Majeshi ya Marekani kubaki Afghanistan

Obama amesema kuwa majeshi ya Afghanistan haviwezi kuhimili vitisho vya Taliban
Rais wa Marekani,Barack Obama ametangaza kuongeza muda wa majeshi ya Marekani kuwepo nchini Afghanistan.
Takriban wanajeshi 10,000 wataendelea kubaki nchini humo kwa kipindi hasa cha mwaka ujao.
Wakati ambapo Rais Obama anaondoka madarakani mwaka 2017, kutakuwa bado kuna wanajeshi 5000 nchini Afghanistan.
Obama amesema vikosi vya Afghanistan havina nguvu bado ya kupambana na tishio linaloongezeka kutoka kwa wanamgambo wa Taliban.
Washington pia imesema inatarajia kuendelea kuungwa mkono na washirika wake, na kuwa mazungumzo kuhusu suala hili yamekwisha anza.
Obama ameweka wazi kwa Taliban kuwa makubaliano ya kisiasa na Serikali ya Afghanistan kutafanya majeshi ya Marekani yaondoke Afghanistan.
Powered by Blogger.