DHANA YA VITAMKWA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
UTANGULIZI
Vitamkwa, ni
neno linalotokana na kitenzi ‘Tamka’ ambalo
lina maana ya kitendo cha kutoa nje ye kinywa au pua ya mwanadamu sauti ambazo
hutumika katika mazungumzo au usemi wowote uwao. (Kihole, Masamba na Hokororo,
2003).
Hivyo
basi, vitamkwa ni sauti ambazo hutolewa na binadamu kupitia katika chemba ya
kinywa na chemba za pua kwa kufuata
utaratibu maalumu. Utaratibu huu huhusu namna au jinsi ya kuzitoa sauti hizo na
mahali pa kutolea sauti hizo.
Mfano: [ p ] + midomo – mahali
[ p ] + midomo ishikane na
kuachana
Lakini
pia sauti hizi zitamkwazo zaweza kuwa ni
konsonanti na irabu (vokali).
Mfano: [ b ], [ d ] kama konsonanti na [ e ],[ u ],[
i ] kama vokali au irabu.
Vitamkwa,
ni sauti zitumikazo katika lugha fulanina hujumuishwa kwa jina la Alfabeti
ambazo ndani yake kuna konsonanti na irabu.
Mfano: a, b, c, d, e, f.
Kuna
baadhi ya wataalamu mbalimbali ambao wameelezea sifa za vitamkwa na baadhi ya
wataalamu hao ni pamoja na Romani Jackobson na Nikolaji Trubertzkoy.
Roman Jakobson,Ni
raia wa Urusi(Russia) alizaliwa October 11,1896,Moscow na alifariki July18,1982.Cambrige
alikuwa mwalimu wa Linguistic na ni mmoja wa waanzilishi wa Prague kwa
kushirikiana na Halle walibainisha sifa Kinzani za lugha katika makund imawili
,Konsonanti na vokali na baadae makundi madogo manne Konsonanti
halisi,Vokali,Vitambaza naViyeyusho kwa kutumia Nadharia ya Sifa Pambanuzi
Nikolaj Trubertzkoy,huyu
nae ni raia wa Urusi(Russia) Alizaliwa
April,16,1890 mjini Moscow na kufariki
June,25,1938 alikuwa mwalimu wa masomo ya Historian a Kiingereza katika
vyuo vikuu vya Moscow,Vienna na Sofia nchini urusi pia alikuwa mwanzilishi wa
mawazo ya Prague.Mwaka 1969 alibainisha sifa za vitamkwa kwa kutumia Nadharia
ya Upambanuzi au Nadharia ya Ukinzani Pambanuzi .zifuatazo ni tofauti za sifa za
vitamkwa zilizoelezwa na Nikolaj Trubertzkoy na Roman Jakobson.
Trubertzkoy,
alizibainisha sifa za vitamkwa kifonetiki na kifonolojia lakini alijikita zaidi
katika Fonetiki kwani katika upambanuzi wake ametumia lugha mbalimbalikama;
Kiingereza,Kijerumani na Kiswahili.Ilhali Jakobson alipendekeza sifa
za vitamkwa kifonetiki na kifonolojia
lakini alielemea zaidi katika sifa za vitamkwa kifonolojia katika lugha ya
Kiswahili.Ambapo alielezea Konsonanti na Vokali za Kiswahili.
Nikolaj
Trubertzkoy,ametumia Nadharia ya upambanuzi Wakati Jakobson alitumia
Nadharia ya Sifa Pambanuzi.
Katika Nadharia ya Upambanuzi, Trubertzkoy
madai yake ya msingi ya Nadhari yake ni kwamba pakiwa na Upambanuzi basi lazima
patakuwepo na ukinzani.kwa mfano Ukinzani wa kiuwili ambapo jumla ya sifa
bainifu zinazochangiwa na sauti mbili kinzani hupatikana katika sauti hizo
mbili peke yake na si kwingineko.Mfano Vipasuo vya mdomo [P] na [b] katika
Kiswahili ambavyo vinachangia sifa ya Vipasuo vya midomo, hakuna vipasuo
vingine vinavyochangiansifa hiyo.Lakini Katika Nadharia ya Sifa
Pambanuzi yake Roman Jakobson, anabainisha sifa za Kimatamshi dhidi ya Sifa
Kiaukustika.Kwa mfano katika sifa za Kiaukustika anabainisha sifa ambazo ni;
Sifa ya Usononanti.
