Jinsi ya kutambua kura zilizoharibika, halali
Elimu ya Mpigakura
Dar es Salaam. Jumapili ni siku muhimu ya
kuhitimisha harakati za kisiasa zilizodumu kwa takribani miezi sita
ikijumuisha kutangaza nia, kuchukua fomu, kutafuta wadhamini, uteuzi
ndani ya vyama mpaka kampeni za majukwaani. Kufanikisha hilo, unatakiwa
kufahamu yafuatayo:
Kura iliyoharibika ni ile ambayo;
1. Haina alama yoyote.
2. Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja,
3. Imeandikwa jina la mpiga kura,
4. Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha
ya mgombea
5. Haina muhuri wenye alama rasmi
Kura sahihi;
1. Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku.
2. Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea.
Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa
mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako