MABADILIKO YA SAUTI KATIKA KUTAMKA

 
ISIMU
  MABADILIKO YA SAUTI KATIKA KUTAMKA.

KUNA MABADILIKO FULANI KATIKA SAUTI ZA KUTAMKWA ZA BINADAMU. SAUTI HIZO HUWEZI KUZIONA KAMA HAUJAZICHUNGUZA VIZURI. JIULIZE KWANINI NENO KAMA JENGA, TUKITAKA KUMTAJA MTENDA JAMBO HATUSEMI MJENGI? AU NENO IBA KWANINI HUGEUKA KWA MWIZI? YAANI SAUTI /B/ IMEGKA KUWA /Z/. Basi kwa Kwa kutumia data ifuatayo tutabainisha mabadiliko ya sauti yanayotokea na kwa njia hiyo basi tunaweza kusema kuwa mabadiliko hayo hutokana na mabadilliko flani flani yaliyosababishwa na mazingira ya kifonoloji, kimofolojia na kimofofonolojia. Ili kuelezea vizuri mabadiliko haya hatuna budi kutumia mifano kadha wa kadha kutoka katika hii.
Data.
Iba
Wizi
Cheka
Mcheshi
Mguu
Miguu
Nkindiza
Nkindiza
Mkuki
Mkuki
Mvuvi
Mvuvi
Ulimi
Ndimi
Katika kujibu swali hili tumeligawanya katika sehemu tatu. Katika sehemu ya kwanza tumetolea maana ya istilahi mbalimbali kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali. Istilahi hizo ni pamoja na maana ya fonolojia, mofolojia na mofofonolojia, sehemu ya pili tumejadili kiini cha swali ambapo tumeonesha mazingira mbalimbali ya utokeaji wa data tulizopewa na suluhisho la wanamofofonolojia katika kutatua matatizo ya kimofofonolojia na sehemu ya  tumehitimisha kazi na kutoa marejeo. Kwa kuanza na maana ya istilahi hizo watalaamu wanatueleza kama ifuatavyo;
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia kama tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Hii ina maana kwamba fonolojia kama tawi la isimu hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia ni utanzu wa isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mbalimbali. Fonolojia huchunguza jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana.
Hivyo kutokana na maana za wataalamu hawa tuanaweza kueleza kuwa; fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa sauti katika lugha mahususi. Mfano Kiswahili, Kiingereza Kichina, Kijerumani na Kihaya.
Baada ya kueleza maana ya fonolojia tuanagalie maana ya mofolojia kulingana na wanataalamu mbalimbali.
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa maneno katika lugha.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanatueleza kuwa; mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa maneno. Fasili hii inamapungufu kwani katika mofolojia hatushughulikii miundo ya maneno katika lugha bali kinachoshughulikiwa ni maumbo ya maneno. Miundo ya maneno katika taaluma ya isimu inashughulikiwa na tawi na sintaksia.
Kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kueleza kuwa; mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa maumbo ya maneno katika lugha. Baada ya kuangalia maana ya fonolojia na mofolojia ifuatayo ni maana ya mofofonolojia;
Massamba (2010) akimnukuu Martinet (1965) ambapo Martinet alinukuu kutoka kwa Trubetzkoy (1929) anatueleza kuwa; mofofonolojia kama ilivyotumiwa na Trubetzkoy ilimanisha sehemu ya isimu ambayo ingeweza kutumia mofolojia kuelezea tofauti fulani za kifonolojia ambazo zisingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia maana za istilahi mbalimbali zilizotumika katika swali hili, kifuatacho ni kiini cha swali kinachoonesha mabadiliko ya sauti yaliyotokea katika data tuliyopewa ambayo ni mabadiliko kifonolojia  pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia.
Tukianza na mabadiliko ya kifonolojia pekee, haya hutokea kwa namna tofauti au katika mazingira tofauti. Kwa mfano mazingira hayo ni; udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuadhiri konsonanti na konsonanti kuathiri nazali.
Hivyo kutokana na data yetu katika kubainisha mazingira ya mabadiliko ya sauti  kifonolojia pekee ni kama ifuatavyo;
                                        Mvuvi     /ɱvuvi/
Badiliko lililotokea hapa ni la kifolojia katika mchakato wa usilimishaji wa nazali yaani konsonanti kuathiri nazali. Hapa tunaona kuwa sauti ya midomo /m/ imesilimishwa na kubadili sehemu yake ya kutamkia na kuchukua sifa ya midomomeno /ɱ/ baada ya kukabiliana na sauti ya midomomeno /v/. Hivyo sauti /m/ imebadilika na kuwa /ɱ/.
Katika mabadiliko ya sauti ya sauti ya kitambaza /l/ kubadilika na kuwa kipasuo /d/ pia ni mabadiliko ya kifonolojia hii ni katika neno;
Nlimi       huwa              /ndimi/
Utokeaji wake  ni kutokana na kanuni ya nazali kuathiri konsonanti. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti / l / inapokabiliana na nazali / n / yenye sifa ya kutamkiwa sehemu moja yaani kwenye ufizi hubadilika na kuwa / d /.
Pia mabadiliko nazali /n/            kipasuo cha kaa laini /ŋ/ ni ya kifonolojia ambayo utokeaji wake ni wakiusilimishaji au kanuni ya konsonanti kuathiri nazali. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti ya nazali kuathiriwa na konsonanti inayoiandamia hivyo kuifanya nazali kuifuata konsonanti mahali pa kutamkia. Mabadiliko hayo yameathiri sauti ya nazali /n/ na kutamkwa kama nazali ya  kaa laini /ŋ/. Hivyo katika uwakilishi litakuwa;
Umbo la ndani /ŋkindiza/
Umbo la nje  nkindiza.
Baada ya kueleza mabadiliko ya kifonolojia, tutazame mabadiliko ya kimofolojia. Kutokana na data hii tunapata maumbo kama;
Mguu                mi-guu
Haya ni mabadiliko ya kimofolajia. Mazingira ya utokeaji wake ni mabadiliko ya uongezaji au upachikaji wa  mofimu ya umoja na wingi ambapo; mofimu m- ya umoja imebadilika na kuwa mofimu mi- katika wingi.
 M-guu        umbo la umoja
Mi-guu     umbo la wingi.
Pia katika neno mkuki          mkuki mabadiliko yaliyotokea ni ya kimofolojia tu kwani hakuna mabadiko ya umbo na kinachoonekana ni uwepo wa mofimu m- ya umoja katika umbo hili pamoja na mzizi -kuki. hivyo kilichofanyika ni kuongeza -kuki katika mofimu hiyo ya umoja na kupata neno m-kuki. Hivyo umbo hili linabakia na umbo lake ambalo hubakia kuwa vilevile.
M-kuki      m-kuki maumbo yote haya yako katika umoja                       
Vilevile katika neno M-dalasini          m-dalasini hakuna mabadiliko ya kimofolojia bali umbo limeendelea kuwa vilevile la umoja.
Baada ya kuangalia mabadiliko ya kifonolojia na kimofolojia katika data tulitopewa, kipengele kinachofuatia ni kubainisha mabadiliko ya sauti yaliyotokea kwa mabadiliko ya kimofofonolojia.
Kutokana na data yetu maneno;
Iba                kuwa                mwizi
                        Cheka      kuwa                     mcheshi
Haya ni mabadiliko ya kimofofonolojia. Sababu ya kuwepo kwa  mchakato huu ni uwepo wa mbadilishano wa sauti ambayo hayakuweza kufafanuliwa kwa utaratibu wa fonolojia pekee na utaratibu wa mofolojia pekee hivyo kukawa na hitaji kubwa kuwa na kiwango kingine cha kuweza kutatua changamoto hiyo. Kwa hiyo kuibuka kwa mofofonolojia kulikuwa na lengo la kumaliza changamoto hiyo iliyokuwepo.
 Hivyo katika mabadiliko iba    kuwa          mwizi, sauti ya kipasuo cha midomo /b/ kubadilika kuwa sauti ya kikwamizi cha ufizi /z/ imesababishwa na kuwepo kwa irabu /i/ ya unominishaji mwishoni mwa sauti /b/. kutokana na kitendo cha kuiba tunapata nomino “mwibi” kutokana na mofimu mu-ib-i hapa konsonanti ya kipasuo cha midomo /b/ hudhoofika na kuwa konsonanti ya kikwamizi cha ufizi /z/ katika mazingira ya kutanguliwa na irabu ya unominishaji /i/.
                     iba    /wizi/
Pia katika neno cheka  kuwa   mcheshi mabadiliko yaliyotokea hapa ni ya kimofofonolojia ambapo sauti ya kipasuo cha kaakaa laini /k/ inabadilika na kuwa suati ya kikwamizi cha kaka gumu /∫/ baada ya kufuatiwa na irabu ya unominishaji /i/.
                           Cheka   kuwa         /mče∫i/
Uwepo wa mabadiliko sauti na umbo ambayo hayawezi kuelezwa, kwa mchakato wa fonolojia na  mchakato wa kimofolojia ndipo palipoibuka mchakato wa kimofofonolojia.
Katika utatuzi wao wanamofofonolojia walikuja na dhana ya umbo kiini. Umbo kiini hili liliwakilisha fonimu mbili. Waliteua umbo kiini kwenye neno la msingi. Na liliwekewa mabano mchirizi { }.
Kwa mfano katika   cheka      kuwa            mcheshi
  Neno la msingi ni “cheka” ambapo waliteua sauti {K} kuwa umbo kiini. Fonimu {K} iliteuliwa kuwakilisha /k/ yenyewe katika neno cheka ambalo ni kitenzi na inawakilisha sauti  /∫ /  kwenye “mcheshi” ambayo ni nomino.
                                                                                           /k/
                                                                      {K}
                                                                                           /∫/
Umbokiini   {K}   linawakilisha sauti  /k/ na /∫/
Pia katika neno iba na wizi umbokiini ambalo liliteuliwa ni {B} ambayo kuwakilisha sauti /b/ na sauti sauti /z/.
                                                                                              /b/
                                                                        {B}
                                                                                           /z/
Baada ya utatuzi huu baadhi ya wataalamu  walitoa maoni yao juu ya umbokiini. Baadhi yao ni Linhtner (1970) akinukuliwa na Massamba (2010) anaeleza kuwa umbo kiini sio halisi ni la kidhahania na kinasibu kwani halioneshi mchakato na namna ambavyo sauti na umbo hubadilika na kuwa katika sauti nyingine na kitu gani hasa husababisha mabadiliko hayo ya sauti. Umbokiini huishia tu katika kuteua sauti moja kuwakilisha sauti nyingine. Basi huo ukawa udhaifu wa dhana ya umbokiini.
Hitimisho kutokanana wanamofofonolojia kushindwa kutatua matatizo ya kifonolojia. Hivyo wakaibuka wanafonolojia zalishi ambao waliokuja na mitazamo mipya katika utatuzi wa matatizo ambayo yalishindwa kutatuliwa na wanamofofonolojia ambapo walikuja na misingi mipya na mihimili ya kufuata ili kubainisha mabadiliko yaliyokuwa yanatokea yaliyoshindwa kuelezeka.
 Marejeo.
Habwe, J. na P, Karanja (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers
                                              Ltd.
Massamba, D.P.B. na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondari
                                              na Vyuo. Dar es Salaam. TUKI.
Massamba, D.P.B. (2010) Phonological Theory: History and Development. Dar es Salaam:
                                             TUKI.


