LUGHA-FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
FASIHI SIMULIZI YA
KISWAHILI NA KIAFRIKA
MODULE 1; UTANGULIZ
I
FASIHINSIMULIZI YA
KISWAHILI
Senkoro (1988:10-11) Anasema Fasihi simulizi ni ile
inayojitambulisha na kujihusisha na utamaduni wa waswahili popote pale walipo
ulimwenguni.Utamaduni wa waswahili ni
ule unaohusu desturi na mila za waswahili sayansi,sanaa zao,uchumi wao na
maisha yao kwa ujumla.
Hali kadhalika inawahusika
,maudhui,falsafa,mawazo,historia, n.k vinvyofanana na maisha ya waswahili. Kwa
upande wa lugha ,Falsafa ya Kiswahili ni ile inayotumia lugha au lahaja ya
Kiswahili.
FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA
Ni ile inayojitambulisha na kujihusisha na utamaduni wanaa zao ,siasa na Afrika kupitia jamii na Lugha zao. Hivyo utamaduni wa Waafrika ni ule unaohusu mila
zao ,siasa na uchumi wao kwa ujumla.
Hivyo Fasihi simulizi ya kiafrika
ina mawazo ,falsafa,wahusika,maudhui,na dhamira zinazoendana na maisha
yao.Imetungwa kwa lugha za kiafrika au lahaja za lugha hizo.
Maswali hapa ya kujiuliza ni;
Ø Je fasihi simulizi ni ya kiafrika?
Ø Je fasihi simulizi
inayotumia lugha za nje zinazotumika nje ya Afrika ni ya kiafrika pia?
Ø Je
fasihi simulizi ya kiafrika inapaswa kuandikwa na nani? Mwafrika au hata
mzungu?
FASIHI SIMULIZI
Mgullu (2003 uk
16) anasema Fasihi
simulizi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama
hutendwa.
Ni fasihi
inayohusu mkusanyiko wa kazi za kisanaa za binadamu zinazowasilishwa kwa njia
ya mazungumzo au utendaji.Siku hizi fasihi
simulizi huhifadhiwa kwa
kuandikwa vitabuni,kanda za video,Redio na santuri.
Mlacha (1985:16)
Anasema Fasihi simulizi ni Nyanja
ya maisha ya jamii ambayo huchangia sana katika kuendeleza na kudumisha
historia ya jamii husika.
Fasihi simulizi huchangia katika
kuelimisha jamii kuhusu asili yake
,chanzo chake na maendeleo ya utamaduni wake na maisha ya jamii hiyo tangu zamani .
Wamitila (2003:44) AnasemaFasihi simulizini dhana inayotumika kurejelea kazi ambazo
kimsingi hudokeza na kwa njia ya masimulizi ya mdomo.Hutumika katika jamii kama
njia ya kupashana maarifa yanayohusu utamaduni fulani,historia fulani ya jamii
na matamanio yao.
OKPEWHO (1992:3) Anasema Fasihi
simulizi ni matini bainifu ambazo huvutia fikra zetu au hisia zetu,kama
vile hadithi,mashairi na michezo ya kuigiza
na sio kwa matini za kweli kama vile Ripoti za magazetini au rekodi za
kihistoria,hata hivyo nazo zikiandikwa kwa kuvutia zinaweza kuwa fasihi.
Mlokozi (1996:24) Anasema Fasihi simulizini fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia yam domo na vitendo bila
kutumia maandishi.
