FASIHI
MADA MPYA 3: KUHAKIKI KAZI YA
FASIHI ANDISHI
MADA NDOGO-1: MAENDELEO YA FASIHI
ANDISHI.
A.Mwelekeo wa kazi za fasihi
andishi nchini Tanganyika na Zanzibar wakati wa ukoloni.
Kimaudhui
Kazi
nyingi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar zilishughulikia masuala
mbalimbali ya kimaisha lakini kazi nyingi zilikuwa na mambo ya mila na tabia
kama njia ya kufundisha maadili .vile vile zilishughulikia utamaduni, mawaidha,
dini, maadili mema na maonyo na kazi zilizoopinga ukoloni .Wakati wa ukoloni
nchini Tanganyika na Zanzibar
kazi za fasihi zilishughulikia mambo kadhaa kama ifuatavyo:
Mosi,Suala
la Utumwa,katika riwaya ya “Uhuru wa watumwa ‘(1934)
cha James Mbotela kinashughulikia uhusiano baina ya mataifa ya magharibi
na ya Afrika.Katika riwaya hii mwarabu
na muislamu wanalaumiwa kwa utumwa uliokuwepo Afrika Mashariki wakati mkoloni
anasifiwa kwa kuleta uhuru japokuwa utumwa ulitiliwa nguvu na ukoloni.
Kwa ujumla hadithi ya uhuru wa watumwa
inaonyesha ubaya wa biashara ya utumwa iliyoendeshwa na waarabu na papo hapo
inaonyesha matukio yaliyowapata watumwa mambo yaliyowaumiza na uchungu
ulowapata watumwa hao.
Mwandishi
anaeleza mateso ya watumwa kwa uchungu
na mchomo mkali.Pia hadithi hii inawatukuza wakoloni wa Kiingereza,ikijaribu
kumfanya mwafrika akubali kutawaliwa.Hadithi hii inausuta utumwa wa kimwili uku
ukiusifu ule wa akili na mawazo ambao ni utumwa ulio mbaya zaidi.
Mwaka
1949-1960 kazi
nyingi za fasihi za Kiswahili hasa riwaya zilifuata mkondo wa ngano na fasihi
simulizi kama za Paukwa pakawa…hapo
zamani za kale palitokea…..,Kimaudhui fasihi simulizi zilijadili maadili ya
kufuatwa katika kujenga jamii inayofaa
katika maisha.Mfano mzuri wa vitabu hivi ni Adili na Nduguzi (1952) utenzi wa
mwanakupona (1858) na Al-inkishafi (1890).
Katika
Adili
na Nduguze mwandishi alitumia
visasili vya jadi ya kiarabu kama vile matumizi ya majini anaonya dhidi ya
uchoyo na kuhimiza moyo wa wema, usamehevu na kutosheka.
Pili Suala la nafasi ya Mwanamke,Katika
utenzi
wa mwanakupona,mama anatoa mafunzo kwa binti yake.Humo ndani ya utenzi
mwanamke anapaswa kujitazama kwa nyenzo tatu.ambazo ni;
Ø Yeye
ni nyenzo ya starehe ya mume wake hivyo inampasa ajitahidi mno kumfurahisha ili
apate rehema zake, kwani Mungu hata acha kumtia hatiani
kwa kutotimizia haja mume wake na atakapomkana mbele ya Mungu.
Ø Inampasa
mwanamke awanyenyekee wanaume wote isipokuwa watumwa tu.Aonyeshe kilicho na
heshima kubwa kwao.
Ø Mwanamke
ajione kuwa yu mmoja wa matajiri au maskini (watumwa).
Binti
anayeandikiwa shairi hili ni tajiri naye anaaswa asichanganyike na watumwa,
watu duni waliodharauliwa duniani
Tatu,suala
la ukombozi/uhuru
, miaka ya 1950-1960 Shughuli za kisiasa zilipamba moto na kusababisha
kuibuka kwa fasihi ya kisiasa ambayo wasanii wake walizitumia kumpinga mkoloni.Shaaban
Robert alionyesha upinzani wake hasa katika riwaya
zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika (1967) ambamo zaidi ya
kuwatetea wajumbe mbalimbali walikuwa wakiutetea
uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. Pia mwandishi anaitetea serikali ya kikoloni
kwa kejeli kubwa kwani ilikuwa inainyonya Tanganyika na Zanzibar kwa ajili tu
ya kukidhi “Ugumba na Utasa” wa mfalme na malkia.Ugumba na Utasa ambao Shaaban
Robert kautumia kwa ishara tu ya mahitaji ya wakoloni.
Nne,suala la
Uongozi,Katika “Kusadikika” mwandishi anajadili suala la haki ya watu
dhidi ya uongozi kandamizi wa kiimla, utawala usio na kiasi wala mpaka ni
utawala ambao hukwamisha maendeleo ya
nchi na watu wake.Kwa sababu huwanyima watu uhuru wa kufikiri na kuchangia katika
maendeleo ya nchi yao. Kwa kutumia mbinu
ya kejeli, tashtiti, misemo, nahau.
mwandishi amejitahidi kufikisha lengo lake la kuonyesha hasara ya kuyakwamisha
maendeleo ya nchi.
Tano
suala la Ukoloni,ukoloni wa kiutamaduni ni mwanzo tu wa ukoloni wa
siasa na uchumi. Hata katika riwaya ya Tafsiri ya hadithi ya ”Chinua Achebe”Shujaa Okonkwo (1932)
ambapo wamisionari walitangulia kuja ili baadae watawala waje na kuiteka nchi
yote. Hivyo wamisionari walishirikiana na watawala katika kuwanyanyasa na
kuwanyonya watu.
TOFAUTI KATI YA MHUSIKA MKUU WA
ZAMANI NA WASASA
Mhusika
wa zamani alikuwa na sifa zifutazo;
Ø Alikuwani
halisi mwenye sifa zisizo za kawaida ambaye alisanifiwa na msanii kwa makusudi
mazima ya kuumba.
Ø Alikuwa
mfano bora wa kuigwa na kumfanya awe kielelezo cha ukweli na ukamilifu wa
maisha na mwenye kupigania na kuleta mambo hayo bila kuwa na dosari.
Ø Alitafakari maisha ya jamii kwa njia ya
matendo makubwa na lugha teule.
Ø Alijitokeza kuwa mtendaji mkuu wa wakati wote
Ø Hakuwa na saikolojia wala hisia
Ø Mhusika mkuu wa zamani kama vile wa kwenye
hadithi ya kifasihi alijitokeza kama mhusika mkuu wa wa wakati wote. Kwa msanii
wa namna hiyo ya wahusika, dhana za wakati na ukweli uliokamilika zilikuwa
katika hali ya kutobadilika wakati na ukweli vilikuwa na vitu vilivyotitia
pamoja.
Kwa
jinsi hiyo maandishi ya kisanii yaliyopewa jukumu la kuzibeba sifa hizo
yalilengwa kuwa ni ya wakati wote, yasizeeke.
Mhusika mkuu wa kisasa anayaona maswala
yasiyotulia bali ni maswala
ambayo yana badilika pamoja na jamii.Na baadhi ya wasanii wa kisasa wanaona
kuwa,suala la ukweli uliokamilika kwa kiasi kikubwa ni ndoto iliyomo katika
vichwa vya watu tu na wala si maisha
halisi.
Mhusika mkuu wa kisasa yuko katika wakati maalumu wa kihistoria ambapo anayazamia maisha
kwa undani na kuyatafakari. Kadri Shaban
Robert alivyozidi kuandika kama Maisha yangu na baada ya miaka Hamsini(1966),Wasifu wa Siti binti Saad (1967) Siku ya
utenzi wote(1968) ndivyo alivyozidi kuwapa wahusika wake sifa zinazokaribia
au zinazoelekeana katika hali halisi ya maisha.Hii ina maana kwamba mkabala
wake ulizidi kuelekea katika hali ya
kueleza ukweli kwa kutumia mbinu za kisanii ambazo hazikutenga kazi ya Sanaa
kwa kiasi kikubwa na uyakinifu wa maisha.Kwa ujumla fasihi Andishi ya awali
ilihusu zaidi maadili na masuala ya kidini kama katika”Adili na nduguze”.
Pia
uwepo wa mvutano baina ya wakoloni na waafrika, Ulikuwa
unadhihirishwa katika baadhi ya kazi za fasihi Andishi za awali.Pia maandishi
mengine ya fasihi yalihusu matarajio ya jamii itakiwayo baada ya ukoloni, kama
katika kufikirika na kusadikika, katika kipindi hiki tanzu za fasihi
andishi zilizokuwapo ni riwaya na ushairi. Baada ya uhuru, tamthiliya zote za
Kiswahili zilizochapishwa zilikuwa zimeandikwa na wakenya, watanzania hawakujitokeza
katika uwanja huu hadi baada ya uhuru.
B:
Mwelekeo w kazi za fasihi Andishi nchini Tanzania baada ya uhuru
Baada ya uhuru kulikuwa na fasihi mchangamano
ambayo ni vigumu kuainisha hadi tukio kuu la kutangazwa kwa Azimio la Arusha,
kabla ya hapo fasihi kwa kiasi kikubwa, ilikuwa ya kushangilia uhuru
uliopatikana hasa katika magazeti ambako mashairi na hadithi nyingi zilionyesha
hoi hoi ya lelemama za uhuru.
Kwa
upande wa mashairi, vitabu kama vile Utenzi
wa uhuru wa Tanganyika(1967) na utenzi
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania(1968) viliandikwa wakati huo. Ni kipindi
hicho cha uhuru utanzu wa tamthiliya ulijitokeza kwa mara ya kwanza kwa upande
wa Tanganyika na Zanzibar.
Mwandishi
maarufu wa tamthiliya aliyejitokeza kipindi hicho Ebrahim Hussein ambaye
tamthiliya yake ya kwanza “wakati ukuta”(1969) ilichapishwa ikifuatiwa na
tamthiliya ya “Kinjekitile”(1969)
Fasihi
ya Kiswahili imepevuka zaidi kwenye miaka ya 1970. Mulokozi(1996) anasema
karibu tanzu zote za fasihi Andishi ya Kiswahili zimepata wawakilishi. Hali hii
imejitokeza fasihi za mokondo mbali mbali.
Kimaudhui,
fasihi andishi nchini Tanzania baada ya uhuru imejadili dhamira mbali mbali
ambazo zinatokana na matukio mbali mbali
ya kihistoria yaliyojitokeza katika jamii yetu ya Tanzania.
Kipindi
maalumu cha maisha kina matukio yake maalumu ambayo huigusa jamii kwa uzuri au
ubaya na kuwa dundo la moyo la kipindi hicho ndichi kinachojenga kilele. Aidha
tukio linapokuwa dundo la moyo la kipindi fulani cha maisha huwa pia mada
kuu(muhimu) ya wakati huo kwa jamii inayohusika.Mada hiyo uweza kujitokeza
kinagaubaga katika taaluma mbali mbali za jamii na fasihi ikachukua nafasi
muhimu.
Kipindi
cha uhuru ( miaka ya 1960)
fasihi ya kipindi hiki ilitawaliwa na ukombozi wa bara la Afrika na ujenzi wa
jamii mpya baada ya uhuru. Masuala haya yaliyojitokeza
katika fasihi andishi ya Tanzania wakati huo. Hivyo palitokea fasihi
andishi za kisiasa na kifalsafa zilizojadili kuhusiana na maisha, utawala na ujenzi wa jamii mpya.Kazi
nyingi za fasihi zilipingana na ukandamizaji,
ubinafsi na pamoja na unyama mwingine uliokuwa unafanywa.
Pia fasihi za kipindi hiki zilijadili suala la ubinadamu,Usawa na Ustawi. Baadhi ya kazi
hizo ni za Shaaban Robert,ambazo ni Utu
bora mkulima (1987) na siku ya watenzi wote(1968)
Pia
zinajadili suala la ukombozi, mfano riwaya ya
kiimbila “Lila na Fila” (1966)
iligusa dhamira hiyo kiishara na
Tamthiliya ya E. Hussein”Kinjekitile”
(1969). Katika kipindi cha miaka ya sitini ilitokea fasihi ya aliyojadili maadili mema na maonyo.
Fasihi
hii ya maadili inawakilishwa na J.M
Somba “kuishi kwingi kuona mengi”(1968)
“Alipanda
upepo akavuna tufani” (1968) Mathias Mnyapala “Diwani
ya mnyapala”(1965) S.A Kandoro “Mashairi ya Saadan”(1972), Akili mali “Diwani
ya Akili Mali”(1967)
Aina
nyingine ya fasihi iliyojitokeza katika kipande hiki ni ile riwaya na hadithi fupi
za upelelezi na za mapenzi.Fasihi ya aina hii ilizuka kutokana na nguvu mbali
mbali za jamii.
Katika Tanzania, aina hii ya fasihi
ililetwa kwa mara ya kwanza na M.S Abdulla alipoandika riwaya ya “Mzimu
wa watu wa kale”(1959) na miaka ya 1960 aliandika riwaya ya “kisima cha giningi”(1968) akafuatiwa na
katalambula aliyeandika kitabu cha “Simu ya Kifo”(1965)
Mwisho kazi za fasihi zilijitokeza miaka ya sitini
ni fasihi ya mila na utamaduni inayowakilishwa na M.S Farsy “Kurwa na Dotto”(1960) F.Nkwera “Mzishi wa baba ana radhi zake” (1968)
Kipindi
cha Azimio la Arusha mwaka 1967, Azimio la Arusha
,Baada ya azimio la Arusha kutangazwa
Azimio lilionekana kwa wanasiasa
na wananchi wengi kuwa ndio dira ya kuitetea jamii ya Tanzania katika maisha
bora ya ufanisi na maendeleo, kwa hiyo kipindi cha miaka mitano hivi baada ya Azimio la Arusha kulikuwa na
fasihi ambayo ilitukuza maadili ya awali yaliyotokana na tamko la Azimio la Arusha.
Maudhui
yaliyotawala fasihi ya kipindi hiki ni ujenzi wa jamii mpya kwa kupitia
nguzo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kazi hizi zilizosisita mabadiliko ya
kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, zilizopigania jamii mpya Ijapokuwa
bila kuonyesha kimantiki (kiyakinifu) vipi jambo hilo lingewezekana. Mfano wa
kazi hizi ni:-Mashairi ya miaka kumi ya
Azimio la Arusha (1977),Mashairi ya Azimio la Arusha (1970),Utenzi wa zinduko la ujamaa
(1972),Utenzi wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha (1970),Matunda ya Azimio la
Arusha (1980),Liwazo la ujamaa (1978),Mtu ni utu (1971),Ndoto ya Ndaria
(1976),Njozi za usiku (1970),Kijiji chetu (1971) n.k
Vile
vile Azimio la Arusha pamoja na siasa yake iliyosisitiza kuhusu umuhimu wa
vijiji na umuhimu wa kilimo, zilitokea kazi za fasihi ambazo zilihubiri kuhusu maisha bora wa vijiji yaliyo linganishwa
na yale ya mjini.
Baadhi ya
watalaam waliolitazama suala la siasa ya
ujamaa ni pamoja na Shaaban Robert
katika riwaya yake ya “Utubora Mkulima”(1968) ,Penina Muhando,”Hatia” (1971) Balisidya Shida (1975) Mnyampala, Ngonjera za ukuta (1968)
Mbogo “Giza limeingia”(1980) mashairi mbali mbali katika magazeti n.k katika
kazi hizi mvutano baina ya mji na kijiji ambao ulileta matatizo ya wizi,
ujambazi, umalaya na mengine ya aina hiyo yalitolewa dawa moja tu ambayo ni kurudi vijijini. Jibu
hili halikuwa sahihi kwani linakwepa kiini hasa cha tatizo na
lilipotosha maana halisi ya kijiji na kilichotakiwa kuundwa katika jamii
ya Tanzani.Kijiji kilionekana kuwa mahali pa kuwa lundika wahuni walioshindwa
maisha ya mjini.
Katika
kipindi hiki cha 1970-1980,zilijitokeza kazi
ambazo zilitazama suala lakujenga jamii mpya kwa kutafakari na
kujiuliza na hata kwa mashaka na wasi wasi pia. Hususani baada ya kubaini
utata, migongano ya kitabaka na ukuaji wa haraka wa ubepari wa kimji. Mfano,Kiu
(1972) Kichwa maji (1974),Gamba la nyoka (1979),Nyota ya Rehema (1978) Dunia
uwanja wa fujo (1979)
Kwa ujumla miaka ya 1980 riwaya ya Kiswahili
imeshuhudia jaribio la muundo wa riwaya ya kifalsafa. Lakini kama ilivyogusiwa
kwa kiasi kikubwa mikondo ya riwaya imeendelea kuwa ile ile ya miaka ya sabini.
Riwaya ya ukasuku katika upande wa riwaya dhati imepotea. Badala yake kuwa
riwaya inayopevuka nakutumia ukweli wa mambo. Inayojaribu kubainisha migongano
ya kijamii katika vipengele mbali mbali vya maisha hususani vya kiuchumiu
ijapokuwa waandishi wanafanya hivyo katika mkabala au mitazamo ya maisha
inayotufautiana,mikabala hiyo ni kama vile;Mfumo wa vyama vingi,Utandawazi
Kipindi cha mfumo wa vyama vingi,
Mfumo wa vyama vingi ulianza miaka ya 1990 hapa nchini ambapo uliambatana na
kuanzishwa kwa utitiri wa vyama vingi.Fasihi andishi iliyojitokeza kipindi hiki
ilizungumzia mfumo wa vyama vingi na athari zake kwa jamii yake. Mfano wa kazi hizo ni riwaya ya “Nyuma
ya pazia” (1996), na mashairi
mbali mbali yaliyokuwa yanaandikwa kwenye magazeti.
