Ubunifu SHAIRI LA KITENDAWILI
Ubunifu
SHAIRI LA KITENDAWILI
KITENDAWILI.
Kitendawili
natega, wateguzi tegueni,
Njiwa
niliyemfuga, sitomla asilani,
Ingawa
kanivuruga, kunitia matatani,
Wateguzi
tegueni, kishindwa nipeni mji.
Hutembea
kwa madaha, na mbawa huziachia,
Nisijepata
fedheha, wangu ndege kujilia,
Nabakia ni kihaha, sijue pakushika,
Wateguzi
tegueni, kishindwa nipeni mji.
Siupati
usingizi, kutwa nakesha nahaha,
Ninamuomba
mwenyezi, niondolee karaha,
Niuone
upuuzi, nisijepata fedheha,
Wateguzi
tegueni, kishindwa nipeni mji.
Miti yote
nitakwea, wa nyumbani tanishinda,
Wahenga
waliomea, usemi waliuunda,
Kwa wote
walozoea, njiwa wao kuwapenda,
Wateguzi
tegueni, kishindwa nipeni mji.
Ngekuwa wa
bwana Juma, ningemla kwa miluzi,
Nisingepata
tuhuma, na wala kipingamizi,
Ningeenda
kiheshima, kuwajulisha walezi,
Wateguzi
tegueni, kishindwa nipeni mji.
Kufuga sasa
ni basi, sijepata vishawishi,
Niepuke
usabasi, wa ndugu wenye utashi,
Uniondoke
uasi, ili niweze kuishi.
Wateguzi
tegueni, kishindwa nipeni mji.
Siye njiwa
wa tunduni, yafaa kuwaambia.
Wala yule
wa porini, na hili kuzingatia,
Iwaingie
kilini, na jibu kunipatia,
Wateguzi
tegueni,kishindwa nipeni mji.
Tamati
nimefikia, wateguzi tegueni,
Maize
mlobobea, kwa kirefu fikirini,
Sahihi
kunipatia, majibu yenye thamani,
Wateguzi
tegueni,kishindwa nipeni mji.
Shairi hili litaendelea; TOA MAONI
YAKO.