Sarufi ni nini? sarufi mapokeo ni nini?
 Kuna wataalamu waliowahi kuzungumzia kuhusu sarufi mapokeo na kuchangia kukua na kueleweka kwake. Hawa ni baadhi ya wanazuoni kumi waliotoa michango yao katika maendeleo ya sarufi ulimwenguni lakini kabla ya kuonesha michango yao lazima tujue maana ya sarufi pamoja na sarufi mapokeo.
Dhana ya sarufi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake, wataalamu hao waliofasili dhana hii ni kama wafuatao.
TUKI (2004) sarufi ni kanuni za lugha zinazotumika ili kupata ufasaha wa usanifu katika lugha.
Massamba (2004) sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na uchanganuzi wa kanuni za vipengele mbalimbali vya lugha.
Massamba na wenzake (1999) sarufi kanuni, sheria au taratibu zinazotawala  kila kimoja kati ya viwango vinne vya lugha ambavyo ni umbosauti (fonolojia), umbo neno (Mofolojia), Miundo maneno (Sintaksia) na umbo maana(Semantiki).
Katika fasili za wataalamu hawa kila mmoja amejaribu kugusa baadhi ya vipengele katika fasili zao, vipengele hivyo ni kama vile kanuni na vipengele vya lugha. Hivyo tunaweza kufasili sarufi kuwa ni kanuni, sheria na taratibu zinazotawala lugha katika viwango vyote vya lugha.
Khamisi na Kiango (2002) wanasema kuwa sarufi mapokeo  ni sarufi ya kale ambayo ilijitokeza kuanzia karne ya 5KK, ambayo ilionekana kutokuwa na msimamo wakisayansi katika kuelezea lugha bali zilikuwa na mwelekeo wa kifalsafa.
Massamba na wenzake (1999) wanafafanua kuwa sarufi mapokeo ni sarufi elekeziilisisitiza usahihi wa lugha kwa kuonyesha sheria ambazo hazina budi kufuatwa, mathalani, kufanya muundo fulani wa sentensi usemekane kuwa sahihi, au sheria ambazo hazina budi kufuatwa  ili kufanya matamshi ya neno fulani yakubalike kuwa ndio sahihi.sarufi hizo za kimapokeo zilikuwa zikisisitiza jinsi ambavyo lugha haikupaswa kuwa kwa mfano sarufi mapokeo ingekubali sentensi (a) mpaka (c) na kuzikataa (d) mpaka (f).
(a)    Kalamu hii ni yangu
(b)   Kiti hiki ni chetu
(c)    Mtoto huyu ni wenu
(d)   Kalamu hii ni ya mimi
(e)    Kiti hiki ni cha sisi
                         (f)    Mtoto huyu ni wa nyinyi
Pia wanasarufi mapokeo waliamini kuwa lugha ya Kilatini ilikuwa ni bora kwa kuwa lugha hii  ilikuwa imeenea zaidi, waandishi wengi walichukulia moja kwa moja kwamba taratibu zilizokuwa zikitumika katika kuainisha au kuchambua sarufi za lugha hiyo ambazo ndizo zilizokuwa sawa na ndizo zilizostahili kutumiwa katika uchambuzi na uainishaji wa lugha yeyote duniani. Hiyo ndiyo sababu sarufi za lugha nyingine zilizoandikwa hapo zamani zilifuata taratibu na muundo wa sarufi ya Kilatini. Kwa mfano umoja na wingi, kwa kuwa lugha ya kilatini zilikuwa na nomino za umoja na wingi, hivyo basi waliamini kuwa nomino za lugha zote duniani zilikuwa na maumbo ya umoja na wingi.
Sarufi ya kimapokeo ni sarufi kama ilivyokuwa ikichambuliwa kwa kutumia mtazamo na mbinu za kimapokeo, ikitazamwa katika mwelekeo wa kimapokeo, sarufi hii ni taaluma ambayo imekuwepo kwa muda wa karne nyingi na kuelezwa na wataalamu mbalimbali wa kale kama wafuatao;
Panin,huyu ni mwanasarufi mapokeo ambaye anakumbukwa kwa kuainisha sauti za lugha ya kisansikriti katika karne ya 5, alizigawa sauti hizo katika  vokali na konsonanti na neno kama vile majina na vitenzi. Utafiti huu ulifanywa huko india ya kale katika karne ya 5.
Kimsingi panin alichangia sana katika maendeleo ya sarufi ulimwenguni kwani kategoria za maneno ambazo aliziainisha kama vilemajina na vitenzi bado zinatumika katika lugha nyingi duniani ikiwemo Kiswahili,
Plato, aliigawa sentensi katika makundi mawili makuu, makundi hayo ni nomino na tendo. Yeye aliamini nomino ni maneno yaliyoweza kufanya kazi ya kiima na tendo ni maneno yenye kueleza  matendo au sifa za kiima.
Mfano;            (a)Alinunua saa
(b)Alikimbia sana.
Makundi haya aliyaita kiarifu.katika falsafa sentensi iliundwa na Kiima na Kiarifu. Sentensi haikuwa kamili kama haikudhihilisha vitu hivyo yaani kiima na kiarifu.mchango wake mkubwa katika dunia yetu ya lugha, maelezo ya sentensi yalitakiwa yaoneshe ukweli wa falsafa ya Kiima na Kiarifu, hivyo sentensi ilitawaliwa na kanuni hii,
                        S    =   KM            +         KF
Ukweli huu haukuwa na mashiko zaidi kwani lugha mara nyingi zilionyesha sulubu tofautitofauti za kuifanya kanuni isifanye kazi. Pamoja na udhaifu huu Plato amechangia sana katika dhana ya kiima na kiarifu katika lugha nyingi duniani mfano Kiswahili;
                        (a)Mama anapika ugali
                        (b)Mama analima shamba
Katika mifano hii Baba na Mama ni kiima na sehemu ya sentensi anapika ugali na analima shamba ni kiarifu.
Donates, huyu ni mwanasarufi mapokeo wa karne ya 4, ambaye aligundua mambo mawili ambayo ni tofauti kati ya nomino na kivumishi. Pia aliangalia upatanisho, utawala na mrejeo sawa katika sarufi, kabla ya hapo aliandika sarufi elekezi na pia aliandika sarufi ya jumla ambayo ilikuwa na mantiki ya lugha zote duniani.
Protagoras nae alitoa mchango wake katika sarufi mapokeo kwa kutumia kigezo cha maana. Aliainisha aina tatu za sentensi ambazo ni swali, maelezo na amri.
Mfano ;        (a) Mwalimu amekuja?  (swali)
                        (b) Mwalimu anfundisha vizuri (maelezo)
                        (c) Njoo hapa mara moja (amri)
Udhaifu wake ni kwamba anaainisha sentensi kwa kuzingatia kigezo cha maana bila kuzingatia vigezo vingine kama vile muundo ambapo tunaweza kupata sentensi sahili, changamano na ambatano.
Licha ya udhaifu wake dhana yake ya kuainisha sentensi kwa kigezo cha maana bado inatumika katika lugha mbalimbali kama vile;
kiingereza.
Mfano (a) What is he doing? (swali)
              (b) Mariam is reading (maelezo)
               (c) Come here (amri)
Kiswahili
Mfano    (a) Mtoto amekula? (swali)
                 (b) Mama ameenda sokoni (maelezo)
                 (c) Kimbia (amri)
Aristotle, pia alichangia kwa kuongeza aina ya maneno ambayo ni kiungo na  njeo. Aliainisha Kiungo kuwa ni neno lolote ambalo sio Nomino wala Tendo. Akaongezea njeo kwa kuzingatia kuwa zilibadili umbile na kitenzi cha kigiriki. Katika uwanja wa kitenzi alitofautisha mtenda na kitenzi  na kutofautisha sentensi na vitenzi hivyohivyo. Pamoja na uainishaji huu aliainisha aina mbili za vitenzi ambavyo ni kitenzi elekezi na si elekezi.
Udhaifu wake ni kuwa aliainisha njeo kwa kuzingatia lugha ya kigirikibila kuangalia lugha zingine duniani mfano lugha za kibantu na lugha za kihindi.
Mchango wake mkubwa katika sarufi ya leo dhana za njeo na kiungo bado zinatumika. Mfano katika kiswahili, kiungo ni kiunganishi ambacho kinaunganisha neno na neno, mfano baba na mama, na njeo ni dhana inayoonyesha wakati katika tungo.
Mfano;   -Mama anapika (wakati ujao)
               -Mvua itanyesha (wakati ujao)
               -Mwalimu alikuja (wakati uliopita)
Mifano hii inapatikana katika lugha ya kiswahili, pia dhana ya uelekezi na si elekezi hujitokeza katika sarufi ya kiswahili.
Mfano; juma amelala (si elekezi) kwa sababu kitenzi hiki hakihitaji maelezo zaidi.
                Mtoto amelalia (elekezi) kwa sababu kitenzi hiki kinahitaji maelezo zaidi ili msikilizaji apate maana iliyokusudiwa.  
Dionysius Thrax, alitenga aina nane za maneno katika lugha ya kigiriki, maneno hayo ni kama vile nomino,kitenzi, faridi peke, kielezi, kiungo,kibainishi, kihusishi, na kibadala.aliona kuwa neno ndio mwanzo na maelezo ya kisarufi na sentensi kuwa ndio kikomo cha maelezo ya sarufi. Pia aliipa sentensi maumbo mawili, umbo la ndani na umbo la nje. Kwake umbo la ndani ndio lenye kufafanua maana ya sentensi na umbo la nje linatokana na mageuzo ya umbo la ndani.
Udhaifu wake ni kuwa hakuangalia kategoria ya kivumishi katika uainishaji wake ambapo lugha nyingi duniani zina aina hii ya maneno.
Licha ya udhaifu huu lakini kimsingi aina hizi alizoziainisha zinatumika katika lugha nyingi dunianiikiwemo lugha ya kiswahili. Pia dhana ya umbo la nje na la ndani linajitokeza katika lugha ya kiswahili.
            Mfano; Juma amempiga mtoto (umbo la nje)
                          Mtoto amepigwa na Juma (umbo la ndani)
Apollonius,mtaalamu huyu anaelezea uhusiano kati ya nomino, hasa kati ya kitenzi na nomino na kati ya maneno haya na maneno mengine ambapo lugha nyingi duniani zinaangalia mahusiano ya karibu ya dhana hizi mbili yaani nomino na kitenzi.
Udhaifu wa hoja za mtaalamu huu ni kuwa alijikita zaidi katika kuangalia uhusiano kati ya kitenzi na nomino bila kutilia maanani uhusiano baina ya maneno mengine mfano kivumishi na kielezi.
Licha ya udhaifu wake kimsingi maelezo yake ya uhusiano yalijenga misingi ya ufafanuzi na maana ya miundo ya lugha.
Varro, ni mmoja ya wanasarufi mashuhuri kabisa wa wakati huo. Anasifika kwa kutenga viambishi na minyumbuliko katika maumbo ya maneno.
Udhaifu wake ni kwamba alijikita sana katika minyumbuliko zaidi kuliko dhana nyingine kama vile uambatizi.
Ubora wake ni kuwa dhana ya viambishi na mnyumbuliko bado zinatumika katika sarufi ya kiswahili.
Mfano; M-toto a-na-pik-a (viambishi)
               Pika, pikia, pikika (mnyambuliko)
Priscian,ni mtaalamu aliyekuwa mashuhuri kuliko wote, yeye alitunga vitabu kumi na nane. Alitafriri msamiati wa sarufi ya kigiriki na kuitumia kuelezea lugha ya kilatini. Pia alitoa maelezo ya kutosheleza na yenye nidhamu kuhusu maumbo.
Udhaifu wa mtaalamu huyu ni kuwa alijikita zaidi katika kutafsiri msamiati wa kigiriki kwenda lugha ya kilatini bila kuangalia lugha nyingine duniani.
Ubora wake ni kwamba kutokana na kuandika vitabu kumi na nane ilisaidia kutoa mwanga kwa waandishi wachanga waliokuwa wakiibuka kwa wakati huo na kupelekea mapinduzi katika sarufi mapokeo na kuibuka kwa sarufi mambo leo.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa licha ya sarufi mapokeo kuwa na mapungufu lakini sarufi hii ndio chemuchemu na chachu ya kuibuka kwa sarufi elekezi na fafanuzi ambayo ilifanya wataalamu mbalimbali kujikita katika uwanja huu wa sarufi.
Marejeo
Khamis M.A na Kiango G.J(2002)Uchanganuzi wa sarufi ya Kiswahili.TUKU Dae es salaam
Massamba D.P.B na wenzake (1999) sarufi miundo ya Kiswahili sanifu: sekondari na vyuo. TUKI.
                                                Dar es salaam.
 Massamba D,PB (2004) kamusi ya isimu na falsafa ya lugha. TUKI. Dar es salaam



ASILI YA MSAMIATI WA KISWAHILI.