Kipindi
cha utandawazi,mfumo huu ulienda sambamba na ubinafsishaji wa soko
huria umewaathiri sana waandishi wa fasihi ya Kiswahili.Katika fasihi ya
Kiswahili utandawazi umesababisha kuzuka
kwa fasihi mpya ya Kiswahili ambayo imezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 1990,muda
mfupi baada ya neno utandawazi kuingia masikioni na kuzama akilini mwetu
kuanzia 1980.
Utandwazi
ni
mfumo wa uhusiano wa
kimataifa katika nyanja mbalimbali kama vile biashara,uchumi au siasa
uliowezeshwa na maendeleo ya teknolojia ya habari yanayofanya mataifa na jamii
kuwasiliana kwa urahisi.Pia katika utamaduni, miongoni mwa jamii tofauti za dunia
zimekuwa na mfungamano na uhusiano uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita
hasa katika biashara na uchumi,na kiutamaduni.Mfungamano na uhusiano huu
unaotofautishwa na uhusiano mwingine wa
aina hii uliojitokeza kabla,kwasababu utandawazi umepata kazi kubwa ya kuwekeza
mitaji na kuvuna faida kubwa kiuchumi kiutamaduni, ikisaidiwa na maendeleo makubwa
ya kiteknolojia yaliyopatikana karibuni hasa ya vyombo vya habari vya masafa
marefu.Utandawazi unahusishwa na kuenea kwa tamaduni za kimataifa (Marekani na
Ulaya) kwa njia ya biashara (kama vile vinywaji vya Cocacola, Bia na pombe kali
ambazo zamani zilikuwa hazijulikani). Mtiririko wa muziki na taswira kupitia
video,luninga,mitandao ya kompyuta/Tanakilishi na simu,CD, DVD na VCD.Mfano wa
fasihi ya Kiswahili ni kama vile Nagona(1990), Mzingile(1990),Babu
alipofufuka(2001). Makuadi wa soko huria(2002),Dunia yao(2005), Mkama duma(2005)
zimeathiriwa sana na utandawazi wa kimagharibi, sifa moja kubwa ya kimaudhui
miongoni mwa kazi hizi ni ile ya kushughulikia kwa kina matatizo ambayo yana
kabili ulimwengu wetu leo.Ingawa bado riwaya hii inajishughulisha kwa kiwango
fulani na matatizo ya ndani ya nchi na jamii husika kwa kiasi kikubwa imekiuka
mipaka ya kitaifa na kuenea kwa kiasi kikubwa inachunguza si jamii ya Tanzania
tu bali dunia yote huku ikionyesha athari za utandawazi kwa jamii hizo.
Katika
riwaya ya Babu alipofufuka (2001), Dunia
yao(2003) na Bina- Adamu (2002), Suala zima
linaloshughulikiwa kifalsafa ni siasa. Nini
maana ya kuishi? Nini maana ya uhuru? Nini maana ya maendeleo? Nini maana ya
uraia wa mtu? Nini maana ya uzalendo? Kwanini kikundi kidogo cha watu wapange
maisha ya watu wengi katika jamii Fulani na nje
ya jamii hiyo? Kuna dunia ngapi katika dunia moja ya jamii fulani? Mipaka ya dunia hizo ni miembamba au mipana kwa
kiasi gani? Nini maana ya kifo? Nini maana ya kuishi? Inawezekana mtu anayeishi
akawa amekufa? Nguvu zipi zinaongoza ulimwengu wetu? Zinaongoza kwa mslahi ya nani? Athari hizi za utandawazi katika jamii na
maisha halisi zimehitimishwa na Chachage, ambaye riwaya yake ya “Makuadi
wa soko huria”(2002) inavua nguo na kusambaratisha utandawazi na
utetezi wake wa ndani.
Kwa jumla maendeleo ya fasihi Andishi nchini
Tanzania baada ya uhuru ni makubwa sana
ukilinganisha na wakati wa ukoloni. Tanzu zote za fasihi Andishi, riwaya, hadithi fupi ushairi na
tamthiliya zimepanuka sana. Vile vile kama waandishi wengi sana wa tanzu hizo
na uandishi wao umekuwa ukibadilika kulingana na mabadiliko mbali mbali
yanayoitokeza katika jamii. Kila tukio la kihistoria lililotokea katika jamii
limezaa kazi zake za fasihi.
MADA
NDOGO 2; KUHAKIKI USHAIRI
USHAIRI
Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa kwa
mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye muwala,kwa lugha ya mkato, picha au
sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kueleza
tukio, wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani kuhusu maisha au
mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.Kutokana na maana hiyo kuna mambo
muhimu yanayojitokeza katika ushairi:
Ø Ushairi
ni Sanaa yaani kazi iliyobuniwa na mtunzi mahususi.
Ø Ushairi
una ufungamano na hisia.
Ø Ushairi
una mpangilio wa aina fulani kuanzia kiwango cha sauti, neno, sentesi hadi
ubeti.
Ø Ushairi
huchota hisia na tafakari zake kutoka katika ulimwengu halisi wa maisha ya
jamii na mara nyingi hufungamana na falsafa ya jamii fulani.
Ø Ushairi
hutumia lugha ya mkato yenye kueleza mambo mengine kwa maneno machache kwa
kutumia mbinu za taswira na tamathali za semi.
Ø Ushairi
huzingatia sana dhana ya urari (ulinganifu wa vitu) kimuundo.
Ø Ushairi
una uhusiano na muziki (nidhimu) ngoma na uchoraji (mchoraji) hutumia rangi na
brashi mshairi hutumia taswira na maneno.
AINA ZA
MASHAIRI YA KISWAHILI
Kuna aina tatu za ushairi waKiswahili.Aina hizo
ni:-
1)
USHAIRI
WA KIMAPOKEO
Ni mashairi na tenzi za
kijadi zenye kufuata kanuni za urari wa mzani na mpangilio wa vina vya mwisho
au kati.Katika ushairi wa kimapokeo kuna mambo ya msingi ambayo ni uti wa mgongo wa ushairi wa
Kiswahili.Shairi la Kiswahili lazima liwe na vina na mizani,mistari ubeti na
kituo.
Katika utenzi
(aina pia ya ushairi wa kimapokeo) kuna kuwa na bahari katika mstari wake wa
mwisho.Ushairi wa kimapokeo unaweza kugawanyika katika sehemu kuu mbili yani Tenzi na
Mashairi
a) TENZI
Ni
utungo ambao kimaudhui huelezea tukio fulani linalotokea katika jamii au
liliwahi kutokea.Pengine huweza kuwa maelezo juu ya wasifu wa mtu fulani, jambo
fulani la kihistoria au jambo lolote zito linaloelezwa kwa maelezo
marefu.Utenzi ni masimulizi marefu juu ya jambo fulani maalumu
Katika upande wa fani utenzi una
sifa za pekee kabisa
v Beti,Utenzi
una beti nyingi kuliko yalivyo mashairi au aina nyingine yoyote ya ushairi.Beti
hizi zaweza kuwa 100,200,300 au zaidi kutegemeana na ufundi wa mshairi
mwenyewe.
v Mizani,Utenzi
huwa hauna mizani ndefu,tenzi zilizoshamiri sana katika jamii hii ni zile zenye
mzani nane nane katika kila mistari zaweza pia kwenda zaidi ya nane kufikia
kumi na moja lakini hazuii zaidi ya hapo
v Vina,Katika
utenzi kila ubeti huwa na mistari minne, mistari mitatu ya kwanza ikiwa ina
vina vyenye urari sawa na ule wa mwisho ikiwa na kina tofauti ingawa vina vya
mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari sawa lakini vina hivyo
hubadilika badilika toka ubeti mmoja hadi mwingine.
v Kina
cha mwisho,Katika utenzi kina cha mwisho katika
msitari wa mwisho wa kila ubeti huwa hakibadiliki badiliki,kina cha mwisho
wataalamu wengi wa ushairi hukiita bahari kwa sababu huwa kimetenda na kuongelewa katika
utenzi mzima Mfano wa tenzi: S.Robert, Mapenzi bora,A.Abdilatif, Utenzi
wa maisha ya Adam na Hawa (1971)
J.K.Nyerere, Utenzi wa Injili
kadiri ya utungo wa Luka (1996).Mfano Utenzi wa Fumo Liyongo
(13 BK)
Ubeti 6: Liyongo Kitamkali
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na hiba huongeya
Ubeti 7: Kilimo kama utukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu hujakumwangalia
Ubeti 10:Sultani pate Bwana,
Papo
nae akanena,
Wagala mumemwona,
Liyongo kiwatokeya
b)
MASHAIRI
Shairi kama sehemu ya ushairi, ni utungo
ambao huelezea kwa ufupi mambo fulani kuhusu binadamu na mazingira
yake.Aghalabu mashairi huelezea mambo yanayomhusu binadamu na maisha yake ya
kila siku.Mashairi ya kimapokeo yanapoandikwa hufuata kanuni za vina, mizani,
mistari, ubeti na kituo mfano:-
KUNTU SAUTI YA KIZA (FUNGATE YA UHURU-UK 38)
Nyuki
ni mtanashati, umbo na zake tabia,
Yeye
yu kila wakati, vichafu huvikimbia,
Mchana
na kulati, hatui kwa kukosea,
Kuntu
sauti za kiza, Nyuki hapendi vichafu.
Ni
inzi na sio nyuki, Nadhafa hajazoea,
Kwa
uchafu ni ashiki, hawezi kuuachia,
Vianzavyo
humiliki, fahari hujonea,
Kuntu
Sauti za kiza, Nyuki hanyoni vichafu.
U WAPI UZURI WAKO
U
wapi uzuri wako, haupo umepotea,
Ya
wapi maringo yako, na hashuo za dunia,
Leo
upo peke yako, sote tumekukimbia.
Sasa
ni chano cha maji, watu wajichanyatia,
Umekwisha
ujuwaji, haya zimekupatia,
Yale
usoyatarajia kwako yamekuhamia.
DAFINA
Paa
ni kuruka angani, kama ndege wa tiara
Paa
ni mnyama porini, ni mwenye nyingi, Papara
Paa
ni kuteka mengine, moto uwako imara
Paa
ni toa migombani, Samaki atie sura
Paa
Pia ni la nyumba, makuti au kurara
Mgodi
wa Kiswahili ni dafina isiyokwisha
2.
USHAIRI WA MLEGEZO / KISASA / MASIVINA
Ni
mashairi yasiofuata urari wa vina na mizani.Vina vinaweza kutoka lakini si
lazima katika mistari.Pia mapigo yanaweza kuwa sawa kwa idadi katika mfululizo
wa vipande kadhaa lakini si katika tungo nzima.Mfano:
CHAI
YA JIONI
Wakati
tunywapo chai hapa upenuni
Na
kuwatazama watotowetu
Wakicheza
bembea kwa furaha
Tujue
kamba ya bembea yetu
Imeshalika
na imeanza kuoza
Na
bado kidogo tutaporomoka
Kulikuwa
na wakati uinisukuma juu
Nikaenda
zaidi ya nusu duara
Kulikua
na wakati nilidaka
Ulipokimbia
na kuanguka
Sasa
tukisubiri ndoto tusizoweza kutekeleza tena
Tumalize
machicha ya chai yetu ya jioni
Bila
kutema tena na kuwa tabasamu
Baada
ya hapo tujilambe lambe utamu utamu
Uliobakia
kwenye midomo yetu
Tukikumbuka
siku ilee ya kwanza
Tulipoutana
jioni chini ya mwembe
Tukifunga
bembea yetu
Naye
umbwa samba akikusubiri
Lakini
kabla hatujaondoka kimya kimya
Kukamilisha
nusu duara iliyobakia
Tuhakikishe
vikombe vyetu visafi
(Kazilahabi
1988)
VIJENZI
VYA USHAIRI WA KISWAHILI
Ushairi
wa Kiswahili unajengwa na vipengele vifuatavyo:-
1.
Mpangilio wa
maneno
Maneno
ya ushairi hupangwa ili kuleta maana
fulani,sauti za aina fulani au urari
fulani wa mizani.Katika shairi la Kazilahabi “Kisu mdomoni” ,(kiuchumi)
uk 10 kuna mstari ufuatao.
“Ya
nyuma sana nisijali ya mbele sana niyakabili. Hapa neno “sana” limewekwa
makusudi kati ya “nyuma” na “nisijali” ili kupata maana mbili. Mambo ya zamani
sana (ya nyuma sana) na kutojali jambo neno (sana nisijali) kama neno sana
kinga kuja baada ya nisijali maana hizo mbili zisingalitokeza.Vivyo hivyo uwili
huu wa maana tunaupata katika kipande cha pili cha mstari huo “ya mbele sana
niyakabili” kutokana na mpangilio wa maneno.
2.
Takriri na Ridhimu au wizani
Takriri ni mbinu ya kurudia rudia jambo
kwa kusudi maalumu, vina na urari wa mizani ni aina ya takriri. Mtunzi anaweza
pia kurudia rudia maneno fulani au silabi fulani kwa shabaha malumu. Kwa mfano
katika shairi la “ Kufa moyo” Shaaban Robert anatumia mbinu ya takriri kwa kurudi rudia
kifungu cha maneno “ siku ya ………. Kwa msisitizo:-
Siku ya panga
kufuta, mashujaa kwenda kona
Siku ya kuja
matata, kwa damu kwenda mdundo
Siku ya watu
kuteta, kufa moyo mfundo
Siku ya kung’ara
nyota za watenzi wa mtindo
(Shaaban Robert 1991 : 48-49)
Takriri
hutumika sana katika nyimbo na mashairi ili kutia msisitizo.
Ridhimu
ni mapigo asili ya lugha ,kila lugha ina mapigo yake.Mawimbi ya sauti yenye
kupanda na kushuka na yanayofunga maana na mfuatano wa sauti usio na maana
yoyote.
Ridhimu
ya ushairi wa muziki hutokana na mlingano wa vipande vya mapigo ya lugha au
sauti . Katika muziki vipande hivyo vya mapigoni lazima vilingane kabisa katika
ushairi.Vinaweza kupitana kidogo ili kupunguza maudhi masikioni.
3.
Taswira au Picha
Taswira ni mbinu
ya kuumba picha ya jambo katika mawazo ya msomaji au msikilizaji wa tungo hilo
kwa kutumia maneno. Picha ya maneno ikichorwa vizuri mtu huweza kuhisi, kuona,
na hata kunusa kile kinachozungumzwa.
Mfano:
Amina umejenga,
umekufa umetangulia
Kama ua
umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea
mwanga, peponi kukubaliwa
Mapenzi
tuliyofunga, hapana wa kufungua
(S. Robert Amina 1966: 3)
Katika
ubeti huu, mshairi analinganisha maisha ya mauti ya Amina kwa njia ya picha na
ua mbalo limekuwa likichanua na kisha likafunga au kunyauka.
4.
Tamathali za Semi
Tamathari ni
umithilishaji yaani uwakilishaji wa jambo kwa kulinganisha au kulifananisha na
jingine.Kwa mfano badala ya kusema “Juma alikuja mbio sana” Mshairi atasema
“Juma alikuja kama umeme” Tamathari nzuri hupanua, huyadumisha na huipa uhai na
uhalisia zaidi dhana inayoelezwa, huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au
msikilizaji wa shairi na athari ya kudumu katika hisia na mawazo yake.
Tamathari
zinazotumika zaidi katika ushairi ni Tashbiha, tafsida, tashhisi, mbalagha,
kejeli, sitiari n.k.
5.
Hisia za kishairi
Hisia hizi
hutokana na msukumo wa ndani wa moyoni alionao mshairi wakati anapotunga shairi
lake na hujidhihirisha katika uteuzi na mpangilio mzuri wa maneno yenye
kuwakilisha maudhui husika kwa mfano, maudhui ya huzuni hudhihirika katika
maneno yanayotumika ambayo aghalabu yanadokeza hali ya huzuni, vina vyenye
sauti ya kilio.Mfano ee, lel, lel, lel, ea, aa, ya n.k.
Mfano mzuri ni
shairi la Shaaban Robert la AMINA ambazo linaomboleza kifo cha mkewe.Hisia za
furaha pia huweza kuwasilishwa kwa njia hizo hizo
Mfano:-Shairi
la Cheka kwa furaha
Dhiki
ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha!, ndio ada duniani,
Basu cheka kwa! kwa!, usifike moyo wako.
(Robert, kielelezo cha fasihi 1968:16)
6.
Lugha ya mkato.
Shairi
huzungumza mambo wa ufupi kuliko ulivyo katika maongezi ya kawaida. Hivyo ni
muhimu kwa mtunzi kujua namna ya kueleza jambo kwa Lugha ya mkato.Hii
inawezekana kwa kutumia taswira na tamathali badala ya maelezo marefu.
7.
Mchezo wa maneno
Mbinu ya
kuchezea maneno hutumiwa na washairi ili kutoa maana ya kile kisemwako na
kuongeza utamu wa usemaji mara nyingi maneno yenye umbile moja lakini maana
tofauti hutumiwa kwa ajili hii mfano katika Shairi la M.Mulokozi la “wale,
wale” maana tatu za neno wake (yaani kundi la watu na hao watafune na kumeza
chakula “na” “wale”wale” kwa maana ya “hao hao” si wengine zinachezewa ili
kuleta ujumbe fulani.Mshairi anaona kuwa hakuna mabadiliko ya msingi
yaliyotokea .Kundi lile la walaji limerejea katika madaraka kadharika maneno
“kura” na “kula” yamewekwa sambamba ili kuonyesha uhusiano uliopo kati ya uchaguzi
(kupiga kura) ulaji.
