VITABU MBALIMBALI
“EPUKA KUFA KABLA
YA WAKATI”
Je wataka kuishi
miaka mingi?
Kifo
Kifo ni nini?
Ni kuharibu au mwisho wa kitu, Maisha ya mwanadamu au uhai wa
mwanadamu hatima yake ni kifo au mauti. Hakuna mwanadamu yeyote anayeweza
kuepuka au kukimbia kifo.
“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kusishi si nyingi,
naye hujaa taabu (Ayubu 14:1-2)
Kifohakichagui wazuri, wabaya, warefu,
wafupi n.k. Bali kila mmoja anakabiliwa na kifo na kila moja anasiku yake ya
kufa.Katika maisha ya mwanadamu kuna aina mbili za vifo,ambazo ni;
i. Kifo cha kiroho
Ni hali ya mtu kuwa hai kimwili lakini kiroho ni mfu au amekufa.
Mtu aliyekufa kiroho maisha yake huwa yamepungukiwa na nguvu ya kimungu na mtu
huyu hubakia na imani isiyo na matendo yaani mtu anakuwa
ni wa kumtaja Mungu kwa mdomo tu lakini matendo yake yanakuwa mabaya, ”Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya
kwamba anayo imani, lakini hana matendo?........vivyo hivyo na imani isipokuwa
na matendo, imekufa nafsini mwake” (Yakobo 2:14-17)
Unaweza kujiuliza,
ni kwa namna gani mtu anaweza kuwa hai kimwili na wakati huo huo asiwe hai
kiroho?.
Kufa kiroho au kuto kufa kiroho hutegemea namna mtu binafsi anavyo
ishi na Mungu wake kwani tukio hili la kufa kiroho huwa kwa katika nafsi au
roho ya mtu binafsi anavyoishi kwani tukio hili la kufa kiroho huwa katika roho
au natsi ya mtu mwenyewe “nayajua matendo yako yakuwa una jina la kuwa hai,
nawe umekufa (ufunuo 3:1).
Ni dhahiri mtu anakuwa hai kimwili, anaweza kuwa mhudhuliaji wa
Ibada na akafanya huduma zote kama kuimba, kusifu, kuhubiri, kuomba nk. Kakini
yeye akawa mfu kiroho.
Hii ni kwasababu huanzia moyoni kabla ya kutokeza nje ya mtu
mwenyewe.kila uharibifu wa kiroho wa mtu huanzia katika ulimwengu wa roho,
huiondoa na kuiharibu ile nguvu ya kimungu au Roho mtakatifu hofu ya mungu
iliyomo ndani ya mtu ili kumfanya mwanadamu afanye matendo au mambo ambayo ni
kinyume na utaratibu wa kimungu bila kuhudumiwa na chochote moyoni yaani bila
hata kufikiri, je ni dhambi au si dhambi?
i.
Kifo cha kimwili
Ni hali ya uhai au pumzi kutoweka kabisa.Aina hii ya kifo mtu
hawezi kuwa na uwezo wa kuongea chochote tena bali mwili huanza kuoza na mwili
huu mfu huzikwa ardhini.Mwanzo wa kifo ya kimwili
Ni pale Adam na Eva walipokengeuka (walipotenda dhambi) Mungu
alitoa adhabu ya kifo kwa wanadamu “………..kwa jasho la uso wako utakula,hata
utakapo irudia ardhi,ambayo katika hiyo ulitwaliwa;kwa maana u mavumbi
wewe,nawe mavumbini utarudi”(mwanzo 3:19)
Mungu alitoa adhabu hii ya kifo baada ya wanadamu kutenda
dhambi,tangu wakati huo hadi sasa kifo humkabili kila mwanadamu.
Je mtu akifa
anaenda wapi?
Mtu akifa huingia peponi (kuzimu) Yesu alipokuwa msalabani
alimwambia Yule mwizi aliyekuwa ametundikwa pamoja nae kuwa “amini nakwambia
leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (luka 23:43). Peponi kuna sehemu mbili
ambazo ni;
Ø Mahali pa mateso kwa watu wanaotenda mabaya.
Ø Mahali pa faraja kwa waliokuwa wanatenda mema.
“…… Basi kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso
Akamwona Ibrahimu kwa mbali, na lazalo kifuani mwake, akalia akasema, Ee baba Ibrahimu
niurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi
wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu…..”(luka 16:23-24)
Hivyo ukifa kama ulikuwa unatenda dhambi hivyo
utaelekea peponi kwenye mateso makali na kama ulikuwa unatenda mema utaelekea
peponi yaani mahali pa faraja.
Katika
habari za tajiri na maskini Lazaro (luka 16:18-25) Biblia inaelezea kuwa Tajiri
alikuwa peponi yaani ile sehemu ya mateso na Lazaro alikuwa peponi yaani mahali
pa faraja.
Wanadamu
wengi hujiuliza maswali mengi juu ya kifo cha kimwili, wapo wanaoamini kuwa
mwili huu utaurithi uzima wa milele. Baadhi ya watu huosha mwili (maiti) kwa
kuubinya ili kuondoa kila kilichopo tumboni kwani wanaamini mwili unaenda
peponi (mbinguni) lakini si kweli, kwani mtu anapokata roho (mwili kutengana na
roho) roho huondoka kwenda peponi na mwili hubaki ardhini, huzikwa kwani huoza
na kunuka,“……Damu na nyama haviwezi kuurithi ufalme wa mungu; wala uhalibifu
kurithi kuto kuharibika” (1Wakorintho 15:50) Hivyo mbinguni hatutakuwa
na miili ya kibinadamu kwani mili hii tuliyonayo sasani miili ya kuharibika,
Miili ya mbinguni ni ile isiyoharibika.
Hata
siku ya ufufuo watakao fufuliwa watakuwa na miili mingine na sio hii tuliyonayo
sasa.“…….Wafufuliwaje wafu?
Nao huja kwa mwili gani?36 Ewe mpumbavu!
Uipandayo haihuiki, isipokufa;37 nayo uipandayo,
huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au
nyingineyo;38lakini Mungu huipa
mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.39
Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani,
nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.40
Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya
mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.41Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine
ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya
nyota na nyota.42 Kadhalika na kiyama
ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika
fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu;44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa
roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu,
akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa
asili; baadaye huja ule wa roho.47 Mtu wa kwanza atoka
katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo
walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa
mbinguni.49Na kama
tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye
aliye wa mbinguni.50 Ndugu zangu,
nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala
uharibifu kurithi kutokuharibika.51 Angalieni, nawaambia
ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika. (1wakorintho 15:36-50)
Je wafu wanaweza kutudhuru?
Baadhi ya watu baada ya kufiwa na baba, mama,bibi,babu nk.
Hujisumbua sana wakiogopa kuwa wasipotambika au kujengea makaburi marehemu
atawaletea madhara .
Kutambika, kuwajengea makaburi marehemu ni kazi bure kwani biblia
inasema;
kwa
sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote,
wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
6Mapenzi yao na machuksio yao, na husuda yao,
imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote
lililofanyika chini ya jua.
Je wafu wanaweza kutusaidia?
Baadhi ya watu huomba kwa wafu pale
wanapokuwa na hitaji wanadhani wafu wanaweza kuwasaidia jambo lolote.“Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao,
imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katikajambo lo lote lililofanyika
chini ya jua. Kupmba kwa wafu au kuhitaji msaada mbele za watu ni chukizo mbele
za mungu wetu hivyo tunapaswa kumwomba mungu wetu na si wafu.
Pia
nikaona waovu wamezikwa, nao wamefika kaburini; tena waliofanya mema wameondoka
katika patakatifu, nao wamesahauliwa mjini. Hayo nayo ni ubatili. (mhubiri
8:10)
Pia (luka 16:19-30)Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya
zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa
mlangoni pake, ana vidonda vingi,21 naye alikuwa
akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata
mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu.
Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu
aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na
Lazaro kifuani mwake.24Akalia, akasema, Ee
baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe
ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya
kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo
alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi
kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala
watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27
Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie,
wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29
Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama
akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
Biblia inawaeleza juu ya habari ya tajiri na
maskini lazaro. Tajiri alitaka lazaro arudi duniani kuwasaidia ndugu zake
tajiri, lakini ombi lake halikukubaliwa, hivyo wafu hawawezi kuwasaidia walio
hai na kuwaomba wafu ni chukizo kwa Bwana Mungu wetu.
Pia baadhi ya watu huwatumia watakatifu wa
kule kama Mariamu (mama yake Yesu) kama wapatanishi na Mungu wetu na Mungu.
Mfano
Maria mtakatifu mama wa Mungu utuombee sisi
wakosefu ……………………
Mariamu alikuwa sawa na wanadamu wengine
isipokuwa alibeba mimba kwa uwezo wa Roho
mtakatifu,Bado haijulikani kama mbinguni kuna watu wanaokesha na kuomba hivyo
hatupaswi kumuomba Mariamu bali tumuombe Yesu Kristo kwani aliyempatanishi wetu
na Mungu ni Yesu kristo peke yake.
“Kwasababu
Mungu ni mmoja na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja ambaye ni Yesu
kristo”(1Timotheo 2:5)
Je
tuwaombee Wafu?
Tukumbuke
kuwa mtu akifa katika dhambi kinachobakia ni hukumu.
“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara
moja na baada ya kufa hukumu”
(waebrania
9:27)
Hivyo hata ukiomba au kufanya ibada juu yao
hawawezi kupata msamaha kabisa kwani Yesu alisema kuwa ,tajiri mwovu
alipokufa,aliingia mahara pa mteso wala hakupata msamaha au huruma hata ya
kupewa tone la maji.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake,
alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu,
nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi
wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
(Luka
16:23-25)
Pia katika “ matendo 5:1-11” Anania na Safira
walipomkosea Mungu na kufa kwasababu ya uongo wao hawakuzikwa kisha wakaendelea
kufanyiwa sala au ibada au Misa kwani ibada,misa au sala haviwezi kumsaidia kitu chochote mtu aliyekufa.