Hii
ni sifa ambayo hujitokeza katika kutamka irabu na huwa na mguno mkubwa
(vokali). Sifa hii ilitumiwa kubainisha sauti za konsonati na irabu. Katika
ubainishaji wake, irabu ingeoneshwa kuwa na sifa ya usonoranti [ +usonoranti],
lakini konsonanti ingeoneshwa kuwa si ya usonoranti [-usonoranti]. Mfano,
kimadende na kitambaza /r/ na /l/ ni konsonanti lakini huwa na usonoranti
[+usonoranti]. Nazali hupewa sifa ya usonoranti, /m/ na /n/ [+usonoranti],
viyeyusho navyo pia hupewa sifa ya usonoranti, /w/ na /y/.
Sifa ya Uprotensi.
Sifa
hii hutumiwa kutofautisha zile fonimu ambazo ni kaze. Sauti kaze, ni zile
ambazo hutamkwa kwa kutumia nguvu nyingi na zinakaa muda mrefu zinapotamkwa.
Mfano, sauti si ghuna huwa ni kaze (+kaze) Ilihali sauti si ghuna ni sauti si
kaze (-kaze).
Mfano:
sauti /t/ si ghuna kwa hivyo ni kaze (+kaze), fonimu /d/ ni ghuna kwa hivyo ni
sauti si kaze (-kaze).
Sifa ya
Utoni
Hii
ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano baina ya sauti mbili au zaidi za
fonimu moja ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa. Mfano, fonimu /k/ na
/v/.
[k] [v]
+Konsonanti +Konsonanti
+Kizuiwa +Kikwamizwa
+Kaka laini +Midomo meno
-Nazali -Nazali
-Ghuna +Ghuna
Katika
kuzieleza sifa za Vitamkwa ,Trubertzkoy alielezea kwa kuzigawa sifa hizo katika Seti tatu za Ukinzani Pambanuzi ,seti
hizo ni kama zifuatazo;
Seti ya kwanza,katika
seti hii alizipambanua katika vipengele vinneambavyo ni; Ukinzani
kiuwili,Ukinzani kiwingi, Ukinzani
kiwiani na Ukinzani kipeke.
i.
Ukinzani
kiuwili, huu ni ukinzani ambao anaeleza kuwa Sifa mbili
kinzani hupatikana katika sauti hizo mbili peke yake na si
kwingineko.Mfano,vipasuo vya midomo [P]
na [b] katika Kiswahili ambavyo vinachangia sifa ya kuwa vipasuo vya kinywa vya
midomo .ukinzani wake unajidhilisha katika kielelezo
[p] [b]
+Kipasuo +kipasuo
-ghuna +ghuna
ii.
Ukinzani
uwingi , ni ukinzani ambao unaeleza jumla ya sifa bainifu
zinazochangiwa na sauti hizo huweza kupatikana katika seti ya sauti nyingine
pia mfano herufi P na R ambazo zote zinachangia mkunjo wa upinda wa kuelekea
kulia ,lakini sihizo tu balizipo na herufi nyingine kama herufi B na D ,hvyo
ukinzani huo uhuhusicha herufi nyingi .
iii.
Ukinzani
kiwiani , ukinzani huu huelezae Sauti mbili zinazowiana na
kukinzana na suti nyingine mbili zinazouwiana .mfano sauti [F] na [v], na
ukinzana na [s] na [z] katika Kiswahili . tazama kielelezo hiki.
[f] na [v] [s] na [z]
[+midomomeno ] [+midomomeno]
[+ufizi] [+ufizi].
ivUkinzani kipeke,
ni ukinzani ambao ni wa kipekee kabisa. Mfano [r] na [l] kaika lugha ya
kiingereza hakuna memba wengine wanaohusiana na uhusiano na wanamna hiyo . na
katika lugha ya Kiswahili ukeli ni kwamba sauti [r] ni kimadende ambacho kipo
peke yake pia sauti [l] ni kitambaza ambacho kipo peke yake pia .
