NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KISWAHILI
NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KISWAHILI
Kiswahili
Asili Yake ni Kongo
Baadhi
ya wataalamu hudai kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni huko Kongo ambayo
baadaye iliitwa Zaire na sasa inaitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Dai hili
linaimarishwa na wazo lingine linalodai kwamba katika vipindi kongwe
vilivyopata kuwako, sehemu za Pwani ya Afrika mashariki hazikuwa zimekaliwa na
watu. Kutokana na hali ya vita, uchungaji na biashara, inadaiwa kuwa Wabantu
walitoka sehemu za Kongo walisambaa na kuja pwani ya Afrika mashariki kupitia
Kigoma. Baadhi ya wabantu hawa walipitia sehemu za Uganda. Wakati wa kusambaa
kwao, walieneza pia lugha zao ikiwemo hii ya Kiswahili.
Udhaifu
wa nadharia hii ni kwamba, madai ya kuwa asili ya Kiswahili ni Kongo hayana
msingi kwani mpaka sasa wataalamu wanaodai hivi hawajaweza kueleza na
kuthibitisha kisayansi ama Kihistoria juu ya lini hasa watu walianza kuishi
pwani ya Afrika mashariki.
Kiswahili ni Ki-Pijini au ni Ki-Krioli
(i) Kiswahili ni Ki-Pijini
Baadhi
ya wataalamu hudai kuwa Kiswahili ni Ki-Pijini. Wataalamu hawa hudai kwamba
Ki-Pijini ni lugha ambayo huzaliwa kutokana na kukutanika kwa makundi mawili (A) na (B) yanayotumia
lugha mbili tofauti. Ili makundi haya yaweze kuwasiliana kunaundwa lugha ambayo
kitabia ni tofauti na zile
zinazozungumzwa na makundi yanayohusika. Lugha hii inaweza kuwa na msamiati
mwingi kutoka lugha kati ya zile mbili, au inaweza kuwa na msamiati wenye uzito
sawa. Lugha hiyo ndiyo inayoitwa Ki-Pijini. Mazingira yanayosababisha kuwepo
Ki-Pijini ni kama vile biashara, utumwa, ukoloni, nk.
Kwa
mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwa kilianza kama
Ki-Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyeji wa pwani ya Afrika
Mashariki na wageni wa kutoka Mashariki ya Kati, hususan Waarabu. Aidha,
husisitiza kuwa lugha ya Kiswahili haikuwepo kabla ya hapo.
(ii) Kiswahili ni Ki-Krioli
Wataalamu
hawa wanadai kwamba watu wanaozungumza Ki- Pijini wanaweza kuishi pamoja kwa
muda wa karne nyingi na kwa hiyo wakaweza kuzoeana na hata kufikia hatua ya
kuoana. Wakioana watoto wao huikuta lugha ya ki-Pijini ama lugha yao ya kwanza.
Inapofikia hatua ya aina hii kwa watoto wanaozungumza lugha hiyo, wao
husemekana sasa wanazungumza lugha ya
Ki-Krioli, lugha ambayo ni hatua ya juu ya Ki-Pijini, yaani Ki-Pijini
kilichokomaa.
Nadharia
hii hutumia kigezo cha msamiati wa Kiswahili kuonesha uhusiano uliopo kati ya
Kiswahili na Kiarabu. Wanadai kuwa, msamiati mwingi wa Kiswahili unatokana na
Kiarabu. Hivyo huhitimisha kuwa hapana shaka Kiarabu kimehusika katika
kuizalisha na kuikomaza lugha ya Kiswahili.
Udhaifu
wa nadharia hii ni kwamba hutumia kigezo cha msamiati tu bila kuzingatia
vipengele vingine vya lugha kama vile matamshi, maumbo ya maneno au muundo wa
sentensi za Kiswahili. Aidha, wataalamu hawa hawakuhoji suala la kufanana kwa
Kiswahili na lugha jirani katika hayo yaliyotajwa hapo juu na katika eneo la Kijografia
ambamo Kiswahili na lugha hizo nyingine hujikuta zikizungumzwa. Vigezo hivi ni
ushahidi tosha unaoonesha kuwa Kiswahili SI Ki-Pijini wala SI Ki-Krioli, bali
ni lugha kama zilivyo hizo lugha jirani.