Kuna madai mengi kuhusu msamiati unaopatikana katika lugha ya Kiswahili. Kuna madai kuwa unatokana na lugha ya Kiarabu, wengine lugha za Kibantu nakadharika. Sasa tuone asili ya msamiati huu ni wapi?
Mjadala kuhusu asili ya Kiswahili umejadiliwa na wataalam mbalimbali na wametumia vigezo mbalimbali kuthibitisha madai yao. Wapo wanaodai kuwa Kiswahili ni kiarabu, wanaoshadidia dai hili, kigezo kimojawapo wanchokitumia ni kigezo cha msamiati, kwamba lugha ya Kiswahili ina msamiati mwingi wa kiarabu na kwa hiyo kwakuwa Kiswahili kina msamiati mwingi wa kiarabu basi pia Kiswahili ni kiarabu, kwa kweli dai hili halina mashiko. Kabla hatujaanza kufafanua kwamba kwa nini dai hili halina mashiko  ni vema tukaangalia fasili ya dhana muhimu kama zinavyojitokeza katika swali la mjadala. Dhana hizo ni kama zifuatazo:
‘Istilahi asili,’ kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) asili ni jinsi  kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza.  Fasili hii ni nzuri na inajitosheleza kwa maana kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa.
Msamiati kwa mujibu wa TUKI (2004) ni jumla ya maneno katika lugha. Fasili hii iko wazi kwamba jumla ya maneno yote katika lugha ndio huunda msamiati wa lugha husika.
Wataalam wanaodai kuwa Kiswahili ni kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati, hoja zao ni kama zifuatazo:
Khalid (2005) anasema kuwa neno lenyewe Kiswahili limetokana na neno la kiarabu sahil katika umoja ambalo wingi wake  ni sawahili likiwa na maana ya pwani au upwa. Hivyo kutoka na  jina la lugha hii ya Kiswahili kuwa na asili ya neno la kiarabu sahil hivyo hudai kuwa Kiswahili ni kiarabu.
Khalid anaendelea kusema kuwa Kiswahili kina msamiati mwingi wenye asili ya kiarabu. Hapa ni baadhi ya mifano ya msamiati wa Kiswahili wenye asili ya kiarabu kama alivyobainisha Khalid:
Maneno yanayoonesha muda.
Asubuhi                         dakika 
Wakati                            alfajiri
Karne                              alasiri
Magharibi                       saa
Maneno yanayowakilisha namba.
Nusu                             robo
Sita                               saba
Tisa                              ishirini
Thelathini                     arubaini         
Hamsini                        sitini
Sabini                           themanini
Tisini                            mia
Elfu
Mtandao wa jamiiforum pia wameonesha  mifano ya msamiati wa Kiswahili wenye asili ya kiarabu kama ifuatavyo:
Kiswahili                            Kiarabu
Dirisha                                drisha
Karatasi                              kartasi
Debe                                   dabba
Samaki                                samak
Mustakabali                        mustakabal
Madrasa                               madrasa
Lodh (2000:97) naye anasema kiasi kikubwa cha nomino za Kiswahili zimetokana na mizizi ya maneno ya kiarabu. Mifano ya maneno hayo ni kama yafuatayo:
Hesabu/hisabu     mahisabu/hisabati
Harka                   harakati
Safiri        -           msafiri
Safari   -               msafara
Fikiri    -              fikara/fikra
Hata hivyo kigezo hiki cha msamiati kina udhaifu; Massamba (2002) ameonesha udhaifu wa kigezo hiki kuwa ni pamoja na kwamba:
Hakuna ushahidi wowote wa kitakwimu ambao unaonesha idadi ya maneno ya kiarabu  yaliyopo katika lugha ya Kiswahili yanayoweza kuhitimisha kuwa Kiswahili ni kiarabu.
Kigezo cha msamiati peke yake hakijitoshelezi kuelezea kuwa Kiswahili ni kiarabu, walipaswa waangalie vigezo vingine kama vile kigezo cha kihistoria kwa kuchunguza masimulizi mbalimbali ya kale na kigezo cha kiisimu; katika kigezo hiki walipaswa kuchunguza fonolojia, mofolojia , na sintaksia ya Kiswahili kwa kulinganisha na kiarabu na ndipo wangepata hitimisho sahihi la madai yao.
Vilevile kigezo hiki cha msamiati hakina mashiko kwa sababu lugha ina tabia ya kuathiriana, lugha huathiriana na lugha nyingine endapo kutakuwa na mwingiliano baina ya wanajamii lugha hizo.  Kwa mfano Kiswahili kimetokea kuathiriana na kiarabu kutokana na uhusiano uliokuwepo hapo zamani katika biashara kati ya waarabu na watu wa upwa wa Afrika Mashariki na hii ikapelekea msamiatia wa kiarabu kuingia katika lugha ya Kiswahili, hivyo kwa hoja hii hatuwezi kusema Kiswahili ni kiarabu kwa sababu msamiati wa kiarabu unaonekana katika lugha ya Kiswahili.
Hata hivyo si lugha ya kiarabu tu ambayo msamiati wake unaonekana katika lugha ya Kiswahili vilevile kunamsamiati wa lugha zingine za kigeni katika lugha ya Kiswahili kwa mfano, neno lenye asili ya kireno katika Kiswahili ni kama vile meza, leso pia yapo maneno yenye asili ya kijerumani kwa mfano schule kwa Kiswahili shule na maneno yenye asli ya kiingereza ni kama vile mashine, televisheni, sekondari, redio, kompyuta na maneno mengine yenye asli hiyo. Basi ingekuwa msamiati wa kigeni kuonekane kwenye lugha fulani huifanya hiyo lugha kuwa na asili ya lugha ya kigeni basi tungesema pia Kiswahili ni kiingereza  kwa sababu tu msamiati mwingi wa kiingereza unonekana katika Kiswahili.
Pia kigezo hiki kinaonekana kuwa ni dhaifu kwa sababu hawakufanya utafiti katika nyanja zote za matumizi ya lugha kwa mfano msamiti unaotumika katika nyanja ya elimu, afya, utamaduni na kadhalika. Kwa hiyo madai haya yanaonekana kutokuwa na mashiko kwa ufinyu wa utafiti wake.
Kutoka na kigezo hiki cha msamiati kutokuwa na mashiko kuhitimisha kuwa Kiswahili ni kiarabu, basi hatuna budi kusema kuwa Kiswahili sio kiarabu bali ni kibantu. Katika kuthibitisha madai haya tutajikita zaidi katika kigezo cha kiisimu ambacho tunaamini kuwa ni kigezo pekee kinachoweza kutupatia taarifa sahihi kwani ni kigezo cha kisayansi lakini pia tutaangalia kwa ufupi vigezo ambavyo vinatoa ushahidi juu ya ubantu wa Kiswahili ambavyo ni ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.  
Kigezo hiki cha kiisimu kimetumiwa na wataalam mbalimbali katika kuonesha ubantu wa Kiswahili Massamba (ameshatajwa) amewataja wataalam mbalimbali ambao wamehusika na utafiti juu ya ubantu wa Kiswahili, wataalam hao ni pamoja na Carl Meinhof katika kitabu chake cha Introduction to the phonology of the Bantu language,  Duke (1935 – 1945), Malcom Guthrie (1967), Dereck Nurse na Thomas Spear (1985). Hawa walijadili ubantu wa Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kiisimu, kihistoria na kiakiolojia.
Kwa kuanza na  kigezo cha kiisimu tutaangalia vipengele kama vile kufanana kwa msamiati wa msingi, muundo wa kifonolojia, muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia mpangilio wa ngeli za majina.
Mizizi ya msamiati wa msingi wa lugha za kibantu na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa, mifano ifuatayo huweza kuonesha ukweli huu.
Mfano,
Kiswahili
Kikurya
Kinyiha
Kijita
Maji
Amanche
Aminzi
Amanji
Jicho
Iriso
Iryinso
Eliso                              
Katika mifano hiyo hapo juu tunaona mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa mizizi maji, manche, minzi, manji inafanana kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo huu ni ushahidi tosha kutuonesha kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.
Pia mofolojia ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa kiasi kikubwa, yaani mfumo wa maumbo ya maneno ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibatu hufanana. Kwa mfano, namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno hufuata kanuni ileile kama inavyotumika katika lugha ya Kiswahili yaani viambishi vinaweza kupachikwa kabla au baada ya mzizi na uwa na uamilifu bayana. Hebu tuchunguze mifano ifuatayo:
Kiswahili
Kisukuma
Kisimbiti
Kinyiha
A-na-lim-a
a-le-lem-a
a-ra-rem-a
i-nku-lim-a
a-na-chek-a
A-le-sek-a
a-ra-sek-a
a-ku-sek-a                               
  Kwa kuangalia mifano hii utagundua kwamba katika kutenganisha viambishi hufuata kanuni moja kwamba mahali kinapokaa kiambishi kwa mfano cha njeo, ndipo pia hukaa kwa upande wa lugha za kibantu, kwa mfano –na- na –ra- katika lugha ya kisimbiti. Hivyo tunaweza kusema kuwa kuna unasaba baina ya lugha hizi.
Vilevile sintaksia ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa karibu sana. Kwa mfano jinsi ya mpangilio wa vipashio na kuunda sentensi hufanana yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo hufanana katika Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili sentesi ina kuwa na pande mbili yaani upande wa kiima na upande wa kiarifu, katika upande wa kiima kipashio chake kikuu ni nomino na katika upande wa kiarifu kipashio chake kikuu ni kietnzi. Hii inamaana kwamba katika kuunda sentensi ni lazima nomino ianze na baadaye kitenzi. Hebu tuangalie mifano ifuatayo:
Kiswahili
Mama / anakula
N (K)           T (A)
Kijita
Mai /   kalya
N(K)  T (A)       
Kihehe
Mama/ ilya
N(K)  T(A)
Kihaya
Mama / nalya
N(K)     T(A)
  Katika mifano hii tumeona kwamba muunndo wa kiima-kiarifu katika lugha za kibantu unafanana sana na ule wa Kiswahili yaani nomino hukaa upande wwa kiima halikadhalika kitenzi hukaa upande wa kiarifu, kwa hiyo kwa mifano hii tunaweza kusema kuwa lugha ya Kiswahili ni jamii ya lugha za kibantu.
Pia mfumo wa sauti (fonolojia) wa lugha za kibantu unafana sana na ule wa Kiswahili, yaani mpangilio wa sauti katika kuunda silabi, na miundo ya silabi kwa ujumla hufanana. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili hakuna muundo wa silabi funge yaani silabi ambayo inaishia na konsonanti, muundo asilia wa silabi za Kiswahili ni ule unaoishia na irabu vilevile katika lugha za kibantu hufuata muundo wa silabi wazi, yaani silabi zote huishia na irabu. Mifano ifuatayo hufafanua zaidi:
Kisawhili
Baba
K+I+K+I
Kikurya
Tata
K+I+K+I
Kiha
Data
K+I+K+I
Kijita
Rata
K+I+K+I
Kipare
Vava
K+I+K+I
Tanbihi: K= konsonanti I= irabu.
Kwa mifano hii tunaona kwamba mifumo ya sauti katika lugha za kibantu hufanana na ule wa Kiswahili, kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lugha hizi ni za familia moja.
Pia vilevile mfumo wa ngeli za majina katika lugha ya Kiswahili hufanana sana na ule wa kibantu hususani katika upachikaji wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vya umoja na wingi hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa neno, hivyohivyo katika lugha za kibantu. Kwa mfano:
Umoja
Wingi
Kiswahili
m-tu
wa-tu
Kikurya
mo-nto
abha-nto
Kiha
umu-ntu
abha-ntu
Kikwaya
mu-nu
abha-nu
Mifano hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kwamba vipashio vyote vya umoja na wingi hujitokeza kabla ya mzizi wa neno, hivyo ni dhahiri lugha hizi zina uhusiano wa nasaba moja.
Vilevile katika upatanisho wa kisarufi lugha  za kibantu na Kiswahili huelekea kufanana viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani viambisha vya nafsi.
Kwa mfano:
Kiswahili
Mtoto a-nalia
Kizanaki
Umwana a-rarira
Kisukuma
Ng’wana a-lelela
Kikurya
Omona  a-rakura
Tunaona hapo juu kwamba kiambishi ‘a’ cha upatanisho wa kisarufi hujitokeza katika lugha zote, hivyo tunashawishika kusema kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa  na kibantu.
Pamoja na ushahidi wa kiisimu kutupatia vithibitisho tosha juu ya ubantu wa Kiswahili pia kuna ushahidi mwingine kama vile ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.
Ushahidi wa kihistoria huchunguza masimulizi na vitabu mbalimbali vya kale ambavyo huelezea asili na chimbuko la wakazi wa upwa wa Afrika Mashariki. Vilevile ugunduzi wa  kiakiolojia huonesha kuwa kulikuwa na wakazi wa asili wa upwa wa Afrika Mashariki ambao walikuwa na utamaduni wao na maendeleo yao hata kabla ya kuja kwa wageni. Katika ushahidi wa kiethinolojia, huchunguzwa tarihi mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu pwani ya Afrika Mashariki na lugha yao.
Kwa ujumla vyanzo hivi vyote huonesha kuwa pwani ya Afrika mashariki ilikuwa na wakazi wake wa asili ambao walikuwa na lugha yao, utamaduni wao na pia maendeleo yao, vyanzo hivi pia huhitimisha kwa kusema kuwa lugha ya wakazi hawa ilikuwa ni Kiswahili.
Kwa hiyo, kwa hoja hizi tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, madai ya kusema kwamba msamiati mwingi wa kiarabu  katika lugha ya Kiswahili hayana mashiko; Kwani hakuna ushahidi wa kutosha kusimamia hoja hiyo. Kama ilvyojadiliwa hapo juu,vigezo vya kiisimu, kihistoria, kiakiolojia na kiethnolojia ndivyo vitoavyo ushahidi wa kina na kutoa hoja za mashiko kuthibitisha kuwa Kiswahili  sio kiarabu na bali ni kibantu.
      
MAREJEO.
Khalid (2005) “Swahili words of Arabic origin” katika www.baheyeldin.com/linguistics/list of                                           Swahili words of Arabic origin.html
Lodh, A.Y (2000) Oriental influences in Swahili: A study in language. Götenbog. Sweden.
Massamba, D.P.B na wenzake (1999) Sarufi miundo ya Kiswahili Sanifu. TUKI. Dar es salaam.
Massamba, D.P.B (2002) Historia ya Kiswahili 50BK hadi 1500BK. The Jomo Kenyatta                                                                                                                                                                                                                                                                                                      Foundation.
TUKI (2004) kamusi ya Kiswahili sanifu. TUKI. Dar es salaam.




