SWALI: Fasihi simulizi siyo mali ya jamii nzima kama kale. Eleza
SWALI: Fasihi simulizi siyo mali ya jamii nzima kama
kale. Eleza
UTANGULIZI
Hapo kale fasihi simulizi ilipotendwa hadharani
iligeuka kuwa mali ya jamii nzima. Ndiyo maana hatujawahi kusikia nani
anamiliki methali hii ama wimbo huu nakadhalika. Fanani alipoitenda tu jamii
nzima ilikuwa huru kuitoa na kuitumia pahala popote pale.
Zama hizi hali imebadilika, watu ama vituo
mbalimbali vya habari na waimbaji mbalimbali huimba na kutangaza uhalali ama
umiliki wa wimbo husika. Mtu yeyote anayeuchuku au kuutoa hata nakala aweze
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Sayansi na teknolojia imeiondoa fasihi simulizi
kwenye dhana ya umiliki wa jamii nzima na kutuingiza katika mfumo wa kibepari
ambapo sasa, fasihi simulizi ni mali ya mtu binafsi. Hali hii inatokana na
sababu zifuatazo:
KIINI
Njia za uhifadhi wa fasihi simulizi kwa sasa
zinahusisha matumizi makubwa ya zana za kisayansi na kiteknolojia ambazo ni
ghali na hivyo msanii huingia gharama kubwa kuiandaa na kuikamilisha kazi ya
fasihi Gharama hizo huifanya kazi hiyo inapokamilika kuwa mali ya yule
aliyeingia gharama ambaye ni msanii.
Hali ya uchumi, kutokana na kushamiri kwa ubepari
hivi sasa kila mtunzi anafanya hivyo akilenga kujipatia pesa kupitia ubunifu
alionao, hali hii inaifanya fasihi simulizi kumilikiwa na mtunzi mwenyewe
kutokana na kazi husika kuwa chanzo cha kipato kwa mtunzi.
Kuibuka kwa matabaka katika jamii nako kunachochea
fasihi simulizi kuwa mali ya mtu binafsi kwa sababu wenye pesa hutumia nguvu
yao kiuchumi kushawishi watunzi kutoa burudani kupitia fasihi na kasha
kuwalipa, kuibuka kwa wasambazaji wa kazi za fasihi huchochea kuwepo kwa
watunzi wengi wanaolenga pesa na hivyo kuzidisha umiliki binafsi wa fasihi
simulizi.
HITIMISHO
Kwa ujumla umiliki wa fasihi simulizi kwa sasa umehama toka kwa jamii nzima hadi kwa mtunzi kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia katika jamii na kushamiri kwa ubepari duniani hali inayochochea kutafuta pesa kuwa ndio kipaumbele.