Kiswahili ni Lugha ya Jamii ya Vizalia
Kundi
la kwanza la wataalamu wa nadharia hii, Bishop Edward Steera, Bwana Taylor,
Dkt. R. Reusch, (Katika Maganga, 1997)
hudai kwamba:
·
Waarabu
na Waajemi waliohamia pwani ya Afrika ya Mashariki waliwaoa wanawake wa ki-Afrika.
·
Watoto
wao walijifunza maneno ya Kiarabu na ki-Ajemi kutoka kwa baba zao.
·
Aidha, watoto hao wakajifunza maneno ya
ki-Bantu kutoka kwa mama zao.
·
Katika
jitihada zao, watoto hao walijirekebisha kutokana na tamaduni za wazazi wao ambazo ni tafauti:
utamaduni wa Kiarabu na utamaduni wa ki-Bantu.
·
Vizalia
hawa wakaanza kutumia lugha mpya ya mseto wa Kiarabu, Kiajemi na lahaja
mbalimbali za ki-Bantu.
·
Kwa kiasi
kikubwa, lugha mpya ya mseto ilikuwa ni upotoshaji wa lugha ya Kiarabu na Kiajemi.
·
Mwarabu
au Mu-Ajemi alikuwa muumini wa dini ya Uislamu.
·
Umo humo,
vizalia hawa wakayaingiza maneno ya Kiarabu, Kishirazi na Kihindi katika hii
lugha mpya.
·
Pamoja na
kuyaingiza maneno ya kigeni, lugha-mpya yao hii (Kiswahili), ilikithiri vionjo
vingi vya lugha mbali mbali za ki-Bantu.
·
Ndipo
baadaye, lughampya yao hii ikajulikana au kuitwa Kiswahili.
·
Kwa maoni
ya wataalamu hawa, sehemu mbili kati ya tano (2/5) ya maneno yanayotumika katika lugha hii mpya ni ya ki-Bantu.
·
Sarufi ya
lugha mpya hii ni mseto wa ki-Bantu (chenye utata na kisicho na mpangilio maalumu)
pamoja na Kiarabu (chenye mantiki na kilichokomaa).
Kundi la pili la
wataalamu wa nadharia hii, B. Krumm na F. Johnson lina mawazo yanayodai kwamba:
·
Kiswahili
kilitokana na visiwa vya Lamu, Kilamu/Kiamu.
·
Wageni
kutoka Ghuba ya Ushirazi/Uajemi na Arabia ya Kusini walikuja katika Pwani ya
Afrika ya Mashariki na lugha tofauti.
·
Lakini kutokana na kuoana kwao na wenyeji,
wageni hawa wakaichukua lugha ya hapo walipofikia, wakaikuza kwa maneno kadhaa
na sentensi kadhaa kutoka lugha zao za asili, yaani Kiarabu, Kiajemi na Kihindi
hususan katika masuala ya biashara,
ubaharia, vyombo vya kazi zao na nguo.
·
Aidha, utumwa na tabia ya kuoa wake wengi ilisaidia
kutoa kundi kubwa la masuria. Hali hii ikaondosha hisia za ugeni katika lugha
zao; na maneno yote yakabatizwa kuwa ya ki-Bantu, na hata kupoteza kabisa sura
ya ugeni.
Kiswahili ni Kiarabu
Kuna
hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumia kutetea nadharia hii
kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.
(i)
Inadaiwa
kuwa maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha
kwamba lugha hii ilianza kama Pijini ya Kiarabu.
(ii)
Inahusu
neno lenyewe Kiswahili ambalo asili yake ni Kiarabu. Neno Kiswahili linatokana
na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani.
(iii)
Inadaiwa
kwamba kwa kuwa Kiswahili kilianza pwani, kwa kuwa idadi kubwa sana ya wenyeji
wa pwani ni waislamu, na kwa kuwa uisilamu uliletwa na Waarabu, basi Kiswahili
nacho kililetwa na Waarabu.