Hivyo ni tukio linalofungamana na
muktadha fulani wa kijamii na kutawaliwa na mwingiliano wa mambo sita,ambayo ni;
Ø Fanani (msanii)
Ø Hadhira
Ø Fani inayotendwa
Ø Tukio
Ø Mahali na wakati
Ø Fasihi simulizi inaendana na tukio
SWALI: ‘’Mbali na jitihada za wataalamu mbalimbali katika kufasili fasihi
simulizi na fasihi simulizi ya kiafrika mpaka sasa hakuna fasihi iliyotoshelevu.Jidili dai hili na pendekeza fasili yako’’
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA YA KIAFRIKA
v Zote zinahifadhi mila ,desturi na
historia pamoja na lugha za jamii husika
v Zote zinahitaji utendaji ambao unajumuisha vifaa mbali mbali kama vile
maleba yaani mavazi maalumu
v Vipera na tanzu vinaingiliana na
kufanana
v Muktadha na maudhui ya lugha maalum
dhana hizi zinajitokeza kote
UTOFAUTI KATI YAFASIHI SIMULIZI YA
KISWAHILI NA YA KIAFRIKA
Ø Fasihi simulizi ya kiafrika ni pana
sana lakini fasihi ya Kiswahili ni finyu
kwani fasihi ya Kiswahili huchota
vipengele fulani katika fasihi simulizi ya kiafrika.
Ø Fasihi simulizi ya kiafrika ni kongwe
Ø Utamaduni wa Fasihi simulizi ya
kiafrika ni tofauti na ule wa kiafrika.
TANZU ZA FASIHI SIMULIZI NA
UAINISHAJI WAKE
Tanzu ni matawi.Uainishaji wa Tanzu za Fasihi simulizi si jambo rahisi.Wataalamu mbali mbali
wamejaribu kuainisha lakini wamepambana na matatizo kdha wa kadha kwani;
v Afrika ina utajiri mkubwa wa tanzu za
fasihi simulizi.
v Tanzu hizo zinafanana sana
v Tanzu hizo zinaingiliana.
Wageni
walipokuja kama vile Finegan (1970),Matteru (1977),Mlokozi (1996),Catheline,
Kitula na king’ei (2005),Wafula na Ndungo (1993),Liongo (1972),Wafula na
Njogu (2007) na wengine wamefanya
jitihada za kuainisha tanzu za Fasihi simulizi.Si rahisi kuainisha Tanzu kwani
hakuna mipaka bayana kati ya Utanzu mmoja na mwingine.Hadithi,methali,Vitendawili
na mafumbo vinaweza kuwekwa katika kundi moja.
Ø Wapo wataalamu walioainisha Tanzu za
watoto na tanzu za watu wazima.Mfano Methali ni tanzu za watu wazima.
Ø Swali; Je ni upi utanzu bora kuliko
mwingine? Baadhi ya wataalamu walisema methali ni uti wa
mgongo wa mazungumzo.
VIGEZO VYA UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Wafula na Njogu wanasema ili tuweze
kuainisha tanzu za fasihi simulizi lazima tuwe na vigezo;
v Majina ya tanzu
v Miundo
v Mitindo
v Wahusika
v Wakati na mahali pa utendaji
Wafula R. na Ndungo .C (1993)
wametumia vigezo vifuatavyo katika uainishaji wao;
Majina
ya tanzu
Miundo
Mitindo
yake
Mianzo
na miisho yake
Maudhui
Kujipambanua
kwake kitabaka
Jinsia
(kuna tanzu za kike na za kiume)
Mahali
na wakati
Wahusika
Materu (1983) ameainisha tanzu za
Fasihi simulizi katika makundi makubwa matatu,ambayo ni;
1. NATHARI
Ni masimulizi au mazungumzo
·
Ngano
·
Visasili
·
Misendu
na n.k
2. USHAIRI
Ø Mashairi
Ø Nyimbo
Ø Tumbuizo
Ø Utenzi
Ø Maghani
Ø Ghibu
3. SEMI
·
Mafumbo
·
Misemo
ya kilinge
·
Methali
·
Vitendawili
Kitula king’ei na Catheline Kisovi wametaja makundi 4 ya tanzu ambayo ni;
1. SEMI
Ø Misemo
Ø Methali
Ø Mafumbo
Ø Vitanza ndimi
Ø Utani
2. Hadithi
v Ngano/Hekaya
v Visasili
v Maghani
v Visakale
3. MAIGIZO
Michezo
ya kuigiza
Sarakasi
Majigambo
Ngomezi
Utani
Mawaidha
Mipasho/Michongoano
Ngonjera
Vichekesho
4. USHAIRI
v Nyimbo kama vile Rege,Chakacha,Nyimbo
za harusi,Mbolezi,Wawe,Mkwaju ngoma,Nyimbo za Unyago,Bembelezi,Nyimbo za
jandoni n.k
v Ngonjera
v Mashairi
v Tenzi
v Kirumbikizi
Mlokozi M.M (1996) ameainisha tanzu kwa
kutumia vigezo vifuatavyo;
Ø Umbile na tabia ya Utanzu
Ø Muktadha wa uwasilishaji yaani wakati
na mazingira
Ø Namna ya uwasilishaji wake kwa
hadhira (Mtindo)
Ø Dhima ya Fani na utanzu wake.