Je
Mungu anaweza kumtaarifu mtu kuhusu kifo chake au siku ya kufa?
Ndiyo Mungu anaweza kumtaarifu mtu juu ya
kifo chake au juu ya kifo cha mtu mwingine.Tuangalie ushuhuda wa Mwl
Christopher Mwakasege juu ya kifo cha Mwimbaji sedekia wa Arusha Tanzania;
Mwalimu Christopher mwakasege alitoa ushuhuda
katika semina iliyofanyika katika viwanja vya Furahisha vya jijini mwanza
semina hiyo yenye somo iliyoitwa “namna ambayo Roho mtakatifu awezavyo
kukusaidia ili upokee kile unachokiomba ilianza tar 19-7-2011 na iliisha tar
23-7-2011.
Alisema “Roho mtakatifu akuambiayo omba hiyo
haina MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate unachokiomba kwa kuwa
gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa kukipata ni ndogo
kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi hayo.
Roho matakatifu atakapokupa mzigo wa
kuombea jambo anakupa na muda ukizembea
muda huo ukipita kinakuwa ni kipolo, na kipolo kinaweza kikalika na kipo
ambacho hakiliki.
Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia kasha
akaanza kuumwa, madaktari waliniambia ubongo wake kwa asilimia tisini haufanyi
kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara nipo pale Hospitalini wakasema kwa
nini usikae Hotelini kasha ukawa unapiga simu kuuliza hali ya mgonjwa? Wao
hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa suala la kupiga simu tu sio tatizo
ningeweza kurudi arusha nikawa napiga simu.
Suala hapa ni kuw nilikuwa naenda kila mara
kwa ajili ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa kando kando ya Bahari ya Galilaya
nafanya maombi juu ya Sedekia kwa masaa sita nikitoka hapo nasikia upako wa
ajabu sana kasha napanda Taxi kuelekea Hospitali. Nikifika hospitali madaktari
na watu wa ICU walikuwa washanifahamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye chumba
cha nguo nabadili nguo kissha naingia ICU alikolazwa. Nikifika nambana Mungu
kwa maswali mengi namuuliza Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu Muda wote huo
si urudi? Na kisha namuuliza Yesu, hivi Yesu unafahamu kuwa Sedekia ana mke ukimchukua
mkewe utamwachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mikono juu yake.
Nilipokuwa naweka mikono juu yake ghafla upako wote unakuwa kama umenyonywa.
Baada ya hapo narudi hotelini naanza tena
kumuuliza Mungu hivi Mungu kama husikii maombi yangu, sikia maombi ya
watanzania kwa kuwa najua watanzania wengi walikuwa wanamuombea sedekia.
Inafika wakati nakata tamaa lakini ndani
yangu najisemea Mwakasege haiwezekani jitie moyo kasha nabadili maombi aina ya
maombi kwa kuwa nilikuwa nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake nikawa
naiweka kati kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini usiku
nazunguka nguo zake na passport yake huku nikifanya maombi.
Taraatibu Mungu akaanza kuniambia Sedekia
harudi, Kipindi hicho mimi na familia yangu tulikuwa tumepanga kwenda kupumzika
nchini uingereza wakati wa sikukuu ya krismass, na booking ya hotel tulikuwa
tumeshafanya, na watoto wote wako nyumbani wakijiuliza tunaendaje kupunzika
wakati Sedekia anaumwa? Chrismass ilipita na mwaka mpya pia kisha Sedekia
akafariki.
Baada ya kifo chake sikuchoka nikarudi tena
kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua Sedekia mikononi mwangu?
Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi nikasema hapa.
Kila siku mimi nikiwa katika maombi nahitaji ya ROHO anifundishe kwa upya
kwa kuwa sijui vita gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu atabaki kuwaMungu kwa
kuwa hufanya atakavyo”.
CHANZO CHA KIFO
Dhambi
Ni hali ya kufanya kinyume na maagizo ya mungu ambayo aliyaweka
ili sisi kama binadamu tuyafuate lakini si kila dhambi mwanadamu akitenda
anakufa kimwili.
“mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo na mauti, ataomba
na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo na mauti (1 yohana
5:16).
Si kila dhambi ukiitenda unakufa kimwili bali dhambi nyingine mtu
anakufa kiroho.Waumini wengi siku ya leo tunaabudu kama desturi, yaani tunaenda
ibadani ili watuone na si kufikiri nafsi zetu kama tunapenda mapenzi ya baba au
la! Wengine wanaenda kanisani ili kuwaheshimu viongozi wa dini na kulinda hadhi
zao walizonazo, serikalini, maofisini na makanisani.
Mungu alituumba kwa makusudi maalum, na hakutuumba kwa kubahatisha
au kwa bahati nasibu. Kama yeye ndiye aliyeumba kuku, nyoka ng`ombe, mimi na
wewe tuwe wanyama lakini kwa makundi maalumu aliweka tuwe wanadamu wenye akili
na utashi.
“Hata walipokaribia
yerusalemu na kufika Bethfage, katika mlima wa mlima wa mizeituni ndipo yesu
alipotuma wanafunzi wawili akawaambia, Enendeni mpaka kijiji kile
kinachawakabili na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye;
mfungueni na watu wakiwaambia neno semeni, Bwana anawahitaji, na mara huyo
atawapeleka (mathayo 21:1-3)
Katika eneo hili la Beth fage ambalo Yesu alikaribia kilikuwa na
punda wengi lakini punda huyu alifungiwa eneo hilo si kwa sababu mwenye punda
bali kwa kusudi la Yesu, yamkini hata mwenye punda hakulitambua hili.
Hata kwangu mimi na wewe leo tuliumbwa kwa makusudi na tu wazima
hadi leo si kwa maamuzi yetu kuwa wazima bali lipo kusudi maalumu la mungu
ambalo amepanga juu yetu ndio maana wengi wamekufa kwa ajali na magonjwa lakini
mimi na wewe tu wazima.
Mungu
alituumbaanategemea kupata matunda Fulani kwetu yaani tuzae matunda au matendo
mema.
Mfano Ukipanda mche wa tunda lolote kama Embe, Parachichiunategemea baada ya mti huo
kuwa mkubwa utazaa matunda hivyo unapalilia na kuwekea samadi (mbolea). Ndivyo
hivyo Mungu anategemea kupata matunda kutoka kwetu.
“hata asubuhi
alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia,
akauendea asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia yasipatikane matunda
kwako tangu leo na hata milele, mti ukanyauka mara. (mathayo 21:18)
Hapa tunaona jinsi Yesu alipoamua kuulaani mti ambao Mungu
aliuumba baada ya kuona hauzai matunda kabisa, tunaona mti huo ulinyauka na
kukauka kabisa, hivyo hata kwetu tunaweza tusifanikiwe katika maisha yetu lakini
pia kufa kabla ya wakati kwani hatuzai matunda.
Kwa nini Mungu alimuumba
mwanadamu.
Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano wake na kwa sura yake. Nia
ya Mungu ni kwmba anataka tuwe na tabia kama yake. Tabia ya kuumba
(creativity), kutawala, kuzalisha, kuponya na tabia nyingine zote nzuri.
Wakati Mungu anapomwokoa mtu kutoka dhambini huwa ………. Kwa mtu
maalumu alitemkusudia kwa wakati huo ili kutimiza mpango wake wa awali wa
kuwafanya wanadamu wawe mfano wake.
Mungu akasema na
tumfanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu
“(mwanzo 1:26)
Ili kulidhihirisha hili Mungu haoki watu wote kwa wakati mmoja,
lakini anafanya kwa kila mtu na wakati wake yeye ndiye anayepanga majira na
nyakati kwani ndiye anayejua mwanzo wa mwanadamu na maisha yake
Hivyo Yesu alivyokufa msalabani nia yake (Mungu) ni kuwarudisha
wale walioondolewa kwenye mpango wa Mungu wa kuwa kama Mungu nakuwa kama mtumwa
shetani.
“Nanyi mfahamu
kwamba mlikombolewa si kwa vitu vihalibikavyo, kwa fedha, dhahabu; mpate kutoka
katika mwenendo wenu usiofaa mliopokea kwa baba zenu “(1petro 1:18).
Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vitu vyote kama vile milima,
mito, mabonde, mbuzi, kuku nk. Angeweza kutuumba mimi na wewe tuwe wanyama
lakini kwa kusudi lake akatuumba tuwe binadamu si kwa kubahatisha bali ni kwa
makusudi maalumu.
SABABU ZA MUNGU
KUTUUMBA WANADAMU:
Ø Alituumba tuwe wanadamu ili tumwabudu yeye katika ukamilifu.
ü Kuabudu ni kutoa heshima ya ya hali ya juu (ya mwisho) kwa
kitu,mtu au kiumbe chochote.
ü Ni kuheshimu kwa nia yote kutoka ndani ya moyo bila kujali athali
au hatari yoyote ambayo yaweza kujitokeza kama athari mbaya za kufanya hivyo.
Kuabudu haimaanishi tu kuimba nyimbo za taratibu bali ni maisha ya
kumheshimu anayestairi kuheshimiwa kwa kila jambo.
Heshima hii anayestaili kupewa ni Mungu peke yake, na hii Mungu
hajaruhu kuchangia (kushare) na yeyote au chochote.
“mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana Mungu wako
niliyekutoa katika nchi ya misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na miungu
mingineila mimi.
Usijifanyie sanamu
ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilichopo juu ya mbingu wala kilichopo
duniani, wala kilicho majini na nchi kavu
(Kutoka 20:1)
Maelezo hapo juu mungu alizuia kuchonga sanamu yeyote na kuiabudu.
(Hesabu 19:4)“Msigeuke kuwandama sanamu
wala msijifanyizie Miungu ya kusujudu. Mimi ndimi Bwana Mungu wako”
Sanamu inayozungumziwa hapa si dhambi anayotenda mtu peke yake
bali hata kuchonga kinyago na kukisujudia pia kuabudu sanamu.