Kiswahili si Kiarabu
Madai kwamba Kiswahili si
Kiarabu yanathibitishwa na hoja kinzani zifuatazo:
Tukianza
na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika
Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya Kiarabu’
tunaona wazi kwamba madai haya hayana mashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa
na maneno ya mkopo yenye asili ya Kiarabu (na kwa hakika yapo yenye asili ya
Kiajemi, Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukweli kwamba
kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyeji wa pwani na
wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbili tofauti wanapokutana
hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lugha kuwa na maneno mengi ya mkopo
kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyo isemekane kuwa imetokana na hiyo
lugha nyingine.
Pili
wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe
Kiswahili lina maana ya Kiarabu.
Kwani linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil”
(wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au
jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewe jina lake, yeye huitwa kwa hilo jina
alilopewa na wengine: Jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. Na hivi ndivyo
ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaani
Waswahili, walipotembelewa na Waarabu na
kuitwa As-Sahilyy au As-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake
Sawahil), yaani pwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko !
Kigezo cha dini
nacho hakikubaliki lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya
Kiarabu yenyewe ilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu.
Hali kadhalika, lugha nyingine za Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla ya
kufunuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani si
ukristo, basi ndivyo vivi hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini ya
uislamu, aslan! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachoweza kufanya ni kuitumia
lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dini kuifasili lugha.
Kiswahili ni Kibantu
Vipengele
vinavyotumika katika kuihalalisha nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kibantu
ni ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa ki-Historia na kuichunguza lugha ya
Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za
ki-Bantu. Wataalamu wa nadharia hii wanahitimisha kwa kudai kwamba Kiswahili ni
mojawapo kati ya lugha katika jamii
kubwa ya lugha za ki-Bantu.
Baadhi ya wataalamu
muhimu wanaoiunga mkono nadharia hii ni Prof. Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf
na Dkt. C. Rohl na Prof. Clement Maganga.
Profesa Malcom
Guthrie ni mtaalamu (mwanaisimu)
mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Alitumia miaka 20 kuchunguza
uhusiano uliopo baina ya lugha za Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo
hukaliwa na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana kama Afrika, Kusini
mwa Jangwa la Sahara.
Alifanya uchunguzi
wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000 kutoka lugha 200 za Kibantu. Katika
uchunguzi wake alikuta mizizi (mashina) 2,300 imezagaa katika lugha mbalimbali za Kibantu na Kiswahili kikiwemo.
Mashina/mizizi 500 yalilingana
katika lugha zote 200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu.
Mashina haya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa
uchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongo kwa asilimia
arubaini na nne (44%).
Katika kuchunguza ni
asilimia ngapi za mashina hayo 500 yaliyomo katika kila lugha, mgawo
uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:
Kiwemba
kizungumzwacho Zambia - 54%
Kiluba
kizungumzwacho Katanga - 51%
**Kikongo
kizungumzwacho Zaire - 44%**
**Kiswahili
kizungumzwacho Afrika Mashariki 44%**
Kisukuma
kizungumzwacho Tanzania 41%
Kiyao
kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji - 35%
Sotho
kizungumzwacho Botswana - 20%
*Kirundi
kizungumzwacho Burundi - 43%*
Kinyoro
kizungumzwacho Uganda - 37%
Kizulu
kizungumzwacho Afrika Kusini - 29%
Baada ya kupata
matokeo haya, Profesa Malcom Guthrie anaiunga mkono nadharia hii ya kwamba Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudai kwamba:
(i) Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wageni;
(ii) Anaonyesha kwamba Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za
Kibantu;
(iii) Mwisho anasema Kiswahili kilianzia Pwani ya Afrika Mashariki.
Dkt. C. Meinholf na
Dkt. C. Rohl: Wataalamu hawa wanaamini kwamba:
(i)
Wakati wa
utawala wa Shirazi katika upwa wa mashariki ya Afrika kulikuwa na kabila la
Waswahili;
(ii)
Kabila
hili ni dhuria ya Wazaramo wa leo.
(iii)
Kwa kuwa
hawa Wazaramo walikuwa wamezaliwa katika harakati za kibiashara, kwa hivyo
wakafuata nyayo za wazazi wao.