Wale wale
Wale wale ndiyo wao
Bado wapo palepale
Wao wale wenye vyao
Na vya kwao vile vile
Wala kale wala leo
Kura huko kule kule
Mwendo huu ndiyo huo
Bado tupo pale pale
(Mulokozi 1990)
FANI NA MAUDHUI
Ushairi
kama Sanaa hujengwa na mambo mawili ambayo ni fani na maudhui.Maudhui ni mambo
yaliyomo (yanayozungumzwa) ndani ya shairi na fani ni njia anazozitumia mtunzi
kuyasawirisha maudhui yake kwa hadhira yake.Fani na maudhui huingiliana
hutegemeana na kukamilishana.Ni mambo ambayo hayatunganiki, fani hubeba
maudhui, na maudhui huathiriwa na fani.Uwiano wa fani na maudhui ndiyo kigezo
bora cha ndani cha ubora wa shairi.
Katika
fani kuna mambo yafuatayo:- Muundo, mtindo, matumizi ya lugha na jina la kitabu
katika kipengele cha lugha kuna mpangilio wa maneno, tamathali za semi,
methali, misemo, picha n.k.
Maudhui
ni mawazo yanayosemwa ndani kazi ya Sanaa.Mada kuu inayayozungumziwa katika
shairi huitwa dhamira.Dhamira inapounganishwa na mtazamo wa mtunzi, Shabaha na
ujumbe hupatikana yanaweza kuhusu jambo lolote linalohusika.Maudhui yanaweza
kuhusu jambo lolote linalomkera mwanadamu kwa mfano maana ya maisha, mapenzi,
mauti, ndoa, elimu, kazi, dini, ukombozi, usaliti n.k.
UHAKIKI
WA VIPENGELE VYA FANI
a)
Mtindo wa
mashairi
Masharti ya Kiswahili yana mtindo mingi
sana katika utungaji wake kwa hakika si rahisi kutambua ama au idadi ya aina za
utungaji wa ushairi,kwani hii hususani kutegemeana sana na ufundi wa mtungaji
mwenyewe.Baadhi ya mtindo ya utungaji wa ushairi ni kama ifuatavyo
a)
Mtindo wa pindu
Katika
utungaji wa aina hii silabi mbil za mwisho wa mstari hurudiwa rudiwa kwa mfano:
kama mstari wa kwanza uliishia na neno “fahamu” basi mstari wa pili utaanza na
silabi mbili za mwisho, yaani “hamu” wakati mwingine huitwa “Mkufu”
Mfano: Zipokeeni Salamu, lamu kilwa na mvita,
Vita kwa wanadamu, damu zinawezachonyota,
Nyota njema ni agumu, gumu jema kulipata,
Pata kwa kuyafuata, fuata mambo mazuri.
Zuri katika dunia, nia mama yanaleta,
Leta kila la sheria, ria huleta matata,
Tata watu hujifia, fia ipo kwa kupita,
Pita usije kupita, pita katika mazuri.
(waniitila,
kichocheo cha fasihi simulizi na andishi Uk 224)
b)
Mtindo wa
msisitizo
Kuna
msisitizo wa aina mbili, kuna msisitizo wa wima na msisitizo wa ulalo
Msisitizo
wa wima ni kule kuwa na neno moja likawa linatokea mwanzoni na linarudiwa
katika kila mistari wa shairi zima
Mfano: Ua langu la moyo, nitunzo nipowe
Ua langu usinitunze, ua nitunze nitowe
Ua nikae shingoni, ua usinichambue
Ua la moyo ua, Ua lichanue kwangu
(Diwani ya Akilimani 1973:63)
Msisitizo
wa ulalo ni ule wa kutumia kibwagizo kama kiini cha habari yote inayozungumziwa
katika shairi lote na ikawa hicho kibwagizo cha rudiwa rudiwa katika kila ubeti
wa shairi
Mfano: Kokoni kucha kuchile, risala enenda hima,
Kufika similatile, ulitimavu si mwema,
Kumbe nao watambule, haya ninayoyasema,
Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
Sipendelei kusudi, na manji mno kusema,
Nendapo hijitahidi, kimya change hatuzamu,
Kanama sio mwadi, watu wengine si wema,
Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
(fani
na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1939:18)
c)
Mtindo wa beti
kubadilisha vina.
Iwapo
katika ubeti wa kwanza kina cha kati kilikuwa “na” na ile ile cha mwisho
kilikuwa “ma” basi katika ubeti unaofuata kina cha kati kitakuwa “ma” na kile
cha mwisho kitakuwa “na”.
Mfano: Kila shairi nalia, chozi latoka machoni,
Na ninyi mwangalia, wala hamniponzeni,
Mpenzi kankimbia, naudhika simwoni
Nirudie we mwandani, roho ipate tulia.
Nakuomba samahani, magoti nakupigia,
Nisamehe nuksani, zote nilo kutendea,
Naapa kwa yangu dini, kamwe sitayarudia,
Narudia we mwandani, roho ipate tulia.
d)
Mtindo wa
kubadilisha vina vya kati toka ubeti ili hali vile vina vya mwisho katika ubeti
vikibaki vile vile
Katika
ubeti wa kina kina cha mwisho kilikuwa “za” basi kina hicho kitaendelea
kujitokeza ubeti mmoja hadi ubeti mwingine wakati vile vya kati vitaendelea
kubadilikabadilika.Mfano: Jalali wangu mchunga, nikidhi yako rehema,
Niweke
natangatanga, nitabaruku kwa wema,
Niweke
kwenye kiunga,cha malisho ya uzima,
Na
majani ya rehema, na vijito vyenye raha.
Tabaruku moyo wangu, nisifikwe na
zahama,
Pasinifike machungu, kwani u mwenye hunena,
Nakutegemea tangu, wala sinayo tahuma,
Uniongoze kwa wema, nami nitakutukuza.
(fani na taratibu za ushairi wa
Kiswahili 1986:38-39)
e)
Mtindo wa kidato
Katika
muundo huu baadhi ya mistari na maneno yake au silabi zake zina maneno machache
au zimefupishwa tofauti na mistari mingine ambayo huwa na silabi au maneno
mengi.Ufupishaji huu wa maneno au silabi katika baadhi ya mistari hufanywa kwa
lengo maalumu.
Mfano:Tohara, kwa wanawake ni hatari
Madhara, kwa wake uke, hushamiri
Hasara, ya peke yake, hudhurika
Zinduka
(Wasakatonge 2004:02)
f)
Mtindo wa kuhoji
Huu
ni mtindo unaotumiwa na mwandishi wa kuuliza maswali ambayo aidha majibu yake
yako wazi au hayako wazi hivyo mtindo huu unaweza kutumika kama tashtiti.
Mfano: Si wewe?
Ukinijia mapema kama ukidayatema,
Nikawa kama wako baba na mama,
Kakulea kwa ugonjwa na uzima,
Ni wewe uso hisani.
Si wewe?
Niliyekunyima chungu kukutafutia tamu,
Kila kichota hakisishi hamu,
Ukazoa bila kufahamu,
Kuhujua kuichota,
Ni wewe ujilaumu.
(Fungate la uhuru 1996:42-43)
g)
Mtindo binafsi
Huu
ni mtindo ambao mwandishi anaweza kutumia nafsi ya umoja au wingi au nafsi
kundi kila nafsi ina maana yake kimaudhui.Nafsi moja huzungumzia mambo fulani
yanayomkabili mtu mmoja tu.Mara nyingi huwa ni maonyo, mawaidha au sifa.
Mfano:
Umeshapwelea nchi kavu,
Wako werevu umekwisha,
Sasa tunatweta,
Utaabani,
Ni wewe ulo mrafi,
Si wewe?
(Wasakatonge 2004:21-22)
Nafsi
nyingi hutokea pale mashairi anapozungumzia na kundi fulani la watu huku na
yeye akiwa mmojawapo.
Mfano: Hatukubali
tena,
Kwetu kurudisha ubwana,
Kwetu kuurejesha utwana,
Kwetu kuurejesha utumwa.
Hatukubali katu,
Ndani ya nchi yetu.
Hiyo huru.
(Wasakaonge 2004:30-31)
Lakini
nafsi kundi hutoka pale ambapo mwandishi au msanii anapozungumza na kundi la
watu huku yeye akiwa ama msimulizi.Hutoa masimulizi kama hadithi au hotuba
fulani.
Mfano:
Jua kali ni wasakatonge.
Wao ni wengi ulimwenguni
Tabaka lisilo ahueni
Siku zote wako matesoni
Ziada ya pato hawaoni
Lakini watakomboka lini?
(Wasakatonge 2004:5)
h)
Mtindo ambao
unaruhusu kipande kizima cha mstari wa mwisho wa ubeti kuweza kurudiwa, kikiwa
ni chanzo cha huo ubeti unaofuata:-
Iwapo
mstari wa mwisho wa ubeti wa kwanza ulikuwa kama “Uwanjani nayanena, leo wote
wataona” Basi ule mstari wa kwanza na ubeti wa pili utaanza na “leo wote
wataona”
Mfano: Chochote
ulichonacho, kilikuwa kwa mwenzako,
Leo yeye hako nacho, kimesha hamia kwako,
Huenda utokwe nacho, kiende kwa mwingine huko,
Kiumbe wacha vituko, sione ulichonacho.
Sione ulichonacho, ukaendesha vituko,
Na upambwe chokochoko, mwishowe ni
pukutiko,
Malao akupambacho, kilipambiwa mwenzako
Kiumbe wacha vituko,sione ulichonacho.
(Sheria za kutungo mashairi na Diwani
ya Amri 1967:30)
Kimsingi mitindo katika ushairi ni mingi
sana na hutegemea ufundi wa mshairi katika kuunda mashairi yake na ushair
unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa.
ii) Miundo ya Mashairi
Muundo
ni neno pana ambalo hujumlisha mjengo wa shairi yaani jinsi ulionekana.Mashairi
yana mundo mbalimbali kutegemea ufundi wa mshairi mwenyewe kimsingi Shairi
linaweza kuwa la kimapokeo au likawa Shairi huni (kisasa) Shairi la kimapokeo
huwa na mpangilio maalumu wa vina na mizani, silabi, vituo, beti n.k.Idadi ya
mistari huzaa aina mbalimbali za mashairi.
a)
Muundo wa Tarbia
Kila
ubeti wa shairi huwa na mistari mine na kila mstari huwa na mizani kumi na sita
(16) vile vile katika muundo huu kila mstari unakua umegawanika katika viande
viwili vilivyo na mizani sawa kila kipande kukiwa na mizani nane.
Mfano: Amkeni
kumekucha, wakubwa hata wadogo,
Wadoho siku waacha, kwa kuogopa kinyongo,
Kinyongo sikuficha, kukificha ni uongo,
Mnapowacha madogo, na makubwa mtawaacha.
Na wakubwa mtawaacha, mnapoacha madogo,
Mfano kama kuchacha, chakula japo kidogo,
Kidogo kinapochacha, kikubwa hakina kingo,
Mnapowacha madogo, na wakubwa mtawaacha.
(Masahiri ya Saadani 1972:25)
b)
Muundo wa
Tathnia
Kila
ubeti wa shairi huwa na mistari miwili muundo huu unatiwa zaidi katika nyimbo
si muundo ambao hutumika sana katika mashairi ya kawaida ya kusomwa kam
mashairi au ya kuimbiwa.
Mfano: Mjamzito,
umelazwa “Thieta”
Lazima kupasuliwa
Chake kitoto tumbo kinatweta
Hawezi kujifungua
Mwili u moto, tumbo linamkeketa
Kwa kite anaunguwa
Jasho na Joto, kiungo cha mpwita
Na mauti yanamwita
Ni jambo zito, daktari kufata
Wauguzi waameitwa
(Fungate
la uhuru 1988:08)
c)
Muundo wa
Tathilitha
Kila
ubeti wa shairi unakuwa na mistari mitatu
Mfano: Kujitawala
si kwema, kuliko kutawaliwa,
Kujitawala ni umma, kila yao kuamua,
Kujitawala si kama, wanguzi na rushwa.
Kujitawala khatamu, na umma kushikiliwa,
Kujitawala hukumu, makosa kushitakiwa,
Kujitawala si sumu, mara kwa mara kuuwa.
Kujitawala kisomo, kupiga kubwa hatua,
Kujitawala kilimo, njaa na kuondoa,
Kujitawala si somo, njiani kusimuliwa.
d)
Muundo wa
Takhimisa
Kila
ubeti wa shairi unakuwa na mistari, mitano
Mfano: Hao
nyani wanaruka, mara hapa mara kule,
Hao nyani wanabweka, hawaoni soga mbele,
Hao nyani wanaanguka, waingiwa na ndwele,
Nyani wanababaika,misitu una upele
Msitu haukaliki, nyani wanahangaika.
Msitu wawaka moto, kufukuzwa hao nyani,
Umeligundua pato, la nyani lenye utani,
Moto waziona kwato, zilizoko mapangoni,
Nyani watupa watoto, hawakubaliki mwituni
Msitu haukaliki, Nyani wanahangaika.
e)
Muundo wa
Sabilia
Katika
muundo huu mtunzi au mshairi anakuwa na uhuru wa kuweka zaidi ya mistari mitano
katika kila ubeti, ubeti unakuwa na mistari sita na kuendelea
Mfano: Mmea
unapokuwa, huifurahisha mvua.
Lakini siposogea, hulisingizia jua
Uliamini ni mola, hata maji kukupatia
Ulikubali kabila, haliishi bila mila
Mwanadamu kadhalika, kukua
kufurahika
Huupenda uhakika, wa nyota yake kufika
Umri wa kuridhisha, huhitaji kujitwisha
Hapa, ukiufikisha, huona, kufanikiwa
Maisha ya hupenda, ni, mazuri ya kwenda
Na siyo yenye kupinda, haya daima hupenda
(Diwani ya Mloka 2002:18)
f)
Muundo wa
mistari mine
Muundo
huu unaweza kuwa na mizani nane au pungufu.Muundo huu ni wa Abdilatifu Abdalla
(1973) mfano ametumia katika mashairi yake ya “Kamili wazi” “mnazi” “Jana na leo na kesho” na “Njia panda” mara nyingi huo mstari wa
mwisho kina chake huwa ni sawa na kina cha mwisho wa mstari mwingine katika
ubeti wao
Mfano: Kimbunga
mji wa Siyu, kilichowahi kufika.
Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika
Kimeingoa mibuyu, minazi kunusurika
Nyoyo zilifadhaika
(Kimbunga 1995:01)
iii) Matumizi ya Lugha.
Hiki
ni kipengele muhimu sana katika kazi yeyote ile ya Sanaa ya kifasihi. Matumizi
ya Lugha ndiyo yanayofanya kazi fulani ionekane tofauti na nyingine au itofautishe
kazi ya Sanaa ya kifasihi na ile isiyo ya kifasihi.Luha ndiyo mzizi wa kazi ya
fasihi kwani fasihi ni kazi ya Sanaa inayotoa maudhui ya kutumia Lugha ya
maneno.Matumizi ya Lugha katika kazi ya fasihi yako ya aina mbalimbali
a)
Methali, misemo
na nahau
Mhakiki
anapaswa avifahamu na ajue kuvichambua katika ushairi.Vipengele hivyo vina kazi
ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi
METHALI
Ni
kazi ya Sanaa ya kifasihi inayotumia mafumbo kwa kwaida semi zote zina hakima
ndani yake.Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha hali ambapo methali
hutumika.Methali pia ina kazi ya kufurahisha, kutisha, kuonya nakadhalika,
waandishi hutumia methali katika kazi zao nani jukumu la mhakiki kuzitambua hizo
MISEMO NA NAHAU
Matumizi
ya misemo na nahau hushabihana na yale ya methali.Misemo, misimu na nahau
huzaliwa, hukua nap engine hufa
-Sekela amenipaka mafuta kwa mgongo wa
chupa (sekela amenipa sifa zilizostahili)
-Juma katutangulia (Juma amekufa)
b) Tamathali za Semi
Mulokozi &
Kahigi wanasema kuwa tamathali za semi ni maneno, nahau au semi ambazo hutumiwa
[H1] na
waandishi wa fasihi ili kutia nguvu na msisitizo katika maana, mtindo, na
pengine sauti katika maandishi hayo.Tamathali za semi zinatumiwa pia [H2] kuipamba
kazi ya Sanaa ya kifasihi kwa kuongeza utamu wa Lugha.
Baadhi ya
tamathali za semi ni:-
Ø Tashbiha
Hii
ni tamathali ya ufananisha au mlinganisha wa vitu viwili au zaidi katika
tashbiha kama ilivyo katika sitiari huwa kuna vitu vitatu vinavyofananishwa
ambavyo wataalamu wameviita kuzungumzwa, kufananisha na kiungo.Katika tashbiha
hakuna maana dhahania bali kuna ulinganishaji wa vitu viwili vilivyobayana.
Mfano: Kweli ni sawa na radi, inapotoa kauli…
Kweli kinywnani ikiwa sawa na moto wa nili
Kweli kama msumeno hukoreza sawa kweli
Ø Tashhisi (uhaishaji)
Washairi
mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa na uhai sifa za kitu chenye uhai,
hasa sifa za binadamu, kisanaa maelezo ya kitashhisi huwa na upekee unaomwingia
msomaji akilini haraka, kwani si jambo a kawaida, mathalani kuona mti
“Ukimpungia mtu mkono” au “nyumba ikimkodolea macho mgeni”
Mfano:
kimya hakineni jambo si kimya
chawatazama…
Kimya chajazua mambo, pasiwe mwenye kusema.