Mlokozi ameainisha Tanzu za Fasihi
simulizi katika makundi sita ambayo ni ;
1. MAZUNGUMZO
Utanzu huu una vipera vine,ambavyo
ni;
·
Hotuba
·
Malumbano
ya watani
·
Mizaha
·
Sala
Dua
Maapizo
Tabano
2. MASIMULIZI
Utanzu huu una vipera vitatu,ambavyo ni
Ø Hadithi za kubuni
Vigano
Istiara
Mbazi
Michapo
Ø Salua
Visakale
Mapisi
Tarihi
Shajara
Kumbukumbu
Ø Visasili
Visasili
vya uzuri
Visasili
vya ibada na dini
Visasili
vya miungu na mizimu
3. MAIGIZO
Utanzu huu unajumuisha maigizo ya
watoto,misiba,Sherehe za kidini n.k
4.USHAIRI SIMULIZI
Vipera vyake ni;
·
Nyimbo
Tumbuizo
-Bembea
-Mbolezi
-Nyiso
Tukuzo
-Kongozi
-Nyimbo za dini
-Nyimbo za taifa
Chapuzo
au kimai
-Nyimbo za kutwanga
-Nyimbo za watoto
-Nyimbo za vita
Tenzi
na Tendi
·
Maghani
Ghani
nafsi-kutamba
Ghani
tumbuizi
Sifo-Vivugo
(majigambo)
-Tondozi
Maghani
simulizi
-Tendi
-Rara
5. SEMI
·
Methali
·
Vitendawili
·
Mafumbo
-Chemsha bongo
-Fumbo jina
·
Simo/misimo
·
Kauli
kaulia
6.Ngomezi
FASILI YA DHANA MBALI MBALI ZA FASIHI
v Mazungumzo
Ni mazungumzo yenye sanaa ndani yake yaliyosheheni mbinu
za kifani (Fani na Maudhui).
Mfano Tamathali za semi kama vile sitiari,Tashibiha n.k
v Mbazi
Ni
hadithi fupi zenye lengo la kuonya
v Salua
Ni
hadithi zinazosimulia matukio ya kihistoria / ya zamani .
v Visakale
Ni
visa vya kimapokeo vya mashujaa
v Mapisi
Ni historia ya matukio ya kweli
v Tarihi
Ni
maelezo au jedwali la matukio muhimu na tarehe zake.
v Visasili
Ni hadithi za kale zinazozungumzia
asili ya kitu au imani ya mtu.mfano asili ya binadamu.
v Mbolezi
Ni
nyimbo za kuliwaza katika msiba.
v Nyiso
Ni
nyimbo za jandoni na unyago.
v Wawe
Ni nyimbo za kazi
v Kongozi
Ni nyimbo za kuaga mwaka,mara
nyingi zinaambatana na tambiko.
v Tenzi
Ni
utungo unaozungumzia tukio fulani.
