MBINU TANO ZA KUWA MTUNZI BORA WA MASHAIRI


 

MBINU TANO ZA KUWA MTUNZI BORA WA VITABU VYA MASHAIRI
Mshairi ni mtu au msanii anayeandika kazi mbalimbali sanaa ya ushairi. katika fasihi ya kiswahili kuna washairi wenge sana mfana hayati Shaaban Robert, Amri Abeid kaluta, M.M mlokozi, Kalikoyela Kahigi, Haji G haji, Mohammed Seif Khatibu, na wengine wengi.

Watu hawa ndio waliotengeneza njia mpaka kizazi cha leo bado kinatamani na kuupenda ushairi. hata hao pia kuna watu ambao waliwatengenezea njia mpaka wakafikia pale walipofika.

Sanaa ya ushairi inajumuisha vitu vingi sana mfano mashairi yenyewe, nyimbo, tenzi/tendi, maghani, ngonjera na n.k.

Utanzu huu wa fasihi ni tofauti kidogo na tanzu zingine kama vile riwaya na tamthilia, kwani miundo ya riwaya na tamthilia ni tofauti sana na ushairi hivyo basi hapo ndipo inapoibuka dhana ya kwamba ushairi ni mgumu. dhana hii ya ushairi ndio imetawala miongoni mwa vijana hata baadhi ya walimu wanadiliki kuwaambia wanafunzi wao kuwa ushairi ni mgumu kwa hiyo mimi sitawafundisha, wakati anasahau kuwa ushairi ndio tanzu taamu kuliko zote katika fasihi ya kiswahili .

Kwa nini vijana wengi siku hizi wanaukimbia ushairi kuuchambua, kuandika vitabu vya ushairi, kughani na hata kuutamba.

1.  Woga/ hofu ya kujaribu kufanya.
2.  Hamasa na motisha toka kwa waliotangulia
3.  Nia ya dhati ya kufanya
4.  Dhana pandikizi kuwa ushairi mgumu.
5.  Vijana wengi husoma kwa ajili ya kufaulu mtihani.
6.  Watu wengi huzania ushairi ni kipaji pekee na huwezi kujifunza mtu akaweza.
7.  Ari ya kujisomea imepotea sana siku hizi miongoni mwa vijana.
8.  Kasumba ( lugha ya kiswahili)
9.  Mchango mdogo kutoka kwa walimu mashuleni.
10.Gharama za vitabi na zana mbalimbali zinazohusu ushairi.


MBINU ZA KUWA MTUNZI BORA WA MASHAIRI PAMOJA NA VITABU YA USHAIRI.
kwa mtazamo wangu mimi nadhani mbinu zifuatazo zinaweza kusaidia wasanii wa ushairi na waandishi wa vitabu vya ushairi kazi zao kuwa bora zaidi
 
1. kusoma kazi nyingi za washairi waliopita pamoja na nadharia za ushairi.
2. kusikiliza vipindi vya kiwahili na kusoma kamusi ili kuongeza msamiati.
3. kutengenesha utamaduni wa kuandika mara kwa mara ( shairi 1 kwa siku)
4. kubari kukosolewa pindi unapoyawasilisha kwa watu.
5. andika kazi kulingana na wakati.
....................... ahsante..................
Powered by Blogger.