(iv)
Lugha yao
ilikuwa ya aina ya ki-Bantu.
(v)
Kwa kuwa
Wabantu ni wengi zaidi kuliko jamii ya makabila mengine, lugha yao ya Kiswahili
ikaanza kutumika na kuenea katika makabila mengine, hususan katika ukanda wa
pwani ya Afrika Mashariki.
(vi)
Baadaye,
Waswahili hawa hawa wakafanya biashara na wageni waliokuja kuvinjari Afrika
Mashariki, hususan Waarabu, Washirazi, Wamalaysia, Wahindi na Wareno ambao
tayari walikuwa wamefurika katika pwani hii ya Afrika Mashariki miaka kadhaa
kabla.
(vii)
Vifaa na
majina ya vitu vya biashara vya wageni hao vikaselelea na kuingizwa katika
mfumo wa lugha hiyo ya Waswahili ambayo ni ki-Bantu.
Madai ya nadharia
hii yakichunguzwa, tunagundua kwamba inazingatia mitazamo miwili yaani, mtazamo
wa ki-Isimu na mtazamo wa ki-Historia. Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea
kukubalika na wataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu asili au historia ya
Kiswahili.
Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwamba Kiswahili ni ki-Bantu.
Kama tulivyoona, lugha ya Kiswahili ilifanyiwa utafiti na uchambuzi na wanataaluma
kadhaa kwa madhumuni ya kuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bantu au
la. Prof. Maganga alifanya uchambuzi wa ki-Isimu na wa ki-Historia kuhusu lugha
hii. Matokeo ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha ya Kiswhili (au lugha kwa
ujumla) unadhihirisha mambo mengi, mojawapo ni asili ya lugha hiyo.
Amethibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha
kwa ushahidi thabiti hoja ya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl kama
tulivyoieleza hapo juu.
(i) Ushahidi wa Kiisimu
(a) Msamiati
Matokeo ya utafiti
alioufanya kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote
yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha
za Kibantu, 30% ni lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama
vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume
chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.
Mfano:
Kiswahili Kindali Kizigua Kijita
Kikurya Kindendeule
Mtu Umundu Mntu
Omun Omontu Mundu
Maji Amashi Manzi
Amanji Amanche Maache
Moto Umulilo Moto Omulilo Omoro
Mwoto
(b) Tungo (Sentesi) za Kiswahili
Miundo ya tungo
(sentesi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana na miundo ya tungo za maneno
ya ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zina kiima na kiarifu.
Mfano:
Lugha za Kibantu Kiima kiarifu
Kiswahili Juma anakula ugali.
Kizigua Juma adya ugali.
Kisukuma Juma alelya bugali
Kindali Juma akulya ubbugali.
Kijita Juma kalya ubusima.
Kindendeule Juma ilye ughale.
(c) Ngeli za Majina
Wanataalamu
wanakubaliana kuhusu ngeli za majina kwa mujibu wa:
maumbo ya nomino
(umoja na wingi wa majina) pamoja; na
upatanisho wa
kisarufi katika sentesi.
Kigezo
cha maumbo ya majina: Kigezo hiki
hufuata maumbo ya umoja na uwingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo
mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja na
uwingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana
maumbo dhahiri ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu Umoja Wingi
Kiswahili mtu - watu
mtoto - watoto
Kikurya omanto - banto
(abanto)
omona - bana (abana)
Kizigua mntu - bhantu
mwana - bhana
Kindali mundu - bhandu
mwana - bhana
Kindendeule mundu - βhandu
mwana - βhana
Kigezo cha
upatanisho wa kisarufi katika sentesi: Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano
uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi) na vivumishi katika
vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu. Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo
vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu Umoja - Wingi
Kiswahili Baba analima - Baba wanalima
Kindali Utata akulima - Abbatata
bbakulima
Kikurya Tata ararema - Batata(Tata)bararema
Kijita Tata kalima - Batata abalima
Kindendeule
Tate ilima - Akatate βhilima
(d) Vitenzi
vya Kiswahili na Kibantu
Kuna uhusiano mkubwa
sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu.
Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na
mwanzo au mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo:
Viambishi: vitenzi
vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za ki-Bantu hujengwa na mzizi
(kiini) pamoja na viambishi vyake vya awali na vya tamati.
Mfano:
Kiswahili - analima =
a – na – lim - a
Kiikuyu - arerema =
a –
re – rem–a
Kindali - akulima = a -
ku –
lim – a
1
- 2 -
3 - 4
Sherehe:
1 - Kiambishi
awali kipatanishi cha nafsi.
2 - Kiambishi
awali cha njeo (wakati uliopo).
3 - Mzizi/Kiini.
4 - Kiambishi
tamati.
Mnyambuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi
vya lugha za ki-Bantu.
Mfano:
Kiswahili - kucheka - kuchekesha - kuchekelea.
Kindali - kuseka - kusekasha - kusekelela.
Kibena - kuheka - kuhekesha - kuhekelea.
Kinyamwezi - kuseka - kusekasha - kusekelela.
Kikagulu - kuseka - kusekesha - kusekelela
Mwanzo wa vitenzi:
Vitenzi vyote vya Kiswahili na vile
vya lugha za ki-Bantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi,
kama ifuatavyo:
Mfano:
Kiswahili - Ni-nakwenda
Kihaya - Ni-ngenda
Kiyao - N-gwenda
Kindendeule - Ni-yenda
Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu
na Kiswahili huishia na irabu –a.
Mfano:
Kiswahili kukimbi-a - kuwind-a - kushuk-a
Kindali kukind-a - kubhing-a - kukol-a
Kisukuma kupil-a - kuhwim-a - Kutend-a
Kisunza kwihuk-a - kuhig-a - kising-a
Kindendeule kuβhutuk-a - kuhwim-a - kuhuk-a
tafiti wa Prof.
Maganga kuhusu ushahidi wa ki-Isimu wa kuthibitisha kama Kiswahili ni ki-Bantu
au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwa mifano mingine ifuatayo:
Mfano wa 1:
Lugha
|
Sentesi
|
|||||
Kiswahili
Kipare
Kindamba
Kichaga
Kihaya
Kikaguru
Kindendeule
|
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
|
anafuga
erisha
kafugha
nao he
n’afuga
kachima
ifuga
|
mbuzi
mbuji
mene
mburu
embuzi
m’ehe
mbuhi
|
kuku
nkuku
nguku
nguku
enkoko
ngu’ku
nguku
|
na
na
na
na
n’
na
na
|
ng’ombe
ng’ombe
senga.
umbe
ente
nn’ombe
ng’ombe
|
Katika mfano huu inaonekana kwamba mpangilio wa maneno katika sentesi
una ufanano kwa sababu katika kila sentesi kuna kiima na kiarifu. Katika kiima
kuna nomino, yaani jina la mtenda (Jongo) na katika kiarifu kuna kitendo
kinachofanyika na nomino mtendwa. Pia nafasi ya viunganishi ni ile ile kwa
lugha zote zilizoonyeshwa katika mfano huu.
Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio huu.
Mfano wa 2:
Lugha
|
Sentesi
|
Kiswahili
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kizigua
|
Sitamkuta kesho
Timushangemu nyenkya
Natusanga intondo
Tumuhanga fadyu
Nesikemkiche yavo
Sirambila luvi
|
Katika sentensi hizo mpangilio wa maneno una ufanano kwa sababu kila
sentensi ina kiima na kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Pia kiambishi cha
nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza mwanzoni mwa neno la kwanza la kila
sentesi.
Sitamkuta; Timushangemu; Natusanga; Tumuhanga; Nesikamkiche; Sitambila.
Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia vinaonyesha hali ya ukanushi
katka kila sentesi na nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.
Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika kitenzi cha kila
sentesi.
Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sitamkuta,
timushangemu, natusanga, tumuhanga, nesikamkiche,
na sitambwila ni vya urejeshi;
vinawakilisha nomino mtendwa.
Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo ya sentensi hizi
inafanana na vitenzi vyake vina tabia mbalimbali, kama vile:
(i) kubeba viambishi vya
nafsi, mtenda na mtendwa,
(ii) kuonyeshga hali ya
ukanushi njeo za wakati na kitendo kinachofanyika.