Heshima ya mungu tumpe mungu na si kupuga magoti mbele ya sanamu
ya bikira maria au mbele ya sanamu ya msalaba wenye sura ya Mungu, hili ni
kosa.
Wanadamu wa leo wapo wanaoabudu mali, magari, simu, nk. Yaani wanaviona
ni vitu vya msingi sana kuliko mungu, utamwona mtu yupo tayari asifike ibadani
ila aende akashughulikie mali yake.
Vitu vyote vilivyopo ni vya kitambo tu.
Mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako
zote.
Mungu
aliwaagiza wana wa Israel kumwabudu na kumpenda yeye tu nasi kitu kingine.
Mungu yupo peke yake katika utatu wake hana mbadala wake wa kufananishwa naye.
Si kila mtu anaweza kumwabudu Mungu kama
tunavyofikiria, ni watu wenye sifa hizi zifuatazo:-
·
Aliyetubu dhambi
Kutubu ni hali ya kuomba msamaha kwa kosa
ulilofanya.
Toba ni kugeuka kutoka dhambini na kumwelekea
Mungu.
“Tubuni basi mrejee ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati
za kuburudishwa kwa kuwako kwa Bwana(matendo
3:19).
Hivyo ili uweze kumwabudu mungu ni lazima
utubu kwanza ili dhambi zako zifutwe ndipo umwabudu Mungu katika roho na kweli
vinginevyo utamwabudu Mungu katika mwili tu hii ndio ibada iliyotawala kipindi
hiki.
Mtu anaabudu Mungu au anaabudisha (ni
muhumini)ndio huyo huyo mzinzi, mwizi,mchawi nk.
Je swali langu mimi na wewe Mtu mwenye tabia hii anamwabudu mungu
katika roho na kweli?
“Mungu ni Roho, na wamwabuduo yeye
imewapasa kumwabudu katika roho na kweli (Yohana 4:24).
Ili uweze kumwabudu mungu katika roho na
kweli ni lazima utubu dhambi zako zote kwanza kwani mungu hawezi kushuka na
kukaa mahali pachafu, endapo hutatubu basi huwezi kumwabudu mungu katika roho
na kweli, utakuwa unajidanganya mwenyewe.
Ø Aliyemsamehe
aliye/waliomkosea
Kusamehe
ni hali ya kumhurumia au kumfutia makosa mtu aliyokukosea bila kujali umri,
kabila wala jinsia, bila kujali kosa alilokukosea kwani bila kusamehe na Mungu
hawezi kukusamehe wewe pia.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na baba yenu wa mbinguni
atawasamehe ninyi makosa yenu. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba
yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu (mathayo 6:14).
Kutosameheni kipingamizi kikubwa cha kumwabudu mungu hivyo
tunapaswa kuwasamehe wengine ili kufanya moyo uwe safi kwa ajili ya kumwabudu
mungu.
Mungu hushuka wakati wa sifa hivyo usipowasamehe waliokukosea
hutaweza kusifu na hutakutana na Mungu katika maisha yako.
“Lakini panapo
usiku wa manane Paul na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za
kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza ............. (matendo16:25).
Kwa mujibu wa maelezo hayo ya mistari ya biblia hapo juu mtu
anapoishi maisha matakatifu hukutana na Mungu wakati wowote.
B.KUMTUMIKIA MUNGU KWA
BIDII
Kumtumikia mungu ni kukubali kuungana na Mungu katika mpango wake
wa wokovu duniani.
Ni kukubali kutumika na Mungu katika kila jambo analolitenda,
yaani kuona ulimwengu kama Mungu anavyouona kuwa umeharibika.
Usimtumikie mwingine yeyote au chochote au vyovyote kuliko mimi
usimtumikie Mungu kwa sababu unahitaji kitu Fulani toka kwake.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana mungu wako
(torati 5:9)
Kumtumikia Mungu ni kufanya kazi ya Mungu, kuna namna nyingi za
kumtumikia Mungu kama ifuatavyo;
Ø
Kutenda mema
Mungu ametuumba ilitutende mema na si
mabayawakati Fulani unaweza kujiuliza mema ni yapi na mabaya ni yapi?
“Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala
hayatendi kwake hayo ni dhambi (yakobo 4:17).
Yapo mambo mangapi ambayo ni mema Na yapo
mambo mangapi ambayo tu kutenda lakini hatuyatendi?
Ni vema kutafakari na kujithamini, je ni
kweli tunatenda mema? Au hatutendi? Mema tunamfurahisha Mungu au
hatumfurahishi?
Na nini matokeo ya kutenda mema? Haya yote
yapo mikononi mwako.Wapo wanaojipotosha wenyewe na kufanya matendo maovu kuwa
mema huku wakimsingizia Mungu kuwa alimruhusu.
Mfano:Wapo watu wanaoamini kuwa ukinywa,
usipolewa si dhambi na wana kunywa kileo au vileo
.(22
Ole “wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu
kuchanganya vileo;”Isaya 5:22).
Kweli halisi kuwa si kweli mungu hakuruhusu
ulevi wa aina yoyote bali alikemea ulevi tena alikemea kwa ukali.Pia si kweli
kuwa mlevi anaweza kunywa lakini asilewe hizi ni ndoto,sni vigumu mlevi kuacha kunywa kama hajalewaacheni
kujidanganya ulevi ni dhambi sawa na dhambi nyingine.
“11 “Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate
kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama
moto ndani yao!”(Isaya 5:11)
Kama unajidanganya kutumia vileo ukidhani
ulevi sio dhambi ni vyema ukatubu leo na dhambi yeyote ile hawezi kutubu kwa
kusali sara Fulani mara kadhaa,wala viongozi wa dini hawana mamlaka ya kusamehe
dhambi bali wanapaswa kutuombea ili Mungu atusamehe na sio wao watusamehe kwani
Mungu husamehe pale mtu anapotubu toba ya kweli.Wapo viongozi wa kiroho
wanaowaonea aibu kuwakemea waumini wao wanapotenda dhambi kwa kuhofia
kuwapoteza au kukosa waumini,viongozi wa namna hii wanatenda dhambi kwani
wanawapotosha waumini hivyo wanapaswa kuwaelekeza njia inayostahili.
Ø Kujitoa na kumtolea Mungu
Mungu alimuumba
mwanadamu akampa vitu vingi avitawale wanyama, ndege wa angani nk. Nasi
tunapaswa kumtolea kwa kumshukuru kwa uhai (afya njema) yeye ndiye mpaji wa
vyote. Wanadamu katika suala ya kutoa huwa tunaona kama ni suala la ziada na
halitiliwi maanani.
Mfano
Mungu anampa pumzi na
uhai na ikumbukwe wengine wamekufalakini mwanadamu hatoi sadaka au akitoa
anatoa vilivyo vinyonge kabisa, kama ni fedha basi anatoa chenji kama shilingi
mia ua mia mbili.
Swali la kujiuliza,
Je Mungu kamgusa atoe kiasi hicho au kwa uchoyo wake ameamua?
Inakuwaje kama
anakuwa na motto, anampa fedha au kitu halafu akimwomba tena anakunyima?
Mungu hapendezwi na
uchoyo wetu hivyo tunapaswa kumtolea sadaka iliyo safi.
Unaweza ukawa
mtafutaji lakini usifanikiwe kwa sababu ya kutomtolea Mungu sadaka, je
atakupatiaje riziki yako ikiwa wewe ni mchoyo
Nasi
twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao
katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. (warumi 8:28)
Kumpenda mungu si kusali au kuimba kwa juhudi
bali ni pamoja na kumtolea sadaka.
Leteni
zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa
njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya
mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. (malaki 3:10)
Hivyo Mungu akubariki unapaswa kuonyesha moyo
wa utoaji na si vinginevyo.
Ø Kumtukuza Mungu na kutumia vipaji au karama
ambayo Mungu ametupatia.
Mungu si mchoyo
alimpa kila mwanadanmu kipawa chake au karama yake kama uimbaji, uombaji nk.
Fanya kila jambo jema ambalo moyo wako au Roho mtakatifu atakavyokutuma
kufanya.
Kipawa
ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo
hufanikiwa. (mithali 17:8).
Ø Kumtafuta Mungu kila iitwapo leo
Wanadamu hujisahau na
kuona uzima na afya ni halali yao kuwa katika hali nzuri kumbe la hasha, ni
rehema za Mungu hivyo tu na huacha kuomba, kutubu na kumtafuta Mungu bali
hujikita katika kufanya mambo yasiyopendeza mungu, kumbukumbu ya kumtafuta au
kumrudia mungu huja pale mmoja anapokuwa amekufa au kufariki na mara baada ya
msiba kumalizika husahau kabisa uweza wa Mungu na nafasi yake kwa wanadamu.
6Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana,
Mwiteni, maadamu yu karibu; 7 Mtu mbaya na aache
njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye
atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. (isaya 55:6-7).
Je
kwanini mwanadamu anakufa?
Kifo
kilitokea wapi?
Chanzo cha kifo ni dhambi baada ya Adamu na
Eva kutenda dhambi pale bustanini ambapo
Mungu aliwaweka,Mungu alitoa adhabu ya mauti
kwa mwanadamu .
kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata
utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe,
nawe mavumbini utarudi.
Ni dhairi kuwa kabla ya Adamu na Eva kutenda
dhambi, Mungu hakuleta mauti kwa wanadamu hivyo kifo au mauti kinapoonekana
pale wanapokengeuka na kutenda dhambi hapo ndipo wanadamu walipoanza kufa.
Lakini swali kubwa la kujiuliza ni hili kwa
nini wanadamu wanatofautiana katika umri wa kufa?
Wengine wanakufa bado watoto wadogo wengine
vijana na wazee.
Hata wakati wa agano la kale wanadamu
walitofautiana katika kufa japo wao waliishi miaka mingi kama vile zaidi yetu.