MAANA IBUKIZI KWA WAZUNGUMZAJI WA KISWAHILI ZAMA ZA UTANDAWAZI.
Mwandishi: Dezidery Kalinjuma.
Chuo kikuu cha Dar es Saalam. 2013-05-31.
Wazungumzaji wa Kiswahili wanaweza kuibua maana mbalimbali kulingana na wanavyotumia maneno. Maana hii huibuliwa mara nyingi na msikilizaji. Wakati msemaji akimaanisha maana fulani msikilizaji huweza kuibua maana ya ziada ambayo msemaji hajamaanisha. mtaalamu mmoja aliyaita maneno hayo ibukizi maneno ya kiungonoshaji. yaani nanafungamana na fikra za kingono. Ashakumu si matusi, maneno yatakayotumika ni makali zaidi kwani tumeyachukua jinsi yalivyo kutoka kwa wazungunzaji wa lugha.
Yafuatayo ni baadhi ya maneno ya Kiswahili ambayo yakitumika kati ya wazungumzaji na wasikilizaji huweza kuibua maana ya ziada. Maneno haya  tutayaainisha kwa kuyatungia sentensi  na kufafanua utata wa maana zake.Kwa uhakika maneno haya hutumika katika mazingira ya kawaida lakini haijulikani ni kitu gani humsukuma msikilizaji kuibua maana ya ziada bada la ya maana ya msingi. Endelea
(i) Sentensi hizo ni kama ifuatavyo;
1.      Juma amemkata Asha jana.
Maana ya msingi; Juma ametumia kifaa chenye ncha kali kama vile sindano, kisu, panga na vinginevyo  kumuweka jeraha mwilini mwa Asha.
Maana ibukizi; Juma amefanya mapenzi na Asha.
2.      Yeye alimwambia rose “naomba tigo
Maana ya msingi; Alimuomba Rose ampatie aidha vocha ya mtandao au kampuni ya mawasiliano ya tigo au laini ya tigo
Maana ibukizi; Yeye alimuomba Rose afanye naye mapenzi kinyume cha maumbile.
3. Nilipokuwa nasafiri kwa daladala kwenda mbagala nilisikia mama mmoja akimwambia kondakta wa daladala “nitakupa ikisimama”.
Maana ya msingi: Alimwambia atatoa nauli endapo gari litakuwa limesimama kituoni.
Maana inambukizi; ana kwamba watafanya nae mapenzi endapo uume utakuwa imesimama.
4.      Rafiki yangu aliniambia “atanipa mbele”.
Maana ya msingi; Rafiki yangu atanipa kitu fulani tulichoaidiana mbele ya safari tunapoelekea.
Maana ibukizi; Rafiki yangu atanipa sehemu ya mbele yaani uke au uume wakati tukifanya mapenzi.
5.      Naomba usinitie hapa tafadhali.
Maana ya msingi; Anaomba usimhusishe au usimjumuishe au kumuhusisha na tendo au tukio lolote.
Maana ibukizi; Anaomba usifanye naye mapenzi katika eneo hilo labda kwa sababu lipo wazi sana au halifai.
6.      Raheli alimwambia Kanyamaishwa kuwa  ndizi yake” ni kubwa kuliko ya Jabiri.
Maana ya msingi; Tunda aina ya  ndizi alilokuwa nalo Kanyamaishwa lilikuwa ni kubwa kuliko la  Jabiri.
Maana ibukizi; Kanyamaishwa ana uume mkubwa kuliko wa Jabiri.
7.      Jamila ana shimo kubwa sana
Maana ya msiingi; Jamila ana sehemu  kubwa aliyoichimba kwenda chini kwa ajili ya kuweka vitu kama vile takataka.
Maana ibukizi; Jamila ana uke mkubwa sana (mpana)
8.      Amina alimwambia Jabiri kuwa “watafanya”.
Maana ya msingi; Wakikutana watatekeleza mambo fulani ya msingi waliyokuwa wameahidiana.
Maana ibukizi; Watakapo kutana hawatafanya mapenzi.
9.      Pita amemchoma Meri
Maana ya msingi; Pita ametumia kitu chenye ncha kali kwa kumjeruhi meri kama vile sindano.
Maana ibukizi; Pita amefanya mapenzi na Meri hadi akaridhika.
10.  Asha alimwambia Deo “leo umenifikisha kileleni”.
Maana ya msingi; Asha ailmwambia Deo kuwa leo amekwea naye hadi mwishoni mwa  kikomo au tamati ya mlima.
Maana ibukizi; Asha alimwambia Deo kuwa leo amefanya nae mapenzi akaridhika.
11.  Juma alimwambia Asha apanue aingize vizuri.
Maana ya msingi; Juma alimwambia  Asha afungue vizuri kitu kama mfuko au gunia ili aweke kitu fulani kwa uangalifu.
Maana ibukizi; Juma alimwambia Asha atanue vizuri miguu ili sehemu zake za siri yaani uke uonekane vizuri ili aingeze uume vizuri.
12.  Jana shangazi alimwambia mjomba achomoe taratibu.
Maana ya msingi; Shangazi alimwambia mjomba atoe kitu fulani kilichokuwa kimeingizwa mahali fulana kama vile msumari ukutani taratibu.
Maana ibukizi;  Shangazi alimwambia mjomba utoe uume wake taratibu kwenye uke wa shangazi.
13.  Daaa!!!! Rafiki yangu anamtambo mkubwa sana.
Maana ya msingi; Rafiki nyangu ana mashine kubwa sana ya kurahisishia kazi kama vile jenereta na n.k.
Mmana ibukizi; Rafiki yangu ana uume mkubwa.
14.  Jabiri amelala na Asha.
Maana ya msingi; Jabiri alipumzika pamoja na Asha kitandani au chini.
Maana ibukizi;  Jabiri alifanya mapenzi na Asha.
15.  Dada alimwambia kondakta “nikikaa vizuri nitakupa”.
Maana ya msingi; Dada atamwambia kondakta atampa nauli aliwa amekaa vizuri.
Maana ibukizi; Dada atampa konda uke akikaa vizuri.
16.  Siku hizi bakari anatembea na dada yangu.
Maana ya msingi; Bakari anaongozana na dada yangu katika matembezi yao.
Maana ibukizi; Bakari anamahusiano ya kimapenzi na dada yangu.
17.  Musa ameacha kusimamisha siku hizi.
Maana ya msingi; Musa ameacha tabia yake ya kuzuia kitu fulani kama vile gari, pikipiki au baisikeli visiendelee na safari.   
Maana ibukizi; Musa, uume wake haufanyi kazi kama mwanaume kamili.
18.  Yeye amemwagia Dada mbegu kichwani.
Maana ya msingi; Ina maana yeye alimmwagia nafaka kama vile mahindi, maharage na kadhalika kichwani.
Maana ibukizi; Yeye alimmwagia manii/ shahawa kichwani.
19.  Alinitaka sana mara ya kwanza nikakataa lakini mara ya pili nilikuballi.
Maana ya msingi; Kunihitaji tushirikiane naye sana katika kufanikisha jambo au mabo fulani aliyokuwa nayo mfano kazi.
Maana ibukizi; Kumwomba awe na uhusiano wa kimapenzi naye.
20.  Jana nilikunwa vizuri sana kuliko siku zote.
Maaana ya msingi; Jana alinikwangua kwangua au kunisugua sugua kwa kutumia kitu kama kucha au kijiti kuliko siku zote.
Maana ibukizi; Jana alinidhisha kimapenzi kuliko siku zote.
21.  Halima hatamwacha Munisi kwa sababu alimsugua vizuri.
Maana ya msingi; Munisi alimkuna / alimsugua vizuri alipokuwa anawashwa.
Maana ibukizi;  Halima alifanya naye mapenzi hadi aridhike
22.  Hapo mwanzo alitulia sana siku hizi anagawa sana.
Maana ya msingi; Alikuwa hatoi vitu kama vile msaada kwa watu.
Maaana ibukizi; Alikuwa hajihusishi na masuala ya mapenzi lakini kipindi hiki anafanya sana mapenzi kwa kila mtu.
23.  Pale nimepita lakini sijafurahi kabisa.
Maana ya msingi; Kuendelea na safari kwa kupitia njia ile ile lakini hufurahii safari.
Maana ibukizi; Kufanya mapenzi na mtu fulani bila kupata raha yoyote.
24.  Juma ndie aliyewabandua wale wasichana wawili.
Maana ya msingi; Kutoa mabango au vipeperushi vya wasichana wawili vilivyokuwa vimewekwa sehemu fulani kama kwenye mbao za matangazo.
Maana ibukizi; Juma ndiye aliyewatoa bikira wasichana wale wawili.
25.  Alipotoka pale alikuwa tayari kaloana.
Maana ya msingi; Nguo alizokuwa amevaa zilikuwa na majimaji.
Maana ibukizi; Alipotoka pale nguo zake zilikuwa zimeloa shahawa.
26.  Juma hajui kulenga mpaka aongozwe.
Maana ya msingi; Hana shabaha hadi aongozwe .
Maana ibukizi; Juma hawezi kuingiza uume wake kwenye uke hadi aongozwe.
27.  Ingawa ya kwangu ni nyembamba lakini ya kwake ni nene zaidi.
Maana ya msingi;  Maneno “ya kwake” na “ya kwangu” yanarejelea nomino yoyote iliyomo katiaka ngeli ya mofolojia ya nomino. Kwa mfano simu, nyumba, chupa na n.k.
Maana ibukizi; Maneno “ya kwangu” na “ya kwake” huweza kurejelea na kumaanisha sehemu za siri za mwanamke au mwnaume. (uke na uume)
28.  Leo nina hamu sana kwasababu nimemkosa siku nyingi.
Maana ya msingi; Nina shauku ya kumuona kwa sababu sijamuona siku nyingi.
Maaana ibukizi; Nina nyege naye za kufanya naye mapenzi kwa sababu sijafanya naye siku nyingi.
29.  Joni hupenda sana kuzama chumvini.
Maana ya msingi; Joni anapenda kuingia sehemu yenye majimaji yenye asili ya chumvi.
Maana ibukizi; Joni anapenda sana kunyonya au kulamba sehemu za siri za mwanamke yaani uke.
30.  Ingawa alinishughulikia vizuri sikuridhika.
Maana ya msingi; Ingaw alifanya haraka katika kufanikisha jambo fulani / kujitahidi kufanikisha jambo fulani.
Maana ibukizi; Ingawa alinipa mapenzi vizuri lakini sikiridhika
31.  Ingawa anamtaimbo mkubwa hawezi kuutumia
Maana ya msingi; Ingawa ana fimbo kubwa ya chuma ya kuvunjia miamba hawezi kuitumia.
Maana ibukizi; Ana uume mkubwa lakini hawezi kuutumia.
32.  Japokuwa amenichokonoa hakufanikiwa.
Maana ya msingi; Japokuwa alinidadisi kwa kuniuliza maswali lakini hakifanikiwakupata majibu aliyoyahitaji.
Maana ibukizi; Aliingiza uume au kidole kwenye uke bila kutimiza haja ya mwanamke.
33.  Jana alinikaza kuliko siku zote.
Maana ya msingi;  Jana alinifanyia uimara kuliko siku zote
Maana ibukizi;  Alinifanyia mapenzi mazuri kuliko siko zote
34.  Ingawa alimpa kidogo ila alikojoa sana.
Maana ya msingi;  Ingawa alipata kinywaji kidogo alienda haja ndogo mara nyingi.
Maana ibukizi;  Alitumia sehemu za siri (uke au uume) kidogo lakini alitoa shahawa nyingi.
35.  Aise! Siku hizi huoni mtu anayefyeka ovyo ovyo.
Maana ya msingi; Siku hizi huoni mtu anayejua kukata miti au  majani ili yawe mafupi ovyo ovyo.
Maana ibukizi; Siku hizi huwezi kuona mtu akifanya mapenzi na kila msichana bila kuchagua.
36.  Yeye ananimegea vizuri kuliko wewe.
Maana ya msingi; Yeye ananivunjia kitu au kunikatia kitu kinacholiwa vizuri kuliko wewe.
Maana ibukizi; Yeye alinipa mapenzi mazuri yasiyokuwa na choyo kuliko wewe.
37.  Kutokana na tundu lako dogo nilishindwa kutimiza haja yangu.
Maana ya msingi; Kutokana na uwazi mdogo mfano tundu la choo nilishindwa kutimiza haja yangu.
Maana bukizi; Kutokana na uke wako mdogo nilishindwa kufanya mapenzi vizuri nikatimiza haja yangu.
38.  Juma hupenda kunyonya maziwa kila siku kabla hajalala.
Maana ya msingi; Juma hupenda kunywa maziwa yaliyosindikwa katika pakiti au mifuko.
Maana ibukizi; Juma hupenda kunyonya matiti kila siku usiku.
39.  Jana yeye alimtafuna kutwa nzima.
Maana ya msingi; Jana alisaga kwa meno kitu fulani kutwa nzima.
Maana bukizi; Jana alifanya nae mapenzi siku nzima.
40.  Juma alipochomoa nilihisi maumivu makali.
Maana ya msingi; Juma alipotoa kitu kama sindano matakoni mwangu nilipata maumivu makali.
Maana bukizi; Juma alipochomoa uume kwenye uke nilihisi maumivu.
41.  Mama alimwambia dada kuwa “usafi unaanzia chini”.
Maana ya  msingi; Mama alimwambia dada usafi huanzia sehemu ya kawaida kabisa tenga katika ngazi ya  chini.
Maana ibukizi; Mama alimwambia dada kuwa usafi unaanzia sehemu za siri yaani uke au uume.
42.  Ikiingia huwa ninasinzia.
Maana ya msingi; Ikipenya kuingia ndani kitu kama sindano ya usingizi huwa ninasinzia.
Maana ibukizi; Kila uume uingiapo ndani ya uke wangu huwa ninasinzia
43.  Alipoiweka ilizama yote.
Maana ya msingi; Baada ya kuingia au kuzama ndani ya kitu kama vile  kimiminika ilizama yote.
Maana ibukizi; Uume ulipoingia ndani ya uke ilizama yote.
44.  Kila nikifikia katikati huwa nndio ninapata utamu.
Maana ya msingi; Kila nikifika katikati ndio nanogawa kwa kitu au jambo.
Maana bukizi; Kila nikiingiza kwenye uke (katikati) ndio napata utamu.
45.  Wewe unapenda nyeti.
Maana ya msingi; Wewe unapenda kudeka
Maana bukizi. Wewe unapenda sehemu za siri ( uke au uume)
46.  Mchi wake unatwanga vizuri.
Maaana ya msingi. Kifaa chake cha  kutwangia vitu kama nafaka na madawa kwenye kinu unatwanga vizuri.
Maana ibukizi; Uume wake unaweza kufanya mapenzi vizuri.
47.  Akina mama huko mbele mtanipa. (aliuliza mgombea). Na akina baba je huko nyuma mtanipa.     
Maana ya msingi; Akina mama mliokaa mbele na akina baba mliokaa nyuma mtanipia kura.
Maana ibukizi;   Neno “mbele” na “nyuma” yana maana sehemu za  siri yaana “mbele” ni “uke” na “nyuma” ni “mkundu”.
48.   Sina hamu kabisa na yule kaka maana kitendo alichonifanyia huko nyuma sitakisahau kabisa.
Maana ya msingi: Sina hamu kabisa na yule kaka, kwani  kuni  jambo alilonifanyi hapo zamani sitalisahau kabisa.
Maana ibukizi: Sina hamu kabisa na yule kaka maana kitendo alichonifanyia kwenye matako/ mkundu sitakisahau.
49.  Jamaa wa lori alilazimishia mpaka akafanikisha  kumchomekea kwa mbele yule dada aliyekuwa anaendesha gari aina ya  Prado.
Maana ya msingi: Jamaa wa lori alilazimisha mpaka akafanikisha kutanguliza gari lake aina ya lori  katika nafasi ya mbele ya gari la yule dada  mwenye Prado.
Maana ibukizi: Jamaa wa lori alilazimisha mpaka akafanikisha  kuingiza uume wake katika uke wa dada yule mwenye  Prado.
50.  Dada  mwenye pikipiki  alimwambia yule kijana yule pale sheli, “ingiza vizuri pipe yako usije ukamwaga nje”.
Maana ya msingi: Dada mwenye pikipiki alimwambia yule kijana pale sheli, “weka mpaka ndani bomba la mafuta  usije ukamwaga mafuta nje.
Maana ibukizi: Dada mwenye pikipiki alimwambia yule kijana pale sheli,
“ingiza uume wako mpaka ndani usije akamwaga shahawa nje”.
 
