UANISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
TANZU ZA FASIHI SIMULIZI.
Utangulizi.
Fasihi Simulizi
imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwa waalamu hao ni M.M.Mulokozi
(1996) anasema Fasihi Simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na
kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi.
TUKI (2004) Fasihi
Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili.
Balisidya
(1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika
kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake.
Wanjara
(2011) anasema fasihi simulizi ni sanaa ambayo vyezo kuu ya utunzi,
uwasilishaji na usambazaji wake ni sauti pamoja na vitendo. Fasihi simulizi ni
sanaa inayotumia mazunguzo na vitendo kisanii ili kuwasilisha maarifa au ujumbe
Fulani kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Kwa
ujumla, fasihi simulizi nisanaainayobuniwa ikiwasilishwa na kusambazwa kwa
(lugha ya) mdomo, na vyombo vyake vikubwa ni mdomo na sauti ya binadamu katika
hali ya kuimba, kusimulia, kuiga ,kughani, kutamba na kutenga. Kama vile
vitendawili vinavyotegwa kwa hadhira.
Tanzu za fasihi simulizi
Tanzu ni
istilahi inayotumiwa kuelezea au kurejelea aina ya kazi mbalimbali za kifasihi,
inawezekana utanzu mkuu kuwa na vitanzu vingine mbalimbali.
Tanzu
za fasihi simulizi ni nyingi na si rahisi kuzianisha zote. Waandishi wafuatao
wamejadili tanzu kadhaa za fasihi simulizi kama ifuatavyo:-
M.M.Mulokozi
katika makala yake ya tanzu za Fasihi Simulizi iliyo katika jarida la Muulika
namba 21(1989) amezigawa tanzu na vipera vya Fasihi Simulizi kwa kutumia vigezo
viwili ambavyo ni,kigezo cha kwanza ni umbile na tabia ya kazi inayohusika na
kigezo cha pili ni muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira. Umbile
na tabia ya kazi inayohusika: katika kigezo hiki Mulokozi ameangalia vipengele
vya ndani vinavyoiumba sanaa hiyo na kuipa muelekeo au mwenendo. Baadhi ya
vipengele hivyo vya ndani ni namna lugha inavyotumika (kishahiri, kinathari,
kimafumbo, kiwimbo na kighani), muundo wa fani hiyo na wahusika. Kwa upande wa
muktadha na namna ya uwasilishaji amezingatia kuwa, Fasihi Simulizi ni tukio
hivyo huambatana na muingiliano wa mambo matatu ambayo ni muktadha, watu na
mahali. Mwingiliano huu ndio unaotupa muktadha na muktadha ndio unaoamua fani
fulani ya Fasihi Simulizi ichukue umbo lipi, iwasilishwe vipi kwa hadhira,
kwenye wakati na mahali hapo. Hivyo hadithi inaweza kugeuzwa wimbo, utendi unaweza
kuwa hadithi na wimbo unaweza kugeuzwa ghani au usemi kutegemea muktadha
unaohusika.
Mulokozi
ameanisha tanzu sita za fasihi simulizi kama ifuatavyo :-
i.
Mazungumzo
ii.
Masimulizi
iii.
Maigizo (drama)
iv.
Ushairi
v.
Semi
vi.
Ngomezi (ngoma)
Mazungumzo
ni maongezi au maelezo yam domo katika lugha ya kawaida juu ya jambo lolote
ile. Si kila mazungumzo ni fasihi mazungumzo ili yawe fasihi lazima yawe na
usanii wa aina Fulani na uhalisia baada ya kuunakili.mfano tanzu zinazoingia
katika fungu la mazungumzo ni kama hotuba, malumbano ya watani, ulumbu,soga na
mawaidha.
Masimulizi
ni fasihi yenye kusimulia habari Fulani Mulokozi (1989) anasema kuwa masimulizi
ni fasihi ya kihadithi na fani zake huwa na sifa kama kuelezea tukio katika
mpangilio Fulani mahususi, huwa na wahusika yani watendaji.Katika Mulika 21
Mulokozi amegawanya fasihi simulizi katika tanzu zifuatazo za kihadithi ambazo
ni ;ngano,visakale,tarihi, istiara,mbazi na kisa.
Semi
ni tungo au kauli fupifupi zenye kubeba maana Fulani au mafunzo muhumu katika
jamii, Mulokozi ameanisha tanzu semi kama ifuatavyo;
methali,mafumbo,vitendawili.
Ushairi
ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa
na vina ushairi una ufasaha wa maneno au muktasari wa mawazo na maono ya
ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu. Ushairi hupambanuliwa na lugha ya
kawaida kwa kutumia lugha na mbinu za kimuktadha. Mulukozi (1989) amegawa
ushairi katika mafungu mawili ambayo ni nyimbo na uwasilishaji.
Maigizo (drama)
ni sanaa inayotumia watendaji kuiga tabia au matendo ya watu na viumbe wengine
ili kuburudisha na kutoa ujumbe Fulani. Maigizo ni sanaa inayopatikana katika
makabila mengi. Mulokozi anasema drama (maigizo) ya kiafrika huambatana na
ngoma mtambaji wa hadithi au matendo ya kimila.
Ngomezi
ni midundo Fulani wa ngoma kuwakilisha kauli Fulani katika lugha ya kabila hilo
mara nyingi kauli hizo huwa ni za kishairi au kimafumbo.