v Tendi
Ni
utungo unaozungumzia tukio la kishujaa
v Sifo
Ni
nyimbo za kusifu
v Tondozi
Ni
tungo za kusifu wanyama n.k
v Rara
Ni
maghani ya kusimulia tukio fulani la kihistoria na huenda sambamba na ala za
mziki.
v Fumbo jina
Ni
mafumbo ya yanayotaja majina .mfano
Mwamvua alizaliwa kipindi cha mvua
v Lakabu
Kupewa jina kulingana na tabia mfano
Mwl J.K Nyere-Baba wa Taifa
v Kauli Taulia
Ni kauli zenye mfuatano wa sauti
UHUSIANO WA FASIHI SIMULIZI NA TAALUMA NYINGINE
Fasihi simulizi haipo katika upweke au Ombwe
bali inahusiana na taaluma mbali mbali .Hii inatokana na ukongwe
wake yaani dhima zake,sifa zake,utendaji wake, na n.k vinafranya
ihusiane na taaluma nyingine.Miongoni mwa taaluma hizo ni
Mziki,Sosholojia,Historia,Isimu ya Lugha,Etimolojia na hata Fasihi Andishi.
A.
UHUSIANO WA FASIHI SIMULIZI NA MUZIKI
Mziki ni nini?
Au ni vitu gani vinafanya utambue kuwa huu ni mziki?
Ø Ala za mziki kama vile
zeze,marimba,ngoma,manyanga,n.k.Fasihi simulizi inahusiana na mziki katika
utendaji kwani katika Fasihi simulizi kwani
vipera mbali mbali vya fasihi simulizi vinahusisha ala fulani za muziki,mfano
Majigambo,Tenzi.
B.Historia
ni taaluma
inayochunguza matukio kisayansi ya wakati uliopita na uliopo.Ni taaluma
inayoshughulika na uchunguzi wa maisha ya binadamu ambayo yanatuwezesha kujua
maendeleo na mabadiliko ya binadamu. Fasihi
ananafasi kubwa katika historia ya binadamu kwa kupitia baadhi ya vipera
vya fasihi simulizi.Hivyo Fasihi
simulizi inatusaidia kuelewa historia
yetu (sayansi fulani) mfano Tenzi,baadhi ya tenzi za kiswahili zinazungumzia
mashujaa wa Afrika,Mfano Fumo Liyongo.Hii inatusaidia kujua mtzamo wa jamii husika katika kipindi
fulani cha kihistoria.Wanahistoria pia
wamechota baadhi ya mambo yao kutoka katika Fasihi simulizi.Data za fasihi simulizi
zinasaidia kujenga rekodi za kihistoria .Vipera mbali mbali kama
Tendi,Visakale,Tarihi,Shajara n.k vinatusaidia kuelewa historia ya jamii japo
kwa kiasi kidogo kuhusu matukio ya watu au mashujaa katika jamii hiyo.
Suala la utendaji/Utofauti wa vipera
vya fasihi simulizi zamani na sasa
vinaweza kutusaidia kuelewa historia ya
jamii fulani.Fasihi simulizi inasaidia kuhifadhi na kuendeleza historia katika
jamii mfano majigambo.
C.
SOSHOLOJIA (Elimu
viumbe,Athropolojia)
Ni taaluma inayoichunguza jamii
kisayansi ili kujua mienendo yake na nguzo mbali mbali zinazoongoza jamii
hiyo.Mfano Matabaka,Dini,kijadi,.Vingele hivi
tunavipata katika sosholojia na
vinatusaidia kuelewa namna ambayo vinweza kuzuia mienendo.
Hivyo Fasihi simulizi tangu hapo
mwanzo inatusaidia kujua hiyo mienendo
au mifumo mbali mbali ya jamii,kipera kinaweza kuwa chombo cha kutetea
utabaka au kuchochotea utabaka.
