MFANANO NA TOFAUTI KATI YA RIWAYA PENDWA NA RIWAYA DHATI
Swali :Linganisha na
linganua riwaya pendwa na riwaya pevu kwa kurejelea Riwaya
ya Nyota
ya
Rehema
na Kufa
na Kupona .
UTANGULIZI
Masebo
(2008) anasema riwaya
ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawanda mapana ,lugha ya
kinathari ,mchanganyiko wa visa na dhamira ,wahusika kadhaa na
matukio yaliyosukwa Kimantiki yenye kufungamana na wakati na
kushabihiana na maisha halisi.
Msokile
(1992) ,anasema kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni
yanye maandishi ya kinathari yanayosimulia hadithi ambayo ina
uzito ,upana, na urefu wa kutosha ina wahusika mbalimbali
wenye tabia za aina nyingi vilevile huwa na migogoro mingi
,mikubwa na midogo ndani yake.
Madumulla
(2009) ,riwaya
pendwa
ni riwaya ambayo inajihusisha na masuala ya mapenzi
,upelelezi, na ujasusi ambapo mara nyingine katika ufuatiliaji
wake kuna mapigano makali ya kimwili au kiakili kati ya
mtu mmoja au wachache na watu wengi.
Masebo
(2008) ; riwaya
pevu
ni riwaya yenye kuchimbua matatizo au masuala mazito ya
kijamii ,kutafuta sababu zake ,athali zake na ikiwezekana
ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na kumfikirisha
msomaji,sio kumstarehesha tu.
Riwaya
pendwa ni kufa na kupona iliyoandikwa na E. musiba na
Riwaya pevu ni Nyota ya Rehema iliyoandikwa na iliyoandikwa
na M.S Mohammed.
Riwaya
pendwa na riwaya pevu hufanana na hutofautiana.Kwa kutumia
kitabu cha riwaya ya “ Nyota ya Rehema” iliyoandikwa na
M.S Mohammed na riwaya ya “Kufa na Kupona” iliyoandikwa
na E .Musiba .
Ufuatao
ni ufanano uliopo kati ya riwaya pendwa na riwaya pevu kwa
kutumia riwaya ya “Nyota ya Rehema” na riwaya ya “Kufa na
Kupona.”
Riwaya
hizi zimetumia mandhari halisi
,mandhari kama eneo ambalo tukio la kifasihi kutendeka .riwaya
pevu na riwaya pendwa waandishi wake mara nyingi hutumia
mandhari ambazo ni halisi na zidhihilikazo katika mazingira
halisi. Kwa mfano katika riwaya ya “Nyota
ya Rehema “
mwandishi ametumia mandhari kama vile Mwembeshomari
(uk 31)
“Unakwenda
mwempeshomari? Rehema aliulizwa.
‘Mwembeshomari’
aliitika upesi upesi.”
Vilevile
katika riwaya ya “kufa
na Kupona” mwandishi
mandhari kama vile
Nairobi-kenya .
uk 18 ,
upanga –Dar –es
–salaam.
“nikaingia
kwenye gari langu huyoo upanga” uk 12
Riwaya
hizi zinaelimisha jamii
;riwaya pevu na pendwa zote zinaelimisha jamii katika mambo
mbalimbali kwa mfano riwaya ya “Nyota
ya rehema
“ mwandishi amewatumia Rehema na Sulubu kuelimisha jamii
suala la kutokata tamaa, baada ya wahusika hawa kufukuzwa
katika shamba la Ramwe wakapata kijieneo kidogo huko pakani
ambapo hapakuwa na rutuba lakini hawakukata tamaa na jitihada
za kilifanya shamba kuwa na rutuba kwa kulitilia moto na
kuanza kulima kwa juhudi (uk -155 -159 ).
Pia
katika riwaya ya Kufa
na
Kupona
mwandishi amewatumia wahusika Sammy na Joe Masanja konesha
suala la kutokata tama ambapo wapelelezi wenzao wanauwawa
mmoja mmoja kwa vifo vya kutisha na kikatili lakini wao
wanaendelea na upelelezi wa nyaraka za siri pasi kuto kukata
tamaa mfano Wiilly Gamba anasema
“lazima
mumkamate na kumuua mimi mwenyewe kama nitakuwa mzima wakati
wote wa madhira kama yao…………
(uk 24)
Zote
zinaonyesha uhalisia wa matukio katika jamii,
riwaya pendwa na riwaya pevu zote huonyesha uhalisia wa
matukio yaliyo katika jamii . mfano katika riwaya ya “
kufa na
kupona”
mwandishi anaonyesha matukio ya rushwa,usaliti ,mauaji ya
kiharifu na upelelezi ambapo mwandishi anamtimia mhusika piter
mpigania uhuru aliyewasaliti wenzake kwa kuiba “nyaraka za
siri “ Uk 91.
