TAFSIRI NA UKALIMANI NI TAALUMA MUHIMU SANA ULIMWENGUNI
DHANA YA
TAFSIRI
Kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake
(2006) wanaeleza kuwa tafsiri ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika
maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine. Woa wanatilia mkazo katika zoezi la
uhawilishaji na kinachohawilishwa ni mawazo katika maandishi.
Pia Catford (1965) anaeleza kuwa,
kutafsiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha mmoja yaani
lugha chanzi na kuweka badala yake mawazo yanayolingana kutoka katika lugha
nyingine yaani lugha lengwa. Hapa msisitizo upo katika matini zilizoandikwa na
kuzingatia zaidi ujumbe au wazo lililopo katika matini chanzi lijitokeze vile
vile katika matini lengwa. Mawazo haya hayawezi kuwa sawa kabisa na ya matini
chanzi bali ni mawazo yanayolingana toka matini chanzi na matini lengwa, hii ni
kutokana na sababu tofauti kama vile utamaduni, historia, kiisimu na mazingira.
Naye Newmark (1982) anaeleza kuwa
tafsiri ni mchakato wa uhawilishaji wa maneno kutoka matini chanzi kwenda
matini lengwa.
Pia Nida na Taber (1969) wanaeleza
kuwa tafsiri hujumuisha kuzalisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutumia
visawe vya asili vya lugha lengwa vinavyo karibiana zaidi na lugha chanzi
kimaana na kimtindo. Wao wanatilia mkazo uzalishaji upya wa kwa kutumia visawe
asili vinavyokaribiana na matini chanzi kimaana na kimtindo. Kutokana na maana
hizi tunaweza kusema kuwa tafsiri hufanywa katika ujumbe uliopo katika maandishi,
ni jaribio la kiuhawilishaji na wazo linalatafsiriwa huwa na visawe
vinavyokaribiana na sio sawa kutokana na tofauti za kiisimu, kihistoria,
kiutamaduni na mazingira.
Kwa
ujumla tunaweza kusema
Tafsiri ni
taaluma inayohusika na
uhaulishaji wa mawazo
kutoka lugha chanzi
kwenda lugha lengwa
kwa maandishi bila
ya kupoteza , kupotosha na
kubadili maaana .mawazo yanayoshugulikiwa katika
taaluma ya tafsiri
sharti yawe kwenye
maandishi na yalingane
kati ya lugha
lugha asilia na
lugha lengwa.
AINA ZA
TAFSIRI
Tafsiri ya
neno kwa neno ,
Hii ni tafsiri
amboyo mofimu na
maneno mengine hufasiriwa
yakawa pwekepweke kwa
kuzingatia maana zake
za msingi bila
kujali muktadha. Mpangilio wa mofimu na
lugha chanzi hubaki
vilivile , maneno
yanayofungamana na utamaduni
hufasiliwa kisisisi .matini ya
tafsiri (matini lengwa) huwandikwa
chini ya matini
ya lugha chanzi
Mfano (1) Kiswahili : a – li – lala – hadi –asubuhi
Kiingereza : she /past /sleep/ until / morning
(ii) kiwahili : a
-likwenda / nyumbani / kwke
Kiingereza : he / past / until /at /house /his.
Ø Ubora wa
tafsiri neno kwa
neno
Tafsiri
ya
aina hii humsaidia
kumsaidia kuelewa jinsi
lugha inavyofanya kazi katika
kuanisha muundo
Ø Udhaifu wa
tafsiri ya moja kwa
moja
Upungufu wa
tafsiri ya neno
kwa neno ni
kwamba mara nyingi
haitoi kwa uangavu
maana inayokusudiwa kwa
sababu nahau na
misemo inayohusika na
utamaduni hufasiliwa kisisisi.
sababu nahau
na misemo inayohusika
na utamaduni hufasiliwa
kisisisi.
Tafsiri sisisi
Kwenye
aina hii ya
tafsiri maneno hufasiliwa
yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia maana
zake za msingi
katika lugha chanzi bila
kujali sana muktadha . lakini kufuatana
na mfumo wa
kisarufi ,hususani sintaksia ya
lugha lengwa
Mfano
kiingereza :He was
taken a centrel
police station
kiswahili : Alipelekwa kwenye
kituo cha kati
cha police ( badala ya
kituo
kikuu cha police)
kiingereza :Dear
listener , lend me your
ears
kiswahili : Wasikilizaji wapendwa , niazimeni masikio
yenu (badala ya naomba
mnisikilize.
Mfano Kiingeza
: Two heads are
better than one
Kiswahili : Mbili
vichwa ni bora
kuliko moja .(badala yake
vichwa viwili ni
bora
kuliko kichwa
kimoja
Kizaramo : Zege dimlemelwe fisi ,mbwa
domgela muhe.
Kiswahili : Mfupa uliomshinda fisi
mbwa utampa pumu
Ø Ubora wa
tafsiri sisisi :
Tafsiri
hii husaidia sana
mfasiri kuwa hakuna maaana
ya kudumu ya maneno , bali
maana halisi .Kutokana na
matumizi yake katika
muktadha maalumu aidha
aina hii ya tafsiri hutumika
sana katika tafsiri
ya vichekesho kwani
huibua ukinzani wa
ajabu katika tungo .(Mfano; My name is Dr Livingstone I
come from Johanesberg
Ø Upungufu wa
tafsiri sisisi : Tafsiri
sisisi agharabu hutoa
tafsiri potofu na kwa hiyo
huwa na uwezekano
wa kuleta utata
na hasara katika
mawasiliano
Tafsiri
ya kisemantiki/maana/uwazi/(semantic
trasilation) hii ni aina ya tafsiri ambayo mfasiri
huegemea zaidi kwenye kugha chanzi. Katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hufasiri
kila neno katika sentensi jinsi ilivyo ila kwa kufuata sarufi hususani
vipengele vya kisemantiki na kistakisia ya lugha chanzi.Katika aina hii ya
tafsiri masahihisho au ya neno au jambo lolote unalodhani limekosewa
haliruhusiwi isipokuwa uweza kuweka haya marekebisho hayo au ufafanuzi katika
tanbihi. (mujibu wa( Catford na Nida 1965)
Mfano
: Kizaramo :
kihanga cha mkulu
kilava nongo ya ugimbi.