Fasihi simulizi kilikuwa chombo pekee cha
kuwasilisha maadili ya jamii kupitia vipera
kama vile kitendawili au nyimbo.Kupitia Fasihi simulizi tunaweza
kurithishwa utamaduni ,mila na desturi za jamii hiyo.Taarifa za kisosholojia
pia zinapatikana katika kazi za kifasihi.Mienendo na mabadilikomifumo ya
kiuchumi na kijamii inapatikana kwa kurejelea kazi za Fasihi simulizi.
D.
UTAMADUNI
Utamaduni unapatikana katika fasihi
simulizi kwani fasihi simulizi ni chombo
kizuri cha kurithisha utamaduni wa jamii husika na utamaduni huo hurithishwa
kupitia utendaji wake katika baadhi ya vipengele kama vil;Maleba
(mavazi),Utendaji,Mazingira ya utendaji,Vifaa,Fani husika.
Hivyo uhusiano kati Fasihi simulizi
na utamaduni pia upo katikaLugha kwani Fasihi simulizi hutumia lugha,na lugha
ni nyenzo muhimu za fani husika hivyo
fasihi kama chombo na sehemu ya utamaduni inasaidia mambo kadha wa kadha kama
vile;
Ø Inakuuza utamaduni
Ø Inahifadhi utamaduni
Ø Inaeneza utamaduni
Ø Kueleza utamaduni wa jamii hiyo.
Kwa ujumla fasihi simulizi ipo katika kila hatua ya maisha yetu.
E.
ETHIOLOJIA
Fasihi simulizi inatumika katika dini kama vile nyimbo na maandiko ya
kidini ambayo yanaweza kuwa hadithi ,nyimbo ambazo zimo katika biblia na vitabu
vya nyimbo za kidini.mfano Utenzi wa sundiata.
F.FASIHI ANDISHI
Uhusiano kati ya Fasihi simulizi na
Fasihi andishi utafiti unaonyesha kuwa karibu tanzu zote za Fasihi andishi zimetokana na Fasihi simulizi.
Ø Maigizo yanazaa tamthiliya,pia
uhusiano huu unajitokeza katika nafasi ya fasihi simulizi katika tanzu za fasihi andishi.Fasihi andishi
inanufaika kwa kiwango kikubwa kutoka katika fasihi simulizi kifani na kimaudhui kama vile vipera,matumizi
ya lugha n.k vipengele hivi vya fasihi simulizi vinatumiwa katika fasihi
andishi.Vitu hivi vinaleta athari kubwa katika fasihi simulizi.
Ø Pia
kuna mianzo maalum katika tamthiliya kuna fomula za kihadithi
mfano,Niendelee nisiendelee?
Ø Vile vile matumizi ya wahusika
wanyama,ndege,mazimwi,majitu n.k, pia matumizi ya wahusika bapa,matumizi y
mbalimbali kama vile taswira,ucheshi n.k
Ø Suala la kuingiliana kwa tanzu,katika
fasihi andishi kuna tanzu za fasihi
simulizi kama vile hadithi,ngano,nyimbo n.k
Ø Pia katika mashairi kuna utambaji
,malumbano na vipera vingine vya fasihi simulizi.
SUALA
LA UTENDAJI KATIKA FASIHI SMULIZI
Katika fasihi simulizi utendaji ni uti wa mgongo
yaani ni suala la msingi.
Mulokozi (1996:24) Fasihi
simulizi ni tukio na linafungamana na matukio ya kijamii na hutawaliwa na
fanani (msanii au mtendaji)
Ø Fanani ni mtendaji au mwasilishaji na
mtunzi wa kipera,fani husika kwa hadhira katika muktadha wa tukio fulani ,kazi
yake yaweza kuwa kichwani au akatunga
papo kwa papo.
Ø Fani inayotendwa au kipera
Ø Hadhira/wasikilizaji,washiriki,wachangiaji
,wahakiki,watazamaji hawa huangalia uzuri au ubaya.