Pia
DR Dikson Njoroge aliyeahidiwa kupewa rushwa na wareno ili
kufanikisha wizi wa karatasi za siri (uk 99 ). Pia Benny
anayefanya mauwaji ya kiharifu ili kulinda “nyaraka za siri
walizoziiba (uk 53). Hivyo hivyo katika riwaya ya
“Nyota ya Rehema”
mwandishi anaonyesha matukio kama vile Dhuruma ambapo
mwandishi anaonyesha rehema anadhurumiwa shamba la Ramwe
aliyopewa na Baba yake (Fuad ) enzi za uhai wake na akina
salma na karim (uk -150).
.Zifuatazo
ni tofauti kati ya riwaya pevu ya “Nyota ya Rehema “ na
ile ya “Kufa na Kupona” unadhihirika katika mambo
yafuatayo ;-
Mtindo
,huu ni upekee wa mwandishi ambao hutofautisha kazi ya
mwandishi mmoja na mwingine katika riwaya ya “Nyota
ya Rehema”
mwandishi ametumia mtindo
wa wimbo.
Kwa mfano pale Rehema alipoanza kukalili nyimbo za
kubembelezea wototo.
“ukimpenda
mwanao
Na
wa mwenzio mpende,
Wako
ukimpa chenga
Wamwezio
chenjegere
Humjui
akufaaye
Akupaye
maji mbele……………”
“Nyamaa
mama nyamaa
Nyamaa
usilie ,
Ukilia
waniliza
Wanikumbusha
ukiwa
Ukiwa
wa baba na mama” (uk 49 na 50)
Vilevile
mwandishi ametumia
mtindo
wa nafsi ya tatu umoja na pia nafsi ya
kwanza
umoja,
mfano “Mansuri alimtazama Rehema aliyekuwa akingojea jawabu
kwa hamu “ (nafsi ya tatu umoja ) (UK 43). Na matumizi
madogo ya nafsi ya nafsi ya kwanza mfano “ningependa kwenda
huko rakwe nikakuona kulivyo “ alisema Rehema (uk 86). Na
katika riwaya ya “Kufa
na kupona”
mwandishi ametumia matumizi ya simu.mfano ni pale polisi
walipompigia willy kumjulisha Benny aliwasiliana na nani. Kama
vile :
Hello ,Joe huyu
“ “polisi stesheni hapa”
Basi hii simu
ilikuwa inapigwa huko laving green ,kwenye nyumba ya Dr.
Dickson Njoroge “ . uk 80.
Vilevile
kuna matumizi ya nafsi ya kwanza umoja “nilipiga simu kwa
chifu saa hiyohiyo nikimweleza kuwa awashauri maofisa polisi
wasishugulike sana na mauaji mengi yatakayotokea “.
Katika
riwaya pendwa mhusika mkuu ni mkwezwa ilhali katika riwaya
pevu mhusika mkuu ni wakimapinduzi.
Mfano katika riwaya ya Kufa
na kupona
mhusika Willy
Gamba
amekwezwa na mwandishi kwa kumpalia sifa kama ,mwenye nguvu
,jasiri na mwenye uwezo mkubwa wa kupambana ,mfano mwandishi
anamwinyesha mhusika Gamba akipambana na kundi la watu kumi
na tatu na bado akawashinda anasema …
“..walipotaka
kuanza kunifyatulia risasi haraka nikawafyatulia mfululizo.sita
tayari chini nilipiga risasi mkono wa pita risasi ikaanguka
chini bila ya kuwa nayo bastolla,ksha nikawamalizia wale wane
waliobaki”………(uk 93).
Pia katika riwaya ya
“Nyota ya Rehema”
mwandishi anamwonyesha mhusika mkuu Rehema
kama mwanamapinduzi pale ambapo moja alipotoroka nyumbani
kukataa mateso ya mama yake wa kambo (uk 22) pia kujiepusha
kuingiliwa kimwili na mansuri kwa kumuuma meno na kupata
nafasi ya kujiokoa (uk 65) tatu ,kupitia jitihada ya kufanya
kazi kama ufugaji na kilimo ili kupambana na maisha yake
na mmewe aliyemchagua kuishi naye (uk 104)
Riwaya
imetumia lugha rahisi na inayoeleweka ilihali riwaya pevu
imetumia lygha ngumu. Kwa mfano katika riwaya ya nyota ya
rehema mwandishi ametumia misamiati ambayo si rahisi kuelewa
maana yake mfano bigija,dhiyaa,ghila (uk 170) pia mwandishi
ametumia mafumbo kama ubwebwe wa shingo haujamtoka………(uk
45) lakini, katika riwaya Kufa na kupona mwandishi ametumia
lugha rahisi na inayoeleweka na iliyo na methali mfano
mtaka cha sharti ainamen (uk 44).