Adamu
(miaka 930 mwanzo 5:3-5)
Adamu
akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake,
akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa
miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamsu alizoishi ni miaka mia
kenda na thelathini, naye akafa.
Sethi
(miaka 912 mwanzo 5:6-8)
6Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa
Enoshi.7 Sethi akaishi baada
ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.8Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi
na miwili, akafa.
Enoshi
(miaka 905 mwanzo 5:9-11)
9 Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.10Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka
mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na
mitano, akafa.
Kenani
(miaka 910 mwanzo 5:12-14)
12Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa
Mahalaleli.13 Kenani akaishi baada
ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.14Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na
kumi, akafa.
Mahalaleli
(miaka 895 mwanzo 5:15-17)
15Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano,
akamzaa Yaredi.16 Mahalaleli akaishi
baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na
wake.17Siku zote za
Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
Yaredi
(miaka 962 miaka mwanzo 5:18-20)18Yaredi akaishi miaka
mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.19Yaredi
akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na
sitini na miwili, akafa.
Henoko
(miaka 365 mwanzo 5:21-24)
21Henoko akaishi miaka sitini na mitano,
akamzaa Methusela.22Henoko akaenda pamoja
na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.23Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na
sitini na mitano.24 Henoko akaenda
pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
Mathusela
(miaka 960 mwanzo 5:25-27)
25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na
saba, akamzaa Lameki.26Methusela akaishi
baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana,
waume na wake.27 Siku zote za
Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
Lameki
(miaka 770 mwanzo 5:28-31)
28Lameki akaishi miaka mia na themanini na
miwili, akazaa mwana.29 Akamwita jina lake
Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono
yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.30
Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana,
waume na wake.31 Siku zote za Lameki
ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
Wanadamu hawa walioishi mwanzoni baada ya
Mungu kuumba ulimwengu walitofautiana umri wao katika kufa japokuwa wao
waliishi miaka mingi zaidi wingi wao waliishimiaka mia tatu (300) hadi miaka
960.
Swali
kubwa ni kwanini hata wao walitofautiana hata kama waliishi miaka mingi?
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano,
akamzaa Methusela.22 Henoko akaenda
pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na
wake.23 Siku zote za Henoko
ni miaka mia tatu na sitini na mitano.24
Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. (mwanzo 5:21-24).
Kwa mujibu wa maelezo haya Henoko hakufa bali
Mungu alimtwaa hivyo ni dhahiri kamba dhambi ni kikwazo kikubwa cha kuishi
maisha marefu.
Wakati wa Nuhu Mungu alileta adhabu ya kifo
kutokana na ukengemfu uliokuwa unafanyika.
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa
nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,2
wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia
wake wo wote waliowachagua.3 Bwana akasema, Roho
yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku
zake zitakuwa miaka mia na ishirini. (mwanzo 6:1-3).
Kwa mujibu wa mistari hiyo hapa juu ya dhambi
ilimfanya Mungu awape adhabu ya kifo kuuangamiza ulimwengu na vyote vilivyomo.
1 Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa
yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu
katika kizazi hiki.2 Katika wanyama wote
walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi
wawili wawili, mume na mke.3 Tena katika ndege wa
angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.4Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea
dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya
juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.5
Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru.6
Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu
ya nchi.7 Nuhu akaingia katika
safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya
maji ya gharika.
8
Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote
vitambaavyo juu ya nchi,
9 wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili
wawili, mume na mke, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.10Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya
gharika yakawa juu ya nchi.11 Katika mwaka wa mia
sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile
chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni
yakafunguka.12 Mvua ikanyesha juu
ya nchi, siku arobaini mchana na usiku.13
Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi,
wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye;14 wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake,
na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa
juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna
yo yote.
15 Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili
wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.16 Na walioingia, waliingia mume na mke, wa
kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; Bwana akamfungia.17 Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku
arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi.18 Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya
nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji.19
Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako
chini ya mbingu ikafunikizwa.20 Maji yakapata nguvu,
hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. 21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi,
na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho
chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;22
kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako
katika nchi kavu.23 Kila kilicho hai juu
ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na
kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu,
na hao walio pamoja naye katika safina.24
Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.
Nuhu na watoto wake ndiyo watu pekee ambao hawakuathiriwa
na gharika hiyo kwani Safina ilielea majini na kwenda kutua katika milima ya
Ararah ipo katika bara la ulaya hata leo hivyo Dunia kuangamizaw kwa maji ni
tukio halisi na la kweli.
Unapojiona wewe binafsi Mungu amekuumba,
mahali na sehemu yoyote ile ulipotambua wewe si wa kwanza, kuishi hapa ulimwenguni,
wapo walioishi hapa Duniani, walipokengeuka aliwahadhibu vikali na kufutilia
mbali vitu vyote alivyokuwa ameviumba, usione kama amejiweka au amejikita yeye
mwenyewe duniani tafakari kwa makini nini hatima ya maisha yako? Je unaenda
vyema kama Henoko na Huhu? Kama sivyo basi tengeneza na mungu leo maana wakati
huo Maana Mungu alitoa adhabu kwa ulimwengu mzima lakini je leo atatoa hivyo?
Bali anaanza na habari ya mtu binafsi ikiwemo kufa kabla ya wakati.
19
Nazishuhudizasi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na
mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; (torati
30:19)
Pia wakati wa Ibrahimu, Mungu aliiangamiza
miji ya Sodoma na Gomora kwa moto.
Sodoma na Gomora ni miji ambayo ilikuwa
karibu na mwisho wa kusini ya bahari ya chumvi lakini kutokana na matetemeko ya
nchi Bahari ilienea zaidi na kufunika mabaki ya magofu ya miji ile.
Eneo la kuzunguka sodoma lilifaa kwa kufuga
wanyama na kwasababu hii Lutu alihamia huko (mwanzo 13: 10-13)
Wakati mmoja, Sodoma ilishambuliwa na maadui,
Lutu alichuuliwa akawa mfungwa. Lakini Ibrahimu alichukua baadhi ya walinzi na
wafanyakazi wake wakawashinda maadui na kumweka Lutu humu. Ibrahimu alitambua
kuwa Mungu ndiye aliyempa ushindi na hivyoalikataa thawabu yoyote kutoka kwa
mfalme wa sodoma na gomora. (mwanzo 14:1-24)
Watu wa Sodoma na Gomora walikuwa wenye
dhambi nyingi, hasa zili dhambi za ufiraji.
1 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa
amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama
kifudifudi.
2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi
mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi
mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku
kucha.
3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia
nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.
4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji
wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande
zote.
5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale
watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
6 Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango
nyuma yake.
7 Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu,
msitende vibaya hivi.
8 Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua
mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu,
ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.
9 Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu
huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu!
Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu,
wakakaribia wauvunje mlango.
10 Lakini wale watu wakanyosha mikono yao,
wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.
11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni
kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.
12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye
mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji,
uwatoe katika mahali hapa;(mwanzo 19:1-12)
Mungu aliamua
kuangamiza miji hiyo lakini Ibrahimu aliamua amwomba azuie hukumu yake kama
mwenye haki kumi wangepatikana mijini
humo. Lakini wenye haki hawakuonekana huko na miji hiyo miwili iliangamizwa
lakini Lutu na familia yake walitoroka kabla ya hukumu yake . (mwanzo 18:22-33)
Mafuta, aina ya lami,
chumvi na kiberiti vilionekana kwa wingi katika eneo lile (mwanzo 14:10) na
vitu hivyo vilitumika kuangamiza Miji. Maafa yale ya moto yalikuwa kazi ya
Mungu kwa sababu wakati wake na ukubwa wake ulikuwa sawasawa kama Mungu alivyokuwa
ametabiri kabla
24 Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na
moto toka mbinguni kwa Bwana. (19:24)
Bwana Yesu alipokuja duniani aliwaonya
wayahudi waliosikia mafundisho yake na kuona matendo yake lakini walimkata,
wangepata hukumu kali kuliko watu wa miji ya Sodoma na Gomora wasiosikia habari
zake.
Hata wakati wa Yesu (kipindi cha agano jipya)
Yesu alionya na kueleza uwepo wa kifo yaani kimwili na kiroho katika mafundisho
yake.
51
Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. (yohana 8:51).
Mauti ya kifo ambacho Yesu anazungumzia hapo
juu ni mauti au kifo cha kiroho, kifo ambacho mtu anakuwa bado kimwili ila
moyoni mwake anakuwa amemkana kristo.
Pia Yesu alionyesha uwepo wa kifo cha mauti
ya mwili pale alipomfufua Lazaro.
4
Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya
utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
5 Naye Yesu alimpenda
Martha na umbu lake na Lazaro.
Hapa
Yesu alidhihirisha uwepo wa mauti au kifo kwa wanadamu lakini bado alionyesha
namna mungu alivyo na nguvu hata katika mauti au kifo kwani alimfufua hata
Lazaro aliyekuwa na siku kadhaa kaburini.(yohana 11:4-5)
Je
ni nani mwenye nguvu za kuzuia mauti au kifo kwa mwanadamu?
Kama ilivyonenwa kuwa chanzo kikubwa cha
mauti au kifo cha kabla ya dhambi, tunapaswa kumcha Mungu na kuachana na
uovu.
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi,
Ewe mauti, uchungu wako?56Uchungu wa mauti ni
dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. (1 korintho 15:55-56)
Dhambi husababisha kifo katika namna mbali mfano, mtu akiwa mzinzi au muasherati
atakufa kwa magonjwa au atafumaniwa na kupigwa na mwenye mume au mke hadi kifo,
mtu akiwa mlevi basi anaweza kunywa vileo vikali mpaka vikaharibu mwili wake
akafa kabla ya wakati, Mwizi anaweza kupigwa mpaka kufa.
MAONO
NA MALENGO YA MUNGU KWA MTU BINAFSI.
Mungu humuumba mtu kwa makusudi yake haumbi
kwa kubahatisha, wala kwa bahati nasibu ila Mungu anakuwa na lengo maalumu,
haijalishi kama mtu binafsi anatambua au hatambui,
Swali
la kujiuliza; Je wanadamu wote wanafahamu kuhusu hilo?
