kila ubeti
una mishororo minne na kila mshororo una mizani 11.
5.
Ukawafi;
Hili ni shairi lenye mishororo mitatu au zaidi katika kila ubeti na vipande
vitatu katika kila mshororo. Mizani zinaweza zikatofautiana au zikawa sawa.
6.
Wajiwaji/Takhimisa;
Una
mishororo mitano kila ubeti na mizanai 15 kila mshororo na vipande vitatu
katika kila mshororo vina muundo wa mizani 6, 4, 5. Maudhui yake ni ya kidini
au kiamisha kwa ujumla, mfano Takhimisa ya Liongo na tenzi ya Inkshafi.
7.
Hamziya;
lipata
jina lake kutokana na kaswida ya Hamziya ambao ni utenzi wa kiarabu. Mishororo
ya Hamziya ina vipande 3 vya mizani 5, 4, 6
8.
Tiyani-Fatiha;
Ni ushairi wa kidini wa
kuomba toba, una mishororo 9 kila ubeti ambayo huweza kutofautiana kwa
urefu/mizani.
9.
Utumbuizo;
Haina
idadi kamili ya mishororo na mizani, urefu wa mstari au mshororo hutegemea
pumzi aliyonayo mwimbaji na lengo lake; mfano ni nyimbo za Liyongo kuna
tumbuizo.
10. Wawe; Ni
ushairi au wimbo wa kilimo, huimbwa wakati wa kulima au kupanda.
11. Kimai; Inahusu
shughuli za majini, ni bahari ya wavuvi na mabaharia. Idadi ya mishororo na
vina si lazima.
12. Zivindo; Ni
ushairi unaofafanua maana za maneno; na kazi yake ni kujifunza lugha na
mkuhifadhi lugha.
Mfano: Kata ni kata ya nyoka
Au kata ya nyweleni
Kata ya tweka, bandikwayo kichwani
Au kata ya nyweleni
Kata ya tweka, bandikwayo kichwani
13. Sama; Neno
‘sama’ ni mahadhi au sauti, hivyo bahari hii hukusanya washairi wote wenye
kufuata mahadhi ya kigeni.