Matumizi
ya taharuki
taharuki kama hamu ya msomaji kujua matokeo ya kitu Fulani
katika riwaya pevu matumizi ya taharuki hutumika kwa kiasi
kidogo mfano katika riwaya ya Nyota ya Rehema,taharuki
imejitokeza ktika (uk
12) mwandishi anasema
“jina lako
nani ? Faud alijisikia akiuliza kwa sauti iliyokuwa si yake
Adili
; alisikia jawabu akija
Aligeuka
kumtazama na macho yao yakakutana ,roho zao zikaumana
…………milele. Baada
ya hapo hakuna chochote kilichoendelea baada ya hapo
mwandishi ametuacha kwenye taharuki. Ilhali katika riwaya
pendwa taharuki hujitikeza kiasi kikubwa mfano katika riwaya
ya kufa na kupona wandiishi anathibitsha katika ukurasa wa 7
kama ifuatavyo “Amani lete madebe ya petrol na kiberiti”.
Hii ni baada ya Sammy na willy kukamatwa na benny hivyo
basi msomaji anapata hamu ya kujua nini kitatokea baadaa ya
kuletwa petrol na kiberiti.
Pia
katika ukurasa 45 taharuki imejitokeza pale willy aliposema
“alinivuta akaanza kufungua tai yangu,kasha shati langu ,
halafu suruali yangu……….. tukajilaza . pia hapa msomaji
atataka kuelewa kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
Pia
katika ( uk 67 ) ni pale ambapo willy anamkuta lina
amechomwa kisu na mtu aliyemfahamu na anataka kumuuliza bila
mafanikio. Hivyo msomaji Napata maswali je? Lina atakufa au
atapona baada ya kujeruhiwa vibaya na mtu asiyefahamika
Vilevile
taharuki nyingine imejitokeza pale ambapo willy Gamba
alivyokamatwa na benny na akaambiwa asali sala yake ya
mwisho kabla sijammiminia risasi kama mwenzake (uk 89 ).hivyo
msomaji anapata taharuki kuwa je? Anaweza kufa au kunusulika?
Lakini hata Gamba mwenyewe anakuwa yuko kwenye taharuki je?
Anaweza kunusulika.
Wahusika
katika riwaya pevu huakisi hali halisi ya maisha ilhali
wahusika katika riwaya pendwa hupewa uwezo mkubwa usio wa
kawaida wa kutenda matukio yanayosawiriwa
Wahusika katika riwaya pevu huakisi hali halisi katika
jamii
riwaya hizi waandishi wametumia wahusika wao ambao ni
tofauti dhidi ya uwakilishaji wao wa uhalisia wa mambo.
Riwaya ya “Nyota ya Rehema” kama Rehema alipokuwa
akipambana kupata mali yake ya urithi wa mali ya baba yake
Faud, ambaye alifariki.hali hii ya urithi wa mali kwa mtu
aliyefariki ni hali halisi kwa sababu yanatokea. katika jamii
. mwandishi anathibitisha katika (uk 143) “
konde zilizomo na shamba lenyewe ni mali ya yangu bwana
muridi na mimi ndiye motto wa maarehemu bwana Faud…………………..
. Na katika riwaya ya “KUFA NA KUPONA “ mwandishi
ameonyesha hali isiyo halisi kwa kumtumia mhusika Gamba
aliyepewa uwezo mkubwa pale anapopambana na watu kumi na
watatu na kuwashinda . hali hii si ya kawaida katika
jamii.Katika (uk 93) walipotaka
kuanza kunifyatulia risasi haraka nikawafyatulia mfululizo.sita
tayari chini nilipiga risasi mkono wa pita risasi ikaanguka
chini bila ya kuwa nayo bastola ,kasha nikawamalizia wale
wakiobaki”
Katika riwaya
pendwa mwanamke amechorwa kama chombo cha anasa na katika
riwaya pevu mwanamke amechorwa kama mlezi na mzazi.