(ii) Kutokana na data ya kwanya kategoria zinazongonoishwa zaidi ni pamoja na;
·         Vitenzi. Kwa  mfano choma, liwa , ingiza, chomoa ,liwa, tia, tiwa.
·         Nomino. Kwa mfano shimo, tundu, mtaimbo, mchi.
·         Vivumishi. Kwa mfano, yake nene, pana.
·         Vihusishi. Kwa mfano, ya kwake, ya Asha
Kategoria zinazongonoishwa zaidi ni vitenzi kwa sababu ndio msingi na muhimili wa sentensi. Vile vile ndio msingi unaobeba utendaji katika tungo.
Kategoria ambazo haziwezi kungonoshwa ni viunganishi na vielezi.
(iii) Wazungumzaji wa Kiswahili hupenda sana kuibua maneno kwa sababu hufikiria zaidi ya maana ya msingi ya neno husika kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia na kusababisha dhana ya ngono kukaa akilini mwa watu hasa vijana.
(iv) Kati ya msemaji na msikilizaji anayengonosha maneno yanayosemwa ni msikilizaji kwani yeye ndiye mlengwa na mfasiri wa dhana inayosemwa. Yeye ndiye anayetafuta maana ya lile lisemwalo.
(v) Hakuna ruwaza maalumu na dhabiti ya ungonoishaji.
(vi)  Kundi la watu wanaongonoisha zaidi ni kundi la vijana kwa misingi ya rika kwa sababu rika hili huwa na mawazo yalivofungamana zaidi na mambo ya ngono.
(vii) Anayeelewa maana ngonoshi za maneno ya Kiswahili ni wazungumzaji na watu waliofungamana na maana hizo za ngono. Wasioelewa maana ya ngonoshi ni wale ambao wapo nje ya muktadha  na rika hilo la vijana. Mfano baadhi ya wazee.
(viii) Katika taaluma ya isimu ungonoshi una mchango kama ufuatao;
·         Huonyesha uhusiano wa maana za maneno. Kwa mfano unaweza kujua ni neno lipi lina maana ya msingi na lipi lina maana ngonoshi.
·         Husidia katika kuonyesha ukubalifu wa maana za maneno kulingana na matumizi. Yaani neno linapata maana kutokana na jinsi linavyotumika, watumiaji wenyewe katika mzingira fulani.
·         Hutusaidia kupata maana za ziada. Kwa mfano neno “mbele” inaweza kuwa na maana ya “kutangulia” na maana ya ziada  ikawa  ni “sehemu za siri” yaani uke au uume.
Athari za maana ibukizi / ungonoishaji ni pamoja na;
·         Kwanza athari ni kupotosha maana ya msingi. Kwa mfano msemaji alikusudia kuomba kura kwa kusema “kina mama hapo mbele mtanipa” kama kuwauliza wanaompiga kura lakini wao wakapata maana potofu ya kuwaomba sehemu za siri yaani uke
·         Pili ni kuongeza uziada dufu katika lugha. Ungonoishaji huaongeza maana ya ziada katika neno. Maana isiyo ya msingi katika neno.
·         Tatu ni kuleta utata katika tungo. Kwa mfano “ikiingia huwa nafumba macho”. Mtu anaweza kujiuliza nini inayoingia.
·         Pia huibua mgogoro katika jamii. Kwa mfano msemajia anapomwambia msikilizaji (kwa mfano wa kike) ambaye hana mzoea naye utungo kama “unashimo kubwa”, kauli hii yaweza kuleta malumbano baina ya msemaji na msikilizaji.
·         Hupelekea uzalilishaji wa kijinsia.
(ix) Ungonoishaji wa maneno ya Kiswahili ni jambo jipya lililoibuka ingawa maneno yanayotumika yalikuwepo. Kimsingi maneno haya yalizingatia maana za msingi za maneno husika. lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia pamoja na utandawazi maneno haya yameanza kupewa maana ya ziada inayofungamana na ngono yaani ungonoishaji. Na hii hutokana na mawazo ya watumiaji kufungamana na ngono.
(x) Suala la ungonoishaji ni suala la kukemewa na kubezwa kwani linapotosha maadili na uwezo wa kukamilisha mawasiliano na lengo lililokusudiwa. Kwa mfano kama mtu anafundisha anaweza kujikuta anachekwa baada ya kutumia neno liloibua dhana ya ungonoishi kwa wanafunzi au wasikilizaji. Hivyo suala hili likiendelezwa mwisho wake maana ya msingi imefifizwa na wanatumia maana ungongoshi tu.


Marejeo.
TUKI,  (2004), Kamusi ya Kiswahi Sanifu. Oxford University Press: Nairobi



 VYANZO VYA KUKUSANYA DATA YA KUUNDA     KAMUSI.
Katika mjadala huu tumeugawa katika sehemu  kuu tatu, sehemu ya kwanza  itaelezwa   maana  ya vipengele muhimu katika swali  kutokana na wataalamu  kama vile kamusi, na data, sehemu ya pili ni   kiini cha swali  ambalo itaelezwa vyanzo mbalimbali vya ukusanyaji data katika kuundia kamusi, na sehemu yatatu na mwisho itaelezwa hitimisho na marejeo ya swali.
Zgusta (1971) akinukuliwa na Mdee (2010)  anaeleza kuwa; Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo  wasomaji wanaweza kuelewa.
Pia Tuki (2004)  wanasema kuwa  Kamusi ni kitabu  cha maneno yaliyopangwa kwa utaratibu wa kialfabeti na kutolewa maana ya maelezo mengine. Fasili hizi kwa kiasi fulani inamapungufu kwani kwa  kuwa kamusi ni kitabu lakini sio kwamba kamusi zote zipo katika muundo wa maandishi ya kitabu bali kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kamusi  zinaweza kuwa  katika mfumo wa elekroniki kama vile kwenye simu, santuri na kompyuta.
Hivyo tunaweza kueleza kuwa; kamusi ni orodha ya maneno yaliyopangiliwa kialfabeti na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu au eletroniki na kufafanuliwa kwa maneno marahisi  namna ambavyo wasomaji waweze kuelewa kwa urahisi.
Kuhusu maana ya data  TUK(I2004)wanaeleza kuwa data ni  taarifa  au takwimu  inayotumiwa kuelezea au kuthibitisha hoja fulani. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kuwan  data ni  mkusanyiko wa  maneno (msamiati) vielelezo, picha,  na takwimu zinazokusanywa na wanaleksografia  kwa lengo la kuundia kamusi.
Hivyo tanaweza kusema kuwa ukusanyaji data ni hatua muhimu katika uundaji wa kamusi na hivyo ndivyo hatua ya muhimu  ambayo inahitaji kuzingatia   sera za kamusi  na mahitaji ya  watumiaji.Kwa hiyo tunasema kuwa kamusi bora  kwa kiasi kikubwa hutegemea  ubora wa wakusanyaji data na ukusnyaji wenyewe.  Vyanzo hivyo vya   ukusanyaji data  zimegawanyika katika makundi makuu  mawili  ambayo ni makundi simulizi na makundi andishi  na  makundi hayo yamegwanywa katika makundi  madogomadogo kama ifuatvyo.
Kutokana  na mawazo  ya Kipfer (1984) akinukuliwa na Habwe (1995) katika  makala yake  kitabu cha utafi na utungaji  kamusi anasema kuwa “tunaweza kupata vyanzo mbalimbali  ukusa nyaji  wa data katika makundi makuu mawili ambazo ni  makundi  mazimulizi na mandishi na hizo makundi zimegwanywa katika makundi madogomadogo”. Tukijikita  katika makundi haya tunawefafanua vyanzo hivyo za yaliyoko katika kundi la kwanza ambayo ni vyanzo simulizi. Katika kundi hili tunaweza  kupata  vyanzo  mbalimb  vya data nazo.
Kwenda uwandani: Kutokana na wazungumzaji wa lugha husika au walengwa ..Hivyo mwanalekiksografia  anapaswa kwenda katika  jamii ya wazungumzaji wa lugha husika  ili kupata data mbalimbali ambazo wanjamii wanazitumia. Data hizo ndizo zitakazomsaidia  katika utungaji  wake wa kamusi.
Majadiliano:Kutokana na majadiliano mbalimbali katika makundi mbalimbali  ya jamii  kutokana na mada mbalimbali, makundi haya yanaweza kuwa ya  wanasayansi, wanasiasa.  wanafasihi na wanaisimu  hivyo wanalekiksografia  huweza kuchambua  msamiati  mbalimbali na kuziorodhesha  katika kamusi anayoilenga.
Mahubiri ya kidini: Kuwepo kwa mikutano mbalimbali ya kidini kama vile  mikutano ya kiinjili katika dini ya kikritu na mawaida katika dini ya kiislamu kutokana matumizi mengi ya maneno  katika shughuli hizo kunakuwepo maneno ambayo mwanalekiksografia kukusanya  data zake kutokana na  mahubiri haya huku akizichambua  na kuzitumia   katika kuundia  kamusi.
Masimulizi ya visa na utambaji wa hadithiti: Kutokana na visa mbalimbali  vya matukio  zinazosimuliwa  na watu mbalimbali kama vile kisa cha kibo na mawezi, na kisa ch Sungura kuwa na mkia mfupi. na visa vingine. Mwanalekiksografia  huchambua  maneno mbalimbali na kuyatumia katika kuundia   kamusi anayoilenga .
Maongezi ya kawaida:Kutokana na mazungunzo yanayofanyika  katika shughuli za  kila siku katika jamii  kunakuwepo misimiati  mbalimbali inayotumika  na ambayo wanalekiksografia  hukusanya  data hizo na  kuzichambua na kuingiza katika kamusi.
Baada ya kuangalia vyanzo mbalimbali  vya  ukusanyaji  data  katika kundi la  masimulizi  basi ni vyema  kutalii  vyanzo   katika kundi la maandishi.Upatikanaji data  kimaandishi ni data zinazopatikana katika maandishi  mbalimbali  za  waandishi wengine na kuhifadhiwa maktabani.  Mwanalekiksografia   huweza kwenda  maktabani  kusoma maandiko  mbalimbali ambapo huweza kumsaidia kukusanya data zake na data zinaweza katika;
Katika kazi za  tafsiri: Kutokana na kazi za waandishi maarufu walioandika  katika lugha mbalimbali  huweza kutafsiriwa katika lugha  nyingine  kama vile tafsiri za kazi za kiingereza kwenda katika kazi za Kiswahili mfano kazi za “Shujaa Okonkwo,”  “Mtaa Mweusi,” na “Nitaolewa  Nikipenda.” tafsiri za kazi hizi humsaidia  mwanaleksografia  kufahamu maendeleo ya tamaduni  mbalimbali  za jamii  na baadhi ya msamiati  itumiwayo katika jamii hizo ambayo  humsaidia mwanalikiksogrfia kupata data  ambazo humsaidia katika kuundia kamusi yake.
Katika kumbukumbu mbalimbali,kama vile.makongamano, mikutano, na shughuli za bunge: Kutokana na  kumbukumbu  hizo  pamoja na warsha,  mwanaleksografia  hukusanya data zilizoandikwa  kama kumbukumbu zao  na kuziingiza katika kamusi lengwa alilokusudia.
Makala mbalimbali za kidini: Kuwepo kwa makala mbalimbali za  kidini zilizoandikwa kwa lengo au kutoa msimamo wa dini zao au kueneza dini hiyo. Mwanalekiksogrfia anapswa  kuyaangalia makala hayo pamoja na vitabu vya kidini kama vile Bibilia Takatifu na Kuruani Tukufu  na magazeti ya kidini kama vile “Tumaini letu” Upendo” Kiongozi” na An-nuar. Hivyo  kupitia makala hizi mwanaleksografia  hupata maneno mbalimbali  ambayo humsaidia yanayotumika katika kuundia  kamusi lengwa.
Kutumia kongoo:Hii ni data za lugha ambazo huhifadhiwa katika kompyuta bila kujali ni maneno ya lugha gani na huhifadhiwa kadri inavyohitaji mtaalamu.  Katika  kongoo kuna nyanja    mbalimbali  kama vile nyanja  mimea,Afya  sheria, wanyama,  uchumi, fasihi na isimu.Hivyo mwanaleksografia huchambua baadhi ya msamiati anayohitaji ya nyanja  na kuziingiza katika kamusi anayoilenga.
Hotuba.Pia mwanalekiksografia huweza kupata data zake kwa kusoma  hotuba  za viongozi mbalimbali maarufu kama vile  Hayati mwalimu Nyerere,  Mkapa, Lowasa, Mwinyi Neson Mandela wa Afrika Kusini  na Jomo Kenyatta wa Kenyia. Hotuba hizo huandikwa na kuhifadhiwa katika maktaba ambapo mwanaleksografia huchumbua misamiati mbalimbali ambazo humsaidia  kuundia kamusi.
Kamusi za awli. Kamusi za  awali pia ni muhimu kwa mwanalekiksografia  katika kupatia data zake kwani humsaidia kuonyesha  maneno ambayo yapo katika kamusi za awali  na pia maana ya matumizi yake kulingana  na kamusi hizo.
Kutoka katika kazi za kifasihi: Kutokana  na kusoma kazi mbalimbali za  fasihi kama vile riwaya,  Tamthiliya na ushairi hasa za watu mashuhuri kama zilizoaandikwa  na  Shaaba Robert , Mathias  Mnampala, Amri Abeid, Mulokozi,  na Kezilahabi  mwanalekiksografia  anapswa  kuzichambu kazi hizo  kwa undani na kuzinukuu baadhi ya misamiati zilijitokeza ili apate data  za kuundia kamusi yake.
Magazeti na majarida:  hii ni vyanzo ambavyo   mkusanyaji data anaweza kupata data zake kwa kutumia  njia hii kwa sababu  magazeti hushughulikia nyanja  mbalimbali katika  jamii na ni rahisi kupata maneno yanayozunguzwa na makundi mbalimbali za jamii na waandishi wake  hujitahidi kutumia  lugha sanifu iwezekanvyo. Mifano  ya magazeti haya ni kama vile  Rai, Mwananchi Nipashe,Mtanzania ,Tanzania daima Habari leo Mwanaspoti Bingwa na The Guardian na Majira. Pia kuna majarida mbalimbali kama vile  Mulika Kioo cha Lugha, na Jarida la femina. Kutokana na misamiati inayopatikana katika majarida haya na magazeti haya mwanalekiksografia huchambua  misamiati anayohitaji katika kuundia kamusi.
Kwa  kuhitimisha  tunaweza kusema kuwa  ili mwanalekiksografia aweze kukusanya  data zilizobora zaidi ni vyema kuwa mmilisi wa lugha husika
 Marejeo
Kiango J.K na Mdee J.S(1995).Utafiti na Utungaji wa Kamusi.Dares Salaam:Tuki
Mdee, J. S. (2010) Nadharia na Historia ya Leksokografia. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI, (2004) Kamusi ya Kiswahili sanifu Nairobi:Oxford university Press.