Kiswahili : uso
wa mkubwa umetoa
mtungi wa pombe
Kizaramo :ngwengwe
hadisolo jake
Kiswahili : dume
la njani huwa
na mamlaka zaidi
katika eneo lake
Ø Ubora wa
tafsiri
:
Ubora wa
tafsiri ni kuwa
na uwezo mkubwa wa
kuendeleza lugha legwa kwa kuingiza
miundo na misemo
toka lugha asilia .
Ø Udhaifu wa
tafsiri
:
tafsiri
hii haitilii maanani
nahau , misemo maalumu inayohusiana
na utamaduni na
lugha inayolengwa katika
tafsiri . Mfano (Assaina married
Mtillah. –kiwahili :Assaina
alimuoa Mtillah) badala Asha
kuolewa na Moses
kwani katika Kiswahili mwanamke
huwa anaolewa na
mwanaume ndiye anaoa
hii huweza kuleta
utata katika lugha
ya kiwahili kwa
mwanamke ndiye kuoa
na mwanaume kuolewa.
Tafsiri
ya kimawasiliano ,
hii ni
aina ya tafsiri
ambayo huzingatia hadhira ya
matini ya lugha
lengwa kwa kumjali
sana msomaji wa
matini hiyo . hii ni
tafsiri huru kwa
sababu mfasiri anaweza
kuongeza au kupunguza
maneno ya matini
ya lugha asilia wakati
wa kufasili ili
mradi ujumbe uwafikie
kwa namna inayotakiwa
na bila kupoteza
wazo la matini
ya lugha asilia, mfasiri ana
uhuru wa kutafuta
maneno au mafungu
ya maneno yanayolingana
na nahau,misemo ,methali ,
utamaduni na mazingira
ya lugha lengwa
Ø Ubora wa
tafsiri mawasiliano
Ubora wa
tafsiri hii ya
kimawasiliano ni kwamba
hufuata kanuni taratibu
na sheria za
lugha lengwa na
kuzingatia mweelekeo wake
wa kiutamadudi ,kiistoria
,kimazingira na kijamii
kwa hadhira lengwa
Mfano
Kiingereza : Veronika
married chris
Kiswahili :chris
alimuoa veronica
Ø Udhaifu wa
tafsiri mawasiliano
Kutokuwa na
uwezo wa kuendeleza
,kuingiza miundo au
misemo kutoka lugha
asilia kwenda katika
lugha lengwa. Hali hii
inatokana na ukweli
kuwa tafsiri hii
haizingatii miundo ,misemo ,
na msamiati wa
lugha asilia wakati
wa kufasiri bali
huzingatia wazo la
jumla la kiutamaduni kwa
lugha lengwa
Udhaifu mwingine
katika tafsiri ya
kimawasiliano hujitokeza
pale mfasiri anapoegea
sana kwenye mawzo , historia ,utamaduni , mazingira na
itikadi ya lugha
lengwa . kwa mfano katika
mwaka 2002 vyombo
vya habari vilisikika
vikitangaza
Mfano
kiingereza : His excellency
president saddam Hussein
(vyombo vya habari
vya
Iraq mwaka
2002)
Kiswahili :Gaidi
saddam Hussein ( vyombo
vya habari vya
marekani mwaka 2002
Kutokuwa na
uwezo wa kuendeleza
,kuingiza miundo au
misemo kutoka lugha
asilia kwenda katika
lugha lengwa. Hali hii
inatokana na ukweli
kuwa tafsiri hii
haizingatii miundo ,misemo ,
na msamiati wa
lugha asilia wakati
wa kufasiri bali
huzingatia wazo la
jumla la kiutamaduni kwa
lugha lengwa
Udhaifu mwingine
katika tafsiri ya
kimawasiliano hujitokeza
pale mfasiri anapoegea
sana kwenye mawzo , historia ,utamaduni , mazingira na
itikadi ya lugha
lengwa . kwa mfano katika
mwaka 2002 vyombo
vya habari vilisikika
vikitangaza
Mfano
kiingereza : His excellency
president saddam Hussein
(vyombo vya habari
vya
Iraq mwaka
2002)
Kiswahili :Gaidi
saddam Hussein ( vyombo
vya habari vya
marekani mwaka 2002)
MAREJEREO
Catford
J.C. (1965) A Linguistic theory of
Translation: OUP London.
Mwansoko, H.J.M. na wenzake (2006) Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu:
TUKI
Dar es Salaam.
Newmark, P. (1988) A Textbook of Translaton. : Prentice
Hall London.
Nida, A. E. na Charles, R. T. (1969) The Theory and Practice of Translation.
The United
Bible Societies:
Netherlands.
Wanjala S. F (2011) Misingi ya ukalimani na tafsiri;
Serengeti Education publisher (T)
L.T.D. Mwanza Tanzania