Lori laanguka na kuziba barabara muhimu Nairobi
Msongamano
mkubwa wa magari umeshuhudiwa katika moja ya barabara kuu za kuingia
jiji la Nairobi baada ya lori kuanguka na kufuziba upande mmoja wa
barabara.
Ajali hiyo ilitokea usiku mita chache baada ya kupita mzunguko wa barabara wa Museum Hill ukielekea Nairobi.
Eneo hilo liko karibu na chuo kikuu cha Nairobi.
Barabara hiyo hutumiwa na watu wanaotoka maeneo ya magharibi mwa jiji na pia magharibi mwa nchi kama vile Naivasha na Nakuru, Eldoret na Kisumu.