Wanadamu wengi hawafahamu chochote kuhusu
kuhusiana na malengo ya Mungu kwa mtu binafsi, wapo walioumbwa kwa ajili ya
kuongoza, kumsifu Mungu, kutangaza habari za Mungu (kuhubiri Injili) nk.
Mungu hujishughulisha na kumgeuza mtu asiyefahamu
kabisa habari za Mungu ili aone umuhimu na nafasi ya Mungu katika maisha yake na
kuanza kumtumikia Mungu popote pale Mungu atakapotaka.
Mungu hashughuliki na mtu aliyeisikia sauti
yake na kuibeza au kuipuuza.
Baadhi
ya wanadamu ambao hawakumjua Mungu lakini Mungu aliwageuza:-
Paulo
au Sauli
Jina la asili la Paulo ni Sauli. Alikuwamyahudi
safi aliyezaliwa mjini Tano huko Asia ndogo yamashariki-kusini.
11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika
njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso;
maana, angalia, anaomba; (matendo 9:11)
Kwa kuzaliwa
kwake alirithi upendeleo wa raia wa kirumi.
37 Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu
wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa
wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe. (matendo 16:37)
Paulo alikulia huko akisema, kusona na
kuandika lugha ya kiyunani na kiebrania bila shida totote. Ushawishi wa
kiyunani katika masomo yake ulimpa uwezo wa kufikiri wazi na akili timamu na
ushawishi wa kiebrania ulisaidia kujenga ndani yake tabia ya ukweli na unyoofu
na maadili safi. (wafilipi 3:6)
Akiwa kijana mwenye bidii ya dini, Paulo
aliamiaYerusalemu alipopokea mafundisho kuhusu sheria ya kiyunani kufuatana na
mapokeo yenye nidhamu ya mafarisayo. Mwalimu wake alikuwa Rabi (mwalimu wa
kiyunani)mwenye sifa sana, yaani Gamalieli (matendo 22:3-6,26:5)
Paulo alikuwa fundi wa kushona hema (matendo
18:3)
Bidii yake ya kiyunani ilimchemsha Paulo
achukie wakristo kwa hasira kali, alifikiri kuwa Stephano alikuwa mwasi dhidi
ya sheria hiyo na hivyo alistahili hukumu ya kifo. (matendo 6:13)
Alipata mamlaka katika baraza kuu la wayahudi
(yaani Sanhedrin) aliongoza adha
kali dhidi ya wakristo, aliwafunga wanaume na wanawake na kuwapeleka magerezani
(matendo 8:3, 9:1-3)
Paulo alifikiri kuwa wakristo walikuwa na
hatia ya kufufua kwa sababu walimwamini masihi aliyekuwa msalabani kwa sababu
mtu aliyekufa msalabani alikuwa chini ya laana ya Mungu. (matendo 26:11)
Paulo alivyokuwa njiani kwenda Dameski ili
akawakamate wakristo na kuwapeleka gerezani, alipatwa na tukio la ajabu sana
lililombadilisha kabisa. Yesu mwenyewe alijidhihilisha kwake na jambo hili
lilimhakikishia kuwa Yesu yu hai.(matendo 9:3-5).
Maana yake ilikuwa Yesu hakuwa chini ya laana
ya Mungu. Alikufa si kwa sababu alikuwa amevunja sheria, bali kwa hiari yake
mwenyewe alichukua laana kwa ajili ya watu waliokuwa wamevunja sheria hiyona
ufafanuo wake ulikwa uthibitisho maalum kuwa Mungu aliridhika naye.(warumi 1:4)Galatia 3:13)(Galatia 6:14)
Wakati huo huo ambapo Paulo alibadilishwa
mawazo yake kuhusu Yesu, ufufuo wa Yesu Ulitokea uliodhihirisha kuwa yeye Paulo
angetumiwa awe mtume/mtumishi wa mungu wa kimataifa.
15
Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu,
alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
Nami
nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe
unaniudhi.(matendo 9:15)
16
Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii,
nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo
ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
17 nikikuokoa na watu
wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao;
18 uwafumbue macho yao,
na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na
kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao
waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. (matendo 26:15-18)
Tangu wakati huo Paulo hakuacha kustajabia
kazi ya Mungu ya kumwokoa mtu yeyote aliyekuwa adui makali wa ukristo na
kumfanya mjumbe wa ukristo huo.
Kwa
njia hii Paulo alitambua sehemu ya maisha yake.
8
na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa
si kwa wakati wake.
9 Maana mimi ni mdogo
katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la
Mungu.
10 Lakini kwa neema ya
Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali
nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya
Mungu pamoja nami.(1 korinth 15:8-10)
8
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema
hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; (efeso 3:8)
Paulo aliokoka (aliongoka) mwaka 32 baada ya
kristo (B.K)
Baada ya kuokoka Paulo alihubili sehemu mbali
mbali kama vile Dameski, Yerusalemu(matendo 9:22-26)Uarabuni wakristo wengi wa
Yerusalemu walikuwa na mashaka kuwa endapo kuongoka kwake haikuwa jambo la
kweli. Laini Barnaba hakuwa na mashaka. Baada ya kumpeleka na kumtambulisha kwa
Petro na Yakobo ndugu yake Bwana wasiwasi ulikwisha.(matendo 9:26-28).
Paulo alipata upinzani toka kwa wayahudi,
Alipanda meli kutoka kaisaria hadi sham (Syria) ya kaskazini na kutoka huko
alisafiri kupitia kilikia hadi tarso.(matendo
9:29-30)Lakini Paulo hakuacha kuhubili habari njema bali aliendelea kufanya
hivyo katika miji mbali mbali kama vile korinth, mileto, na troa. . (2 timotheo
4:13-20)
Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso.
Alifungwa gerezani lakini hakuacha kumtumikia
Mungu, alipokuwa gerezani aliandika barua kwa wajoli wake ambao ni kwanza
Timotheo
Tito alipotoka gerezani aliandika waraka wa
mwisho ambao ni waraka wa mwisho wa timotheo. Paulo aliuawa mjini Rumi mwaka 65
baada ya kristo (B.K)
Je
unajifunza nini kutoka kwa Paulo.
i.
Mungu hamuokoi mtu
bila dhumuni/lengo maalum Paulo aliokolewa ili awe mtumishi au mtume. Mimi na
wewe leo “Mungu hajatuokoa ili tukae
kanisani tu” bali tuwaeleze wengine habari za Yesu kama alivyofanya Paulo Je
tumewashuhudia wangapi ili wamjue Mungu?
ii.
Tunapaswa kumuuliza
Mungu kuhusiana na kazi yake, kumuuliza Mungu ili akwambie kalama yako ni
vyema, Je nikutumikie katika lipi katika uhai wangu? Mungu atakuambia nini
ufanye.
iii.
Katika kufanya kazi
ya Mungu usiogope kitu chochote hata kifo kwani mungu alikuwa na Paulo hata
alipokuwa gerezani alifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu Mungu hawezi kukuacha,
atakuokoa dhidi ya kifo hadi pale kazi na lengo la kukuokoa litakapotimia hivyo
utaishi maisha marefu.
YUSUFU
Mungu alikuwa aaamemuhaidi Ibrahimu na uzao
wake nchi ya kaanani, lakini wazao wake wangeweza kumiliki nchi ile kama idadi
yao ingetosha kwa kazi hiyo, lakini kabla ya yote walipaswa wajengeke na kuwa
taifa.(mwanzo 15:1)
Biblia inaeleza matukio yalivyosababisha
wazao wale wahamie misri ili wapate kuongezeka.
22 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia,
akamfungua tumbo. 23 Akapata mimba,
akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu. 24Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana
aniongeze mwana mwingine. Mwanzo
30:22-24)]
Ingawa walipoamia misri walipata mateso ya
wakati wa utumwa baada ya kkufa kwaeke Yusufu, wakati ulipotimia walihama
kutoka misri na kuhamia kaanani.
13Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya
kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale,
nao watateswa muda wa miaka mia nne. 14
Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali
mengi. 15Lakini wewe utakwenda
kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. 16Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana
haujatimia uovu wa Waamori bado. (mwanzo 15:13-16)
KUPELEKWA MISRI
Yusufu alikuwa mwana wa 11 wa Yakobo, lakini
akiwa mwana wa kwanza wa Raheli, Alipendwa sana na baba yake. Yusufu alipopata
umri wa miaka 17, kaka zake walimchukia kiasi kwamba waliamua kumwondoa.
Walimwuza kama mtumwa kwa wafanyabiashara wa misri, ingawa walimwambia baba yao
kwamba Yusufu ameliwa na mnyama mkali.
23Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake,
wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa,24wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo
birika ilikuwa tupu, hamna maji. 25 Nao wakakaa kitako
kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja
wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane,
wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.26
Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu,
na kuificha damu yake? 27 Haya, na tumwuze kwa
hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu
yetu. Ndugu zake wakakubali.28 Wakapita wafanya
biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza
Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu
mpaka Misri. (mwanzo 37:23-28)
Ingawa Yusufu alikuwa na maisha safi
kimaadili, alifungwa gerezani. Kwa sababu ya tabia yake nzuri alipewa kazi ya
madaraka gerezani iliyonufaisha wafungwa wengine gerezani lakini alingojea watu
wafikena kumsaidia.
1Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa,
akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao
Waishmaeli waliomleta huko.2Bwana akawa pamoja na
Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja
naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.4 Yusufu akaona neema machoni pake,
akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo
akayaweka mkononi mwake.5 Ikawa tokea wakati
alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana
akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu
ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa
Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula
alichokula tu.7 Ikawa baada ya mambo
hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana
wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote
alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi,
wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje
ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?10 Akawa akizidi kusema
na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende
kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema,
Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.13 Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo
yake mkononi mwake, naye amekimbia nje,14
akawaita watu wa nyumbani mwake, akasema nao, akinena, Angalieni, ametuletea
mtu Mwebrania atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa
sauti kuu.15 Ikawa, aliposikia ya
kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake kwangu, akakimbia,
akatoka nje.16Basi akaiweka ile nguo
kwake hata bwana wake aje nyumbani.17
Naye akamwambia kama maneno hayo, akisema, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta
kwetu, aliingia kwangu anidhihaki.18
Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje.19Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe
aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake
ikawaka.20Bwana wake akamtwaa
Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo
humo gerezani. 21 Lakini Bwana akawa
pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. 22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu
watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye
aliyeyafanya.23 Wala mkuu wa gereza
hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu; kwa kuwa Bwana alikuwa pamoja
naye. Bwana akayafanikisha yote aliyoyafanya. (mwanzo 39:1-23)
Kutokana na Yusufu kukataa kulala na mke wa
potifa, mke wa potifaalimshika nguo zake alimwambia lala name, lakini Yusufu aliacha
nguo yake na alikimbilia nje.
Mke wa Potifa aliwaita wote watu wa nyumbani
mwakena kuwaambia Yusufu ameingia chumbani ili alale na alipotaka kupiga yowe
Yusufu alikimbia alikimbia na kuacha nguo. Taarifa hizi zilimfikia Potifa na
aliamuru Yusufu awekwe gerezani. Lakini bado Mungu hakumwacha Yusufu bali
alikuwa pamoja naye.
Mwishoni mtu mmoja alimwambia mfalme habari
ya hekima ya Yusufu, yeye mfalme aliweza kumwonya mfalme kuhusu maafa ya njaa
yaliyokabili nchi yake, akatoa ushauri juu ya kushinda maafa yale. Mfalme
akastaajabu sana hata akamfanya Yusufu awe mtawala wa miradi ya kukabiliana na
maafa ya njaa, kasha Yusufu akawa mtawala wan chi yote ya misri (mwanzo
41:1-45)
YUSUFU
KUTAWALA MISRI
Yusufu aliwekwa kuwa mtawala wa misri alikuwa
na umri wa miaka 30.
46 Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini,
aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa
Farao, akapita katika nchi yote ya Misri. (mwanzo 41:46)
Alimwona mwanamke wa mmisri na akapata wana wawili
yaaniManase na Efraimu.
Misri ilikuwa nchi pekee iliyokuwa imefanya
maandalizi kwa ajili ya maafa ya njaa na hivyo watu walitoka kila sehemu ili
wanunue chakula. Miongoni mwao walikuwa kaka zake Yusufu aliwatambua nduguze.
Bali wao hawakumtambua yeye.
8 Yusufu akawatambua nduguze, bali wao
hawakumtambua yeye. (mwanzo 42:8)
Yusufu aliishi kwa muda zaidi ya miaka tisini (90) na aliendelea kuamini
kuwa Kaanani ilikuwa nchi ambayo watu wake siku moja wangeipokea kama nchi
yao.kablaya kufa kwake aliionyesha imani yake katika ahadi za Mungu akitoa
maaagizo kwamba kama watu wake siku moja wangeamia Kaanani wachukue maiti yake
na kuizika Kaanani.
JE
TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA YUSUFU
a) Mungu hakumuumba kila binadamu kwa kusudi
maalumu. Lakini si binadamu wote ambao hujitambua na kumuuliza Mungu nini
anawaagiza wafanye bali huona kama wamezaliwa kwa bahati mbaya tu. Mungu
alimwandaa Yusufu kuja kuwa mtawala wa misri na hakutaka apite mojakwa moja
kuwa mtawala bali alimwandalia njia maalum ya kufikia kuwa mtawala.
b) Mungu huyatimiza mambo yake kwa wakati na
majira yake. Mungu alikuwa na uwezo wa kumwondoa Farao haraka na kumweka yusufu
hatakama alikuwa na umri mdogo lakini wakati wake Mungu wa kumweka mtawala wake
ulikuwa bado haujafika. Hata katika maisha ya kawaida unapokuwa namaisha ya
shida, adha, dhiki unaweza ukaona kama Mungu hakuoni kutokana na kumuomba jambo
Fulani kwa muda mrefu lakini Mungu anawakati wake wa kutenda ili ukuu wake
uonekane.
c) Mungu hamwachi mtu mwaminifu na anamwagiza
tuwe waaminifu. Yusufu alishawishiwa na mke wa Potifa ili alale nae lakini Yusufu
alikataa kwa kujua kuwa angelala naye angekuwa amemkosea Mungu. Hata sisi leo
tunapaswa kuwa waaminifu hata kufa bila kujali mazingira wala kuogopa kitu
chochote kile na tusishawishike na kitu chochote kile kumkosea Mungu.yusufu
alifungwa gerezani lakini bado alikiri ukuu wa Mungu bila kukengeuka wala
kumkosea Mungu.
d) Mtu yeyote anayejitambua yeye ni nani mbele
za Mungu humuepusha na mauti/kifo.ndugu zake Yusufu walitaka kumuuwa lakini MUNGU
Salimtumia kaka yake Yusufu aitwae reubeni kuzuia wasimuue na mawazo yao
yalibadilika na wakamweka kwenye birika na baadae wakaamua kumuuza.
Hata sasa Mungu
huzungumza na wanadamu kuhusu kuacha njia zao mbaya na kumtumikia lakini
binadamu wengi hupuuza kile ambacho Mungu anawaagiza wafanye, hali hii humfanya
Mungu atuache na matokeo yake ni kufa kabla ya wakati. (luka 13:6-9)
e) Ikiwa Mungu yu pamoja nasi tusiogope wala
tusiwe na hofu
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa
mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo
yako vyanifariji. (zaburi 23:4)
Mungu ndie aliyetuumba, anatuongoza na anajua hata siku ya kufa
iliyo halali kwa kila mtu.
Si kila mauti/kifo Mungu anakuwa amemwita mtu huyo, bali kulingana
na uasi wetu shetani hutusababishia kifo bila ya hata sisi wenyewe kujua.
Hivyo si kweli kuwa “BWANA
AMELETA NA BWANA AMETWAA” kwani si kila anaye kufa Bwana amemwita.
Mfano
Umekimbiza pikipiki
au gari kupita kiasi ukapata ajali ukafa nayo utasema Bwana ameleta na Bwana
ametwaa?
Mungu anaweza kuzuia mauti kwa mtu yeyote kwa kumpa taarifa
mwenyewe au kutoa taarifa hapa kupitia kwa mtu mwingine, mara nyingi Mungu
hufanya hivyo kwa mtu aliyekuwa amekengeuka ili amrudie kwa kumpa taarifa mtu
ambaye ni mzee hivyo kwa wakati wake wa kufa umefika au mtu aliyetembea vyema
na mungu. Tuone hahari za “Hezekia”
1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika
hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia,
Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake
ukutani, akamwomba Bwana, 3 akasema, Ee Bwana,
kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo
mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. 4 Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,
5 Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa
Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi
yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.(isaya 38:1-5)
Hezekia alikuwa mfalme wa Yuda alitawala
mwaka 716 hadi mwaka 657 B.K yake ilikuwa katika hali ya kusikitisha. Siasa ya
Ahadi aliiicha Yuda katika hali ya udhaifu ya kiuchumi na upnde wa dini
isiharibike kwa kufuata dini za kinyume. Hezekia alijitwisha kazi ya kuimarisha
hali ya nchi kuhusu uchumi, kupindua utawala wa washauri na kutengeneza dini ya
Yuda. (2 wafalme 18:1-8)
Manabii wa wakati wa mfalme Hezekieli
walikuwa Hosea, Isaya na Mika. Baada ya kuondoa uchafu wa dini za kinyume mjini
Yerusalemu mfalme Hezekiel alisafisha nchi. (2 nyakati 31:1)
Lengo lake lilikuwa taifa lote lifuate kanuni
za dini zilizowekwa na Musa na zilizoendelezwa na Daudi.
Mashambulizi dhidi ya waashauri ya yerusalemu
yalileta madhara makubwa kuliko Hezekia alivyokuwa ametazamia.
Siku moja Hezekia alikuwa mgonjwa sana hata
ikaonekana kama angekufa. Kwa jibu la maombi yake, Mungu alimwongezea maisha
yake miaka 15 hivyo alimwezesha kutawala Yuda katika matatizo yake. Kwa
kumshukuru Mungu Hezekia alitunga wimbo wa sifa kwa kupona kwake. (isaya
38:9-22)
Hivyo ni dhahiri kuwa Mungu anaweza kuzuia
Muti/kifo kwa mtu hasa anayeishi kwa kulifuata kusudi la Mungu, pale anapokosea
Mungu hutoa maonyo na kuelezea matokeo yake ili mtu huyo abadili njia zake
mbaya na amfuate yeye. Biblia inasema.
12
Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye. (mithali 3:12)
Mungu hutumia njia mbalimbali kuwaonya
wanadamu, lakini binadamu hukaidi yale Mungu anayoagiza na matokeo yake Mungu
huacha wanaokaidi wakaenda kama vipofuna matokeo yake ni kufa kabla ya wakati.
SABABU
ZA KUFA KABLA YA WAKATI
1. Uzinzi
au Uasherati.
Uzinzi ni ushiriki wa
kimwili ni baina ya watu waliooa au kuolewa wakishirikiana na watu wasio wa
ndoa yao yaani ushiriki wa kimwili nje ya ndoa au na mtu wa ndoa mwingine .
Uasherati ni ushirika
wa kimwili baina ya watu wasiooana.Uchafu unaofanyika au unaotokana na
uasherati na uzinzi kwa jumla tunaita zinaa.
2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na
awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. (1 korintho 7:2)
Maana ya kufanyika umoja au mwili mmoja wa
mwanamke na mwanaume mmoja katika ndoa ni kwamba, hakuna nafasi kwa mtu
mwingine awaye yote.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na
mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. (mwanzo 2:24)
Chanzo cha uzinzi au uasherati ni tamaa
mbaya, uasherati au uzinzi hutokea kwa sababu watu baada ya kujaribu kuzuia
majaribu ya tama ya kimwili, huichochea tu. Hawatawali mawazo na hisia zao na
baada ya muda mfupi hujiona kuwa hawawezi kutawala tabia zao.