Ø Tukio-ni shughuli yoyote ya kijamii
ambayo ndio muktadha wa utendaji.mfano msiba,ibada,harusi,sherehe,n.k
Ø Mahali –eneo mahsusi ambapo sanaa
hiyo inatendwa.
Ø Wakati na muda maalum au majira
maalum ya utendaji .Vipera vingi vina
wakati wake.mfano Sifo huimbwa wakati wa kuomba.Mwingiliano huu wa vipengele
hivi ndiyo unaoamua fani hiyo iwasilishwe vipi.
OKPEWHO (1992) Anasema
Utendaji unaotofauta kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
Ø Umri wa fanani
Ø Umri wa hadhira
Ø Nguvu ya fanani,baadhi ya vipera
vinahitaji fanani awe na nguvu mfno majigambo
Ø Tukio husika mfano Msiba hauwezi
kufanana na sherehe
Ø Aina ya mandhari au
jukwaa maalum la kutendea yaani pale inapotendewa.
Ø Vifaa ambatani vinavyotumika na
fanani katika utendaji mfano maleba,mkuki
Ø Idadi ya fanani
Pia utendaji unatokana au
unatawaliwa na;
Ø Dhima ya kipera( tukio ),muktadha wa
uwasilishaji na namna ya uwasilishaji hutegemea dhima ya kipera katika jamii.
Ø Muda na mahali,ni muhimu kuzingatia kwa kipera chochote
hutegemea au husukumwa na muda na mahali.mfano matambiko yanafanywa muda gani?
Ø Mila na utamaduni ,kila jamii ina
mila na utamaduni wake na hivyo huathiri
utendaji wa vipera husika.mfano Mavazi au maleba maalum ya kisanaa yaani kipera
hiki kinahitaji aina ipi ya maleba?
Ø Sifa za wahusika au watendaji wa
kipera fulani wanapaswa wawe akina nani?
SWALI; JE UTENDAJI NI NINI?
Muluka (1999) anasema Utendaji ni uwasilishaji
wa hadithi au ngano unaofanywa na
msanii kwa hadhira kwa kutumia mdomo na
kuambatana na matendo ya viungo mbalimbali
vya mwili na ishara uso.Hivyo
kila kipera kipo kwaajili ya kutendwa.
UTENDAJI KATIKA VIPERA MBALI MBALI
Finnegan
(1970) ‘’Oral Literature in Africa’’ anasema kuwa katika utendaji kuna kanuni maalum,jamii
nyingi zina utamaduni wake.Hadithi ni utanzu muhimu katika jamii za
kiafrika.Hadithi ni utanzu wa jioni na mtambaji
anazungukwa na hadhira.
SWALI; Je kwanini hadithi inatambwa jioni?
Ø Kwasababu mchana mtambaji anakuwa katika utafutaji
yaani katika shughuli zake za kila siku.
Ø Hadithi ina fomula zake za kuanza na
kumalizia yaani mianzo na miisho maalum ya kihadithi.
Ø Katika kutamba hadithi fanani habanwi kutumia vipera vingine
katika utendaji wake.
Ø Katika kutamba hadithi msimuliaji hatakiwi
kukalili ila anapaswa kuleta upya fulani wa utendaji wa hadithi hiyo.
Ø Mtambaji anapaswa kutumia sauti vizuri na
iendane na utanzu wenyewe.
Ø Kuna wasimuliaji wazuri na wabaya au
wasiowazuri
Ø Msimuliaji awe mbunifu ili kunogesha
hadithi
Ø Katika utendaji msimuliaji aoneshe
hisia zake.
UFALAGUZI
Ni uwezo alionao fanani katika kuunda
kutunga ,kugeuza na kuiwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo kwa papo bila ya
kujifunga na muundo asilia au na muundo uliozoeleka. Hivyo katika utendaji wa kipera fulani kuna
utungaji mpya kutokana na mbinu fulani unazotumia.