Kimya kipimeni sana, msione kutosema.
Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama.
Kimya chaja watukana, na kizuwe yalozama.
Katika
ubeti huu “kimya” (ambayo ni nomino dhahania) kimepewa sifa za binadamu
kinaweza kunena, kutazama, kuzua mambo, kusimama na kutukana.
Ø Metonumia
Hii
ni tamathali inayotumia neno (au semi) kuwakilisha neno, kitu, mtu au dhana
nyingine yenye kuhusiana nalo neno hilo huweza kutumiwa kwa kuwa dhana
inayozungumziwa au kwa kuwa linataja ktu ambacho ni sehemu na kuwakilisha cha
kitu kingine kikubwa zaidi.
Mfano neno “kitambi” huweza kutumiwa
kuwakilisha tajiri au kabila “meno” huweza kuwakilisha kicheko
Ø Mubalagha
Ni
matumizi ya lugha yaliyotiwa chumvi ili kuongeza utamu na kuleta athari fulani
katika ushairi wa majigambo, tamathili hii hutumika sana maana huo ni ushairi
wa kujitapa na mtu mwenye kujitapa aghalabu hujilimbikizia sifa. Mara nyingi
mubalagha hutumika katika tenzi zenye kusimulia habari za mashujaa.
Mfano:
katika utenzi wa fumo Lyongo kuna mfano unaokusudiwa kuonyesha ukubwa wa (kimo
na umbo) na nguvu za Lyongo.
“Ruhu zikienda kishindo
Zima zao hukoma ondo
Huyo ni bwana wa kondo
Ashindaye jeshi miya
Ingawa
wagala wanajulikana kuwa ni watu warefu akini vimo vyao vilifika magotini tu
(ondo) pia Lyongo
Ø Kejeli
Ni
usemi ambao maana ya ndani ni kinyume cha maanayake halisi. Ni usemi wa kebehi
ambamo kisemwacho na msemaji. Pia kejeli ni tukio ambalo ni kinyume cha lile
linatazamiwa au lililotakiwa na ambalo kutokea kwake huwa ni namna ya dhihaka
Katika
shairi la “Ibada na Haki” Shabaan Robert anatumia usemi wa kejeli kukebehi watu
wanothamini fedha kuliko dini.
Anasema
hivi: Huifanya fedha mungu wao
Itazame adha na Imani yao!
Na mwenye akili kama hana fedha
Hatajwi mahali ila kwa rakadha
Na kuadhiriwa kuwa mtu chini,
Tazama dunia ilivyo na dini
Katika
mstari wa pili “Itazame adha na Imani yako!” kuna kejeli, mshairi anachotaka
kutuambia ni kwamba watu hao hawana adha wala Imani katika mstariwa mwisho
“Tazama dunia ilivyo na dini” Anakusudia kutuambia
“Tazama
dunia ilivyo na dini kwa hiyo semi hizo ni kejeli kinachosemwa ni kinyume na
maana yake halisi kadha toka alama za mshangao!) zimetumika kusisitiza hali ya
kejeli.
MBINU ZA KISANAA
Kuna
mbinu mbalimbali za kisanaa ambazo hutumika katika kazi za kifasihi ya ushairi
na ambazo mhakiki atatakiwa azitambue na kuzifafanua mbinu hizo ni kama vile
Ø Takriri
Ni kurudia rudia neno, sauti, herufi au
wazo katika kazi ya Sanaa ya kifasihi.
Mfano: kweli
kitu mahabubu, mwenyezi nijaze kweli
Kweli siri ya ajabu, huwapa watu fadhili
Kweli chimbo la johari, linahimili la kweli
Kweli inatafakari, husema na kujadili
Katika
ubeti huu neno “kweli” limerudiwa rudiwa. Neno hili linasisitiza wazo kuu la
mwandishi
Ø Onomatopea
Ni
mwigo wa sauti. Hutumiwa na washairi kutoa picha au dhana ya kile
kinachowakilishwa au kupambanuliwa na sauti hizo. Mfano tukisema “maji
yalimwagika mwaaa!” neno mwaaa! Ni onomatopea linawakilisha sauti au kishindo
cha maji yanayomwagika. Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa sehemu za
msamiati wa kawaida. Mfano: pikipiki, bomboni, kata n.k.
Katika shairi la
“Cheke kwa furaha” Shabaan Robert ametumia onomatopea ili kuleta dhana ya
kucheka
“Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha! ha! Ndiyo ada duniani
Basi cheka kwa! kwa! kwa! Usafike moyo wote
Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko
Maneno ha! ha!
ha! na kwa! kwa! kwa! Ni onomatopea
yanayotoa sauti ya kusikika ya sauti ya mtu anayecheka. Huu ni mpangilio
maalumu wa sauti ili kutoa picha ya kusikika ya dhana inayozungumzwa
Ø
Mjalizo
Ni kuunganisha
maneno yanayofwatana bila kutumia viunganishi mfano: bila kutumia “na, kwa”
n.k. Mfano: Nilikaa, nikashangaa,
nikachoka
Niliimba, nikanuna, nikacheka
Ø
Mdokezo
Hii ni mbinu ya
kisanaa ambapo mwandishi anaukatiza usemi fulani na kumuacha msomaji. Aghalabu
pana vielekezi vinavyoweza kumsaidia msomaji katika kukamilisha.
Mfano: wimbo la mauaji limezidi
Mashaka…ah! Shida tupu
Maneno…tena anyway…
Labda tusubiri.
Ø
Tashtiti
Ni matumizi ya
maswali ambayo majibu yake kwa kawaida yanakuwa yameeleweka. Swali hili
linakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa kwa ajili ya msisitizo tu au
mshangao.
Mfano: Mtu anayemfahamu amekufa anauliza
-Adela ameachana nami?
Au mtu anayemfahamu amekutembelea
- Jamani hata Luiza naye kaja?
-Aisee ni wewe?
Ø
Usambamba
Ni takriri ya
sentensi au kifungu vya maneno vyenye kufanana kimaana au kimuundo. Usambamba
huonekena sana katika ushairi simulizi
Shabaan Robert
amekitumia kipengele hiki mara kwa mara atika mashairi yake katika shairi lake
“kinyume” anasema
Tulifululiza mwendo lakini sana
twasita
Tulikwenda kwa mshindo lakini sana
twanyata
Katika mistari
yote miwili wazo linalosisitiza ni moja maneno tu ndiyo yanabadilika uwezo wao
wa zamani katika utendaji mambo unalinganishwa na udhaifu “wao” wa sasa.
c) Taswira au Picha
Dhana hii
hutumiwa kueleza neno, kirai au maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika
akili ya msomaji. Taswira zinaweza kuwa za kimaelezo (yaani maelezo fulani
yanaunda picha) au za ki-ishara (zinazounda picha ambayo inaashiria jambo
fulani au imeficha ujumbe mwingine). Taswira huweza kuundwakwa matumizi ya
tamathali za semi hasa tashbiha na sitiari.
Kimsingi taswira
nyingi ni taswira za uoni (yaani zinamchochea msomaji kuona picha fulani)
Mfano: Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho,
Wa huku hafiki huko,wala halina
matisha.
Halishibishi huchosha, wala hapati utuvu,
Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka.
Na milima akapanda, apendako akafika,
Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dinani
Hupati kupenda bara, na hushuki baharini
Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia
Katika shairi
hili tunapewa picha tatu mahususi picha ya kwanza ni neno linalozunguka mshairi
anatuambia kuwa neno ambalo halifuati njia iliyonyooka neno lenye mzunguko
halifiki mwisho wake na halileti mradi uliokusudiwa “Halina malisho”
Hapa neno
limefanya kuwa kitu chenye uwezo wa kutembea na kuzunguka
Picha ya pili ni
ya mtu aendaye safari ngumu kwa ujasiri na moyo wa dhati akipanda milima na
kushuka na mabonde akipenya misitu na kuvuka mito hadi kufika kule anapokwenda.
Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu,
alimradi anajua kuwa itamfikisha kwenye lengo lake. Ni mtu anayepamana na
matatizo badala ya kuyakimbia mtu wa kwenda njia iliyonyooka
Piha ya tatu ni
dira, dira ni chombo kitumiwacho na mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha
majira yao, wasipotee njia. Dira ni chombo cha mviringo na mshale wake aghalabu
huzungukia palepale ulipo, katu hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo
la mwandishi kuwa njia yenye kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye lengolake.
Mshale wa dira huzunguka daima lakini haufiki kokote.
Picha hizi tatu
kwa pamoja zimefaulu kufikisha ujumbe wa mwandishi kuhusu maisha na namna ya
kuyakabili tuyakabili kwa juhudi na ujasiri na nia.
JINA
LA KITABU
Jina la kitabu ni vyema liwiane na yale
yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Mfano: “Fungate la uhuru” (1988) jina hili
linawiana vipi na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?
PICHA YA JALADA KATIKA UCHAMBUZI
Kazi
ya kifasihi kuwa na picha au michoro fulani kwenye majalada yao. Inawezekana
majalada hayo yakawa na uhusiano fulani na dhamira na maudhui ya kazi
zinazohusika. Picha hizi huweza kuwa kielelezo muhimu cha fani kwenye uchambuzi
wa kazi ya kifasihi. Hata hivyo si kazi zote za kifasihi ambazo zinaonyesha
uwiano kati ya majalada yake na yaliyomo.
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA MAUDHUI
Maudhui
katika mashairi hupatikana baada ya mhakiki kupitia beti zote za shairi lile
ili kupata ujumbe wa shairi lazima itambidi mhakiki ajumlishe yaliyo katika
beti mbalimbali za shairi lile.
Kwa ufupi katika ushairi uchambuzi wa
maudhui mhakiki anapaswa kuangalia:
Ø
DHAMIRA
Ni wazo kuu
katika kazi ya fasihi.
Ø
UJUMBE
Ni mafunzo
mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazifulani ya fasihi.
Ø
FALSAFA YA
MWANDISHI
Ni wazo ambalo
mtu anaamini lina ukweli fulani unaitawala maisha yake.
Ø
MSIMAMO WA
MWANDISHI
Ni hali ya
mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa
halikubaliki na wengi, lakini yeye atalishikilia tu.
Ø
MTAZAMO WA
MWANDISHI
Ni hali ya kuyaona mambo katika maisha
kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe
HATUA ZA UCHAMBUZI WA USHAIRI
Katika
uchambuzi huu wa vitendo, kielelezo tutatumia shairi la “Wauwaji wa Albino
wapigwe vita” Shairi hilo linasema hivi:
Kwa
kweli inashangaza, ni mambo hufikirika,
Ukijaribu
kuwaza, wenzetu wanatutukana
Albino
wanaweza, kifo kimeshawafikia
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Ni
unyama wa kuzidi, albino kuwashika
Huu
wote ni ukaidi, utajiri kuusaka
Tena
ni kwa makusudi, maovu umeyashika
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Mikononi
wanawakata, kwa mashoka na mapanga
Kuwasema
sita sita, huu wote ni ujinga
Kwa
vitisho wajikita, kusikiliza waganga
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Albino
tuwalinde, wamekuwa almasi
Wasakwa
kila upande, sababu ya ibilisi
Yatupasa
tuwalinde, binadamu kama sisi
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Majumba
kuyabomoa, pande zote kuzunguka
Damu
isiyo hatia, kwa wingi inamwagika
Mola
inamlilia, hukumu ipo hakika
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Albino
ni wenzetu, uzao wao ni halisi
Acha
tofauti zetu, tena tuwape nafasi
Tujenge
taifa letu, tuuache ukakasi
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Ujinga
na upumbavu, kuwaua albino
Wajawa
maumivu, mikono na visigino
Sahitaji
utulivu, upole mshikamano
Ni
wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Zamu
yako inakuja, mwisho wao utafika
Wenyewe
watajitaja, tena bila ya mashaka
Sote
tuwe na umoja, kufungua mashtaka
Kuwasaka
wauwaji, kusudi wahukumiwe.
HATUA ZA KUCHAMBUA SHAIRI
1.
Lisome
shairi zima toka manzo hadi mwisho ili upate picha ya jumla, kimaana na kiumbo
ya shairi hilo. Katika hatua hii kama shairi ni gumu linaweza lisieleweke, kwa
bahati shairi la “wauwaji wa albino wapigwe vita” linaeleweka bila tatizo
2.
Rudia
kulisoma tena shairi hilo polepole, andika maana ya jumla unayoipata. Unaweza
kupata maana zaidi ya moja katika “Wauwaji wa albino wapigwe vita” maana ya
jumla inayojitokeza ni maombolezo ya mauwaji ya Albino
3.
Huku
ukiwa na kalamu yako ya risasi, rudia kulisoma tena shairi hilo mstari baada ya
mstari. Pigia kila neno usemi, sentensi au kipengele kinachoelekea kuwa na
umuhimu au dhima maalumu ya kifani au kimaudhui.
Katika shairi
ili pengine utayapigie mstari mafungu ya maneno yafuatayo:
-Albino wanaweza kifo kimeshawafikia
-Ni wauwaji wabaya vikali walaaniwe
-wasakwa kila upande sababu ya ibilisi
-damu isiyo hatia kwa wingi inamwagika
-Albino ni wenzetu uzao wao ni halisi
4.
Jaribu
kufanya kisisisi maneno hayo yalyopigiwa mstari au kuorodheshwa katika hatua ya
tatu bila shaka yapo mambo ambayo undani wake hutauelewa katika hatua hii,
hivyo aghalabu itabidi
a)
Urejee
mambo hayo yalivyotumika
b)
Urejee
katika muktadha wa shairi hilo kama una ufahamu kwa upande wa wauwaji wa Albino
wapigwe vita, muktadha huo ni mauaji ya Albino
Jiulize semi,
sentesi hizi zinasema/zinaonyesha au zinadokeza nini? Kwa nini mtunzi kaamua
kutumia maneno hayo na si mengine? Je yanahusiana vipi na maana ya jumla
uliyopata katika hatua ya pili.
5.
Chunguza
vipengele vingine vya kisanaa na kimuundo alivyovitumia mtunzi. Jiulize kama
vinaoana na madokezo ya maana uliyoyapata katika hatua ya nne. Vipengele
unavyoweza kuchunguza katika hatua hii ni muundo wa shairi, vina, mizani,
wizani, takriri, milio ya maneno, tamathali n.k. kwa mfano hadhihirika kuwa
muundo wa shairi ni kijadi ambao hautuambii lolote kuhusu maana ya shairi hili
vifanye uchambuzi vipengele vya kisanaa ulivyovipambanua
6.
Husisha
ufafanuzi wake hadi hatua hiina maana ya shairi iliyokwisha kujitokeza kuona
kama mambo hayo yanaoana barabara au bado kuna pengo au mkinzano.
Baada ya hatua
hii utakuwa umepata maana kamili ya shairi ambayo unaweza kuitetea kifasihi kwa
kurejea katika shairi lenyewe si lazima maana unayopata/unazopata ioane/zioane
na maana watakazopata wengine jambo muhimu ni kuwa na ushahidi wa kutosha
kuweza kutetea hoja zako.
Maana ambayo
umepata hadi sasa yaweza kuelezwa iwe:
Mshairi
anaomboleza mauaji ya Albino ambayo yanafanywa na watu mbalimbali kwa Imani za kishirikina
anaonyesha kuwa kuua binadamu wenzetu ni unyama na ni ukatili. Anamwomba Mungu
awaepushie Albino na mates ohayo.
7.
Hadi hatua hii umepata maana ya shairi lakini bado
hujapata maudhui yake. Ili kupata maudhui unatakiwa upambanue dhamir kuu
ya/za shairi hili na uonyeshe mtazamo wa mshairi kuhusu dhamira hizo. Katika
shairi hili ni dhahiri dhamira kuu ni “Mauaji ya Albino” mtunzi anasawiri tukio
la mauaji ya Albino mwandishi anaonyesha kuwa mauaji ya albino ni tukio lenye
kuleta majonzi na kilio. Mtazamo wake kuhusu mauaji ya Albino ni kwamba
wanaofanya hivyo hawana utu hivyo ni sawa na wanyama wa porini na anaonyesha
kuwa kuwaua albino ni kinyume cha utu
Mtunzi
anazungumzia pia dhamira ya ujinga. Mwandishi anaonyesha kuwa ujinga ni kikwazo
cha maendeleo ya jamii kwani wote wanaojihusisha na mauaji ya albino ni wajinga
na wanataka kupata utajiri kwa njia za mkato.
8.
Katika hatua hii mchambuzi ana uhuru wa kuithamini
kusifu au kwaani.
Baada ya kulichambua na kulielewa vizuri shairi hilo katika hatua saba
zilizotangulia sasa unaweza kulitolea tathmini ya kifani na kimaudhui katika
kufanya tathmini ni muhimu kuzingatia muktadha wa wakati lilipotungwa na wakati
wa leo.
Tathmini yako
itazingatia muktadha yote miwili unaweza kusema kuwa, shairi hilo lilipotungwa
ulikuwa na umuhimu wake leo labda umepungua kwa kuwa muktadha huo wa vifo vya
Albino umepita. Hata hivyo labda shairi limebaki na umuhimu wa kihisia na
kifalsafa kuhusu tatizo la maisha na mauti na ufumbuzi wake.
HISTORIA NA
MAENDELEO YA KISHAIRI WA KISWAHILI
Wataalamu
wengi wanakubali kuwa ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na
nyimbo. Kabla ya karne ya 10 BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na
kugharura kwa ghibu bila kuandikwa.