UCHAMBUZI WA MATUMIZI YA MISEMO KWENYE MAGAZETI : MIFANO KUTOKA MAGAZETI YA TANZANIA.
                                                   MWANDISHI: KALINJUMA, DEZIDERY.
                                           CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
                                                            SURA YA KWANZA


YALIYOMO
Shukuranu………………………………………………………………………………….iii
SURA YA KWANZA
1.0. Ikisiri……………………………………………………………………………………1
1.1.Utangulizi……………………………………………………………………………….1
1.2.Tatizo la utafiti…………………………………………………………………………2
1.3.Malengo ya utafiti……………………………………………………………………...2
1.3.1.Lengo kuu ……………………………………………………………………………2
1.3.2Malengo mahususi……………………………………………………………………2
1.4.Maswali ya utafiti…………………………………………………………………….3
1.5. Umuhimu wa utafiti…………………………………………………………………...3
1.6.Eneo la utafiti…………………………………………………………………………..3
1.7.Nadharia ya utafiti…………………………………………….........................................3
SURA YA PILI
2.0.Mapitio ya machapisho……………………………………………………………….5
SURA YA TATU
3.0.Mbinu za ukusanyaji data…………………………………………………………….7
SURA YA NNE
4.0.Matumizi ya misemo…………………………………………………………………..8
4.1.Kwa nini magazeti hutumia misemo………………………………………………….9
4.2.kusisitiza jambo………………………………………………………………………..10
4.3.Maana ya misemo magazetini………………………………………………………...11
                                                                                                                                        i.             
SURA YA TANO
HITIMISHO………………………………………………………………………………..13
MAREJEO………………………………………………………………………………......14
KIAMBATISHO…………………………………………………………………………..,,15
                                                                                                                                     ii.             
SHUKURANI
Hatuna budi kutoa shuklani kwa wote walio changia kufanikisha utafiti huu. Hatutaweza kuwataja wote waliotoa usjirikiano wao, badhi ya waliotoa msaada wa karibu ni hawa wafuatao; kwanza shukrmi za pekee ziwaendee Dk. George Mlikalia  na Elizabeth Mahenge ambao ndio walimu  na washauli wa somo napenda kuwashukuru pia watumishi wote katika ofisi ya mwalimu mahenge kwa msaada walioutoa wa kupokea kazi zetu na kutushauli.
Pili tunapenda kuwashukulu wanafunzi wote waliotoa msaada wa knipatia magazeti,pamoja na maoni yao.
Tatu shukrani za dhati ziwaendee watumishi wa maktaba waliowezesha uwepo wa magateti kila siku.
1.0 Ikisiri.
Utafiti huu unahusu  uchambuzi wa misemo kama inavyojitikeza  magazetini nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Kihole(2004) baada ya kupitishwa kwa sheria iliyohusu kuanzishwa kwa magazeti binafsi mnamo mwaka (1992) kumeibuka magazeti mengi ya lugha ya Kiswahili nchini Tanzania yanayochapishwa kila siku, kila wiki, ama mara kadhaa, kwa wiki kwa mwezi nakadharika. Magazeti kama haya hufikia kama hamsini nchini humu hii ni kwa mujibu wa Kihole.Miongoni mwa magazeti haya kuna magazeti yanayochukuliwa kama magazeti rasmi. Kwa mujibu wa Kihole (2004) anasema magazeti hayo ni yale yanayohusu matukio halisi ambayo kwa kawaida huwa yanahusishwa na mamlaka au chanzo fulani malumu na kutolewa kwa  namna na mazingira rasmi. Anazidi kusema kuwa mazingira ya kutolea habari husika ni yale yanayoendana na kaida katika jamii, kisheria na kiutamaduni. Kihole ameyagwa magazeti katika makundi tofauti, Magazeti katika kundi jumuishi, Magazeti katika kundi la michezo mfano, Dimba,Mwanaspoti, Lete raha nakadhalika. Pia ametaja kundi jingine kuwa ni magazeti ya mitaani.
 1.1.Utangulizi:
 Magazeti mbalimbali ya Tanzania huandika habari mbalimbali zenye matukio halisi yanayoshuhudiwa na waandishi au hupatikana kwa vyanzo  fulani maalumu.  Hii ni kwa mujibu wa Kihole (keshatajwa) Kihole katika utafiti wake alioufanya alikusudia kuchunguza masuala ya kisarufi katika maelezo yanayojitokeza katika magazeti ya mitaani.
                                                                   1.
 Katika uchunguzi wake amegusia vipengele vya msamiati, na misemo inayotumiwa na magazeti haya, miundo ya sentensi zinazohusika na matumizi mengine ya lugha kwa ujumla katika magazeti haya.
Pia kwa mujibu wa King’ei (2000) katika utafiti wake amechambua juu matatizo  ya matumizi ya lugha katika vyombo vya habari, jinsi lugha inavyotumika katika kazi mbalimbali kama vile maelezo, ufananishaji, au uunganishaji, usisitizaji, ukinzani(utatanishi) nakadharika.
1.2. TATIZO LA UTAFITI:
Katika tafiti za wataalamu kama vile Kihole (2004) na King’ei (2000) wamefanya utafiti wao; ambapo Kihole amefanya utafiti juu ya masuala ya kisarufi magazetini kwa kuzingatia  vipengele vya matumizi ya lugha, misemo na miundo ya sentensi. King’ei naye (2000)alitafiti juu ya lugha katika vyombo vya habari, Hivyo utafiti huu utachunguza kwa undani kipengele cha matumizi ya misemo ambacho hakikuchunguzwa kwa undani na na  watafiti. Hivyo katika kipengele hiki tutaangalia jinsi misemo inavyojidhihirisha na jinsi inavyotumiwa katika magazeti ya Tanzania.
 1.3.MALENGO YA UTAFITI:
Utafiti huu una malengo mbalimbali, malengo hayo tutayafafanua katika kipengele kinachofuata. Malengo hayo tumeyagawa katika sehemu mbili kama inavyoonekana hapa chini.
1.3.1.Lengo kuu
 Ni kuona jinsi kipengele cha misemo kinavyotumika katika magazeti mbalimbali ya Tanzania. Pia kuona sababu kubwa inayofanya magazeti mengi yatumie misemo.
1.3.2.Malengo mahususi.
·         Kuonyesha jinsi misemo inavyotumika katika magazeti.
·         Kueleza kwa nini magazeti hutumia sana misemo.
·         Kufafanua maana ya misemo kama inavyotumika magazeti.
                                                       2
1.4. MSWALI YA UTAFITI:
1. Je, misemo inatumikaje katika magazeti?
2. Je, ni kwa nini magazeti hutumia misemo?
3. Je, misemo ina maana gani magazetini?
1.5.UMUHIMU WA UTIFITI:
 Kutafiti juu ya matumizi ya misemo katika magazeti. Misemo hii huwa na maana tofauti na jinsi inavyotokea katika magazeti. Hivyo kulingana na nadharia ya uchambuzi inayosema kuwa fasihi haina maana finyu  bali ina maana nyingi kutokana na matumzi ya yake katika miktadha tofauti. Hivyo ni muhimi msomaji  kuzingatia maana inayopatikana katika muktadha husika wa misemo ilivyotumika katika magazeti. Hii itamsaidia msomaji kuielewa kazi ya fasihi iliyo katika maandishi kwani atazingatia maana tofauti  kwani atakuwa anasoma kwa kuzingatia si   maana moja tu bali manaa mbalimbali kulingana na muktadha.    
1.6. ENEO LA UTAFITI:
Utafiti huu ulifanywa katika eneo la chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambacho ni moja ya vyuo vikubwa vinavyopatikana Tanzania. Utafiti huu umehusisha kuingia maktaba inayopatikana katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambayo ndiyo ilikuwa chanzo cha upatikanaji wa data.
1.6.NADHARIA YA KIUCHAMBUZI:
Kabla ya kuelezea nadharia tutakayoitumia katika uchambuzi wetu, ni bora tujue  maana ya nadharia kama ilivyofasiliwa na wataalamu mbalimbali;
Kwa mujibu wa Wamitila (2002) nadharia ni nyenzo au maelezo yanayotusaidia kufikisha lengo fulani. Pia anasema kuwa nadharia huzuka na kutoweka katika mazingira fulani ambayo yana wasifu na utamaduni husika.
                                                                      3.
Wafula na Njogu(2007) wao wanasema kuwa nadharia ni istlahi ya kiujumla inayoainisha miongozo inayomwezesha msomaji wa kazi ya fasihi na kuifahamu kazi hiyo na vipengele vyake. Hivyo baada ya kuona maana ya nadharia  sasa tuelezee nadharia ya kiuchambuzi tutakayotumia katika uchambuzi wa data.
Katika utafiti huu nadharia itakayotumika ni ile ya kihemenitiki. Msingi wa nadharia hii ni wa uchunguzi wa matendo mbalimbali ya binadamu kama usomaji, upendaji, uchukiaji na kadhalika. Nadharia hii huchunguza jinsi wasomaji wanavyoielewa matini au kazi fulani pamoja na mbinu au njia za welewa wenyewe. Kwa mujibu wa Friedrich Schleiemarker na wenzake(1768-1834) wakinukuliwa na Wamitila(2006).
Nadharia hii kwa mujibu wa Schleiemrker(keshatajwa) inajihusisha sana na suala la uelewaji wa watumiaji wenyewe . Anaeleza kuwa suala mojawpo kubwa na muhimu katika fasihi ni kujitahidi kujiepusha na uelewaji mbaya kazi unayoisoma. Anaendelea kusema kuwa elementi ya kazi husika inapoandikwa . Kwa mujibu wa mtaalamu huyu  kazi ya kifasihi haina maana finyu, mawezekano ya maana hayana mipaka. Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa mkabala huu wa kinadharia unahusisha lugha na misemo. Schleiemarker (17678-1836). Mkabala huu ungekuwa wa manufaa zaidi katika uchunguzi wa misemo magazetini kwani msingi huu wa nadharia umekitwa katika fasihi.
                                                   SURA YA PILI.                                
2.0.MAPITIO YA MACHAPISHO:
Katika kufanikisha utafiti huu machapisho mbalimbali ya wataalamu yamepitiwa ili kutoa mwanga juu ya utafiti tutakofanya .Katika mapitio ya machapisho mbalimbali tumebaini sifa mbalimbali za magazeti.
Kwa mujibu wa King’ei (2000) katika utafiti wake amebainisha sifa mbalimbali za magazeti sifa hizo ni kama zifuatavyo:
1.Vichwa  vikuu na vichwa vidogo,
·         Uzito na uhafifu wa chapa
·         Mpangilio wa makala
·         Uakifishaji
·         Mpangilio wa aya
·         Matumizi ya visitiari
2. Muundo wa sentensi usio wa kawaida (aya ndefu zilizounganishwa kwa visitiari na viunganishi).
3. Matumizi ya istlahi bila maelezo.
4.Msisitizo (mtindo wa mazungumzo) na mafumbo.
5.Mgawanyo kati ya maelezo ya maudhui na maoni halisi au mwelekeo wa mwandishi.
Pamoja na kuainisha sifa hizi za magazeti lengo la King’ei lilikuwa ni kutafiti na kufafanua matatizo ya lugha katika vyombo vya habari mifano yake ametumia ya Kenya.
      Pia Kihole (2004) katika utafiti wake ameainisha sifa tofauti tofauti za magazeti sifa hizo amezigawa katika makundi mawili ambayo ni sifa mahususi na sifa za jumla.  Katika sifa mahususi Kihole (2004) amezitaja kuwa ni pamoja na; magazeti kueleza vituko, mfano visa na vitimbi ambavyo hata watoaji wake huwa wanajua kuwa vinaweza kuwaweka wasomaji katika
                                                                            5.
hali isiyo ya kawaida. Mfano gazeti la kasheshe na sani. Sifa nyingine ni kuwa magazeti hubeba mambo ambayo hayastahili kusomwa mbele ya watoto au  watu wazima mbele ya watoto wao, pia magazeti hutumia maneno ambayo humfanya mtu ajiulize kama kile kinachoongelewa ni kweli au cha kubuni. Kihole anendelea kusema kuwa maelezo hayo huishia na maneno [.….]. Sifa nyingine ni kuwa mada chache zilizo haririwa  ni aina ya msamiati wa misemo ambayo kawaida hujitokeza katika magazeti rasimi. Katika kuainisha sifa Mahususi za magazeti Kihole (2004) anasema kuwa sifa hizo ni pamoja na; magazeti hayo kujihusisha na mambo binafsi ya watu au makundi ya watu mfano vituko vya watu maarufu, sifa nyingine ni kuwa magazeti huwa na uhuru wa kutumia lugha ya kiingereza moja kwa moja au kama maneno ya kawaida yanayopatikana katika kamusi  sanifu.
      Pia  mtandao wa A.P.A Citation syte 6th edition (www.landmark.edu/library/citation-guides/apa.cfm) wametoa baadhi ya sifa ya magazeti ambazo ni pamoja na :
·         Magazeti huhusisha matangazo.
·         Magazeti huwa na picha nyingi.
·         Ni rahisi kusoma, huwa na matangazo mengi ya kibinafsi mfano biashara, ufundi mapendekezo nakadharika.
·         Yanavuta umakini wa msomaji juu ya maneno yanayotumika.
                                                                             
                                                        SURA YA TATU.
3.O.MBINU ZA KUKUSANYA DATA:
Baada  ya kuchunguza mapitio mbalimbali ya wataalamu tungependa kuchunguza kwa undani misemo inayotumika magazetini. Lakini kabla ya kufafanua matumizi ya misemo ngoja tuangilie kwanza mbinu ya utafiti. Mbinu ya utafiti iliyotumika  katika ukusanyaji wa data  ni pamoja na  mbinu ya  kusoma na kuchambua data kutoka katika magazeti mbalimbali. Katika ukusaji wa data, magazeti yaliyokusanywa ni 11 ambayo ni pamoja na  Mtanzania, Rai, Bingwa, Majira, Uhuru, Nipashe, Mwananchi, Sani, Dimba,Mwanaharisi, na Ijumaa ya kuanzia mwezi Mei 2011 hadi Julai 2011
                                                                   7.
                                                    SURA YA NNE.
4.0. MATUMIZI YA MISEMO MAGAZETINI:
Misemo magazetini hutumika kwa namna tofauti. Matumizi haya ya misemo hutumiwa moja kwa moja kwenye vichwa vya habari au katika maelezo. Baadhi ya vichwa vya habari hutofautiana na mada ambazo huwa zinakuwemo  ndani ya habari.Hii ina maana kuwa misemo inayotumika huwa na maana iliyotofauti kabisa na maana inayoonekana magazetini.Misemo mingine tumeionyesha kwenye kiambatisho.  Ngoja uangalie mifano ifuatayo:
a)      Nesi  Kitete ajikaanga (Mtanzania, mei, 23,2011.)
b)      Sarakakasi za Sitta Mwakyembe CCJ (Mtanzania, Mei 9, 2011).
c)      Vigogo CCM  wakaangwa (Manzania, Mei,23,2011)  .
d)     Spika, Zitto jino kwa jino, Mkulo  apigilia msumali wa mwisho(Uhulu, Juni, 14, 2011).
e)      Ujamaa wampofusha Mukama(Rai,mei 19-25,2011).
f)       Lady Jaydee kutembea uchi live(Sani,Mei, 14,2011).
g)      Akina Ukwa waja tena (Kiu, ya jibu Juni, 23,2011).
h)      Ngeleja kitanzini(Uhuru, Juni; 6, 2011).
i)        Mashabiki Yanga wafurika kushuhudia majembe yao (Bingwa, Juni, 14, 2011).
j)        Ulimwengu ndiye muuaji (Uhuru Juni 6, 2011).
k)      Morocco yafanya mauaji (Uhuru, Juni 6, 2011).
l)        Mbowe balaa Dar (Majira, juni,6, 2011) .
m)    Mganda awasili kumvaa Mwakyembe(Bingwa Mei, 20 , 2011).
n)      Lowassa amkatia Kiwete rufaa (Mwananchi, juni, 16, 2011).
o)      UPDP kuunguruma Dar kesho (Mtanzania,Mei,25,2011).
p)      CDA yakabwa koo na kamati ya bunge(Bingwa,Mei, 20,2011).
Katika mifano hii, ni dhahili kuwa maana inayoonekana katika msemo hii sivyo ilivyo katika maelezo au habari nzima. Mfano, katika (a) siyo kwamba ‘nesi alijikaanga kiaangoni’ bali alijiweka katika mazingira magumu ya kuendelea na kazi baada yahuduma  kumzalisha mama
                                                                         8.
 na mwanae kufichwa. Pia katika (f) haimaanishi Ukwa waigizaji wa Nigeria bali kuna vijana waliojifananishwa na waigizaji hao. Katika (h) ‘majembe’ haimaanishi majembe vifaa bali anamaanisha wachezaji wapya waliosajiliwa na timu ya Yanga.Mifano mingine mingi tutaitolea maana katika sehemu inayofuatwa.
                                                                     