Ø Hivyo
hadithi moja inaweza simuliwa
tofauti na wasimuliaji tofauti.Utendaji wa kipera hurithishwa toka
kizazi kimoja hadi kingine.
SIFA ZA FANANI BORA
Senkoro anasema Fanani bora anatakiwa
afanye kazi ya ualimu ,awe mtoa maoni,msanii,mburudishaji,muigizaji
Ø Fanani aifanye hadithi ionekane
mpya kila mara anaposimulia.
Ø Fanani aifurahie na kujivunia fani anayoitenda,kuisimulia
ipasavyo.
Ø Fanani awe mbunifu na awe na
kumbukumbu.
Ø Suala la utamaduni katika utendaji
fanani azingatie utamaduni wa kipera
anachotamba.
Ø Fanani awe tajiri wa lugha yaani ajue
kutumia mbinu mbalimbali za lugha
kama vile nahau,semi,n.k.
Ø Fanani asiwe na aibu katika utendaji
atumie vema lugha na viungo mbali mbali.
Ø Kujua mambo ya kihistoria kwani
Fasihi inapitia vipindi mbalimbali.
UTENDAJI WA KIPERA CHA SEMI
1. METHALI
Ni usemi mfupi wa
kimapokeo unaodokeza mafumbo mazito au fikra zinazotokana na uzoefu wa jamii
husika.Katika utendaji unaweza
kutofautiana na vipera vingine kwani utendaji wa methali lazima unajitegemeza
wakati wa kutenda fani nyingine mfano mkutano,maongezi ya
kawaida,majadiliano,hadithi,wakati wa kukanya mtu n.k.
Kimsingi watambaji wa
methali ni watu wazima (wazee) kutokana na kuishi kwao katika jamii kwa muda
mrefu.
2.VITENDAWILI
Utendaji katika vitendawili si tegemezi
kama methali bali kitendawili kinasimama chenyewe kwa kufuata kanuni zilizowekwa na
jamii husika.Mfano katika kabila la wajaluo
ukishindwa kutegua unaombwa mke au mme na katika jamii nyingine unapewa mji.
2. MAJIGAMBO
Katika Jamii ya wahaya ni jamii
ambayo ni maarufu kwa majigambo.Huu ni utafiti wa kitaaluma uliofanywa na Rubanza
(2004) na Method Samwel ,hawa wote wameangalia jamii ya wahaya.
Katika jamii ya wahaya majigambo
yalikuwa na muktadha wake maalum walikuwa wanatamba mbele ya mtemi kabla
ya kwenda vitani au baada ya kurudi toka vitani n.k
Ø Kwa wahaya mjigambi hujigamba mbele
ya watu ,sherehe ambayo inahudhuriwa na mtemi na kuna namna ya kuanza na kumaliza.Mfano wakati wa kuanza mjigambi anaweza kuanza kwa
kujitambulisha kwa kujigamba na anaweza kumalizia kwa shukrani au heshima kwa
mtemi au kiongozi aliyepo pale.
Ø Katika majigambo ,mjigambi yupo huru
kutumia lugha ya kujikweza akiwa amevaa maleba maalumu mfano katika kujigamba mjigambi anavaa kanzu ndefu au nguo za majani
ya migomba na hushika silaha kama vile mkuki ,panga,n.k
Ø Pia majigambo huambatana na ngoma
yenye mapigo ya pekee na maandamano
fulani.
Ø Katika majigambo kuna zawadi,shujaa
aliyeshinda au aliyerudi toka kuwinda ,vitani n.k hupewa zawadi kama pombe.
Ø Wale walioenda vitani au kuwinda wakashindwa zawadi yao
ilikuwa maji ya kunywa na kinyesi cha ng’ombe.Hii ilikuwa inaleta umakini kwani
kurudi na kinyesi ilikuwa ni aibu.
Miaka ya 1960 utendaji katika majigambo uliathiriwa sana kutokana na
mabadiliko ya kijamii na kiutawala