Kuanzia
mwaka 1000 B, mambo mawili yaliletwa na kuathiri ushairi, mambo hayo ni Dini ya
kiislamu na Uandishi wa hati ya kiarabu waswahili wengi walijifunza kusoma na
kuandika hati za kiarabu, hali hiyo ilienda sambamba na ustawi wa miji ya Pwani
katika biashara na majengo ya mawe mashujaa mashuhuri wa miji ya Pwani
wanokumbukwa katika tendi na masimulizihuenda waliishi katika hicho ni Fumo
Lyongo wa Shangapate kaskazini mwa upwa wa Kenya kati ya karne ya 8 na 9
Katika
kipindi hiko washairi wengi walitunga mashairi mengi kwa ghiba kwa sababu
hayakukusudiwa kuhifadhiwa kwa maandishi kwa kipindi kirefu ni tarihi na baadhi
ya mswada hiyo imepotea. Tungo zilizosalia ni Fumo Lyongo ambayo ilandikwa 1500
BK kutoka katika mapokeo ya mdomo.
-“kumswifu”
yanga au suifa ya mwana ning utingo wa mwanzo kuhifadhiwa kwa maandishi.
Mwaka
1500-1700 BK kulikuwa ni kipindi cha uvamizi wa maneno katika kipindi hicho
tungo chache zilihifadhiwa zikiwasifia maneno mashairi yaliyo wasifia
wareno> mfano
· mzungu mgeli}
1630
· Portugezi Afala}
1630
Lakini tungo mashuhuri za wakati huo ni:
·
Utendi
wa Hamziyya (Seyyid Aidamis bin Athumani 1652)
·
Siri
lasirari (Binti Lamba 1668)
·
Utendi
wa Tambika (Taboka) {Mwango bin Athumani 1728}
·
Siri
Lasirari ni kisa cha kubuni
·
Hamliyya
ni tafsiri ya utendi wa kiarabu kuhusu maisha ya Mtume Muhamadi
· Tabuta (tambuka)
ulihusu vita kati ya waislamu na warumi walikuwa chini ya mfalme Hela kali
1750-1900 kipindi cha waarabu
Sehemu
kubwa za tendi mashuhuri za wakati ambazo mpaka leo zipo ni:
· Tendi za dini na vitu
-
Utenzi
wa Shufaka
-
Utenzi
wa masahibu
-
Utenzi
wa kijamaa
-
Utenzi
wa mayasa na mikidadi
-
Utenzi
wa Ras L Ghuli (unahusu vita vya waarabu kati ya waislam na makafiri-{1855})
· Tungo za kitamaduni, mawaidha na Tumbuiza
Tungo
hizi zilikuwa nyingi na zilikuwa katika maandishi na zilihusu (maudhui yake)
kueleza mandhari ya Afrika Mashariki mfano tungo hizi ni:
-
Utenzi wa
Inkishafi (1810)
Mtunzi: Seyyid
Abdallah bin Nasri.
Utenzi huu unazungumzia matokeo ya
uvamizi wa waarabu na wareno ambapo matokeo yake ni kuporomoka kwa mji wa Pate.
Ø Utenzi wa Mwana kupona (1858)
Unahusu
utamaduni na misingi ya Dini. Utenzi huu uliandikwa kama wosia kwa binti yake
na kwa kiasi kikubwa unahusu unyumba pia ndani yake kuna mafundisho ya unyago
kwa watu wa Pwani.
Kundi
jingine kubwa ni mashairi ya siasa kundi hili liliwakilisha/lilisimamiwa na
akina Muyaka bin Haji wa Mombasa. Huyo alitunga mashairi ya kupinga waarabu wa
Oman mfano;Suid bin Said (1810-1876),Kibabina
(1776-1834) na wengine.
Wote
hawa walitunga mashairi yaliyohusu harakati za kisiasa na kijamii za wakati
huo, wa baadhi yao walifungwa au kuuwawa gerezani kwa sababu ya kupinga
kutawaliwa. Mchango mkubwa wa hawa ni kuendeleza mashairi ya unne (tarbia)
Kwa
ujumla katika kipindi hiki mambo yaliyojitokeza katika maendelezo ya ushairi ni
manne:
Ø Umbo la tarbia
(unne) ulifika kilele
Ø
Utendi
Ø
Kanuni
ya utunzi ziliwekwa wakati huo
Ø
Hati
ya maandishi (Kiswahili n kiarabu) ilisanifiwa kuzingatia sauti za lugha ya
Kiswahili.
1885-1918 USHAIRI WAKATI WA UKOLONI WA
KIJERUMANI
Ushairi
wa wakati huo unaweza kugawanyika katika makundi matatu.
Ushairi wa
kawaida-mashairi haya yalihusu mawaidha, mapenzi na dini.
Ushairi wakusifu
wakoloni- huu uliandikwa kwenye magazeti na vitabu mfano kitabu maarufu cha Dr.
C,kinachoitwa Velter (1907) Prose and Poesie der Sua heli .Kitabu hiki
kilisifu utawala wa kidachi
Ø Ushairi wa
upinzani.
Ushairi huu
ulipinga utawala wa kikoloni.
Mfano: utenzi wa
vita vya wadachi (H.Abdallah)
Ø Utenzi wa vita
vya majimaji
Katika kipindi
hiki mambo matatu yalitokea katika ushairi kwa upande wa Tanzania.
Kuandika kwa
kutumia hati ya kirumi hati hii ulienea kwa kupitia Elimu kanisa na ilianza
kutumiwa na watunzi baada ya hati ya kirabu
Utafiti kuhusu
ushairi ulianza wakati huo na wachambuzi maarufu walikuwa C.Velter Buttner na
K.Mein holf n.k
Hawa walisaidiwa
na waafrika kama vile Mohamed Kajunwa, utenzi wa Fumo Lyongo Rev.Taylor ndiye
aliyekusanya mashairi ya Fumo Lyongo.
1918-1961 UKOLONI WA KIINGEREZA
Kipindi
hiki kiliambatana na mambo matatu mapya:-
a)
Elimu .Hii ilieneza
lugha ya Kiswahili na ushairi katika maeneo ya bara kupitia shuleni maarifa ya
kusoma na kuandika. Hati ya maandishi ya kirumi ilienea kupitia elimu
b) Kuanzishwa kwa mashirika ya uchapishwaji.Katika kipindi
hiki magazeti mengi yalichapwa kwa lugha ya Kiswahili na kusambazwa. Baadhi ya
magazeti yalikuwa na kurasa maalumu ya ushairi ambapo ulisaidia kuwakutanisha
watunzi kutoka Afrika Mashariki.
Mfano: Gazeti la
“Mambo leo” 1923 kupitia gazeti hilo watunzi maarufu kama S.Robert, Mdanzi
Hamasa, Mzee Waziri (kijana) walipata umaarufu kupitia mambo leo
Pia kuanzishwa
kwa shirika la wachapishaji vitabu Afrika Mashariki (E.A.L.B) kulisaidia sana
kukuza na kueneza Sanaa ya ushairi.
c) Shughuli za siasa za kudai Uhuru ziliibua ushairi
wa kisiasa mnamo mwaka 1950-1960.
Mfano: S.Kandoro
alitunga mashairi mengi pia kipindi hicho ushairi ulikuwa wa aina.
1.
Mashairi
yaliyosawili mfumo wa uchumi wa kikoloni. Mfano Matatizo ya kazi, umanamba,
mshahara mdogo n.k haya yote yalitolewa na gazeti la mamba leo.
2.
Mashairi
yaliyohusu utaifa yalianza miaka 1930. Haya yalijiuliza mwafrika ni nani? kwa
nini mzungu yupo hapa?
Mfano: S.Robert- mashairi ya kutetea weusi mfano Shairi la Rangi zetu,S.A.Kandoro kwetu ni kwao kwa nini
Pia kulikuwa na mashairi ya kutetea Lugha
mfano S.Robert (Titi la mama li
Tamu) S.Kandoro (Kitumie Kiswahili)
3.
Mashairi
ya kisiasa ambayo yalihimiza watu waungane ili waweze kujitawala wenyewe mfano,S.Kandoro
shairi la siafu wamekazana
4.
Pia
kipindi hiki walitokea wachunguzi wengi sana wa ushairi wa Kiswahili.
Mfano: Withchens (1930), A.Wine, B.E.Damman
(1930-50) Lumbart, H.Cory W.Whitely n.k. “wazungu”. Waafrika Sr. Mbarak Hisway,
Hamis Kitumbe
USHAIRI
BAADA YA UHURU
Baada
ya uhuru ushairi ulisambaa zaidi kutokana na msukumo wa kisiasa fani mpya mfano
Ngonjera na mtiririko au tungo huru zilizanziashwa ili kuzingatia mahitaji
mapya ya kisiasa na kisanaa. Ushairi wa Kiswahili baada ya uhuru ulikuwa wa
aina kuu mbili
v
Mashairi ya
kawaida:
Haya yalitungwa sana magazetini na vitabu vya mashairi mbalimbali vilichapishwa
ambapo Dhamira za malezi, mapenzi , dini, mawaidha n.k.
o
Akilimali
snow- white
o
Mwinyi
khatibu- Mohamed
o
Andanenga
o
S.Kandoro
o
S.Robert
1.
Mashairi ya
kisiasa: Hapa
kuna makundi mbalimbali ya mashairi ya kushangilia Uhuru.Mfano: Utenzi wa uhuru
wa Tanganyika,Utenzi wa jamhuri wa Tanzania
Utenzi wa uhuru wa Kenya.
a)
Mashairi yanayojadili dhamira ya ujenzi wa jamii
mpya. Katika mashairi
yao walisisitiza watu wafanye kazi ili kuinua pato.
Mfano: S.Kandoro
katika shairi la kujitawala,J.K.Nyerere-chombo cha taifa letu
b) Mashairi ya
Ujamaa
Hayo yalitokea
baada ya Azimio la Arusha ambalo yalisisitiza siasa ya ujamaa na kujitegemea,
ambapo walipinga unyonyaji, ukupe, ukabila na ubepari. Walitukuza kilimo na
kuwashawishi watu kurudi shamba (kijijini)
Mfano: Mashairi
ya Azimio la Arusha (kamaji), Ngonjera za Matias Mnyapara, Mashairi ya miaka 10
ya Azimio la Arusha ( Abdulah)
Tatizo kubwa
lilijitokeza katika hiki ni ukasuku ambapo waandishi wengi walikariri hotuba za
viongozi bila kuzifanyia uchambuzi na kuziandikia mashairi.
c)
Mashairi
yaliyohakiki siasa iliyokuwepo na hawa walikuwa na mitazamo mbalimbali.
· Wanauhalisia
Walihakiki
dhana ya ujamaa na ukombozi na kuchambua mafanikio ya matatizo yake hasa katika
utekelezaji wa malengo ya Azimio la Arusha. Waandishi hao ni E.Kezilahabi,
E.Husein, Z.Mochiwa na T.A.Mvungi.
· Washairi wa Mlengo wa kushoto
Hawa walikuwa na
mambo yafuatayo walichukua msimamo wa kufanya kazi na mkabala wa kitabaka
katika kutolea tungo zao
· Waliona usoshalisti kama suluhisho la matatizo yao.
Ili usoshalist upatikane waliona
ni lazima kumwaga damu (kutumia nguvu). Kundi hili lilikuwa na K.Kahigi, na M.Mulokozi, Ally Salehe,
M.S.Khatibu, A.Abdullah na S.A.Mohamed.
Hivyo Sanaa hii ambayo ilianza upwa wa
Kenya na Tanzania katika karne ya 10-15 sasa imeenea Afrika Mashariki nzima
hadi Rwanda, Burundi na Kongo
MGOGORO
KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI
Mgogogro
huu ulianza mwisho mwa miaka ya sitini (1968) na mwanzoni mwa miaka ya sabini.
Mgogoro ulihusisha pande mbili yaani washairi wa kimapokeo (wasiokubali
mabadiliko hawa walisisitiza kuwa vina na mizani ni uti wa mgongo wa shairi la
Kiswahili) lakini wanamabadiliko waliona
kuwa si lazima shairi liwe na vina na mizani.
Sababu
kuu zilizozua utata ni mbili
v Maana ushairi
kwa ujumla
v Maana ya shairi
la Kiswahili
Mvutano
huu unahusisha na mabadiliko ya kidunia yaliyotokea miaka ya Sitini na Sabini
katika Nyanja mbalimbali za maisha hata kupelekea washairi nao kuhitaji
mabadiliko katika tasnia ya ushairi kwa upande wa fani.
Msukumo
huu wa kuleta mabadiliko katika tasnia ya ushairi uliletwa na wanazuoni akina
E.Kezilabahi, Jared Angira na E.Husein wasomi hawa walijishughulisha na utunzi
wa mashairi hivyo baada ya kusoma fasihi za nchi mbalimbali waligundua kuwa
vina na mizani ni wazo lilizofuatwa na washauri wote duniani hivyo waliamua
kuasi sharia hizo ili kuleta mabadiliko ya kuondoa minyororo iliyowafunga
kuhusu utungaji wa shairi la Kiswahili kwa pamoja waandishi hawa waliweza
kutunga mashairi mengi au tungo zisizofuata ruwaza ya vina na mizani na pia
waliungwa mkono na watunzi wengi kama vile M.M.Mulokozi, K.K.Kahigi miaka ya
themanini washairi wengi waliibuka kuungana na kundi hilo. Mfano: Henry Mhanika na T.Mvungi.Madai ya wana mabadiliko kutunga
tungo zao yalikuwa kama ifuatavyo:
v Mbinu na njia za
kutunga mashairi ya Kiswahili zilikuwa chache mno.
v Kutunga kwa
kufuata taratibu za muundo wa tungo za Kiswahili (mapokeo) kuliwanyimia uhuru
walidai kuwa hakuna sharia za utunzi wa mashairi katika (diwani ya Amri)
(sharia za kutunga mashairi).
v Muundo wa tungo
zao zisizofuata kaida ni wa kiasilia. Hii ina maana kuwa ushairi wa mwanzo
haukuwa na mizani wala vina.
Kwa maana
nyingine kuwa mgogoro huo
ulijitokeza baina ya wazee akina Kuluta Amri,Saadam Kandoro, Ustadhi, Andanenga,
n.k na vijana akina E.Kezilahabi.
MADA
NDOGO ;KUHAKIKI RIWAYA
Riwaya
ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawaidha, lugha ya nathari, mchanganyiko wa
visa, wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa kimantiki yenye kufungamana na
wakati na kushabihiana na maisha halisi.
SIFA
ZA RIWAYA
1. Urefu,
Riwaya
kwa kawaida huwa ndefu ikilinganishwa na tanzu nyingine za kinathari kama vile
hadithi fupi. Mfano wa Riwaya ya Bwana Mnyombokera na Bibi Bagomoka (198 )
iliyoandikwa na Kiterezi, Hii ina mamia ya kurasa
2.
Matukio,Riwaya humulika hali halisi ya maisha
ya binadamu ingawa matukio ya riwaya si lazima yawe ya kweli yametokea,
yanaweza kupatikana katika ulimwengu halisi wa binadamu matukio kama vile
rushwa, wizi wa mali ya umma, matabaka, uongozi mbaya, athari za pesa katika ndoa
na mapenzi na tatizo la usafiri Dar-es-salaam katika “Pepo ya mabwegwe” (1981) iliyoandikwa na Mwakyembe, mambo
yaliyoandikwa yamo katika jamii yetu kwa sasa.
3.
Muundo,Riwaya huwa na miundo changamano
ukilinganisha na kazi nyingine za kinathari. Riwaya inaweza kua na muundo wa
msago, rejea au rukia, wakati mwingine inaweza kuwa na muundo changamano yaani
inakuwa na muundo miwili katika kazi moja.
1.
Mandhari yake ni pana
Mandhari
ya riwaya ni mapana na kikamilifu kwani riwaya hushughurikia mawazo mengi, hujishughulisha
na vipengele vingi vya maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali
tofauti kama vile shuleni, mijini, vijijini, nyumbani, barabarani n.k. ili
kushughulikia mazingira mapana mwandishi hutumia kipindi kirefu cha wakati
ikilinganishwa kazi nyingine kama vile hadithi fupi ambayo huweza kuchukua
kipindi kimoja tu kukuamilika.
2.
Wahusika ,Wahusika wa riwaya ni wengi na
waliokuwa zaidi. Riwaya hushughulikia masuala mengi huwa na wahusika wengi
wanaomwezesha mwandishi kukidhi haja hiyo kuna wahusika wanaobadilika kwa lengo
la kuonyesha hali halisi ya maisha kuna wale wasiobadilika ili kutumiwa
kukashifu au kuhimiza hali fulani n.k. Riwaya ya Ziraili na Ua la faraja na
Mkufya na Makuadi wa Soko Huira iliyoandikwa na Chacha Gezina wahusika wengi.
3.
Mtindo,Riwaya hutumia mtindo wa wasimulizi,
monolojia au dayolojia na nafsi zote tatu. Mwandishi anaweza kuwa ndiye
msimulizi au mhusika fulani akawa ndiye anayesimulia au wahusika wakawa
wanajibizana wao kwa wao.
Mfano:
Njama (1981), Uchu (2000), Kikosi cha Kisasi(1979) vya musiba ametumia zaidi
mtindo wa monolojia na dayolojia kidogo.
AINA/TANZU ZA RIWAYA
Kuna
michepuo miwili ya riwaya ambayo ni;
A.