Nae
Wanjara (2011) anaainisha tanzu mbalimbali za fasihi simulizi ambazo ni
zifuatazo :-
i.
Hadithi za kihistoria
ii.
Hadithi za kubuni
iii.
Ushairi (nyimbo)
iv.
Semi
v.
Maigizo
vi.
Mazungumzo
vii.
Ngomezi.
Ndungo
na wangali, wao wanaziainisha tanzu tano za fasihi simulizi wanaanza na :-
i.
Hadithi
ii.
Ushairi na nyimbo
iii.
Sanaa za maonyesho
iv.
Methali
v.
Vitendawili.
Njogu
na Chimera (1999) anaanisha tanzu zifuatazo za fasihi zifuatazo za fasihi
simulizi:-
i.
Hadithi
ii.
Nyimbo
iii.
Methali
iv.
Vitendawili
Nyambari na Masebo (2007) wanaainisha tanzu zifuatazo
za fasihi simulizi ambazo ni hadithi,
semi, ushairi na sanaa za maonesho.
Wataalamu
wote wana mitazamo inayoendana katika kuainisha tanzu za fasihi simulizi, baada
ya kutambua mawazo yao sasa ni vyema kutumia nafasi hii kuziweza tanzu hizi
katika makundi jumuishi manne (4) ambayo ni `:-
FASIHI SIMULIZI
|
|||
HADITHI
|
SEMI
|
USHAIRI
|
SANAA ZA MAONYESHO
|
Ngano
|
Methali
|
Nyimbo
|
Majigambo
|
Tarihi/visakale
|
Vitendawile
|
Maghani
|
Tambiko
|
Visasili
|
Misimu
|
Ngonjera
|
Miviga
|
Soga
|
Mafumbo
|
Michezo ya watoto
|
|
Visoga
|
Lakabu
|
Ngoma
|
|
Misemo
Mizungu
|
Utani
Ngonjera
Vichekesho
Jukwaani
|
Hadithi
Ni
tungo za fasihi simulizi zitumiazo lugha ya nathari (lugha ya ujazo ya maongezi
ya kila siku). Mtiririko wa matukio ndio unaotawala masimulizi. Hadidhi
hizozaweza kuwa ngano zitumiazo wahusika kama wanyama,miti na watu kueleza au
kuonya kuhusu maisha, tarihi ni hadithi zinazohusu matukio yaliyotendeka
zamani; visasili ni hadithi ambazo huwa na wahusika wa aina tofautitofauti
ambao ni bapa hasa miungu na binadamu husimulia uu ya matukio ya kiada, vigano
ni hadithi fupi zinazoeleza makosa au uovu wa watu Fulani na kueleza maadili
Fulani; soga huumuisha hadithi ndogondogo ambazo huteta utani vilevile huwa na
ucheshi.
Hivyo
tunaona kuwa hadithi huumuisha tungo yeyote ya kubuni inayosimuliwa kwa lugha
ya nathari.
Mfano,mfano
katika fasihi simulizi ni za aina nyingi lakini zote huanza kwa njia moja
inayofuata mtindo huu.
Msimulizi : paukwa!
Wasikilizaji : pakawa!
Msimulizi : paukwa!
Wasikilizai : pakawa!
Msimulizi : hapo zamani za
kale…………..
Semi
Ni
tungi au kauli fupifupi za kisanaa zenye kubeba maana au mafunzo . kigezo
kilichotumika kugawa utanzu huu ni kigezo cha lugha ambacho ni lugha ya mkato
na kigezo cha kidhima ambacho hufunza mfano methali, vitendawili, misimu,
mafumbo, lakabu, missemo na nahau.
Ushairi
Ni
utungo unaojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo kwa utaratibu maalumu.
Mapigo ya kimziki, mathalani mapigo hayo yanaweza kupangwa kwa muala wa urari.
Hivyo basi ushairi huweza kuwa wa namna tofautitofauti kama vile nyimbo,
maghani na ngonjera. Katika vipera hivi zinakusudiwa ni zile zinazotungwa kwa
mdomo( bila maandishi) na kusambazwa kwa mdomo.
Sanaa za maonyesho
Katika
kudadavua zana ya sanaa ya maonyesho ni vema kujua dhana ya sanaa ya yenyewe.
Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa; umbo ambalo mtu
hulitimia kuelezea hisia zinazo mgusa kwa kutolea kielelezo/vielezo vyenye
dhana maalumu. sana za maonyesho ni
sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo ambalo linaweza kuifadhiwa na
uzuri wake huonyeshwa wakati wote. Sanaa hizo ni kama vile uchorai, utalizi,
ufinyanzi na uchongaji.
Hivyo
basi sanaa za maonyesho hujumuisha
vipera kama vile majigambo, tambiko, miviga, ngoma, utani, ngonjera,
vichekesho, michezo ya jukwaani ya watoto.
MAREJELEO
Mulokozi,
M.M. (1996). Utangulizi wa Fasihi
Simulizi ya Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam.
Mulokozi,M.M.
(1989).Tanzu za fasihi simulizi.Mulika.21:1-24.Dar-es-salaam.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Toleo la
Pili). East Africa: Oxford University Press
na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
(TUKI).
Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Focus Publications Ltd.
Nairobi.
Wamitila,K
W (2003) Kichocheo cha fasihi simulizi: Focus Publications Ltd.
Nairobi