4.1.KWA NINI MAGAZETI HUTUMIA MISEMO:
Kihole (2004) anasema kuwa ; ‘ni kwa hali hii ya kushangaza kile kinachotajwa katika mada hiyo ama hufanya baadhi ya wasomaji kukosa hata hamu ya kufikiria kununua magazeti haya au kuwachochea watu  kufanya juhudi za kuyapata magazeti hayo’. Hivyo baadhi ya magazeti hutumia misemo ili kuvuta umakini wa wasomaji. Ngoja sasa tuangalie baadhi ya misemo ambayo huweza kuvuta wasomaji.
a)      Nilitema big G kwa karanga za kuonjeshwa
b)      Ray C akimbia nchi.
c)      Ngono Big Brother sasa(Kiu ya Jibu,juni,22,2011).
d)     Nilipopiga ramri kumtafuta Mungu(Kiu ya jibu,Juni,22,2011).
e)      Lady  Jay dee kutembea uchi(Ku ya jibu,Juni,22,2011).
f)       Kituo cha kuoshea nyeti za kike Dar(Sani,Mei,11-14).
g)      Mganda awasili kumvaa Mwakyembe (Bingwa Mei,20,2011).
h)      Spika Makinda mbumbumbu anasimamia asichokijua (Rai,Juni,20,2011).
i)        Freemason na ugaidi katika kanzu ya uislamu (Mtanzania,Juni,17,2011).
j)        Wanaume kumeza vidonge vya kuzuia mimba(Uhuru, Juni, 7-14,2011).
k)      Sauti ya radi awa makamu wa Rais(Ijumaa mei, 20, 2011).
l)        Waziri, changu wateta kwa nusu saa Dom(Ijuma,Julai,15,2011).
m)    90% mastaa wauza ngono bei chee(Ijumaa, Julai,15,2011).
n)      Badra aanika chachandu zake adatisha midume(Ijumaa,Julai,15,2011).
o)      Mchumba aliyevua nguo (Dimba, Juli,17,2011).
p)      Linah sina mtu sasa niko single(Sani,juni,12,2011).
q)      Mrembo anaswa akichimba dawa hadharani(Iumaa,Julai,15,2011).
                                                            9.
Kwa kuitazama  misemo hii katika vichwa vya magazeti  tunaweza kubaini kuwa inavutia wasomaji hata kununua magazeti ili kupata taarifa iliyomo ndani ya gazeti hilo. Kutokana maoni ya Kihole (2004) anaposema kuwa ni kutokana na matumizi ya misemo hiyo wasomaji huweza kukatishwa tamaa au kufanya juhudi za kuyapata magazeti hayo, tumeshuhudia magazeti mengi yakitumia misemo hiyo ili kufanikisha
nia ya wasomaji. Mfano gazeti la sani, Ijumaa na Kiu.
4.2.KUSISITIZA JAMBO:
Katika utafiti wetu tumegundua kuwa magazeti hutumia misemo, na misemo hiyo huwa inajirudiarudia katika magazeti mengi. Misemo hii hulenga kuweka msisitizo juu ya jambo lilopita, lililopo au lijalo. Mfano misemo tuliyoitumia katika utafiti wetu baadhi inasisitiza juu ya mambo yaliyokuwepo katika kipindi hicho cha utafiti ulipofanyika. Ngoja sasa tuione baadhi ya misemo hiyo.
a)      Tibaijuka ang’aka(Mtanzania,Mei,20,2011).
-Hi ilkuwa kipindi cha mchakato wa watu kurudisha ardhi walizochukua na wananchi bila kukubaliwa na serikali.
b)      Wabunge CCM wakaangwa (Mtanzania, Mei,23,2011).
Misemo hii imesikika sana kipindi cha wabunge wanahusihwa na migogoro ya chama   ilyojulikana kama (kujivua gamba).
c)      DC walimu wa shule za kata wasiitwe Voda fasta.
d)     Kujivua gamba hakutoshi.
Katika mifano hii misemo mingine huibuka kulingana na mada iliyopo na baadae misemo hiyo haisikiki tena. Hivyo ni kutokana na msisitizo huo wasomaji huweza kuwa na ufuatilizi juu ya tukio fulani kulingana na jinsi linavyotokea mara kwa mara.
                                                                      10.
4.3.MAANA YA MISEMO MAGAZETINI:
 Katika utafiti huu tumegundua kuwa magazeti hutumia misemo mbalimbali yenye maana tofauti. Kulingana na nadhalia iliyotumika kuchambua utafiti huu tumeona kuwa kazi ya fasihi huwa haina maana moja hivyo maana inaweza kutokana na kazi iliyopo au kulingana mukutadha uliopo. Hivyo maana ya misemo mingine hutokana na mukutadha wa kazi iliyopo. Hivyo katika maana ya misemo  hii tuliyotoa tumezingatia jinsi misemo hii ilivyotokea magazetini.  Mfano wa ,misemo hii ni kama ifuatavyo;
a)      Kalenga aipiga tafu Vodacom miss Bagamoyo(Mtanzania,Mei, 20,2011).
-‘Kupiga tafu’       kusidia .
b)      Aahidi kuanika hadharani vielelezo walivyoshiriki(Mtanzania,Mei, 20, 2011).
                -‘Kuanika’ maana yake ni kuweka wazi.
c)      Azzani asiwe mbuzi wa kafara CCM (Rai, Mei, 19-25,2011).
-‘Kuwa mbuzi wa kafara maana yake’ asiangaliwe kama mkosaji kutokana na makosa
                    yanayofanywa na wakuu wake wa kazi.   
d)     TAKUKURU inabweka lakini haing’ati(Rai, mei, 19-25, 2011)
-‘Hii ina maana kuwa takukuru inatishia lakini haitendi.
e)      Niyonzima aotambawa jangwani(Bingwa, Mei, 20,2011).
-Kuota mbawa maana yake ni kushindwa kufikia mwafaka.
f)       Nyota wa Man U walipoanika vifaa vyao kwenye ‘pati’Bingwa, (Mei,19-25,2011).
           -Kuanika vifaa maana yake walikuusanyika na nakujumuisha wake zao. Vifaa ni
wanawake.
g)      Mshindi wa Tanzania ajishebedua ‘BBA’.(Bingwa, Mei,19-25,2011).
-Kujishebedua maana yake kujifanya hutaki kitu fulani huku unakitaka.
h)      Blatter amekalia kutikavu FIFA? (Majira,23,2011).
-Kukalia kuti kavu maana yake amejiweka katika nafasi ngumu ya kazi yake.
i)        Bimman abwaga manyanga (Majira,Mei,23,2011).
-Kubwaga manyanga maana yake kuacha kazi.
                                                           11.
j)        Harambee ya Yanga yadoda (Uhuru, Mei, 3,2011).
-Kudoda maana yake kushindwa.
k)      Wadai hukumu inanuka rushwa(Majira,Mei,23,2011).
-Kunuka rushwa ina maana kuwa kuna hali ya kutoa rushwa katika hukumu hiyo.
l)        Mwakalebela aibwaga TAKUKURU.
-‘Kuibwaga’ ina maana ya alishinda kesi iliyomkabili kuhusu TAKUKURU.
Hivyo kama tulivyoeleza kabla hatujaanza kutoa mifano hii kuwa kazi ya fasihi huwa haina maana moja, nidhahili kuwa maana nyingine katika mifano hii imetolewa kulingana na muktadha wa kazi yenyewe au taarifa ilivyo kwenye magazeti.
Waandishi wa magazeti nchini Tanzania wanatumia misemo katika magazeti, kwanza ni kwa sababu ya kutaka siko la magazeti yao,hii ni kwa mujibu wa mwafunzi mmoja mwenye namba ya usajiri (2009-04-03894). Anasema kuwa waandishi hutumia misemo katika vichwa vya habari kwa kudokezea kile kitakachokuwa ndani ya habari yenyewe.Mfano ‘endelea na habari hii ndani upate uhondo’ ‘usijinyime uhondo huu’ Hivyo misemo hii imekuwa chanzo cha waandishi kuuza kazi zao. Mfano gazeti la SaniIjumaa, Kiu.
Pia kwa muuza gazeti katika kituo cha mabasi kilichoko ubungo jijini Dar es salaam namba ya simu 0713750941)  anasema kuwa amekuwa akiuza magazeti kwa muda mrefu na kusema kuwa magazeti yanayonunuliwa saana ni yale yenye maneno yanayovutia.
hivyo tukizingatia maoni na maelezo ya watu hawa tunaweza kukubaliana nao kwani tunaona maagazeti mengi yakitumia misemo mingi.   
                                                           12.
5.0.HITIMISHO:
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa misemo ni kipengele ambacho ni kipana sana kwani katika utafiti wetu tumegusia tu misemo bila kangalia dhima zake, fani na maudhui yake. Hivyo ni bora zaidi kufanyike uchunguzi mwingine ili kuweza kubaini vipengele hivyo vya fani na maudhui. Vile vile misemo mingi huanza kama misimu na ikitumiwa sana huweza kuwa na mashiko na kutumika maeneo tofauti.
                                                                       
                                                           13.
KIAMBATISHO
1.      Tibaijuka ang’aka.
2.      Nesi kitete ajikaanga.
3.      Kalenga aipiga tafu Vodacom miss Bagamoyo.
4.      Sarakasi za sitta Mwakyembe CCJ.
5.      Akili kuanika hadharani vielelezo walivyoshiriki.
6.      Vigogo CCM wakaangwa.
7.      Wafumania nyavu 10 kukumbukwa.
8.      UPDP kuunguruma Dar kesho.
9.      Ujamaa wampofusha Mkama.
10.  Azzan asiwe mbuzi wa kafara.
11.  Wizara ya elimu imulikwe.
12.  Takukuru inabweka lakini haing’at.i
13.  Gamba laCCM halivuliki, ibueni mafisadi.
14.  Mganda awasili kumvaa Mwakyembe.
15.  Nyota wa Man U walipoanika vifaa vyao.
16.  Mshiriki wa Tanzania BBA ajishebedua.
17.  Mbowe balaa Dar.
18.  Bimman abwaga manyanga.
19.  Wadai hukumu inanuka rushwa.
20.  CDA yakabwa koo na kamati ya bunge.
21.  Mwakalebela aibwaga TAKUKURU.
22.  Harambee ya Yanga yadoda.
23.  DC walimu wa shule za kata wasiitwe Vodafasta
24.  Ris wa zamani wa FIFA amkingia Blatter kifua
25.  Wamer amkaanga Bin Hamman
26.  Sauti ya radi awa makamu wa Rais
27.  Kujivua gamba hakutoshi
28.  Balozi wa Tanzania UK katikati ya mkutano.
29.  CCM itambue ugumu na urefu wa gamba.
30.  Mkata  tawi Gbagbo hakumsikiliza Odinga kawasikliza mijusi
31.  Basi lakanyaga kombe la Real Madrid
32.  Ulimwengu ndiye muuaji
33.  Kauli hizi za viongozi CHADEMA mauti yetu
34.  Mateja wageuza kituo cha mabasi ‘Gesti bubu’
35.  Kiburi chamuondoa duniani
36.  Spika Zitto jino kwa jino
37.  Kujivua gamba si ndoto ya mchana
                                                                      15.
38.  Tulivyozunguka kuitafuta vaselini Kampara
39.  Mashabiki wafurika kushuhudia majembe yao.
40.  Basena akunwa na beki wa Motema pembe.
41.  Wyne Rooney apandikiza nywele.
42.  Ngeleja kitanzini.
43.  Wanaume kuanza kumeza vidonge vya kuzuia mimba.
44.  Ikulu – viongozi wa dini si Malaika.
45.  Lady Jaydee kutembea uchi live.
46.  Kituo cha kuoshea nyeti za kike Dar.
47.  Wabunge wamchefua Spika Makinda awafananisha na watu wa kariakoo.
48.  CCM mnahangaika na Lowassa CHADEMA haoooo..
49.  Pinda hajui idadi ya mawaziri wanaoishi hotelini.
50.  Freemasoni na ugaidi ndani ya kanzu yabuislamu.
51.  Julio amtolea nje nyota wa Chelsea.
52.  Jenerali mchana nyavu ageuka balozi Japan.
53.  Mjadara wa posho waitikisa nchi.
54.  Dr. Slaa pakacha na chujio hayahifadhi maji.
55.  Abebwaye hukitazama kisogo cha ambebaye.
56.  Nani mwanamke shujaa ajitokeze tumuone?
57.  CCM ikiwatimua mapacha watatu tutawapokea AFP.
58.  Spika Makinda mbumbumbu asimamia asichokijua.
59.  Lowassa amkatia Kikwete rufaa.
60.  Munge arusha mpira Masijala.
61.   Mlema sijiudhulu ng’o.
62.  Bajeti iliyotolewa na Zitto haina masilahi kwa taifa.
63.  Ngono Big Brother sasa.
64.  Aliyezama baharini kusaka mwili wa osama aibukia patupu.
65.  Nilivyopiga ramli kumtafuta Mungu.
66.  Aki na Ukwa waja tena.
67.  Nilitema big ‘G’ kwa karanga za kuonjeshwa.
68.  Ray c akimbia nchi.
69.  Waziri, changu wateta kwa nusu saa Dom.
70.  Mainda, Steve Nyerere Mhhhh!.
71.  90% Mastaa wauza ngono bei cheee.
72.  Mrembo anaswa.
73.  Badra aanika chachandu zake adatisha midume.
74.  Asha Bakari vimwana Twanga pepeta ni zaidi ya miss.
75.  Mchumba aliyevua nguo shereheni.
76.  Lina sina mtu kwa sasa niko single.
                                                                              16.
77.  Belina alizwa viatu, atangaza dau.
78.  Kalala Juniour bifu za kijinga siyo ishu.
79.  Kuolewa si kila kitu dada’ngu vuta subila.
80.  Aliyemwaga radhi hadharani aachwa kwa taraka tatu.
81.  Jenifer Aniston amwenzi mbwa wake kwa totoo!
82.  Wanaomjua waanika siri zke.
83.  Mrembo anaswa akichimba dawa hadharani.
84.  Lina sina wakumpa penzi.
85.  Mbunge CHADEMA amlipua Sitta.
86.  Lowassa alizwa na kujiudhuru kwa Rostam.
87.  Mikopo ya elimu ya juu yaitafuna wizara ya elimu.
88.  Lowassa amlilia Rostam.
89.  Rostam adaiwa kumkejeli Kikwete.
90.  Ngeleja uso kwa uso na wabunge leo.
91.  Uamuzi wa Rostam kuachia ngazi watikisa nchi.
                                                                 17.