RIWAYA YA DHATI
Riwaya
dhati ni riwaya yenye kuchambua masuala mazito ya kijamii, kutafuta sababu zake
athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na
kumfikirisha msomaji, sio kumstarehesha mtu.
MATAWI
YA RIWAYA YA DHATI
1.
Riwaya ya
kijamii
Ni
riwaaya inayosawiri maisha na matatizo ya kawaida ya jamii. Matatizo haya
huweza kuwa ya kifamilia, kiuhusiano wa kitabaka ya kisasa ya kiutamaduni n.k.
Utanzu huu ndiyo wenye idadi kubwa zaidi ya riwaya.Mfano:
Shabaan Robert
“Siku ya watenzi wote” (1968)
M.S.Moamed
“Nyota ya Rehema” (1978)
S.A..Mohamed
“Dunia mti mkavu” (1980)
E.Kezilahabi
“Rosa mistika” (1971)
J.N.Somba
“Alipanda upepo Akavuna Tufan” (1969)
Alex Banzi “Titi
la mkwe” (1972)
2.
Riwaya ya
kisaikolojia
Ni
riwaya inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia, mawazo, Imani, hofu, mashaka
na matumaini na matamanio yake binafsi na athari za mambo hayo kwake binafsi na
labda jamii yake. Baadhi ya watunzi waliojipambua katika utanzu huu ni
E.Kezilahabi
“Kichwa maji” (1974)
M.S.Mohamed
“Kiu” (1972)
S.A.Mohamed
“Tata za Asumini” (1990)
K.G.Mkangi
“Ukiwa” (1973)
3.
Riwaya ya
kitawasifu
Ni
riwaya ambayo husimulia habari za maandishi tangu kuzaliwa kwakwe hadi pale
inapokomea au hadi kufa.Mfano:
Shabaan Robert
“Maisha Baada ya miaka Hamsini” (1966)
Maisha ya Hemed
Bin Muhamed “Tipu Tipu” (1950)
4.
Istiara
Ni
riwaya ya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara au kuwakilisha tu cha jambo
jingine.Mfano:
Riwaya ya
Nathanuel Swift (1926)
Safari za
Gulliver (Mfasiri F.Johnson) (1945)
Shamba la
wanyama (Msafiri F.Mkwegere)
Ni
ishara ya mfumo wa utawala wa dikteta wa kisovieti wa enzi za Staliri. Yaelekea
pia riwaya Shabaan Robert (1951) kusadikika ni ishara kuhusu utawala na mabavu
wa kikolono.
5.
Riwaya ya kigano
Ni
riwaya yenye umbo la mtindo wa ngano mathalani huweza kuwa na wahusika wanyama,
visa vya ajabu ajabu, mandhari ya kubuni na visa vyenye kutendeka nje ya wakati
wa kihistoria.
Mfano: -Shabaan Robert (1952) “Adui na nduguze”
-J.K.Kimbila (1966) “Lila na fila”
6.
Riwaya teti
Ni
riwaya inayosimulia vituko na masahibu ya watu, wapuuzi, walaghai, wajanja na
kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Aghalabu hao huwa ni watu wanaovutia wa
tabaka la chini na bapa. Matukio ya Riwaya hii hayana msukumo ulioshikamana
vizuri shabaha yake mojawapo ni kuziteta na kuzikejeli tabia za matabaka na
watu mbalimbali katika jamii.
Mfano: Hadithi za “Hekaya za Abunuasi na Hadithi
nyingine (1915) imefanana na vituko vya riwaya teti.
7.
Riwaya ya wasifu
Ni
riwaya inayoandikwa na mtu mwingine kuhusu maisha ya mtu mwingine tangu
kuzaliwa hadi kufa kwake.Mfano:
J.Makabarah
“Maisha ya Salum Abdallah” (1975)
S.Robert “Wasifu
wa Siti bint Saad” (1967)
8.
Riwaya chuku
Ni
riwaya ya vituko na masaibu yasiyokuwa ya kawaida ni riwaya isiyozingatia
uhalisia mara nyingi masaibu ya Riwaya chuku huambatana na mapenzi, mfano;
baadhi ya hadithi za Alfu-lela-Ulela (1929) ni chuku katika fasihi ya
Kiswahili. Riwaya za Shabaan Robert za “Adili na Nduguze” (1952) na
“Kusadikika” (1951) zinaingia katika kundi hili.
9.
Riwaya ya
kihistoria
Hii
huchanganya historia halisi na Sanaa kwa makusudi ili kutoa maudhui fulani.
Mara nyingi riwaya hii hujikita kwenye matukio makuu ya kihistoria yalioathiri
mwenendo na mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika na historia ya kubuni,
matukio ya kweli na ya kubuni. Hata hivyo riwaya hiyo inazingatia zaidi namna
matukio makuu ya kihistoria yalivyomwathiri na yalivyoathiriwa na matendo ya
mtu binafsi aliyeyashiriki baadhi watunzi mashuhuri wa riwaya za kihistoria niMfano:
Olef Msewa “Kifo
cha ugenini” (1977)
M.Karuthi
“Kaburi bila msalaba” (1971)
S.A.Shafi “Kuli”
(1979)
A.Lihamba “Wimbo
wa Sokomoko” (1990)
B.Mapalala “kwa
heri iselemaguzi” (1992)
G.Ruhumbika
“Miradi Bubu ya wazalendo” (1992)
10.
Riwaya ya
kimaadili.
Ni
riwaya inayowapa watu maadili mema na wengine maadili hayo ni ya kidini wausika
wanakuwa na sifa za kudumu kama vile upendo wa ukarimu.Mfano:
Shabaan Robert
“Adili na Nduguze” (1952)
M.Mnyapala
“Mrina Sali na wenzake wawili” (1961)
G.Mhina “Mtu ni
Utu” (1971)
11.
Riwaya ya
kimapinduzi
Ni
riwaya inayojadili matatizo ya kisiasa katika jamii. Riwaya hii ni mwelekeo
fulani wa kuleta mabadiliko ya kisiasa katika jamii.
Mfano:
wa riwaya hizi ni “kuli” (1978), Kabwela (1978), Mzalendo (1977) Ubeberu
Utawashinda (1971) n.k.
12.
Riwaya ya
kifalsafa
Ni
riwaya zinazojadili migogoro ya kimaisha kifalsafa. Riwaya hizi hujuliza
maswali kama vile
· Ukweli ni nini?
· Maisha ni nini?
· Kifo ni nini?
· Kuwepo na
kutokuwepo ni nini? n.k
Muundo
wa riwaya hizi ni wa kimchangamano au a mviringo na wahusika huvunjwa vunjwa
hivyo mhusika wa riwaya hizi ni wazo tu au hawapo kabisaMfano:
· E.Kezilahabi- “Nagona” (1987) Mzingile (1991)
· S.Mohamed- “Kiza
katika nune” (1988)
· K.G.Mkangi-
“Mafuta” (1984) n.k
13.
Riwaya Barua
Ni
riwaya ambayo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia ya barua wanazoandikiana
baadhi ya wahusika.Mfano:
Mariam Ba “Barua
ndefu kama hii “(1980) Msafiri Maganda
Walter Tribisch
“Nampenda mvulana. Barua ya siri” (1964)
14.
Riwaya ya
vitisho
Ni
riwaya yenye visa vya kutisha na kusisimua damu mara nyingi visa hivyo
huambatana na mambo ya ajabu au miujizaMfano:
C.Mung’ong’o
“Mirathi ya Hatari” (1977)
N.J.Kuboja mbojo
Simba-mtu (1971)
15.
Riwaya pendwa
Ni
riwaya iliyokusudiwa kuwastarehesha na kuburudisha msomaji tu lengo hili kulihimiza
kwa kusawiri visa na vituko vya kusisimuwa damu
Mfano:
Vituko vya majambazi na uhalifu, ususi na mahaba ya waziwazi.
Riwaya
pendwa huwa na mafunzo kidogo kama lengo la ziada katika Tanzania aina hii ya
riwaya ililetwa kwa mara ya kwanza na Abdull alipoandika riwaya ya “Mzimu wa
watu wa kale“ (1957/8) na miaka ya 1960
-
Katalambwa (1965) simu ya kifo
SIFA ZA RIWAYA PENDWA
1. Matumizi makubwa ya taharuki na utendaji
Taharuki
hutumika kuelezea hamu kubwa anayokuwa nayo msomaji katika kujua yatakayotokea
katika hadithi fulani. Taharuki hutokea pale ambapo msomaji ana hamu kubwa au
anajua yanayoweza kutokea laikini hajui jinsi yatakavyotokea.
Riwaya pendwa ni
riwaya ya taharuki kwa sababu ya kimsingi ya fani yake hujiweka katika mbinu ya
kisanaa ya taharuki. Taharuki imepewa nafasi kubwa katika aina hii ya riwaya
kwa njia ya vituko vya kusisimua vinavyojibainisha kwa njia ya mkingano
iliyosukwa kwa namna ya ufundi usiokuwa wa kawaida.
Kwa upande wa
utendaji wahusika wake n hodari sana katika kutenda, katika kuwindana, kupigana
kwa silaha na mikono mitupu na kufanya matukio yake utendaji unaojitokeza humu
unaziteka nafsi za wasomaji wake.
2.
Hutumia wahusika
walewale.
Riwaya pendwa
inasifa ya kutumia wahusika walewale hivyo ikawa na uwezo wa kujiendeza katika
vijitabu kadhaa. Karibu kila mwandishi maarufu wa aina hii ya riwaya ameandika
vitabu zaidi ya kimoja. Sifa hiyo ya kuwatumia wahusika walewale imefanya
kijitabu kimoja katika mfuatano wa vitabu kadhaa vya mwandishi mmoja kionekane
kama tukio linalojitegemea katika mfululizo wa matukio. Ili kuustawisha na
kuwisisitiza mfuatano huo, baadhi ya waandishi wameweza hata kudondoa kazi za
nyuma katika kazi zao za baadae mfano Abdallah “Kosa la bwana Musa”,Hofu (1988)
musiba,Salamu Toka Kuzimu (1993) Mtobwa,Tutarudi na roho zetu?? (1987)
3.
Mhusika mkuu
hupewa sifa zisizo za kawaida
Mhusika mkuu
ameumbwa juu ya wahusika wengine anatawaliwa, hivyo ana sifa ya ubabe sifa ya
kuwa kielelezo chenye ukamilifu, yaani kutokana na dosari.
Mfano: Abdallah
“ Kosa la Bwana Musa”
Mhusika
mkuu ndiye mshindi hata apitapo katika taabu na mashaka ya aina gani tunajua
hatimaye ni mshindi katika mambo yake. Wahusika hawa wakuu hutenda na kuendesha
mambo yao kama miungu wadogo pasi na kukosea hata wakawa wasioaminika.
4. Mandhari yake huundwa kwa namna ya pekee
Wasanii wa
riwaya pendwa wanatumia mandhari ya kitanzania au kiafrika, lakini sehemu kubwa
ya matukio ama imo ndani ya vichwa vya wasanii au filamu za upelelezi, uhalifu
na mapenzi za kigeni.
5.
Upangaji holela
wa matukio
Katika riwaya pendwa
kuna upangaji wa haraka wa mtiririko wa matukio kiasi kwamba sehemu zingine
zinakosa upatanifu na mantiki.
6.
Kuenzi jinsia ya
kike kama chombo cha anasa na uhalifu.
Riwaya pendwa
hua zina mapenzi ndani yake kana kwamba upelelezi au shughuli inayofanyika
haiwezi kusisimua bila mapenzi, yaani hazina dawa, dawa ya kazi ni mapenzi.
7.
Hutumia lugha ya
kila siku
Mara nyingi
riwaya pendwa hutumia mitindo wa masimulizi na monolojia na kwa kiasi kidogo
dayolojia. Lugha yake ni rahisi ya mazungumzo ya kila siku.
ATHARI
ZA RIWAYA PENDWA
1. Hudumaza vipaji vya waandishi wetu kwani huiga kila
kitu.
Kazi hizi
zinadhihirisha jinsi gani fasihi pendwa za kigeni pamoja na filamu zinaathiri
waandishi wetu. Riwaya pendwa ni matokeo ya mwigo ambayo yameathiri uasili wa
waandishi wetu katika ubunifu kimaudhui na kifani kazi hizi zinashindwa kabisa
kudhihirisha umahiri wa waandishi wetu katika kubuni kazi na sanaa zenye mawazo
yao wenyewe.
2.
Hufundisha
majangili na wahalifu mbinu mpya katika shughuli zao za kufanya uhalifu.
Riwaya pendwa
husababisha uhalifu katika jamii.Mfano: Athari mbaya za tamaduni za kigeni
zinazokuja kwa njia ya filamu na riwaya pendwa ni kama vile kuzuka kwa makundi
ya kiharamia hapa nchini ambayo yanavamia benki, baa, maduka na kuwaibia watu
kwa kutumia silaha mbalimbali.
3.
Hazichambui kwa
undani misingi ya matatizo ya jamii.
Riwaya hizi haziingi kwa undani katika
misingi ya matatizo ya jamii kama kuna tatizo linalosababisha upelelezi je
kiini chake ni nini? Riwaya hizi zinataja juu ya wivu, tamaa, uovu wa aina hiyo
bila kuyahusisha vilivyo mazingira ya jamii (mfano filamu zinaitwa 24)
AINA
ZA RIWAYA PENDWA
1.
Riwaya ya Mahaba
Ni riwaya yenye
kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati ya mvulana na msichana au mwanaume na
mwanamke. Siku hizi zipo zenye kusawiri mapenzi haramu pia.Kwa mfano: Mapenzi
baina ya watu wa jinsia moja (mashoga)
Mfano: J.Simbamwene
“Mwisho wa mapenzi” (1972),J.D.Kiango “Jeraha la moyo” (1974),S.M.Komba “Pete”
(1978),J.Simbamwene “Kweli unanipenda” (1978)
2.
Riwaya ya
Uhalifu/Ujambazi
Ni riwaya
zinazosimulia vituko vya uhalifu. Mfano: wizi, ujambazi, uuaji, magendo,
utapeli, n.k. Aghalabu polisi huhusishwa katika kuwasaka na kuwadhibiti
wahalifu hao.
Mfano:J.Simbamwene (1972) “Kwa sababu ya
pesa”,H.Katalambula (1975) “Buriani”,L.O.Omolo (1970) “Mtu mwenye miwani
meusi”,S.J.Chadhoro (1972) “Kifo changu ni fedheha”,Hammie Rajab (1979) “Ufunguo wa
Bandia”
3.
Riwaya ya
Upelelezi
Riwaya hii
huelezea mambo mawili kosa au uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mwalifu
anapopatikana.
Hivyo wahusika
wake ni wahalifu, wadhulumiwa (waliotendewa kosa) na upelelezi wakiwemo polisi.
Mtunzi wa kwanza wa riwaya ya upelelezi nchini Tanzania ni mfano;M.S.Abdallah na riwaya zake ni:-Mzimu wa watu wa
kale (1958),Kisima cha giningi(1968),Duniani kuna watu (1973),Siri ya sifuri
(1974),Mwana wa yungi Hulewa (1976),Kosa la Bwana Musa (1984),Watunzi wengine wa riwaya ya upelelezi ni:-H.Katalambwa
na E.Ganzile,Simbamwene (1984) “Dimbwi la Damu”,E.Ganzele (1980) “Kijasho
chembamba”
4.
Riwaya ya
Ujasusi
Ni riwaya ya
upelelezi wa kimataifa majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na nchi, serikali au
waajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za
kijeshi (silaha walizonazo) siri za kisayansi na kiuchumi n.k ili taarifa hizo
ziwanufaishe waliowatuma wakati Fulani hutumwa kwenda kuharibu silaha zao au
nyenzo za uchumi na maadui
Mfano wa riwaya
za ujasusi ni:-E.Musiba (1979) “Kikosi cha kisasi”,E.Musiba (1981) “Njama”,K.M.Kassani
(1982) “Mpango”,Mtobwa (1987) “Je tutarudi na roho zetu?”,Hammie Rajab (1984)
“Roho mkononi”
UHAKIKI
WA VIPENGELE VYA FANI
Vipengele
vya fani ni kama vile:-
a)
Muundo
Muundo hutumika kueleza mpangilio wa
kazi ya kifasihi. Mpangilo huu hujionyesha kwenye maumbo ya kazi za kifasihi
kama hadithi fupi au riwaya. Muundo ni namna au jinsi kazi za fasihi
inavyoonekana yaani umbo lake, ilivyogawanyika. Mfano sura, mfuatano wa matukio
yake (mtiririko wa matukio), msuko n.k. matukio yanaweza kufuatana kwa njia
sahihi nay a moja kwa moja (msuko sahahi) au yakawa na uchangamano ambao
unahusisha kwenda mbele na kurudi nyuma (msuko changamano)
b)
Mtindo
Ni jumla ya
mbinu au sifa zinazomwezesha mandishi kuwasilisha ujumbe wake.Mtindo huelezea
jinsi mwandishi anavyoiunda kazi yake.Dhana hii inarejesha sifa maalumu za
mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake.