24 Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na
kukuponya na ubembelezi wa mgeni. 25
Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho
yake. (mithali 6:24-25)
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye
mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. (mathayo 5:28)
Kufanya uzinzi au uasherati ni kuhatarisha
maisha pia ni chukizo kwa mungu, kwani matokeo ya uasherati na uzinzi ni
kuambukizwa magonjwa kama vile upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kaswende,
kisonono nk.
Ni vema ikumbukwe kuwa miili yetu ni hekalu
la roho mtakatifu hivyo tuinapaswa kuepuka uzinzi na uasherati kwani roho
mtakatifu huwa hakai mahali pachafu na Mungu atamwadhibu mtu yeyote anayechafua
hekalu lake.
15Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya
Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja
naye.18 Ikimbieni zinaa.
Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa
hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.19
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;20maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu. (1 korintho 6:15-20)
Mungu anasisitiza kupitia mtume paulo
kuzikataa tamaa za ujanani na kuziepuka kwani chanzo cha uzinzi na uasherati
husababisha kuvunjika hali ya kupelekea watoto kutangatanga na kukosa mwelekeo.
Wanandoa kuambukizana magonjwa kama vile ukimwi, kaswende, kisonono nk. Na
hupelekea kifo au mauti.
Uasherati au uzinzi hupelekea uzinzi
uliokithiri
2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza,
Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.3Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru
nini? 4 Wakasema, Musa
alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. 5Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo
yenu aliwaandikia amri hii.6 Lakini tangu mwanzo
wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.7
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;8na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata
wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.9
Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza
habari ya neno hilo.11 Akawaambia, Kila mtu
atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu
mwingine, azini. (marko 10:2-12)
Baadhi ya watu huacha wake zao na kutoa
taraka kasha anaoa tena, hali hii inasababisha uzinzi uliokithiri kwani
watakapoendelea kuishi na huyo mwanamke watakuwa wanazini.
Athari
za kufanya tendo la ndoa kabla ya kuoana (ndoa)
i.
Kufanya
tendo la ndoa kabla ya kuoana ni dhambi kufanya ngono kabla ya kuoana ni dhambi
kubwa kwani wanaofanya hivyo huhatarisha maisha yao kwa kuambukizana magonjwa
na baadaye kufa.
23Kwa maana mshahara wa
dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu
Bwana wetu. (warumi 6:23)
Hivyo kufanya tendo la ndoa kabla ya kuoana husababisha kifo cha kimwili
na kasha kuhukumiwa na kutupwa jehanamu.
ii.
Kuvamiwa
na maroho machafu katika kufanya ngono, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa
kienyeji na huko wanapewa madawa ya ajabu ambayo yanapelekewa kuvamiwa na
mapepo na kupenda au kuwa na hamu ya kufanya ngono kila wakati. Pia kutokana na
kupenda ngono wengine wamefanya na majini bila ya wao kujua na majini hayo
yanawamiliki na wao hawajui watatokaje katika vifungo hivyo .
iii.
Husababisha
majeraha na fedheha kubwa maishani katika kufanya ngono kuna majeraha ya maisha
kama vile magonjwa hatari kama Ukimwi, kaswende, kisonono nk. Majeraha haya ya
magonjwa yatapelekea mwili kupata maumivu makali na kumfanya mtu ashinwe
kufikia malengo aliyopanga,mwisho hubakia kujuta na kuwajutia watu walio
msababishia majeraha wakati huo upo kitandani. Mungu anaonya uzinzi kwa kukemea
kuwa kuzini na mwanamke ni upumbavu kabisa.
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33Atapata
jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
Hivyo kuzini ni chukizo kubwa kwa mungu wetu,
epuka kabisa ili uishi vyema na mungu wetu.
iv.
Kuwapa wengine miaka yako, uchunguzi unaonyesha mtu anayependelea
kufanya ngono mara kwa mara kabla ya ndoa hawezi kuishi miaka mingi/muda mrefu
na si hivyotuvijana hujiua kwa kujinyonga, huuana na kufa kwa sababu ya
mapenzi, wengine wanaugua hadi kufa angali wadogo na kupatwa na magonjwa mabaya
na hivyo waliostaili waishi hapa duniani na hivyo wanakuwa wamewapa
wengine miaka yao.
9 Usije ukawapa
wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; (mithali 5:9)
v.
Ni kuiangamiza nafsi yako. Nafsi kwa kiyunani Psuche, ndani yake kuna
hisia, akili na maamuzi ya mtu.
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. (mithali 6:32)
Hivyo kuiangamiza nafsi yako na kuangamiza
malengo/matarajio (future) yako na mipango yako uliojiwekea mwanzoni.
vi.
Utavunjiwa heshima
32
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.33Atapata jeraha na
kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. (mithali 6:32-33)
Siku zote Yule
unayefanya nae tendo la ndoa kwanza atakuona wewe ni mpumbavu kwa sababu
atakujua jinsi ulivyo sirini na hivyo atakudharau zaidi na kukutangaza kwa
wengine na wewe pindi utakapooa au kuolewa kwa kuwa nguvu zako uliwashibisha
wengine basi utavunjiwa heshima na wengine.
vii.
Kuwashibiasha wengine nguvu zako
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi
zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; (mithali 5:10)
Tendo la ndoa ni tendo ambalo linahitaji mtu
atumie nguvu (hasa mwanaume) hivyo kadri mtu anapofanya mara kwa mara
anajipotezea nguvu zake na kuwashibisha wengine na hivyo dhoruba itamkuta
katika ndoa yake kwa sababu hatakuwa na nguvu tena kama awali.
Ni vyema kuacha kufanya tendo la ndoa kabla
ya wakati ili kuishi maisha marefu.
(http://sanga .wordpress.com/2007/02/06/ndoa-2/) (Partick sanga ministries)
2.
Kutowaheshimu wazazi (Baba na mama)
16
Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku
zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu
wako.(torati 5;16)
Ni wazi kuwa uhusiano
mzuri na wa uhakika kati ya kijana na mtu wa wazazi wake humfanya afanikiwena
kinyume chake ni laana katika maisha na mtu huyo hawezi kuishi maisha marefu.
1Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika
Bwana, maana hii ndiyo haki.2 Waheshimu baba yako
na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,3
Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. (efeso 6:1-3)
Kwa mujibu wa maneno ya Mungu hapo kweli kuwa
usipowaheshimu wazazi ni vigumu kufanikiwa bali ni laana itakufatilia na mwishowe
unakuwa na muda mfupi wa kuishi yaani unakufa mapema.
3.
Kutokumcha Mungu
Kumcha mungu ni hali ya kuishi maisha yanayoongozwa na Hofu ya
Mungu yaani kuishi kwa woga dhidi ya Mungu bali kuishi maisha ambayo moyo,
mwili, nafsi na roho ya mtu inakuwa imejazwa na kiu pamoja na njaa ya
kumpendeza Mungu na kufanya mapenzi yake yote kwa furaha.
27 Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu; Bali
miaka yao wasio haki itapunguzwa. (mithal 10:27)
Pia ili ufanikiwe katika mambo yako yote ni
lazima umche Mungu kwani yeye ni kila chanzo cha kila kitu kitu iwe fedha,
mali, kazi vyote vyatoka kwake.
7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali
wapumbavu hudharau hekima na adabu. (mithali 1:7)
Hivyo ukimcha Mungu utaishi maisha marefu na
hata katika mambo yako utafanikiwa kabisa yaani rohoni na mwilini pia.
4.
Kutomtumikia Mungu.
25
Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji
yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26
Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na
hesabu ya siku zako nitaitimiza. (kutoka 23<25-26)
Watu wengi hukwepa kazi ya
kumtumikia huona kazi ya kumtumikia Mungu ni ya watu Fulani tu. Mungu alituumba
ili tuzae matunda kwake (tumtumikie)
Hata asubuhi
alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.19Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake
ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele.
Mtini ukanyauka mara. (mathayo 21: 18-19)
Kukwepa au kukimbia kufanya kazi ya Mungu ni
laana. Biblia inasema kuwaYesu alipouona mti aliuendea asione matunda aliulaani
kwani aliuumba kwa makusudi maalum. Swali langu mimi na wewe Je tangu
tulipookoka/kumjua Mungu tunamtumikia?
Kama hatumtumikii basi anapoona atumtumikii
anatulaani kamailivyokuwa kwa mti na matokeo yake tunakufa mapema. Hivyo
tafakari mwenendo wako na nini umefanya kwa Mungu kama hakuna ulichofanya
chukua hatua leo ili usife mapema.
5.
Kumwekea Mungu
mipaka.
Ni hali ya kuamini kuwa Mungu anaweza mambo Fulani tu na mengine
hawezi. Kitendo hiki ni kumdharau Mungu.
41 Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu; Wakampa mpaka Mtakatifu wa
Israeli. s Hawakuukumbuka mkono wake, Wala siku ile alipowakomboa na mtesi.43 Alivyoziweka ishara
zake katika Misri, Na miujiza yake katika konde la Soani. (zaburi 78:41-43)
Maelezo hayo hapo juu yanaeleza namna wanaisrael
walipokuwa safarini kwenda kanani walivyosahau mambo makubwa ambayo Mungu
alikuwa amewafanyia na kuona kuwa baadhi ya mambo Mungu hawezi
Pia hesabu 13 na 14 Biblia inaeleza jinsi gani Musa
alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi (kaanani) waone
kama kweli ni nchi ya ahadi na maziwa, wapelelezi hawa walileta walileta habari
ya ile ni nchi ya ahadi na maziwa lakini inakaliwa na wafeli –wana wa Anaki,
Ameleki (negebu), Mhiti, Myabusi na
mwamori wapelelezi hao walisema waliwakuta huko ni majitu na wao (wanaisrael)
ni kama panzi tu hivyo wawezi kwenda wakaimiliki. Lakini Musa, kalebu, Haruni
na Joshua walizungumza mbele ya wana wa Israel wakiamini kuwa Mungu anaweza
kuwapaile nchi wamiliki kama walivyomwapia Ibrahimu. Na watu wote waliomwekea
mungu mipaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi.