Mfano wa 3:
Lugha
|
Sentesi
|
Kiswahili
Kizigua
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kindendeule
|
Akija mwambie anifuate
Akeza umugambe anitimile.
Kalaija omugambile ampondele
Ulu nahali anikubije
Newaja mwele ang’onge.
Ekiza umti aniratere
Anda ahikite n’nongerera angobhekeraye
|
Katika sentesi hizo inaonekana kwamba sentesi zote zinafanana kimpangilio. Pia maneno yake yanakubali
uambishaji, kwa mfano:
(i) Katika
maneno ya mwanzo:
akija,
akeza. kalaija, akuja, newaja, ekiza, herufi zilizopigiwa vistari ni viambishi
vya nafsi vinawakilisha dhana ya mtenda.
(ii) Vivyo
hivyo katika maneno:
anifuate, ampondele, anitimile, ang’nge, aniratere,
angobhekeraye, viambishi vilivyoko katika viarifu vya sentesi hizo
vinawakilisha nafsi za watenda.
(iii) Pia
vitenzi vya sentesi hizo vina tabia ya kubeba virejeshi vya nafsi kama ilivyo
katika, mwambie, omugambile, nahali,mbwele na umti, vinaonyesha njeo na hali ya
uyakinifu- hali inayoonyesha ufanano wa maumbo ya maneno.
(iv) Licha
ya kuwa na mpangilio unaofanana na wa lugha nyingine za kibantu, kwa mfano,
katika mifano tuliyoiona hapo juu, baadhi ya maneno yanafanana: tazama maneno:
kafugha (Kindamba); nafuga (Kihaya);
nifuga (Kindendeule); anafuga (Kiswahili).
Pia maneno:
nkuku (Kipare); nguku
(Kindamba);
nguku (Kichaga); enkoko (Kihaya);
ng’uku (Kikaguru); nguku(Kindendeule);
nguku (Kindendeule)
Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana ufanano:
Akeza (Kizigua); kalaija (Kihaya); alize (Kisukuma),
newaja (Kinyaturu); ekiza (Kipare); anda
ahikite,... (Kindendeule);
akija, (Kiswahili.)
Pia maneno;
umugambe (Kizigua); omugambile (Kihaya); unongeraye
(Kindendeule); na mwambie (Kiswahili).
Ufanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno pamoja na wa mpangilio wa
maneno katika sentesi, vyote vinathibistisha kwamba lugha ya Kiswahili ni ya
kibantu kama zilivyo nyingi nyinginezo.
(ii) Ushahidi wa Kihistoria Kwamba Kiswahili ni
Kibantu
Baada
ya kuangalia ushahidi wa kiisimu kuhusu asili ya Kiswahili, katika sehemu hii
Maganga (1997) aliendelea kuchambua ushahidi wa Kihistoria unaothibitisha kuwa
lugha ya Kiswahili ilizungumzwa katika upwa wa Afrika Mashariki hata kabla ya
ujio wa wageni kama vile Waarabu na Wazungu. Ushahidi huu ulitolewa na wageni
mbalimbali waliofika hapa Afrika Mashariki. Wote wanathibitisha kuwa lugha ya
Kiswahili ilizungumzwa hapa Afrika Mashariki kabla ya ujio wa wageni.
(a) Ugunduzi wa Ali-Idris (1100-1166)
Ugunduzi
huu yasemekana ulifanywa huko Sicily yapata mwaka 1100-1166. Kwenye mahakama ya
mfalme Roger II. Licha ya kufahamika kuwa Kiswahili, kilipata kuandikwa kabla
ya 10BK. Ali-Idris alikuwa wa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa
ni Unguja. Katika maelezo yake anaandika pia majina kama vile kikombe, mkono wa tembo, muriani, na
kisukari, ambayo ni ya ndizi mbalimbali zilizokuwa zikipatikana huko.
