MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA SITA KISWAHILI - 1
MTIHANI WA UTAMILIFU
KIDATO CHA SITA
KISWAHILI - 1
121/1
Muda:
Saa
3:00
FEB 2017
Maelekezo
1. Karatasi hii ina maswali kumi (10) katika sehemu A, B, C, D na E.
2. Jibu maswali saba (7) kwa kuzingatia maelekezo kutoka katika kila sehemu.
3. Kila sehemu ina alama ishirini (20)
4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
5. Vikokotozi haviruhusiwindani ya chumba cha mtihani.
6. Swali lisilo na namba halitasahihishwa.
SEHEMU A (Alama 20)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kasha jibu maswali yanayofuata.
“Kwa
watu ambao walikuwa watumwa au ambao walikuwa wakionewa, wakinyonywa na
kunyanyaswa kwa sababu ya ukoloni, ukabaila na ubepari, “maendeleo”
maana yake ni “Ukombozi.” Kitendo chochote kinachowapa uwezo zaidi wa
kuamua mambo yao wenyewe na kutawala maisha yao wenyewe ni kitendo cha
maendeleo japo kama hakiongezi afya wala shibe, kitendo chochote
kinachowapunguzia uwezo wao wa kuamua mambo yao wenyewe na kutawala
maisha yao wenyewe si kitendo cha Maendeleo, ni kitendo cha kuwarudisha nyuma japo kama kitendo hicho chenyewe kinaongeza afya na shibe kidogo.
Kwetu sisi, maendeleo
ya maana ni yale yanayotuondolea kuonewa, kunyonywa, kunyanyaswa na
mawazo ya kufungwa na kutuongezea uhuru na utu wetu. Kwa hiyo katika
kufikiria maendeleo ya taifa ya watu na kupanga mipango ya maendeleo ya wakati wote mkazo mkubwa utiliwe kwenye maendeleo ya watu na sio vitu. Ili maendeleo
yao yaweze kuwa ya watu, watu wenyewe ni lazima washiriki katika
kufikiria kutekeleza mipango iliyoamuliwa na wataalamu na viongozi
wachache. Wajibu wa chama na serikali ni kuona kama viongozi na
wataalamu wanatekeleza mipango yao ya maendeleo iliyoamuliwa na wananchi wenyewe.
Uamuzi
huu wa wananchi unapokuwa unahitaji ujuzi wa hao viongozi na wataalamu,
ni wajibu wa viongozi na wataalamu hao kufikisha ujuzi huo kwa wananchi
ili waweze kujifanyia uamuzi wao. Lakini si haki kwa kiongozi au
viongozi na wataalamu kujinyakulia wajibu wa kuamua kila jambo badala ya
wananchi wenyewe, ati kwa sababu wao ndio wenye ujuzi. Ili wananchi
wawe na ari ya kuilinda na kuitumikia nchi yao lazima serikali ya chama
kwanza itilie mkazo sana hali ya uchumi wa wananchi. Mtindo wa uchumi,
tuliorithi kwa wakoloni ambao umewatupa wananchi wengi nje ya uchumi
lazima ubadilishwe bila kukawia na kuanzisha mipango ya kuongeza
matumizi na kuweka rasilimali katika wilaya zote. Kwa mfano; mpango wa
fedha za maendeleo mikoani inaweza kusaidia kuamsha shughuli za
kiuchumi na kuleta manufaa ya waziwazi kwa wananchi. Mpango huo
ukitiliwa mkazo kwa kuongeza fedha hizo, wajibu wa chama na serikali ni
kutilia mkazo na kuwashirikisha wananchi katika kazi mbalimbali za
kujenga taifa.
Maswali
(i) Taja kichwa cha habari kinachofaa kwa habari hii.
(ii) Kulingana na kifungu cha habari, maendeleo ni nini?
(iii) Maendeleo yanaweza kuwa ya watu kwa kufanya nini?
(iv) Wajibu wa viongozi ni nini?
(v) Mwongozo unapendekeza nini katika suala la maendeleo?
(vi) Ili wananchi wawe na ari ya kulinda nchi yao serikali haina budi kufanya nini?
(vii) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma.
(a) Ukabaila
(b) Kunyanyaswa
(c) Mawazo ya kufungwa
(d) Rasilimali
(e) Ukoloni
2. Fupisha habari uliyoisoma katika swali la kwanza (1) kwa maneno yasiyozidi 100.
SEHEMU B (Alama 20)
MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
Jibu maswali mawili 2 kutoka sehemu hii.
3. Onesha matumizi matano ya mofimu – ku - na utoe mifano miwili kwa kila tumizi.
4. Taja maneno manne yenye mzizi wa silabi moja na kwa kila neno tunga sentensi mbili.
5. Eleza kwa ufupi jinsi kamusi inavyomwezesha mtumiaji lugha kujitegemea.
6. Utengaji wa mofimu katika maneno ya Kiswahili si jambo rahisi. Fafanua matatizo manne
yanayoweza kujitokeza wakati wa kutenga mofimu za maneno.
SEHEMU C (Alama 20)
UTUNGAJI
Jibu swali la saba (7)
7. Andika barua kwa mhariri wa gazeti la Mwangaza ili kutoa mchango wako wa mawazo
kuhusu ajali za barabarani. Jina na anwani yako viwe: Maisha Mapambano, S.L.P 60213
MBEZI BEACH-DAR ES SALAAM
SEHEMU D (Alama 20)
MAENDELEO YA KISWAHILI
Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.
8. Huku ukitoa mifano fafanua mambo matano yanayochangia kudhohofika kwa lahaja za
Kiswahili.
9. Fafanua hoja tano zinazothibitisha umuhimu wa kusanifisha lugha.
SEHEMU E (Alama 20)
TAFSIRI
Jibu swali la kumi (10)
10. Tafsiri matini ifuatayo katika lugha ya Kiswahili.
What the Arusha Declaration Said
As
we celebrate 50 years of Independence of Mainland Tanzania, it is
inevitable that we look at some salient features of the Golden Jubilee
and some of the most talked about issues at home, abroad and is still a
subject for hot debates, is the Arusha Declaration.
This
is because the Arusha Declaration has politically, socially and
economically heavily impacted on the lives of individuals and the nation
in general, both positively and negatively.
There
are people who still think the Declaration was timely and bore with sit
enormous and equal economic, social and political opportunities for
all, and its abandonment is the cause for the present economic and
social calamities.