Seti ya pili ,katika seti hii Trubertzkoy ameigawa katika
seti ndogo ndogo tatu ambazo ni seti ya kuzinzani kibinafsi, ukinzani
kimwachano taratibu na ukinzani kisawa .
i.
Ukinzani
kibinafsi , ni ukinzani ambao sauti moja inakuwa na alama ya
ziada (sifa ya ziada) na suti nyingine inakuwa haina .mfano sauti moja inakuwa
ghuna na nyingine inakuwa sighuna kama vile sauti [p] na sauti [b], pia sauti
moja yaweza kuwa nazali na nyingine ikose sifa hiyo , kama vile sauti [m] na [k] .
ii.
Ukinzani
kimwachano taratibu ,ukinzani huu unaeleza kuwa memba wa
seti wanapishana kwa viwango tofauti vya sauti ile ile, mfano sauti ya vokali
[o] na [u] . Tazama kielezo kifuatacho
[o] [u]
+vokali +Vokali
+Nyuma +Nyuma
+Mviringo +Mviringo
+Nusu juu +Juu
iii Ukinzani wa kisawa,
ukinzani wa memba wa kundi moja ni sawa na ukinzani baina ya kundi jingine.Kwa
maana kwamba ukinzani wao si wa kupishana kwa viwango vya sifa ile ile.Mfano sauti
[p]na [t],[f] na [k] katika lugha ya Kijerumani.
Seti ya tatu,
hii ni seti ambayo inaelezea ukinzani imara na ukinzani usio imara.Ukinzani imara ni ule
ambao Usio badilifu,Mfano ni ukinzani baina ya sauti [t,d na l] ambazo zote ni sauti za ufizi. Na ukinzani usoimara ni ule ukinzani ulobadilifu yaani
hubadilika . mfano katika mazingira ya sauti [l] hubadilika na kuwa sauti [d]
katika mazingira ya kutanguliwa na Vokali [i] ,mfano Ulimi-Ndimi.Hivyo sauti [l] si imara na sauti
[d] ni imara.
Ilhali,
Roman Jakobson amependekeza sifa za
vitamkwa katika makundi makuu mawili ambayo ni Kundi la sauti za Konsonanti na
Kundi la sauti za vokali. Ambayo pia aliyagawa katika ,makundi madogo madogo
manne.ambayo ni Konsonanti halisi,Vokali,Vitambaza na Viyeyusho.Mfano
Konsonanti halisi huwa na sifa ya ukonsonanti pekee na hukosa sifa ya
vokali.Kama vile fonimu /p/ .Vokali ni vokali peke yake bila kuwa na sifa ya
konsonanti ,kama fonimu /a/, vitambaza ni muunganiko wa konsonanti na vokali,
viyeyusho,hivi viko pekee havihusishi konsonanti wala vokali,kama /y/. Uainishaji
huu una maana kwamba kuna sauti zinazochangia sifa kama inavyodhihirika katika
mfano ufuatao.
Konsonanti+Vitambaza [+konsonanti]
Konsonanti+Viyeyusho [-Vokali]
Vokali+Vitambaza [+Vokali]
Vokali+Viyeyusho [-Konsonanti]
Hitimisho.
Kutokana
na tofauti za sifa za vitamkwa zilizoelezwa na wataalamu hawa,pia kuna uhusiano
wa sifa za vitamkwa kwa kigezo cha uwili.
MAREJELEO.
Massamba,D.P.(2011).Maendeleo ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi:
Phoenix Publishers
Matinde,R.S.(2012).Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia.Mwanza:
Serengeti Educational
Publishers
Mgullu,R.S.(2010).Mtalaa wa Isimu:Fonetiki,Fonolojia,na
Mofolojia ya Kiswahili.Dar-es-
salaam :Longhorn Publishers.
Hokororo
J.I, Kihore Y.M, & Masamba D.P.B, (2003). Sarufi Miundo ya Kiswahili
Sanifu.SAMIKISA.Dar-es
Salaam: TUKI Publisher.