Mazoea hayo ya mwandishi yanapambanua msanii huyu na wenzake kiasi kwamba
msomaji anaweza kusema hii ni kazi inayoandikwa na fulani kwa kusoma tu katika
mtindo wa riwaya kuna vipengele vifuatavyo
· Matumizi ya
Lugha
· Usimulizi wa
nafsi (Msanii anaweza kusimulia matukio kwa kutumia nafsi ya 1,2 na ya 3)
· Matumizi ya
masimulizi (msanii hutoa masimulizi yake juu ya mfululizo wa matukio kama
yalivyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya wahusika. Msanii husema nini
kilitokea jinsi gani kilitokea na mahali ambapo hayo yalitokea
· Matumizi ya
monolojia ni masimulizi yanayofanywa na mhusika mmoja katika hadithi au kazi
nyingine za kisanaa katika mbinu hii, hadithi inayojitokeza kama inasimuliwa na
mhusika aliye hadithini. Mwandishi anaonekana kuwa hayupo. Pia hadithi inaweza
kujitokeza ikisimuliwa katikaa nyakati mbalimbali.
· Matumizi ya
dayolojia, ni mazungumzo baina ya wahusika wawili au zaidi katika riwaya.
· Matumizi ya
tanzu nyingine za kifasihi simulizi kama vile nyimbo, mashairi, majigambo,
hadithi matumizi ya barua n.k.
· Uteuzi wa
wahusika na ujengaji wa mandhari.
c)
Wahusika
Ni viumbe wa
sanaa wanabuniwa kutokana na mazingira ya msanii. Hatua ya kwanza katika
utungaji wa kazi ya sanaa ni wazo, wazo kutokana na hali halisi anayoiona
msanii ili kueleza fikra rai au falsafa yake kuhusu kile akionacho anaichukua
Lugha na kuifinyanga.
Wahusika wake
pia huwaweka katika mandhari yatakayomsaidia kuwakilisha hoja zake kutokana na
vitendo, maingiliano na fikra zao kuna wasanii wanaotumia wanyama au wadudu
kama wahusika kwa lengo la kufikisha maudhui fulani kwa jamii au dhamira,
mitazamo yao, kwa jamii.
d)
Mandhari
Ni mahali au
makazi maalumu yaliyojengwa na mtunzi na yanamatokeo, matukio mbalimbali ya
fasihi. Mandhari ni mazingira ya wahusika na matukio na inahusu mahali
wanamokaa wahusika na kuingiliana, mazingira ya kijamii na kiuchumi ya wahusika
hao na nafasi zao za kitabaka kufahamu mandhari kunatusaidia kuelewa hisia,
imani, tabia, na maumbile ya wahusika. Mandhari hutupatia mwelekeo kuhusu
maudhui.
e)
Matumizi ya
Lugha
Lugha ina nafasi
kubwa sana katika fasihi kwa kuwa fasihi yenyewe ni sanaa ya lugha. Lugha hiyo
ndiyo nyenzo inayotofautisha fasihi na sanaa nyingine kama uchoraji, ufinyanzi,
udarizi n.k
Lugha ni nguzo
kuu ya kazi za kifasihi na uchunguzi wowote wa kazi hizo hauna budi kuangalia
suala la lugha kazi ya kifasihi
huyawasilisha maudhui yake,
dhamira yake kwa kutegemea lugha. Baadhi ya wahakiki wa fasihi wa kwanza
kuwa fasihi hutumia lugha kwa namna
maalumu, inayozoea lugha ambayo inajulukana kama lugha ya kifasihi. Katika
matumizi ya lugha kuna vipengele kama:-
Tamadhali za
semi, kama vile tashibiha, sitiari, tafsida, tashihisi, kejeli, mubalagha,
dhihaka n.k
· Mbinu nyingine
za kisanaa ni kama vile takriri, tanakali sauti, mdokezo, tashititi, mjalizo
n.k
· Matumizi ya
majali maana ya watu aghalabu huwa na maana. Wasomaji wa riwaya ni vyema
tuyachunguze majina na kuyahusisha na matukio, dhamira, maudhui na ujumbe wa
riwaya husika. Mfano wa riwaya ni “Adili na Nduguze” (1952) mhusika Adili ni
mwadilifu
· Matumizi ya
jazanda au Taswira ni mafumbo ambamo ndani maana ya kitu imejificha na mfano
katika riwaya ya “Dunia mti mkavu” (1980) mvua inatumiwa kama jazanda na
matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.
· Uteuzi na
mpangilio wa maneno. Lugha ni nyenzo ya kimsingi ya msanii na jinsi anavyotumia
huathiri jinsi msomaji atakavyoisoma, kuielewa na kuathiriwa na riwaya fulani
mfano wa matumizi ya miundo fulani huweza kuathiriwa na maswala
yanayozungumzwa.
· Matumizi ya
semi, kama vile methali, misemo, nahau, misimu mafumbo n.k vipengele hivi vina
kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi
· Matumizi ya
taharuki. Hii ni mbinu inayotumiwa na watunzi wa kazi za kubuni ili kutetea
hisia na hamu ya msomaji ili kujenga taharuki. Mtunzi husuka matukio yenye
mshikamano na kutiririka kwa muwala ambao unamfanya msomaji asiitue kazi hiyo
hadi kikomo chake kazi yenye taharuki haichoki kuisoma bali inaburudani ndani
yake.
JINA
LA KITABU
Jina
la kitabu ni vyema lisadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu. Mfano Je Shetani
msalabani (1982) linasadifu vipi yale yaliyomo ndani ya riwaya hiyo?
UHAKIKI
WA MAUDHUI
Maudhui
ya riwaya kama kazi yoyote nyingine ya fasihi yaweza kuwa kitu, mtu, tukio au
jambo lolote katika maisha yetu. Maudhui hudhihirika baada ya kuangalia mambo
mengi, mathalani tukio mbalimbali
Kwa ujumla, maudhui ni muhimu katika
riwaya hasa ndiyo msingi wa riwaya kwa hivyo ni lazima tutegemee mambo
yaliyojitokeza katika ile riwaya yaani maudhui lazima itoke ndani ya riwaya na
sio nje.
Katika bahari hii ya maudhui, hatuna
budi kuichunguza jumuiya iliyozungumzwa.
Matokeo yote katika utunzi ule yatapimwa kwa mujibu wa hali ya jumuiya. Mhakiki
astahili kuichunguza jumuiya ili kuweza kuhukumu kama mtunzi amezingatia kutoa
hali halisi ya jumuiya yake.
Maudhui
huwa ni ya aina mbalimbali kwa ujumla huwa yanalenga migogoro na mikinzano
katika jamii. Baadhi ya maudhui ya kazi zote za riwaya na sanaa kwa jumla ni
kama vile:-
Mgongano wa
tabaka kati ya watawala na watawaliwa
Migongano kati
ya wenye elimu na wasiopata elimu
Migongano kati
ya walio na mali na wasionayo
Migongano kati
ya mwenye kupigania usawa kati ya mume ne mke na wenye kupinga usawa huu n.k
Kwa ujumla maudhui hutupa mafunzo,
ujumbe na kutufahamisha falsafa
MADA
NDOGO ;UHAKIKI WA TAMTHILIYA
Tamthiliya
ni utungo wa kidrama ambao ni aina mojawapo ya maandishi ya sanaa za maonyesho.
Ni sanaa inayoonyeshwa kwa vitendo katika sanaa hii ili mtu apate maadili au
utamu uliomo katika sanaa mpaka asome vitendo vya wahusika waliotumiwa na
msanii na kuvitafakari kwa makini.
Tamthiliya huonyesha matendo ya
wanajamii kwa njia ya kuigiza, maigizo ambayo hatimaye huweza kuonyeshwa kwenye
majukwaa katika sanaa za maonyesho wahusika wake huonyesha matendo waziwazi kwa
njia ya kuigiza. Wausika hawa huzungumzia nafsi zao wakati zamu zao za kuongea
zinapowafikia ili mradi kila mmoja hujaribu kuonyesha waziwazi kuridhika au
kutoridhika kwake kufutana na nafasi anayoiwakilisha katika jamii inayohusika.
Sifa za tamthiliya
Tamthiliya
huwa na sifa za kawaida za sanaa za maonyesho, sifa hizo ni:
· Dhana inayotendeka
Dhana
inayotendeka ni kile kinachoongelewa katika tamthiliya na kinaweza kuwa cha
kubuni au cha kweli. Dhana inayotendeka kwa kawaida huhusu mzozo fulani
unaohusisha pande mbili. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kilio chetu” (1995), dhana inayotendeka ni “Vita dhidi ya ugonjwa
wa UKIMWI”
· Kuwepo kwa mtendaji
Hapa
ni wale wanaotenda ile dhana, yaani wahusika. Ili tamthiliya ikamilike lazima
wawepo wale wanaotenda lile tendo ambao wanaitwa wahusika. Kwa mfano, katika
tamthiliya ya “Mashetani” (Hussein) watendaji wakuu ni: Juma na Kitaru na
watendaji wadogo ni: Mama Kitaru, Baba Kitaru, Daktari, Bibi, Mama Juma, n.k
· Kuwa na uwanja maalumu wa kutendea
Tamthiliya
huigizwa sehemu fulani. Hapa kuna jukwaa ambako wahusika wanaingiliana katika
uigizaji wao. Ukubwa au upana wa eneo hilo ni muhimu sio tu kwa athari, bali
pia kwa kuupitisha ujumbe fulani.
· Kuwepo kwa watazamaji
Hawa
hutazama dhana inayotendeka. Kwa tamthiliya iliyoandikwa, watazamaji hapa ni
wasomaji, yaani wale wanaosoma kazi hiyo ya sanaa. Kwa hiyo, tamthiliya
inaingizwa mbele ya watazamaji (hadhira).
· Kusudio la kisanaa.
Hili
hutupa uhakika kuwa kinachotendeka hapo kimedhamiriwa kuwa sanaa na si kitu
kingine kwa mujibu wa kanuni za jamii inayohusika.
vi.
Muktadha wa
kisanaa
Ni sifa nyingine ya tamthiliya.
Muktadha wa kisanaa unafafanua mazingira
ya tukio hilo. Kwa mfano, ugomvi wa walevi kilabuni au baa si sanaa za
maonyesho kwa sababu muktadha wa tukio hilo haulipokei kama sanaa.
vii.
Tamthiliya ni
kazi ya kubuni kama kazi nyingine za kifasihi.
Hii ni muhimu
ili kutofautisha kati ya tendo la dhati katika maisha na tendo la sanaa.
viii.
Matukio ya
tamthiliya huigizwa kwa hadhira hai.
Hapa basi pana mawasiliano ya moja kwa
moja kati ya wahusika, ambao ni vipaza sauti vya mtunzi na hadhira.
ix.
Tamthiliya,
hadithi yake imegawika kimuundo katika matendo na maonyesho
Matendo na
maonyesho huonyesha matukio mbalimbali. Kila tendo huzingatia tendo moja kuu
ndani ya mchezo; na hugawanyika katika sehemu ndogo ziitwazo maonyesho. Onyesho
moja kwa kawaida huwasilisha tuko moja linalotendeka mahali pamoja.
x.
Mgogoro wa
tamthiliya huwa mwanzoni
Mwandishi hana
wakati wa kutoa maelezo mengi. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kifo Kisimani “ ya Kathaka wa Mberia,
mgogoro kati ya Mtukufu Bokona na wanyonge unajitokeza mwanzoni
AINA ZA TAMTHILIYA
1.
Tanzia
Tanzia
ni ile inayohusika na mambo yenye uzito, kifikirika na kihisia katika maisha ya
binadamu. Mhusika mkuu ambaye hupewa sifa nyingi zinazovutia, hukabiliwa na
shida au tatizo;tatizo ambalo linaweza kumkabili mtu yeyote. Lakini namna
anavyojitahidi kulitanua tatizo hili, namna anavyopigana vita kushinda shida
inayomkabili, hali ya ulimwenguni na tabia za binadamu, zinamfanya asiweze
kufaulu na mwishowe anashindwa katika vita hii. Kwa mfano, tamthiliya ya “Mzalendo Kimathi” (1978) “Kinjekitile” (1969), “Pungwa” (1988), “Kilio cha haki” (1981) ni mfano wa tanzia. Katika tamthiliya zote
hizi mhusika mkuu anashindwa na hata anakufa au anauawa, lakini kifo chake si
kile cha ajali barabarani, bali ni kifo kinachokuja baada ya mapambano marefu,
mapambano yanayochepuza hisia za ushujaa wa binadamu
2.
Ramsa (komedia)
Ramsa
ni ile inayokusudiwa kufurahisha au inayochekeshachekesha na yenye mwisho
mwema. Aina hii ya tamthiliya ni kwamba hutuchorea picha yakini ya maisha yetu,
huwa haijaribu kuisawiri picha hiyo kwa undani na uzito kama uleunaojitokeza
katika tanzia. Mfano wa ramsa ni tamthiliya ya Aliyeonja Pepo (1973)
3.
Melodrama na
vichekesho
Melodrama
inafanana sana na tanzia, ingawa mara nyingi mhusika mkuu wa meleodrama
humaliza kwa ushindi, matokeo yake huwa yanasisimua sana, na mwendo wa msuko
wake huwa ni wa harakaharaka zaidi.
Vichekesho,
kwa upande mwingine; huwa vinakusudia
kutuonyesha vituko vitakavyotuchekesha tu. Ujenzi wa wahusika huwa ni muhimu,
matukio huwa hayawekewi sababu zozote au sababu za kuturidhisha na msuko wake
huwa hauna uchangamano mzuri. Tamthiliya nyingi zinazoonyeshwa katika
televisheni ni vichekesho.
4.
Tamthiliya ya
kihistoria
Hii
ni aina ya tamthiliya inayoelezea tukio fulani la kihistoria katika jamii
fulani. Msomaji wa tamthiliya hii huweza kukutana na sifa za tanzia pamoja na
tamthiliya chekeshi. Mhusika mkuu wa tamthiliya hii mara nyingi huwa ni shujaa
aliyejitoa mhanga kuipigania na kuitetea jamii yake ili iweze kuondokana na
matatizo yanayoiandama, hususani ya kisiasa na kiuchumi.
Tukio
la kihistoria linaloelezewa kwenye tamthiliya hii huwa limeiathiri jamii husika
kwa kiasi kikubwa na hivyo huwa si rahisi kusahaulika. Vitabu vya tamthiliya
vinavyoelezea matukio ya kihistoria ni kama vile Kinjekitile, Mzalendo Kimathi, Mkwawa wa Uhehe (1979) pamoja na Tone la Mwisho.
UHAKIKI
WA VIPENGELE VYA FANI
Uhakiki
wa tamthliya kimsingi huzingatia kanuni na misingi ileile ya uhakiki wa Riwaya.
Kuna mambo ya msingi yz hizo tanzu mbili kufanana na kutofautiana. Mambo muhimu
yanayochunguzwa wakati wa kuhakiki fani ya tamthiliya ni:
a)
Utendaji/tukio/tendo.
Kitu muhimu sana
katika ujenzi wa tamthiliya ni tukio. Kutokana na tukio moja, msanii anao uwezo
wa kuibua dhamira mbalimbali. Wataalamu wa taaluma hii husisitiza umuhimu wa
tendo au tukio katika tamthiliya kwa kusema “drama ni tendon a wahusika ni
tendo”
Tendo huanza
pale mhusika anapoulza, “Ninataka nini? Je, lengo langu ni nini?” Kwa kawaida,
aina ya tendo/tukio litaathiri matokeo ya tamthiliya itakayoandikwa.
Mwandishi
mwenyewe anapaswa kuamua juu ya aina ya tamthiliya anayotaka kuandika, lugha,
mtindo, wahusika au mandhari anayotumia. Kwa hali hiyo, uteuzi wa tendo/tukio
la kuandikia tamthiliya lazima uende pamoja na uteuzi mzuri wa vipengele
vingine vya kisanaa kama vile lugha, wahusika, mandhari, n.k.
b)
Lugha
Lugha ndiyo
nyenzo kuu ya kazi ya fasihi. Dhamira na maudhui ya kazi ya kifasihi haziwezi
kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Uchunguzi wa
matumizi ya lugha ni muhimu katika uhakiki wa tamthiliya. Je, mambo gani ya
kuchunguza hapa? Hapa tunachunguza:
·
Matumizi
ya nahau na misemo.
·
Uteuzi
na mpangilio wa maneno/msamiati.
·
Tamathali
za semi. Kwa mfano, sitiari, tashibiha, tafsida, tashihisi, n.k.
·
Mbinu
nyingine za matumizi ya lugha. Kwa mfano, takriri, tanakali sauti, majazi,
mdokezo, mjalizo n.k.
·
Matumizi
ya taswira na ishara mbalimbali.
·
Matumizi
ya mkopo na kutohoa.
c)
Wahusika
Katika
tamthiliya, wahusika ni nguzo muhimu sana. Wahusika si watu halisi bali ni watu
wa kubuniwa, wenye sifa muhimu za binadamu. Wahusika huwa na athari kubwa kwa
hadhira kutokana na sababu mbalimbali:-
Wahusika
wanabebeshwa sifa nyingi tofauti ambazo zinawakilisha maisha halisi ya watu
hai.
Mwandishi wa
tamthiliya hulazimika kumjenga mhusika mmoja kwa kuvutia na kumpa mbinu za
ki-drama, mambo ya kushangaza au mbinu yoyote ile anayoichagua mwandishi. Kama
tamthiliya inaigizwa jukwaani, wale waongozaji wa tamthiliya hiyo wanaweza
kuathiri mchezo huo pia. Kama ilivyo katika riwaya, tamthiliya huwa na wahusika
wakuu na wahusika wadogo.
d)
Muundo wa
tamthiliya
Muundo katika
tamthiliya humaanisha msuko wa vitendo na mgogoro kuanzia mwanzo wa mchezo,
kuingia kwenye kilele (upeo) na kuhitimisha kwenye ufumbuzi/masuluhisho ya
mchezo huo (mwisho). Kwa upande mwingine, muundo huonyesha mpangilio wa
maonesho kutoka mwanzo hadi mwisho wa tamthiliya.
