MITIHANI
WIZARA YA ELIMU
NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE
YA SEKONDARI EFFORTS
MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA
KIDATO CHA
SITA
KISWAHILI-2
MUDA
: SAA 3
Novemba,2018
MAELEKEZO
1.
Karatasi hii ina jumla ya maswali tisa ( 9 )
2.
Jibu swali moja kila sehemu na kila
swali lina alama 20
3.
Soma swli kwa mkini kabla ya kuanza kujibu
4. Andika jina lako vizuri na mchepuo
wako
SEHEMU A
(Alama 20)
FASIHI KWA UJUMLA
1.
“Usambazaji
wa sanaa za maonesho nchini Tanzania unakabiliwa na changamoto lukuki’’.Kwa
hoja sita na mifano thibitisha dai hili.
2.
“Tangu
wakati wa uhuru hadi sasa Tamthiliya ya Kiswahili imetoa mchango mkubwa sana
kwa jamii ya Tanzania”.Kwa hoja sita pamoja na mifano kutoka katika tamthiliya
za Kiswahili thibitisha dai hili.
SEHEMU B (
Alama 20 )
USHAIRI
Kimbunga - Haji Gora
Fungate ya Uhuru
-M.S.Khatibu
Mapenzi -S.Robert
Chungu Tamu
-T.Mvungi
3.
“Matumizi
ya Jazanda ni moja ya mbinu za mwandishi
katika kufikisha ujumbe kwa jamii lengwa’’.Jadili dai hili kwa kutoa
Jazanda nne (4) kwa kila diwani kwa kutumia diwani mbili
ulizosoma huku ukirejelea Tanzania ya leo.
4.
“Wasanii
wa ushairi ni nguli wa kutumia tamathali za semi”.Kwa kutumia diwani mbili
thibitisha dai hili
SEHEMU C
(Alama 20)
RIWAYA
Usiku
Utakapokwisha -Mbunda Msokile
Mfadhili -Hussein Tuwa
Kufikirika
- Shaaban Robert
Vuta
n’kuvute -Shafi Adamu
Shafi
5.
“Mara
nyingi mandhari husaidia kuibua dhamira lengwa za msanii wa kazi ya
fasihi’’.kwa kutoa hoja kwa kila riwaya toka katika riwaya mbili ulisoma
thibisha dai hili
6.
Wasanii
wa kazi ya fasihi hutumia mbinu za kifani ili kujenga ,kuzipa mvuto na kuleta
radha tamu kwa wasomaji wa kazi zao.Fafanua mbinu tano ( 5 ) za kifani
zilizotumika katika kila tamthiliya ,tumia tamthiliya mbili ulizosoma.
SEHEMU D
(Alama 20)
TAMTHILIYA
Kwenye Ukingo wa Thim - E.Hussein
Morani -E.Mbogo
Kivuli
Kinaishi
-S.Mohamed
Nguzo Mama -P.Mhando
7.
“Jina la kitabu
ni ishara tosha ya yote yanayojadiliwa na mwandishi”. Thibitisha dai hili kwa hoja nne (4) kwa kila Tamthiliya,Tumia tamthiliya
mbili ulizosoma.
8.
Ubunifu
wa kisanaa ni nguzo muhimu sana katika
kufikisha ujumbe kwa jamii yeyote ile.Kwa
kutumia Tamthiliya mbili ulizosoma jadili vipengele vya fani vilivyotumiwa na mwandishi kufikisha ujumbe.
SEHEMU E (Alama
20 )
USANIFU W MAANDISHI
9.
Soma habari
ifuatayo kisha eleza mbinu za kisanaa zilizotumika;
Wakati
wanakijiji wanazungumza na mgeni,mipango mingine ya utoro ilikuwa inafanyika Samson na mkewe wakaona
kuwa wamekabiliwa na jambo kubwa,hahahaha!!!!!,Mti na macho.Waliona vigumu
kungoja hadi kesho yake mashauri yatakayofanyika.
Waliposoma sura za wanakijiji walihisi kuwa hakutakuwa na usalama
wowote.Kwa hiyo walikata shauri na
kuondoka kisirisiri usiku wa manane
pamoja na watoto wao,watoto walianza kuchukua tabia za wazi wao.Amaa!!!
kweli !!! mtoto wa nyoka ni nyoka tu.Ilipofika
usiku walianza kufunga funga vitu na visivyo vyao ambavyo walijua wataweza kuvichukua,Amaah! Kweli!! Tabi haina dawa.
Mnamo saa saba usiku,Samson alimtwaa punda mmoja na kumbebesha mzigo ile
mizigo?. Maskini ya MUNGU!!!!,
Mnyonge mnyongeni ……………..siku zote kiumbe wa Mungu huonewa sana!!,Hubebeshwa mizigo
mizito.Usiku ulikuwa wa nuru kama mchana
na safari ikaanza.
Walisafiri
usiku mzima lakini hawakuwa wamefika mbali sana kulipoanza kupambazuka
kutokana na mwendo mdogo wa punda.Hata hivyo walipiga hatua
kulipopambazuka watu walianza
kusalimiana.Kwa bahati mbaya mzee Hengaipinge aliamka mapema sana siku
ile na kuamua kwenda kwa Samson.Alishangazwa na jinsi vitu vilivyokuwa
vimetupwa hovyo hovyo kama nyumba ya kichaa,hivyo alihisi kuwa jamaa wale wamekata mbuga.
Wanakijiji walipata taarifa za kutoroka
kwa Samson,watoto na mkwewe.Watu
walikwenda kushuhudia maajabu ya Mussa.
Ilipofika
mchana mtu mmoja mgeni kutoka madongo kwinama aliwasili katika
kijiji cha Magwale.Samaki mmoj akioza wote wameoza,kwani mgeni huyohuyo
hakupokelewa kwa furaha.Kwa ufupi Samson na mkewe waliwatia wageni katika mtego wa panya.
Yule mgeni alipowasili walisalimiwa kama
ilivyo kaida,lakini baada ya kumsalimia wanakijiji wakazidi kujadiliana juu ya
lile lililotokea.Wengine waliwashauri kuwa lazima watu wale wasakwe na
kukamatwa lakini wengine waliona kuwa
Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
Mgeni
aliwaomba wamsindikize pia, ‘’Napenda
kuwaeleza kuwa nilipoanza safari yngu,hao watu nilikutana nao” Ooooh!!!,Watu
wote walishangaa.Aliendelea kwa kusema kuwa Punda wao alitembea kama kinyonga kwa mizigo
aliyobebeshwa.Tulishasikia habari za watu hawa
habari za watu awa kuwa walimtesa sana mtoto Lukemelye na kumdhulumu
kupita kiasi,wana tama ya fisi.Watu hawa
watakuwa katika kijiji cha Ihang’ana hivi sasa.Mgeni aliahirisha safari
yake na kurudi Ihang’ana kuyawahi mambo kabla hayajaenda mrama.