Mwandishi wa riwaya ya kufa na kupona anaonyesha ambavyo
lina na lulu wanavyojidhihirisha na masuala ya anasa kama
kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mhusika Benny aliyekuwa
mharifu katika wizi wa nyaraka za siri (uk 3) lakini
mwandishi wa riwaya ya “Nyota ya Rehema “ anamwonyesha
Bii kiza katika nafasi ya mlezi kwa kumlea Rehema baada ya
kifo cha mama yake (Aziza) pia Rehema anachorwa kama mzazi
na mlezi wa mwanae aliyeitwa Faud baada na kuonana na
sulubu mume aliyemchagua mwenyewe (uk 44)
Suluhu ya
matatizo katka Riwaya pevu hutolewa hali ambayo ni tofauti
na riwaya pendwa .
suluhu ya matatizo katika riwaya ya “Nyota ya Rehema “
imedhihirika pale ambapo mhusika Rehema baada ya kupiia
mikasa mingi katika maisha ambayo ilimfedhehesha, mfano kufa
kwa mama yake (Aziza ) safari yake ya kutoroka nyumbani kwao
,maisha magumu aliyokuwa nayo mjini ,kudhurumiwa haki ya
urithi lakini badi hakukata tama,hatimaye akampata sulubu
ambaye kwake alimuona ni mume mchapakazi na chaguo lake katika
maisha. Ilhali katika riwaya pendwa, suluhisho la matatizo
haijaonyeshwa , kwani mwandishi wa riwaya ya kufa na kupona
anaonyesha mwisho wa riwaya kuwa Lulu anawapigia simu
Tofauti nyingine
ni riwaya pevu imejikita katika mkondo wa kihalisia ilihali
riwaya pendwa imejikita katika mkondo wa kipelelezi,
mkondo wa kiuhalisia ni aina ya mkondo ambao hueleza jambo
katika uhalisia wake. Katika riwaya ya nyota ya rehema
mwandishi amejaribu kueleza matatizo mbalimbali yanayoakisi
jamii zetu. Mfano; ugumu wa maisha ,watu kunyimwa haki zao
mwandishi katika (uk 143) anathibitisha
“
Konde zilizomo
na shamba lenyewe ni mali yangu bwana Mudiri na mimi ndiye
mototo wa marehemu bwana Faud……………”
. Hapa mhusika Rehema alikuwa akijitetea pindi alipokuwa
anataka kudhurumiwa shamba wakati ni haki yake kabisa. Hivyo
basi haya ni masuala ya kihalisia kabisa katika jamii zetu.
Lakini mkondo wa kipelelezi ni aina ya mkondo ambao hujikita
kuzungumzia masuala ya mapenzi, upelelezi na ujasusi katika
riwaya ya Kufa na kupona tunaona mwandishi ameeleza na
kuonyesha vya kutosha masuala ya upelelezi na mapenzi mfano
katika (uk 66) mwandishi anasema
“ kwa
hiyo kazi kubwa sasa ni kutafuta kwa kila njia tumjue huyo
“ bosi mi nani. Na habari nilizozipata kwa James hizo
karatasi zinabadilishwa kesho usiku………. .Hapa
ni Willy alikuwa anazungumza na Sammy.hivyo basi hapa
inasibitisha kuwa hawa wanajihusisha na vitendo vya upelelezi.
Pia masuala ya mapenzi katika riwaya hii pia yapegusiwa kama
sifa mojawapo mwandishi katika (uk 105)
“Oh
Willy,nilikuwa nakuota sasa hivi umenikumbatia ,kumbe ni kweli
.Oh ,sasa nimepona kabisa ,nibusu Willy nirejewe na uhai”.
Hapa ni lina baada ya kukutana na Willy.hivyo basi hii
inathibtisha riwaya pendwa imejikita katika mkondo wa
kipelelezi.
Kwa
kumalizia riwaya pendwa na riwaya pevu zote kwa ujumla
hubeba dhima za fasihi nia na madhumuni ni kufikisha ujumbe
mzito uliokusudiwa kwa jamii lengwa ,mfano wa dhima hizo ni
kuelimisha ,kukosoa ,kuburudisha kuonya ,kutunza historia ya
jamii hivyi basi fasihi ya riwaya inamchango mkubwa katika
jamii.
MAREJELEO
- Madumila, J.A. (2009),Riwaya ya Kiswahili,Nadharia Historia na Misingi ya Uchambuzi Dar-es-Salaam:Mture Education Publishers.
- Masebo, J.A.(2007), Nadharia ya Fasihi (Fasihi kwa Ujumla).Dar-es- Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers.