TANZU ZA RIWAYA KATIKA KISWAHILI

 
 DHANA YA RIWAYA
Riwaya ni hadidhi ndefu ya kubuni yenye mawanda mapana , lugha ya kinathari , mchanganyiko visa na dhamira, wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa kimantiki, yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na maisha halisi.( Masebo J A & Nyangwine N)
Encyclopedia Americana (EA) , Jz . 20 , (1982 :510f) inasema ni : “prose fiction of book length” – hadithi inayotosha kuwa kitabu.
Kwa ujumla
Riwaya ni hadithi ndefu yenye kujitosheleza kimaudhui na kifani yenye kushabiana na kusawili maisha halisi ya jamii lengwa kwa wakati Fulani.
TANZU ZA RIWAYA.
Kwa mujibu wa M.M.Mulokozi(1996),Tanzu ni matawi au aina mahususi za sanaa Fulani.Wataalamu mbalimbali wamejaribu kuainisha riwaya kitanzu.Katika uainishaji huo wengi wao wamejaribu kuainisha tanzu za riwaya kwa kutumia kigezo cha maudhui (kidhamira) na kifani.
Kwa kutmia vigezo hivyo,kuna michepuo miwili ya riwaya,kuna riwaya dhati na riwaya pendwa.
riwaya ya dhati
Ni riwaya yenye kuchimbua matatizo au masuala mazito ya kijamii, kutafuta sababu zake, athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake.Ni riwaya inayolenga kumkela na kumfirisha msomaji,sio kumstarehesha tu.Ndani ya riwaya ya dhati kuna matawi yake kama yafuatayo;
Riwaya za wasifu ;
ni maelezo yanayoandikwa kisanaa kuhusu mtu mwingine . riwaya hizi mara nyingi hutoa sifa za mtu Fulani na mara nyingine huandika mambo yake mazuri tu . mfano wa riwaya hizi ni kam vile Wasifu wa Siti bint saad – Shaaban Robert , Mukwawa na kabila lake – Michael Musso .
Misingi ya kimaudhui ;
Msisitizo unakuwa katika matukio Fulani katika maisha ambayo mwandishi anadhani ni ya kusisimua na hayajatokea kwa wengi .lengo ni kueleza ugumu wa maisha ya mhusika mkuu jinsi alivyopambana nayo na kuyashinda ili kuwatia hamasa wasomaji.
Misingi ya kifani ;
mwandishi anaweza kutumia nafsi ya tatu katika masimulizi yake ijapokuwa hata hivyo atakuwa na matatizo ya kuingia katika undani wa nafsi na anayesimuliwa yaani hata msomaji anaweza kupata kitu Fulani kutoka katika kazi hiyo.
Riwaya ya kijamii (sociological novel).
Hii ni riwaya inayosawairi maisha na matatizo ambayo huwa ni ya kifamilia,kimahusiano,ya kitabaka,ya kisiasa,ya kiutamaduni,pia mkazo wa masuala ya mila na destiri ya jamii.
Msingi ya kidhamira
Utanzu huu wa riwaya huwa na msingi wa kdhamira ambao hulenga maudhui katika jamiii kama vile : ujenzi wa jamii mpya , mngongano kati ya ukale na usasa , migongano ya kijamii kama motto na wazazi , jamii na jamii nyingine , hali ngumu ya maisha . suala la umaskini na matabaka . dhamira hizo zinaweza kuwa za kifamilia na kupanuka kuwa za kitaifa na hata ulimwenguni riwaya hizi hueleza matatizo na suruhu ya matatizo hayo.
Msingi wa kifani
Mwandishi anakuwa na muundo wa mbinu ya kuchagua mambo , maelezo ,matukio au sehemu ya maisha ya binadamu na kisha kuyaunganisha pamoja kuwa hadithi moja .vilevile wahusika mara nyingi huwa halisi ambao hukuwa kimawazo ,kimatendo na kisaikolojia . mfano
Nyota ya rehema ;- M S mohammed
Rosamistika ;- E. kezilahabi
Titi la mkwe ;- Alex Banzi
Riwaya ya kisaikologia
Hii ni riwaya inayododosa au kuhusu nafsi ya mhusika , fikra , hisia , mawazo , imani , hofu na mashaka yake binafsi na athari ya mambo hayo kwake binafsi na labda jamii yake kinafsi kiakili na kijinsia .
Msingi wa kidhamira
Maudhui yake hulenga kuonyesha uwezo na udhaifu wa binadamu katika kuzikabili hali ngumu za maisha , hujumuisha matumaini ya binadamu katika kuyaishi maisha , mateso na furaha ambavyo vinaweza kusababishwa na kosa , wizi , mauaji , njaa na ugonjwa . migogoro ya kinafsia pia mgongano kati nafsi na mambo ya nje ya jamii .
Msingi wa kifani
Mhusika mara nyingi husukwa katika ukingo wa kuamua kati ya kufa ili kuyaepuka matatizo au kuishi. Matatizo yaliyo mengi hutokea akilini mwa wahusika pia muundo wa matumizi ya mazungumzo ya kibinafsi
mfano Kiu – M S Mohammed
Nyota ya rehema - M S Mohammed
Riwaya ya kiimadili
Hii ni riwaya ambayo inawapa watu maadili mema na wakati mwingine maadili hayo ni ya kidini . mara nyingi maadili haya huwa na msingi wa kufundisha mwenendo mwema katika maisha ya kila siku.
Msingi wa kidhamira
Utanzu huu mara nyingi hulenga kuelezea mambo ya kiimadili . huwa na dhamira kama “ matendo mema kwa wenye shida kama wazee na watoto , mateso na uvumilivu , uamuzi wa busara , kufunza utii na kuheshimu wakubwa
Msingi wa kifani
Riwaya huchukua muundo wa safari ,methali hutumiwa kama msingi wa hadithi nzima mfano Rila na Fila. Huwa na wahusika wanaokuwa na sifa za kudumu.
Mfano Adili na Nduguze - Shaaban Robert
Mtu ni utu - G. Mhina
Mrima asali na wenzake wawili - M mnyampala
RIWAYA PENDWA
Ni riwaya iliyokusuda kuwastarehesha na kuburudisha msomaji tu . lengo lake hutimizwa kwa kusawili visa na vituko vya kukusisimua damu kama vile ujambazi na uhalifu , ujasusi , upelelezi na mahaba ya waziwazi .rwaya hizo huwa na mafunzo kidogo kama lengo la ziada na masuala ya mapenzi uhusishwa zaidi.katika Tanzania riwaya hii ililetwa kwa mara ya kwanza na M S abadallah alipoandika riwaya “ mizimu ya watu wa kale”.
Riwaya pendwa ina matawi yake kama . riwaya ya mahaba ,uhalifu au ujambazi ,upelelezi na ujasusi.
Riwaya ya upelelezi
;hii huwa na vitu viwili kosa au uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mharifu anapopatikana ,hivyo wahusika huwa wahalifu wadhulumiwa (waliotendewa kosa) .Riwaya hizi zimeandikwa kwa mara ya kwanza na M .S Abdullah mfano wa riwaya hizi ni kama vile mzimu wa watu wa kale , kisima cha giningi na kosa la bwana musa – M .S Abdullah
Misingi ya kidhamira ;
riwaya hizi huwa na lengo au dhumuni kuonyesha matukio ambayo ni ya kiupelelezi na jinsi polisi wanavyofanya na kupambana na matukio ya kihalifu na kuhakikisha kwamba matukio yote ya kiharifu yanakomeshwa .
Misngi ya kifani ;
riwaya hizi hutumia wahusika ambao wameonekana mahili katika kutafuta chanzo cha uhalifu na kutafuta mbinu mbadala za kuondoa uhalifu unaotokea .
Riwaya ya mahaba
Ni aina ya riwaya ambayo husawili mahusiano ya kimapenzi kati ya msichana na mvulana au mwanamke na mwanamme pia kuna zinazoeleza mapenzi ya jinsia moja ( mashoga) . Riwaya hizi hupendwa sana na wasomaji ambazo mara nyingi ni vijana.
Msingi wa kidhamira
Maudhui yake hushamiri dhamira ya kimapenzi na ndio huwa dhamira kuu inayotawala wahusika wote . kila mhusika hubeba uhalisia wa kimahaba ndani ya kazi ya fasihi .
Msingi wa kifani
Muundo wa ke huwa na mtiririko unaofuatika wawahusika na matukio pia hutumia wahusika walewale na mandhari yanayoundwa kwa namna ya pekee.
Mfano mwisho wa mapenzi -S D kiango
Jeraha la moyo - S D kiango
Riwaya ya uhalifu
Ni riwaya zinazosimulia vituko vya kihalifu kama wizi ujambazi , uuwaji , magendo na utapeli. Mara nyinyi hujiusisha kuelezea uhalifu ndani ya jamii
Msingi wa kidhamira Maudhui yake hutawaliwa na dhamira ambazo mara nyingi huelezea matendo ya kiovu ndamni ya jamii kama vile suala la wizi , unyanyasaji , dhuruma , suala la mauaji na suala la magendo
Msingi wa kifani Wahusika wake hujengwa kutokana na matukio ya jamii kama majambazi ,wezi ,wauwaji ,matapeli ambapo mwandishi hutumia majina kuwakilisha watu wa aina hiyo.
Mfano kwa sababu ya pesa - J Simbamwene na Buriani -H katambula
                                                         MAREJELEO
Madumila, J.A. (2009),Riwaya ya Kiswahili,Nadharia Historia na Misingi ya Uchambuzi.Dar-es-Salaam:Mture Education Publishers.
Masebo, J.A & Nyangwine, N.(2007), Nadharia ya Fasihi (Fasihi kwa Ujumla).Dar-es-Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers. 

Mulokozi, M.M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili.Dar-es-Salaam.Chuo Kikuu Hulia cha Tanzania.
Powered by Blogger.