                                                                                                                                    iii.             
                                                            
                                                           MAREJEO.
Kihole, Y.M.(2004) Maswala ya kisarufi katika magazeti ya mitaani ya kiswahili: Tanzania.
              Mtandao www.ifeas-uni-mainz.de/SwaFo/SF11%20 kihore.pdf
King’ei, K.(2000) Matumizi ya Lugha kwenye vyombo vya habari. Kenya:  Mtandao
Mgazeti, Mtanzania, Kiu ya jibu, Ijumaa, Rai, Majira, Uhuru, Nipashe, Mwananchi, Bingwa,
             Mwananchi,Sani,: ya kuanzia Mei-Julai (2011).
Mulokozi .M.M.(1996)Utangulizi  wa  Fasihi. Dar  es  salaam:Taasisi  ya  Uchunguzi wa
               Kiswahili.
Wafula. R.M. na K.  Njogu (2002) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta
               Publishers Ltd.
Wamitila. K.W. (2006)Uhakiki wa Fasihi:Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi:Kenya Litho
                Ltd.
  www.landmark.edu/library/citation-guides/apa.cfm Iliyosomwa Tarehe 23 juni 2011 saa
                11:41
                                                                        14
 
Kidahizo ndiyo msingi wa kamusi. Fafanua kauli hii ukizingatia maumbo ya maneno yanayoweza kukaa katika nafasi ya kidahizo.
Swahili litajibiwa kwa kuligawa katika sehemu tofauti ili liweze kueleweka vizuri. Ambapo  tutaangalia maana ya kidahizo, maana ya kamusi, maelezo ya kina kuhusu kidahizo na kisha tutaangalia jinsi maumbo ya maneno yanavyoweza kukaa katika nafasi ya kidahizo.
Istlahi kidahizo imefafanuliwa na wataalamu wengi miongoni mwao ni pamoja na hawa wafuatao;
TUKI (1981) wanaafasili kidahizo kama neno linaloingizwa katika kamusi kwa chapa ilyokolezwa.
BAKIZA (2010) nao wanaeleza kuwa; kidahizo; ni neno linalochapishwa kwa hati zilizokozwa na pengine kutiwa rangi kwenye kamusi ambalo taarifa zake zinafanuliwa. Tunaweza kuwaunga mkono wataalamu hawa fasili yao kwani kidahizo huwa katika wino uliokolezwa na huingizwa katika kamusi ili kutolewa maana. Lakini kwa fsili ya jumla tunaweza kusema kuwa,
Kidahihizo ni neno linaloingizwa katika kamusi ili liweze kufafanuliwa kwa kupatiwa maelezo yanayohusu taarifa za kisarufi, maana, matumizi, etimolojia semi mbalimbali za lugha na nyingine.
Oxford (2010) wanaeleza kuwa; kamusi ni kitabu ambacho huwa kinaorodha ya maneno ya lugha fulani katika mpangilio wa alfabeti na huelezwa maana ya maneno hayo. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyopo katika mfumo wa eletroki kwa mfano yanaweza kuhifadhiwa katika kompyuta. Faslili hii ionekena kuwa na mashiko kwani kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia si sahihi tene kufasiri kamusi kama kitabu bila kuihusisha na elektroniki katika uhidhi wake.
Kamusi hutungwa ikiwa na malengo mbalimbali kulingana na mahitaji na matumizi ya taaluma au mtumiajia fulani. Mfano zipo kamusi za uwanja husika kama sheria, isimu, falsafa na nyingine. hivyo uteuzi wa msamiati hulingana na uwanja unaotungiwa ambapo kama ni uwanja wa jumla lazima tutakuta msamiati wenye lugha sahili au lahisi. Hivyo msamiati unaokusanywa na kuwekwa katika kamusi ili kufasiliwa ndiyo huitwa kidahizo. Vidahizo hufafanuliwa kwa kupatiwa taarifa za kina ili anayetaka taarifa hizo azipate bila utata wowote.
Katika kamusi za Kiswahili vidahizo huwa na maneno ya kawaida yanayotumika katika Nyanja mbalimbali za mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji wa Kiswahili. Msamiati unaoingizwa katika kamusi kama vidahizo hukusanywa katika sehemu tofauti  mfano machapisho mbalimbali, kama matini magazeti na vitabu mbalimbali.
Kidahizo kimegawanyika katika sehemu mbili yaani kidahizo huru na kidahizo mfuto. Hii ni kwa mujibu wa TUKI (2000). Kidahizo kikuu katika kamusi huwa ni umbo la msingi la neno. Mfano “lim.a” “li.a” wakati kidahizo mfuto, ni kinyambuo  kisichotumika sana au neno ambatani ambalo limeingizwa ndani ya maelezo ya kidahizo kikuu. Na kusoma maelezo ya maana ya kisarufi. Iwapo halitumiki sana au halijapata kutumika lakini likatumika tu kwa siku moja hupatiwa maana ya kisarufi tu. Kinyambuo cha kitenzi ambacho kina kategoria tofauti huingizwa kama kidahizo mfuto ndani ya umbo la msingi bila maelezo ya maana na kisha huingizwa tena kama kidahizo kikuu katika herufi ya alfabeti inayohusika.
Kidahizo kama msingi wa kamusi, hupangwa kwa kufuata utaratibu wa alfabeti. Kwa kila ukurasa neno la kwanza na la mwisho katika ukurasa limechapwa sehemu ya juu ya ukurasa ili kumwongoza msomaji atambue nafasi ya neno analohitaji au analotafuta, iwapo lipo katika ukurasa anaousoma au lipo nyuma au mbele ya ukurasa unaohusika maneno ya kumuongoza msomaji humwezesha kupitia kamusi na kugundua neno unalotaka kuliko kusoma ukurasa na kila kidahizo ili kupata neno unalotafuta.
Kidahizo ni msingi wa kamusi kwa kutokana nacho ndipo tunapata maana ya maana ya neno, etimolojia yake, matumizi na matamshi yake. Kwa hiyo bila kidahizo hatuwezi kuwa na kamusi. Msamiati wote unaokusanywa huwa ni kwa ajiri ya kutolewa maana katika kamusi ili kusaidia watumiajia wa lugha Fulani au wenye kuhitaji kujua msamiati wowote kutumia kamusi. Kwa hiyo naweza kusema hakuna kidahizo hakuna kamusi. Huo ndiyo umuhimu wa kidahizo katika kamusi.
Baada ya maelezo hayo mengi sasa tuone maumbo yanayoweza kutokea katika kamusi kama kidahizo.  Maumbo hayo ni kama haya yafuatayo.
Maumbo sahili; haya ni maumbo yanayoumbwa kwa neno huru yaani lisilo na utegemezi au lisiloweza kuambishwa.
                    Kwa mfano; maneno kama
                barua”,nyumba”, “bakuli” na “baba”.
Maneno haya ni huru. Hivyo maumbo haya huingizwa  katika kamusi kama kidahizo.
Maumbo ambatani; haya ni maumbo ya maneno ambayo huumbwa kwa kuunganisha maneno mawili tofauti, mfano nomino na kitenzi, nomino na nomino na mengine. Katka kamusi maneno haya huchukuliwa kama neno moja lenye kuwakilisha dhana fulani. Kwa mfano maumbo haya yametoka katika kamusi ya tuki (2001).
Kipeleleza-nyanbizi nm vi- [ki-vi-] asdic.
Kipazasauti nm vi- [ki-vi-] loud speaker.
Kipashamoto nm vi- [ki-vi-] chafing-dish.
Kipimahewa nm vi- [ki-vi-] barometer
Kitanguakimbanga nm vi- [ki-vi-] anticyclone
Maneno yote haya ni mwambatano lakini katika kamusi husimama kama neno moja na siyo kuwa tunaangalia maana ya neno moja moja. Hapa nisawasawa na maneno ya nahau, misemo nayo katika kamusi huchukuliwa kama neno moja lenye kuwakilisha dhana fulani. Mfano; TUKI (2001)
Kifungua kinywa,
 kick the bucket,
tia  nanga.
Maumbo changamani, ni maumbo ya maneno yanyokuwa na uchangamani. Ni maneno ambayo hayawezi   kusimama pekee katika kamusi. Maneno haya huwa na viambishi vinavyotenga mzizi wa  neno pia maneno haya hutengwa ili kuonesha uwezo wa kunyumbuliwa au kuchukua viamshi tofauti tofauti. Mfano;
M.toto 
M.tu
Nufaik.a
Nui.a
Maneno haya huweza kunyumbuliwa na kuleta maana nyingine tofauti na maneno sahili ambayo hayawezi kunyumbuliwa. Kwa mfano neno “nui.a” linaweza kunyumbuliwa na kupata maneno mengine kama, nuilia,nuilika, nuiana nuiza.
Maumbo hulutishi, haya ni maumbo ambayo kutokea kama kidahizo katika kamusi. Maneno haya huundwa kwa kuunganisha sehemu mbili za maneno tofauti na siyo kuunganisha maneno mazima. Kwa mfano;
Telephone
Mobitel
Telefax
Maumbo ya akronimia, haya ni maumbo yanayoingizwa katika kamusi kama kidahizo. Maumbo haya huwa katika ufupisho na huwakilishwa kwa herufi kubwa ambazo kila herufi hubaeba dhba Fulani. Mfano; kutoka Oxford (2006).
ISBN International Standard Book Number
ISA Industry Standard Architecture
ISDN Integrated Services Digital Network
SAD Seasonal Affective Disorders
Akronimia hizi hutokea upande wa kidahizo kuwakilisha maana  ama dhana iliyondefu kuwa katika maneno machache.
Maumbo rejerezi, katika kidahizo kuna maumbo ya maneno ya kumfanya msomajia arejelee neno jingine ili kupata ufafanuzi zaidi, maneno yanayorejelewa katika kamusi huoneshwa kwa mshale. Mshale huu ulenga kumuonesha msomaji kulitafuta neno analooneshwa. Kwa mfano;
Pally   → PAL
Pas.try  →see also CHOUX PASTRY
Pipe  → see also PIN PIPES
Mshale huu huwekwa baada ya kuwa taarifa zote kuhusu kidahizo hicho zimetolewa, na huenda kunahitajika maaelezo ya ziada kuhusu neno hilo kwa hiyo msomaji huoneshwa neno jingine kwa mshale ili aone tena maelezo hayo.
Maumbo dondoshi, haya ni maumbo ambayo huingizwa katika kamusi kama kidahizo baada ya sehemu ya neno hili kudondoshwa. Mfano wa maumbo hayo ni kama vile; kutoka katika Oxford (2006).
Phone kutokana na neno telephone
Gram kutokana na neno telegram.
Bike  kutoka na neno bicycle
Maumbo haya fupishi tunayakuta katika kidahizo cha kamusi na hubeba maana ambayo inapatikana katika neno zima ambalo halijafupishwa.
Maumbo radidi, haya ni maumbo ya neno linalojirudia rudia katika kamusi. Neno hili hubeba dhana  moja katika kamusi. Kwa mfano maneno kama,
Uramberambe nm [u-] coconut kernel
Mzengazenga nm mi-n[u-i] carrying two things by using a pole across the soulder
Mzikoziko nm mi [u-li- ] ipecacuanha.
Mnyunginyungi.
Maneno haya hubeba dhana moja inayowakilishwa na uradidi huo.
Maumbo mengine yanayoweza kuingizwa katika kamusi kama kidahizo ni maumbo ya homonimia. Maneno haya huwa na maumbo sawa na matamshi sawa lakini maana huwa tofauti. Katika kamusi huingizwa kama vidahizo vyenye maana tofauti na maana hizo hutofautishwa kwa kupewa namba.
Mfano
Kaa1.
Kaa2,
Kaa3
Panda1,
Panada2
Panda3
Vidahizo hivyo huonekana katika kamusi kama ilivyo mifano hapo juu.
Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema kuwa uorodheshaji wa vidahizo katika kamusi hutegemea lengo la kamusi. Mfano kama kamusi ni ya kisheria huorodhesha vidahizo vyake katika  misingi ya kiseria. Maana za msingi ndizo huorodheshwa kwanza na kufuatiwa na maana zilizozuka baadaye au maana zinazohusishwa na neno hilo. Kidahizo ni cha msingi katika kamusi kwani huonesha herufi rasimi zinazopaswa kuunda neno.
Marejeo
BAKIZA (2010) Kamusi ya Kiswahili Fasaha. Kenya: Oxford University Press.
Mdee, J. S. (2010) Nadharia na Historia ya Leksokografia. Dar es Salaam: TUKI.
Oxford (2010) Oxford Advanced Learner’s Dictionary. New York: Oxford University Press.
TUKI (2001) Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI (2006) English-Kiswahili Dictionary. Dar es Salaam: TUKI

Powered by Blogger.