Pia Joshua 24:1-29 inaeleza kuwa Joshua
alikufa akiwa na miaka 110 akiwa na nguvu zake kamili mpaka Bwana
alipompumnzisha.
Kama unataka kuwa na maisha marefu unataka
kuziongeza siku zako za kuishi kwa imani usimwekee Mungu mipaka.
8
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. (isaya 55:8)
Hivyo kila unachofanya Mungu anajua ni vema kumuomba ili akuongoze
kwa kila jambo.
6.
Uongo na
udanganyifu.
Uongo
ni matendo na maneno ya udanganyifu nayo yanakataliwa na Mungu. Mtu
anayehesabiwa kuwa na hatia hata kama amesema nusu ukweli pia mtu anapata hatia
kwa kusema uongo kuwa ukweli.
10Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira
iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja.11
Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, Bwana asema hivi, Hivyo
ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia
muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii
Yeremia akaenda zake12Ndipo neno la Bwana
likamjia Yeremia, baada ya Hanania, nabii, kuivunja ile nira iliyokuwa juu ya
shingo ya Yeremia, kusema,13Enenda ukamwambie
Hanania, ukisema, Bwana asema hivi, Umezivunja nira za mti; lakini badala yake
utafanya nira za chuma.14Maana Bwana wa
majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo mataifa
haya yote, ili wamtumikie Nebukadreza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami
nimempa wanyama wa nchi pia.15 Kisha nabii Yeremia
akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini
unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo.16
Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi;
mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana.17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo,
mwezi wa saba. (yeremia 28:10-17)
Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, nabii Hanania
alitabili uongo hivyo alikufa ndani ya mwaka huo huo
Pia matendo
5:1-11 biblia inasema.
1Lakini
mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,2akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake,
mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.3Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani
amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu
ya thamani ya kiwanja?4Kilipokuwa kwako,
hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa
katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia
uongo mwanadamu, bali Mungu.5Anania aliposikia
maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia
haya.6Vijana wakaondoka,
wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika.7 Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe
akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.8Petro
akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa
thamani hiyo.9Petro akamwambia,
Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika
mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. 10Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale
vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na
mumewe.11 Hofu nyingi ikawapata
kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.
Hivyo
Mungu hafurahishwi na udanganyifu unaofanywa na wanadamu hivyo anafikia uamuzi
wa kukatisha uhai wa mtu kabla ya wakati wake
Ni
vema kuacha tabia ya kinyonga yaani leo mkweli kesho mwongo, ndugu yangu hata
kwa Hanania na Safira waliona kama Mungu hawaoni lakini aliamua kuwaadhibu mara
moja. Acha tabia ya uongo tubu ili uishi miaka mingi.
7. Kukosa bidii katika kumpenda Mungu
14
Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua
Jina langu.(zaburi 91:14)
Ukizishika
sheria na Amri alizotoa Bwana maishani mwako yeye atajidhihirisha kwako na
upendo wako wake kwako na kadri unavyoongeza bidii ya kumtii na kumheshimu
Mungu atakushibisha au atakuongezea siku za kuishi, wewe ndiye unayeweza kumwambia
Bwana miaka 90 inatosha nataka kurudi nyumbani kupumnzika au 50 inatosha nataka
kurudi kwa Bwana.
1Mwanangu,
usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka
ya uzima, na amani. ( mithali 3:1-2)
Hivyo ukitaka kuishi miaka mingi fanya juhudi za kumpenda Mungu.
8. Maisha
ya dhambi
Dhambi ni kuvunja sheria ya mungu ambayo ni
sheria ile inayoeleza ukamilifu unaodaiwa na utakatifu wa Mungu. Dhambi ni
mbaya kwani inkutenga mbali na Mungu.
1
Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si
zito, hata lisiweze kusikia;2 lakini maovu yenu
yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia. (isaya 59:1-2)
Dhambi inakufanya ufe kabla ya muda wako. Usifurahie kuishi katika
dhambi epuka uzinzi, oungo, uasherati, usengenyaji na kulipiza kisasi nk. Kwa
kutenda dhambi unajipeleka jehanamu (kaburini) kabla ya wakati.
23Kwa
maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
katika Kristo Yesu Bwana wetu. (warumi 6:23)
Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi, swali la
kujiuliza ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa
kushindwa kuikwepa dhambi ya uzinzi na uasherati? Ni wezi wangapi wamekufa kwa
kuchomwa moto? Epuka dhambi ili uishi maisha marefu.
Ninaamini baada ya kujifnza sababu za kufa kabla ya wakati
utafanya mabadiliko makubwa katika maisha yako na utaishi maisha marefu. “Mungu
akubariki”
MAMBO YA KUFANYA ILI
USIFE KABLA YA WAKATI
i.
Kufanya maamuzi ya kuokoka sasa kabla hujafa.
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.
(yohana 3:16)
Mungu hafurahii kifo cha mtu mwovu na hivyo kaukosa uzima wa milele hivyo
kama hujaokoka nakushauri chukua hatua n a maamuzi ya kuokoka leo. Kama
ujaokoka sema maneno haya kwa kumaanisha;
“mungu baba naomba unisamehe kwa yote
niliyofanya kinyume na mapenzi yako kwa kuwaza, kunena, na kutenda. Naomba
ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu, uniandike kwenye kitabu cha uzima,
kuanzia leo unifanye kuwa mpya, uniongoze kwa kila jambo, Asante Yesu mana
umeniokoa “Amen”
Baaada ya kusali sala
hii ishi maisha matakatifu na usitende dhambi tena.
ii.
Kulitumikia kusudi la Mungu
Maana
yake kulitambua wewe ni nani na unapaswa kufanya nini kwa ajili ya Mungu. Yaani
ni kutekeleza au kukamilisha wajibu ambao ulimfanya Mungu. Mungu humuumba kila
mtu kwa kusudi maalum. Ni muhimu kutambua lengo la Mungukuumba kasha fanya
jambo ambalo litalenga kutekeleza wajibu wako. Mungu haruhusu kifo kwa mtu
anapokuwa amemaliza wajibu wake duniani.
36
Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake,
alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. (matendo 13:36)
Hivyo katika maisha jiulize umefanya nini kwa ajili ya Bwana
ambacho unaweza kujivunia.
iii.
Kuishi maisha ya kumpendeza Mungu au kufanya
mapenzi ya Mungu.
Katika maisha yako unapaswa kuishi maisha ya
kumpendeza Mungu kwa kusali tu haitoshi
22
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na
kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? (mathayo 7:22)
Hivyo ishi maisha yanayompa Mungu utukufu na ishi maisha
matakatifu.
iv.
Kuishi kwa imani
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;
kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba
thawabu wale watafuata”
Sote tunaamini kuwa Yesu kristo atarudi
kulichukua kanisa lake au watakatifu.
Swala la kuaini kuwa Yesu atarudi ni la imani
hivyo tunapaswa kuendelea kuamini hivyo hadi siku ya kufa, usije ukafika wakati
ukasema huyu Yesu mbona harudi afadhali nianze kutenda dhambi, uwe na imani
kwani siku akija utamwona. Usiruhusu kitu chochote kikuondolee imani kwa ‘Yesu’
kwa sababu huwezi kumwona Mungu bila kupitia kwa Yesu.
6Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi. (yohana 14-6)
Hivyo tumwamini yesu ili alij au ukifa ufe katika Bwana.
v.
Kufanyika msaada na sababu ya wokovu kwa
walimwengu
Kuna orodha ya watu katikauflme wa Mungu
ambao wanakusubili wewe uwaambie habari za Yesu.
Yesu anataka tuungane nae katika kuwarejesha
mateka kwenye ufalmu wa Mungu, unapomwambia mtu habari za Yesu anaonyesha
kuikubali (kuunga mkono) kazi aliyoifanya Yesu pale msalabani.
Swala la kujiuliza “je kuna mtu/watu yeyote
ambye amewahi hata kumshukuru Mungu na kuwashukuru wazazi kwa kukuleta hapa duniani
baada ya kuona mambo mazuri ya kiungu uliyowafanyia?
15
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini,
atahukumiwa. (marko 16:15)
Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuzitangaza habari za Yesu kunyamaza
kimya ni kutozaa matunda hivyo ni kutafuta kufa kabla ya wakati ni muhimu watu
watambue uwepo wako duniani.
vi.
Kujithamini juu ya uhusiano wako na kristo
25Iko njia ionekanayo
kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti. (mithali 16:25)
Ni
muhimu kufikiri kama maisha yako yanaleta utukufu kwa Mungu au hayaleti na kama
hayaleti unafanya nini mpaka ili yalete?
Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, Mungu hutuvumilia ili tujitambue na
tubadilike, tuishi maisha yenye utukufu. Unapokuwa umeshindwa kubadilika
anaamua kukatisha maisha yako yaani KUFA
KABLA YA WAKATI.
Hivyo kama kuishi maisha marefu chukua hatua
Ø
Tubu toba ya kweli
Ø
Jitathimini juu ya
mwenendo wako
Ø
Anza maisha mapya
Ø
Mtumaini Mungu katika
kila jambo
Baada ya kufikiri kwa makini Sali sala hii:-
Mungu baba naomba unisamehe mimi mwenye
dhambi kwa kufanya mambo bila kutambua unisaidie nitambue kusudi la kuumbwa
kwangu na nitekeleze agizo lako kasha niishi maisha marefu, unisaidie,
unilinde, uniepushe na ajali pamoja na mauti/kifo cha aina yoyote kisicho cha
halali hadi hapo Bwana utakaponiita, Amen.