Kwa ujumla,
tamthiliya inakuwa na mwanzo unaomwelekeza msomaji kwenye wahusika na migogoro
au mkinzano unaokuwa na kufikia upeo kasha msuko wa aina fulani kabla ya
kufikia ufumbuzi. Muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja au muundo wa rejea.
e)
Maelekezo ya
jukwaani
Haya ni yale
maelezo ambayo huandikwa kwa mabano katika tamthiliya na huandikwa kwa hati ya
mlazo. Je, maelezo hayo hufanya kazi gani?
Hueleza mienendo
na miondoko ya wahusika.
Hutoa maelezo
kuhusu wasifu wa wahusika, mavazi, lugha ya ishara za uso, n.k.
Hutoa maelezo
kuhusu mandhari au mahali pa mchezo.
Hufafanua
matendo mbalimbali yanayotokea jukwaani.
Hueleza wasifu
wa mazingira na hata malebaya wahusika.
Hutoa vielekezi
vy jinsi ya kuandaa jukwaa kwa ajili ya uigizaji
Hutoa tathmini
ya matendo ya wahusika au lugha; kwa kuonyesha wapi pana kinaya, n.k
f)
Mandhari
Madhari hutumiwa
kuelezea sehemu ambako tendo fulani hutendeka. Neon hili huweza kutumiwa kwa
mapana kuelezea pia mazingira ya kisaikolojia ya tendo fulani. Mandhari huweza
kurejelea yale mazingira ya jukwaani na hata wakati wenyewe katika tamthiliya.
Mandhari yanaweza kuwa ya kubuni au ya kweli (halisi)
g)
Upeo/kilele
Upeo ni sehemu
ya tamthiliya ambamo taharuki na
matamanio ya hadhira hufikia kilele.sehemu ambapo hadhira huanza kupata
suluhisho la mgogoro uliomo katika tamthiliya. Peo katika tamthiliya ni za aina
mbili upeo wa juu na wa chini
·
Upeo wa juu ni ule ambao unakidhi haja za
hadhira au jamii inayoipokea. Katika sehemu hii, jamii hupata majawabu muhimu
ambayo tamthiliya huwa imeyachelewesha kwa kutumia mbinu kama vile za taharuki,
mbinu rejeshi, mtindo telezi, n.k. Sehemu hizi mara nyingi husisimua hadhira
kwa hali ya juu sana.
·
Upeo wa chini ni ule ambao haukidhi haja ya
wasomaji wa tamthiliya inayohusika. Katika baadhi ya kazi za tamthiliya upeo wa
chini huonyesha udhaifu wa kazi ya sanaa ya msanii anayehusika. Wakati mwingine
upeo wa chini umekusudiwa na msanii na huutumia sana katika hadithi fupi na
lengo kubwa huwa ni kuipa hadhira mshangao.
h)
Jina la kitabu
na jalada lake
Kama ilivyo
kwenye uhakiki wa riwaya, katika tamthiliya vilevile tunaangalia uhusiano wa
jian la kitabu na yaliyomo katika kitabu, hali kadhalika jalada na uhusiano
wake na maudhui ya kazi inayohusika.
i)
Mtindo katika
tamthiliya.
Tamthiliya
yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni mazungumzo au dayolojia.
Mazungumzo/dayolojia hutumiwa kuelezea majibizano baina ya wahusika wawili au
zaidi waliopo kwenye jukwaa au katika tamthiliya maongezi au majibizano si kwa
ajili ya kujibizana tu. Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa, mazungumzo hayo si
mazungumzo tu, lazima yaendeleze tendo kuu katika tamthiliya. Mazungumzo ndiyo
nguzo ya kukuza dhamira na maudhui.
Mazungumzo
mazuri yana uhalisia na uthabiti.
Mazungumzo sio
maelezo tu bali yanaonyesha matendo ya ndani.
Mazungumzo
mazuri hukuza na kuendeleza tendo kuu na msuko
Mazungumzo sio
maongezi yanayovutia tu, lazima yawe na lengo.
Ikiwa mazungumzo
yanakuza na kuendeleza tendo kuu, basi yanatekeleza jukumu la kidrama.
Mazungumzo
yanaweza kutokea sambamba; kwa kuwako kwa wahusika kadhaa jukwaani.
Mazungumzo na
uzungumzi nafsi wa wahusika huchukuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya tamthiliya
kwa sababu ya kuliendeleza tendo kuu.
Mazungumzo
huweza kuonyesha sifa zisizokuwa za kawaida katika maongezi ya kila siku ikiwa
mwandishi anataka kulimulika jambo fulani.
Mazungumzo ya
mhusika yanaweza kuyavunja mtarajio fulani wa wasomaji au hadhira katika hali
fulani kwa ajili ya kupitisha ujumbe fulani.
Mazungumzo ndiyo
njia kuu ya kuindeleza hadithi iliyopo katika tamthiliya kwa kuwa mwandishi
hana uhuru wa kutumia mbinu za usimilizi, isipokuwa katika maelezo ya jukwaani.
Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni dayolojia.Dayolojia
ndiyo mtindo mkuu wa tamthiliya nyingi.
Dayolojia ni
majibizano baina ya wahusika wawili au zaidi, ambao hujadili jambo fulani.
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui
hutujulisha lile lililomgusa mwandishi mpaka kuunda ile kazi yake. Hili
linaweza kuwa ni wazo tu au aliloshuhudia au hata likawa ni jumuisho la mambo
mengi.
Maudhui pia
hutuangazia jinsi jumuiya ya mwandishi ilivyo kwa kuwa fasihi ni kioo cha
jamii. Kupitia maudhui, tunaweza kugundua mazingira ya mwandishi yalivyo.
Mwandishi
hutumia maudhui yake kutudhihirishia mivutano, misuguano na pia maendeleo ya
jamii yake. Maudhui ndiyo lengo la mwandishi. Ndicho chombo chake cha kutuonyesha furaha na matatizo ya jumuiya
iliyomzingira na kuwathiri kimawazo. Kuathirika huku kwa mwandishi hasa
hujitokeza zaidi baada ya kusoma kazi zake nyingi.
Kwa hivyo, basi
maudhui ya kazi yoyote ile ya fasihi yatahusu mambo ambayo yalimsukuma
mwandishi hadi akaiunda kazi ile. Pia yatahusu mafunzo ambayo mwandishi
aliliengea hadhira yake. Zaidi ya haya, kwa kuwa maudhui hayatenganishwi na
mazingira na jamii, itambidi mwenye kuyachambua ayalinganishe na hali ya jamii
ya mwandishi katika vipengele mbalimbali vya maisha. Mathalani, itambidi
achunguze siasa, uchumi, utamaduni, n.k.
Mwanafasihi
mmoja, Senkoro (1981), amefafanua maudhui kama yanayojumlisha mawazo nap engine
mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzinama msanii hadi akatunga kazi fulani ya
sanaa. Huwa msanii huyo amekusudia hadhira yake ya wasomaji, wasikilizaji ama
watazamaji wayapate mawazo au mafunzo hayo. Kwa hiyo, haya twaweza kuyaita kuwa
ni lengo la msanii kwa hadhira. Mawazo na mafunzo haya hayazuki hivi hivi tu.
Kwa hiyo, kuna umuhimu wakati wa kuyachambua na kujadili yahusishwe na hali
halisi ya jamii.
Mhakiki
anachunguza maudhui ya kazi ya fasihi anaweza kuongozwa na maswali yafuatayo:-
Je, wazo kuu la
msanii n nini?
Je, msanii
ametazamia hadhira ya aina gani?
Je, kuna kundi
lolote analoliunga mkono?
Je, kuna kundi
analolibeza?
Je, msanii
ameipa hadhira yake mbinu zipi za kuitatua migogoro aliyoichunguza?
Katika
tamthiliya ya Kiswahili, kuna dhamira mbalimbali ambazo waandishi
wamezishughulikia kwa mujibu wa Mulokozi (1996). Dhamira hizo ni:-
1.
Migongano ya
kiutamaduni
Hizi
zinonyesha mvutano kati ya utamaduni wa jadi wa Kiafrika na utamaduni wa
Kizungu au kati ya mji na shamba. Suala hili limejadiliwa kwa dhati zaidi
katika
§ E.Hussein
“Wakati Ukuta” (1969)
§ E.Hussein
“Kwenye Ukingo wa Thim” (1989)
§ P.Mhando “Hatia”
§ J.Ngugi
“Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi” (1961)
§ H.M.Liyoka
“Dunia Imeharibika” (1978)
§ C.Riwa na
M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!” (1976) n.k
2.
Matatizo ya
kijamii
Kwa
mfano, mapenzi, ndoa, ufukara na urithi. Karibu
tamthiliya zote za mawazo zilihusu kipengele hiki. Kwa mfano, Nakupenda Lakini…(1957) na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (1961),
zilizungumzia matatizo ya mapenzi yanayokumbana na vikwazo vya kiuchumi na
vinginevyo. Tamthiliya za Hyslope zilihusu matatizo ya urithi, rushwa, fitina
na tama. Tatizo la mimba limejitokeza katika Hatia, katika Mke Mwenza (1982),
tunakutana na tatizo la wivu katika ndoa za mitala.
3.
Dini
Hizi
ziko katika makundi mawili:
· Tamthiliya za
kanisani zenye kufundisha dini. Kwa mfano, zile tamthiliya zinazoingizwa
kanisani kukiwa na shughuli au sherehe fulani.
· Tamthiliya
zinazochambua na kuhakiki asasi na maundisho ya dini kifasihi. Hizi ni kama
vile
· F.Topan
“Aliyeonja Pepo” (1973)
· Muba-“Maalimu”
(1980)
· Mulokozi “Mkwawa
wa Uhehe” (1979).
Hawa wanaonyesha mikinzano iliyomo ndani ya
mafundisho ya kidini, hasa pale mafundisho hayo yanapogongana na maisha halisi,
sayansi au mantiki. Tamthiliya nyingine zinazoonyesha mgongano huo ni Kinjekitile (1969) na Njia Panda (1981).
4.
Ukombozi
Hizi
zinazungumzia juu ya harakati za kumwondoa mkoloni hapa Afrika. Mfano wa
tamthiliya hizo ni Nkwera “Mkwawa Mahinya” katika “Johari Ndogo” (1968),
E.Hussein “Kinjekitile” (1969) na “Mashetani” (1971), M.Mulokozi “Mkwawa wa
Uhehe” (1979), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), P.Muhando, N.Balisidya na
A.Lihamba “Harakati za Ukombozi” (1972) na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na
Paulo! Paulo!” (1976), n.k. Tamthiliya hizi licha ya kujadili ukombozi wa
kisiasa, vile vile zinajadili ukombozi wa kiuchumi na kiutamaduni.
5.
Ujenzi wa jamii
mpya
Baadhi
ya tamthiliya zinazojadiliwa zinazojadili suala hili ni za Ngahyoma “Kijiji
Chetu” na M.Rutashobya “Nuru Mpya” (1980). Hawa walipendekeza marekebisho
katika mfumo uliopo. Baadhi wameonyesha tu kuwa mambo siyo sawa. Mfano: Mbogo- Giza Limeingia (1980) na Hussein- “Mashetani” (1971) na wengineo
wanalitazama suala hili kitabaka na kuhimiza mapambano ya wafanyakazi dhidi ya
mabepari na ubepari- Kahigi na Ngemera- “Mwanzo
wa Tufani” (1976) na Mazrui “Kilio
cha Haki” (1981).
6.
Uke na matatizo
ya kijinsia
Hawa
wanaonyesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya sasa, kutafuta sababu za hali
hiyo na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya tamthiliya hizo ni P.Muhando-“Nguzo
Mama” (1982), Ngozi-“Machozi ya Mwanamke” (1977), Mulokozi-“Mkwawa wa Uhehe”
(1979), Mazrui “Kilio cha Haki” (1981),
E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989).
7.
Uchawi, uganga
na itikadi za jadi
Suala
hili limejitokeza katika tamthiliya kadhaa. Kwa mfano, Mhanika-“Njia Panda”
(1981), Mbogo “Ngoma ya Ng’wanamalundi” (1988), Hussein “Kinjekitile” (1969) na
Kitsao “Mfarakano” (1975). Kwa ujumla, uganga na itikadi za jadi katika
tamthiliya hizi husawiriwankama amali muhimu za jamii zifaazo kutatua baadhi ya
matatizo ya kimaisha.
8.
Tatizo la ugonjwa
wa UKIMWI
Hawa
wanaonyesha madhara yanayotokana na ugonjwa wa UKIMWI kwa jamii. Tamthiliya
hizo ni Ushuhuda wa Mifupa (1990), Mwalimu Rose (2007), Orodha (2006) na Kilio Chetu (1995).
TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI
Tenzi
na mashairi hutofautiana, hasa katika vipengele muhimu vifuatavyo:
1.
Muundo,tenzi hutumia
muundo wa tarbia tu katika beti zake ambapo mashairi yana uhuru wa kutumia
miundo mingine tofauti kama vile tathlitha, takhmisa n.k
2.
Urefu,tenzi kwa
kawaida huwa ni ndefu kwa vile hutokea
zikiwa katika mtindo wa usimulizi, na hivyo kuwa na beti nyingi sana ili
kkamilisha usimulizi wa kisa ambapo mashairi kwa kawaida hutumia beti chache
3.
Vina,tenzi zina vina
vya mwisho tu; hazina vina vya kati ambapo mashairi yana vina vya kati na vya
mwisho.
4.
Urefu na mistari ,tenzi mistari
yake ni mifupi; haigawanyiki katika nusu ya kwanza nay a pili, mashairi yake ni
mirefu; na hugawanyika mara mbili, nusu ya kwanza na nusu ya pili (huitwa
vipande).
5.
Idadi ya mizani, tenzi katika mistari yake huwa na mizani nane tu,
mashairi huwa na mizani 16 katika mistari yake.
6.
Kituo,kituo cha tenzi
hubadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kituo cha shairi kinaweza
kubadilika au kutokubadilika
KANUNI ZA UTUNZI WA NGONJERA
Ngonjera
ni tungo za kishairi zinazowasilishwa kwa kutumia mazungumzo ya majibizano
baina ya watu wawili au zaidi. Mazungumzo hayo huwa na mjadala wa malumbano
yenye lengo la kutoa ujumbe maalumu kwa wasikilizaji
Katika
majibizano hayo, mhusika mmoja hueleza jambo fulani kwa ubeti mmoja, mhusika wa
pili naye hujibu kwa kupinga au kuunga mkono hoja za mhusika aliyetangulia.
Mwishoni mwa ngonjera wahusika hao huwa wanaondoa tofauti zao na kuwa na
msimamo mmoja. Hali hiyo hutokea pale mhusika mmoja anakubali kulegeza msimamo
wake na kukubaliana na mtazamo wa mwenzake.
Kanuni
za utungaji wa ngonjera hazitofautiani na kanuni za utungaji wa mashairi ya
kimapokezi. Ngonjera sharti iwe na kichwa, beti, vina, mizani, muwala,
utoshelezi, kituo na urari wa mistari ya beti. Ngonjera pia, hutakiwa kutumia
lugha ya kisanaa kama ilivyo kwa mashairi.
Mfano wa ngonjera: Mwenye nyumba na
mhitaji
MWENYE NYUMBA: Nakwambieni jamaa, vya nyumbani mwangu visa,
Mpangaji amekaa, huu mwezi wa tisa,
Mpangaki ana baa, atoapo zangu pesa,
Hivi sasa nimenusa, nataka
kumfukuza.
MHITAJI: Taibu maneno yako, yananipata
kabisa,
Mimi mhitaji kwako, chumba sina
nimekosa,
Sema kodi iliyoko, unayopokea sasa,
Name nitakupa pesa, upate kumfukza.
MWENYE NYUMBA: Kwa hesabu iliyoko, mimi sipati halasa,
Thelethini ndizo ziko, alipazo Bwana
Musa,
Kinipa sitini zako, atatoka hivi
sasa,
Himiza unipe pesa, nipate kumfukuza.
MHITAJI: Sitini ni hizi hapa, pokea ni
kama posa,
Na kodi hasa talipa, daima bila
kukosa,
Tena Wallahi naapa, kulipa sitakutesa,
Nenda kafanye mkasa, upate kumfukuza.
(Kutoka: Ngonjera za UKUTA, uk 86-87)
TOFAUTI KATI YA NGONJERA NA MASHAIRI
Ngonjera
hutofutiana na mashairi katika vipengele vine, navyo ni wahusika, namna ya
uwasilishaji, kituo, na matumizi ya lugha.
1.
Wahusika,ngonjera hutumia
wahusika wanaojibizana. Wahusika hao wanaweza
kuwa wawili au zaidi, ambapo shairi hutumia mhusika mmoja tu
anayezungumza au anayetoa mawazo yake pasipo kujibizana na mtu.
2.
Uwasilishaji, ngonjera
huwasilishwa kwa njia ya uzungumzaji wa kujibizana, mashairi huwasilishwa kwa
njia ya uimbaji.
3.
Kituo,ngonjera huwa na
vituo tofauti kwa vile kila mzungumzaji huwa na ktuo chake, lakini shairi huwa
na kituo kimoja tu na hata kama kitabadilikabadilika huwa hakilengi kuonyesha
mtazamo wa ukinzani wa mada inayojadiliwa kama ilivyo kwa vituo vya ngonjera.
4.
Matumizi ya
lugha,
ngonjera hutumia sana lugha rahisi lakini mashairi hutumia sana lugha ya kuzama