(b) Ushahidi wa Marco Polo
Huyu
ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na masuala mbalimbali ya kijiografia na
alisafiri sehemu nyingi duniani. Marco Polo aliandika hivi:
“Zanzibari
ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wa maili 200. Watu wote
wanaabudu (Mungu), wana Mfalme na wanatumia lugha yao, na hawalipi kodi
(ushuru) kwa mtu.” Safari za Marco Polo
1958:301
Marco
Polo anasemekana aliandika pia kitabu cha jiografia ambacho hakikupata
kuchapishwa lakini sehemu zake zimepata kufasiriwa kwa Kirusi na Kifaransa.
Mfano mmojawapo ni huu unaofuata:
“Katika
visiwa vya Sjawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii, ni kile kisiwa cha
Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao. Zanguabar/Ungudya,
na wakazi wake, japokuwa ni mchanganyiko, kwa sasa wengi wao ni Waislam…chakula
chao kikuu kikiwa ndizi. Kuna aina tano ambazo zinajulikana kama kundi, fili,
ambazo uzito wake waweza kuwa wakia 12, Omani, Marijani, Sukari....”
Maelezo
haya ya Marco Polo yanathibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa Pwani ya
Afrika ya Mashariki na lugha yao; mintarafu ya dini, chakula na utamaduni wao
kwa ujumla.
(c) Ushahidi wa Al-Masudi (915 BK)
Katika
moja ya maandiko yake, Al-Masudi anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao
walijulikana kwa jina la “wazanji”. Kwa dhana hii, neno Zanzibar linatokana na
Zenzibar yaani “Pwani ya Zenji”. Katika maelezo yake Al-Masudi anaonyesha kwamba
Wazenji walikuwa “Watawala Wakilimi”
ambao waliaminiwa kuwa walitawala kwa nguvu za Mungu. Kuna maelezo kuwa huenda
neno “wakilimi” lina maana ya “wafalme”. Al-Masudi alisisitiza katika maelezo
yake kuwa Wazenji walisema lugha kwa ufasaha na walikuwa na viongozi
waliowahutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno “zenji” kuna uwezekano kuwa
kabla ya majilio ya Waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au “Kizanji” na
wageni waliofika pwani.
(d) Ushahidi wa Ki- Historia wa Mji wa Kilwa
Kimsingi
habari zinazoeleza historia ya mji wa Kilwa katika karne ya 10-16BK zinataja
majina ya utani kama vile: mkoma watu,
nguo nyingi, nk. ambayo walipewa Masultani wa kwanza wa Kilwa Ali Ibn
Hussein na mwanae Mohamedi Ibn Ali. Kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahili
ilishaanza kusemwa mnamo karne ya 10 au ya 11 BK. Maelezo ya kihistoria
yanaeleza juu ya Sultani aliyeitwa Talt Ibin Al Husaini ambaye alipewa jina la
utani “Hasha Hazifiki”.
(e) Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK) kama
Ushahidi
Shairi
la zamani kabisa lililopata kuandikwa la Kiswahili, linalojulikana ni lile la Utenzi wa Fumo Liyongo. Utenzi huu
inasemekana uliandikwa karne ya 13BK. Kuweko kwa shairi hili kunadhihirisha
kuwako kwa lugha ya Kiswahili kabla ya karne hiyo, na kwa hivyo, huenda
Kiswahili kilianza kutumika kabla ya karne ya 10BK. Baadhi ya beti za utenzi wa
Fumo Liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti 6: Liyongo
Kitamkali,
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na hiba huongeya.
Ubeti
7: Kilimo kama mtukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu huja kwangaliya.
Ubeti
10: Sultani pate Bwana
Papo nae akanena
Wagala mumemwona
Liyongo kiwatokeya.
(Kutoka
E.A. Swahili Committee 1973)
Lugha
hii ndio mfano wa lugha iliyokuwa ikitumika kunako karne ya 13BK. Ni wazi kuwa
lugha hiyo ilianza kusemwa mapema kabla ya muda huo. Hoja za kihistoria
inaelezea historia ya lugha ya Kiswahili toka karne ya 10BK hadi karne ya 18BK.
Kutokana na ushahidi huu ni dhahiri kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Wabantu
wa Afrika ya Mashariki.
MAREJELEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N.
(2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili,
Kidato cha 5 na 6. Aroplus
Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu,
Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
tunapatikana kwa 0787 613746