Siasa Paul Kagame anarudi Madarakani mwaka 2017? Hii hapa kutoka Mahakamani Rwanda..
Mahakama Kuu Rwanda imepokea Shauri kutoka Vyama vya Upinzani Rwanda ambavyo vinahitaji Rais Paul Kagame asigombee Urais kwa awamu nyingine tena baada ya kumaliza awamu mbili za kuiongoza Nchi hiyo.
Jopo la
Majaji nane litajadili ishu hiyo, japo Serikali iliweka pingamizi
Mahakamani kwamba kisijadiliwe chochote lakini jopo hilo linaloongozwa
na Jaji Immaculee Nyirinkwaya lilitupilia mbali pingamizi hilo na Shauri litaendelea kusikilizwa Mahakamani September 23 2015.
Rais Kagame hakuwahi
kutamka kama atagombea awamu ya tatu ya Urais au hapana, lakini kila
alipoulizwa amekuwa akijibu kwamba hayo ni maamuzi ya Watu wa Rwanda
wenyewe kumruhusu aendelee au hapana.
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu ishu ya Katiba ya Rwanda kufanyiwa mabadiliko ili kumruhusu Kagame agombee tena Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2017 lakini upande wa Upinzani wameonekana kutokubaliana kabisa na mapendekezo hayo.
Rais wa Marekani Barack Obama ni mmoja ya Viongozi ambao hawakubaliani na kitendo cha Kiongozi yoyote kubadili Katiba ili aendelee kubaki Madarakani >>> ‘Nadhani
mimi ni Rais bora kabisa, hata nikisema nigombee Urais wa Marekani kwa
mara nyingine ninashinda… Hakuna mtu anatakiwa kuwa Rais milele, ni
vizuri mkapeana nafasi na mwingine aje aongoze akiwa na mawazo mapya‘- Hii ni nukuu ya alichokisema Rais Obama akiwa kwenye ziara Ethiopia July 2015.