DHANA YA SARUFI GEUZI NA SARUFI MIUNDO
Swali:
Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi?
DHANA YA SARUFI
Sarufi ni taaluma ya
lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali
zinazotawala muundo wa lugha, (Matinde, 2012.
Sarufi ni utaratibu
wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi
zinazoeleweka mara zinapotamkwa. (Kapinga, 1983).
Dhana
ya sarufi inatafsiriwa katika mitazamo tofauti lakini yenye
kuhusiana. Mtazamo wa kwanza tunaweza kusema Sarufi
ni
taaluma ya uchambuzi walugha inayojumuisha viwango vyote vya
uchambnuzi yaani kiwango cha umbo sauti (fonolojia), kiwango cha umbo
neno (fonolojia), kiwango cha miundo maneno (sintaksia) na kiwango
cha umbo maana(semantiki), (Massamba, 1999).
DHANA YA SARUFI
MUUNDO VIRAI
Sarufi muundo virai
ni mkabala wa kimapokeo ambao haujihusishi na sarufi miundo katika
marefu na mapana yake, ambapo zilijihusisha sana na sentensi sahili,
(Massamba 1999).
Sarufi muundo virai
ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi, ambacho hujikita katika
matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo,
ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa, (
Matinde, 2012).
Sarufi muundo virai
ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa pamoja na kujenga kitu
kikubwa zaidi. Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa
kuigawa sentensi katika virai vinayoiunda na kasha kuvichanganua
zaidi hadi kufikia neno mojamoja lililokiunda kirai, (Massamba,
2001).
DHANA YA SARUFI
GEUZI
Ugeuzi ni
utaratibu unaotumiwa kubadili umbo la tungo kuwa umbo jingine kwa
kutumia kanuni maalumu. Kwa hiyo ugeuzaji ni mbinu ya kisarufi ambayo
hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki
kwa kufuata sheria mahususi, (Matinde, 2012).
Sarufi geuzi hueleza
ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao ujuzi anaomwezesha kutumia
lugha (Habwe na Karanja,2007).
Sarufi geuzi maumbo
ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo meng kwa kufuata kanuni
maalumu (Matinde,2012).
Zifuatazo ni tofauti
kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi:
Hutofautiana
katika lengo. Lengo
la sarufi muundo lilikuwa halifahamiki zaidi ya kutumia taratibu za
kijarabati zinazohusu ukusanyaji wa data na kuzichambua pamoja na
kuunda kanuni kwa kutumia data hizo. Lakini,
Lengo la sarufi
geuzi liko bayana, hujitokeza dhahiri. Lengo la sarufi hii ni
kufafanua umilisi wa ujuzilugha ambao huwa mwanalugha anao. Umilisi
huo humfanya mwanalugha kutambua viambajengo kati ka tungo, katika
mtazamo wa ndani yaani muundo wa ndani.
Hutofautiana
katika miundo. Sarufi
miundo virai, hii huwa inajikita katika miundo ya nje, ambayo
huchunguza na kuchambua sentensi katika umbo la nje.
Mfano; Mama
anakula ugali
Hivyo huonyesha tu
aina ya maneno husika katika sentensi au tungo kama vile: Mama-
Nomino, Anakula- Kitenzi, na Ugali- Nomino. Ilihali,
Sarufi geuzi, hii
huwa imejikita katika kuchungaza sentensi kama umbo la ndani na umbo
la nje. Muundo wa ndani ni uchopekwaji katika miundo hiyo ambapo
muundo wan je lazima upitie katika muundo wa mofofonemiki na kuweka
katika kitengo cha fonolojia.
Hutofautiana
katika vitengo. Sarufi
geuzi
ni
sarufi ambayo inafumbata vitengo vyote vya lugha ambavyo ni
fonolojia, sintaksia, semantiki, na mofofonemiki ambapo kitengo cha
fonolojia hushughulikia sauti za lugha, kitengo cha kisintaksia
hushughulika na uundaji wa sentensi, kitengo cha semantiki
hushughulika na ufasili wa maana, na kitengo cha mofofonemiki huwa na
kazi ya kuibadili njeo za wakati. Ilihali
Sarufi miundo virai
hufumbata kitengo cha mofolojia ambapo sentensi iligawanywa katika
kiunzi cha aina za maneno kama Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kielezi na
kihunzi hicho kilijulikana kama utaratibu wa uchanganuzi wa
viambajengo.
Hutofautiana
katika uhusiano wa sentensi. Sarufi
geuzi ilipiga hatua kubwa, kwanza huonyesha uhusiano uliopo kati ya
maumbo mbalimbli ya sentensi au tungo. Na pia kuonyesha uhusiano
unaoweza kuwepo baina ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Mfano: (1) Mtoto
mrefu anacheza, na si kusema kuwa Mtoto anacheza mrefu
Huu ni uhusianao
kati ya maumbo.
Mfano: (2) Juma
alipiga mpira
Mpira
ulipigwa na Juma
Huu
ni uhusiano wa sentensi moja na sentensi nyingine. Ilihali
Sarufi
miundo virai haionyeshi uhusiano kati ya sentensi moja na sentensi
nyingine.
Hutofautiana
katika uwazi. Sarufi
geuzi huonesha sentensi sahihi na ambazo sio sahihi pia huonesha
sentensi ambazo zinakubalika na sentensi zisizokubalika kwa msemaji
mzawa. Ilihali
Sarufi
miundo virai yenyewe haina uwazi huo.
Hitimisho
ni kwamba, Sarufi geuzi ilianzishwa kutokana na mapungufu katika
sarufi muundo virai. Sarufi iliyokuwepo, sarufi miundo virai,
ilishindwa kuonyesha mahusiano yaliyokuwepo baina ya sentinsi zinazo
husiana kimaana. Hivyo kutokana na upungufu huo kulikuwa na haja ya
kuonyesha uhusiano huo.
MAREJELEO
Kapinga,M.C.(1983).
Sarufi
Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA).
Dar-es-Salaam:
TUKI.
Massamba,
D.T., Kihore,M.Y.& Hokororo.(1999). Sarufi
Miundo ya Kiswahili Sanifu
(SAMIKISA).
Dar-es-Salaam: TUKI.
Matinde,S.R.(2012).
Dafina
ya Lugha Isimu na Nadharia.
Mwanza: Serengeti Educational
Publishers
(T) LTD.