Wenger atangaza kung’atuka 2017


Kocha wa Arsenal, Arsenal Wenger
London, England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametikisa kiberiti kwenye klabu hiyo ya London Kaskazini akieleza kuwa anafikiria kuiacha ifikapo 2017.
Kauli hiyo ya Wenger kwenye mkutano wa mwaka wa klabu hiyo juzi, iliwachochea mashabiki wa klabu hiyo kusema yaliyo mioyoni mwao.
Wakiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii, mashabiki wa Arsenal walionyesha kugawanyika, baadhi wakieleza kuwa kauli yake ilikuwa imechelewa.
Wengine walieleza kuwa haifai kocha wao kuiacha klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa mwishoni mwa msimu ujao.
Wenger kwa upande mwingine alisema: “Nimedhamiria kuendelea na kibarua changu hadi mwisho wa mkataba wangu, ndoto yangu ni kuiachia klabu hii mafanikio ili nikumbukwe kokote niendako.
“Kitu muhimu kwangu ni kuona naiacha klabu ikiwa vizuri, inaweza kufanya vizuri zaidi.”
Hadi sasa, Wenger ndiye kocha aliyeitumikia klabu ya Ligi Kuu England kwa miaka mingi, akifuata nyayo za aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.
-
Powered by Blogger.