VIGEZO VYA UAINISHAJI WA MANENO

 

Kuna vigezo vitatu vya uainishaji wa maneno ambavyo ni;

1) Kategoria ya kisintaksia
Msingi wa mkabala hutazama nafasi ya neno ktk tungo, hivyo kwamba nafasi ya neno inapobadilika na kategoria ya neno pia hubadilika.
Aina za maneno kwa kigezo cha kisintaksia
Nomino, kitenzi, kivumishi, kiunganishi, kihusishi, kielezi, kionyeshi, kiwakilishi.
Udhaifu wa kigezo hiki ni kuwa;
Kuna maneno ambayo huhama na sifa zake,
Kwa mfano,
Mtoto alikuja jana
Jana mtoto alikuja
Neno jana linaendelea kushikilia maana moja ya kielezi ktk s. zote
2) Kategoria ya kimuundo
Ni kategoria ambayo huangalia zaidi maumbo yaundayo maneno, maumbo yanayofanana,
Kwa mfano;
Katika vitenzi hutazamwa zaidi viambishi awali, mzizi na viambishi tamati.
Katika nomino hutazamwa ngeli za majina.
Dosari ya mtazamo huu ni kwamba
Kuna uwezekano wa maneno kuingiliana, kwa mfano, neno vizuri lina kiambishi
ngeli vi, pia neno lenyewe ni kivumishi.
Je maneno km vielezi, viwakilishi, viunganishi na vihusishi yana maumbo gani?
3) Kategoria ya kikazi/kidhima
Mkabala huu umetumiwa zaidi na wanamapokeo. Huzingatia uamilifu wa neno zaidi katika tungo.
Kwa mfano uainishaji wa maneno umetumia istlahi za kidhima zaidi
Nomino huitwa jina
Kitenzi huitwa tendo
Kivumishi huitwa kisifa
Udhaifu wa kategoria ya kidhima;
Ni vigumu kuelewa maana ya maana
1) Sikuwa na maana hiyo
2) Mawingu ya maana ya mvua
Powered by Blogger.