DHANA YA TUNGO


 Dhana ya tungo imeweza kufasiliwa na wataalamu mbalimbali,


 Massamba,Kihore na Hokororo  (2012;67) wanasema tungo ni nomino ambayo hutokana na kitenzi tunga ambacho kina maana ya kushikanisha vitu kwa pamoja kwa kuptsha kitu kama uzi,ungwe, ndani yake,hivyo kataka taaluma ya sarufi neno tungo lina maana ni ambayo ni kuweka  au kupanga pamoja vipashio sahihi li kujenga kipashio kikubwa katika tungo.

Kamusi teule ya Kiswahili (201;1015)  tungo kifungu cha maneno kinachoongozwa na kanuni kisarufi kataika lugha inayo husika ambapo vipashio vipashio vinapoungana huunda kipashio kikubwa zaidi.

Kamusi teule ya Kiswahili(2014;632)  tungo ni kipashio cha kimuundo kipatikanacho kwa kuunganisha vipashio sahihi kuweza kupata kipashio kikubwa zaidi katika sarufi Kwa ujumla tungo ni kipashio cha kimuundo ambacho huweka pamoja il kujenga vipashio vikubwa zaidi katika sarufi.

Tungo hujidhihilisha katika miundo minne ambayo ni tungo neno,tungo kirai,tungo kishazi,tungo na tungo sentensi.

Kwa kuanza na tungo neno wataalamu mbalimbali wameweza kufasili maana ya tungo neno kama ifuatavyo,
Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004) neno ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazoandikwa au zinazotamkwa na kuleta maana.

Kamusi kuu ya kiswahili (2015;787) tamko moja wapo miongoni mwa mengi ambalo mtu hutamka katika mchakato wa mazungumzo.

Massamba,Kihore na Hokororo  (2012;69) wanasema tungo ni mahusiano ya viamba jengo vyake yamekitwa katika kiwango cha neno.

Kwa ujumla tunapochunguza tungo neno katika kiwango chochote kile tunajikita katika kuangalia jinsi tungo hizo zinavyoundwa pamoja na vipashio vyake vinavyohusika.

Maelezo yaliyotolewa  na Massamba na wenzake ni kwamba ili kupata tungo neno katika lugha ya Kiswahili taratibu mbili muhimu lazima zifuatwe.Utaratibu wa kwanza ni mpangilio wa vitamkwa ili kupata silabi,mpangilio wa pili ni mpangilio wa mofimu.

Mpangilio wa vitamkwa katika kujenga silabi,huhusu vitamkwa kupangwa katika mfuatano unaotupatia silabi zinazokubalika katika lugha yoyote iwayo,pia silabi ni kipashio cha utamkaji ambacho huruhusu sauti za lugha kutamkwa kama fungu moja hivyo tunaposema kwamba lugha zote zinampangilio wa vitamkwa zinazokubaliwa katika kujenga silabi na lugha zote hutumia utaratibu wake katika vitamkwa.

Katika lugha ya Kiswahili taratibu zitumikazo ni kama zifuatazo,
(i)irabu peke yake
                mfano,au,

(ii)konsonanti na irabu
                 mfano wa,na,za

(iii)kiyeyusho na irabu
                  mfano wa,ya

(iv)konsonanti,kiyeyusho na irabu
                 mfano kwa

(v)konsonanti,konsonanti,irabu
                mfano (a)mbaya
                            (b)nyenzo
                  
(vi)konsonanti,konsonanti,kiyeyusho,irabu
                  mfano (a)kushindwa
                             (b)kinazungumzwa


Mpangilio wa mofimu katika kujenga  tungo neno unahusu hasa mpangilio wa viambishi na mzizi katika neno,katika lugha ya kiswahili tungo neno huweza kujegwa  na mzizi huru(usiohitaji viambishi katika kukamilisha maana yake) au hujengwa na viambishi  na mizizi,
mfano(i) mzizi huru sayansi ,bunge
          (ii)mzizi tegemezi watoto,wanaume

Pia mizizi na viambishi huandamana katika kuunda tungo neno kwa kufuata taratibu maalumu taratibu hizo ni kama zifuatazo
               (i)Mizizi kufuatwa na kiambshi au viambishi
                  mfano (a)somo,mzizi ni{som}
                              (b) soma,mzizi ni {som}

                (ii)Mizizi kutanguliwa na viambishi
                      mfano  (a)M-toto
                                   (c)M-zazi

                (iii)Mizizi kutanguliwa kufuatiwa na viambishi
                      mfano (a)wa-toto
                                  (b)ana-lind-a
                                  (c)anapo-kul-a

 Katika lugha ya Kiswahili kuhusu aina za maneno wataalamu wa mitala mbalimbali ya Kiswahili wamekua wakitofautiana,ingawa pengine tofauti hizo si kubwa sana.Baadhi wamehitilafiana katika istilahi wanazotumia,na wengine wamehitilafiana katika idadi ya aina yenyewe.Kwa mfano Nkwera ana aina saba za maneno Nomino,Vivumishi,Viwakilishi,Vitenzi,Vielezi,Viunganishi na vihisishi. Kapinga ana aina saba za maneno Majina,Vivumishi,Viwakilishi,Vitenzi,Vielezi,Vihusishi,Viigizi na Kihore ana aina nane Majina,Vitenzi,Vivumishi,Vielezi,Viunganishi,Kiwakilishi,Viingizi na Viigizi. Kwamba Nkwera na Kapinga wanatambua aina saba za maneno,ambapo Kihore ana aina nane za maneno.Aidha wakati Kihore na Kapinga wanatumiia istilahi ya majina wakati Nkwera anatumia nomino,Hivyo kutokana na wataalamu hao ninamtumia mtaalamu Nkwera kuonyesha aina za maneno na mifano kutoka katika makala elekezi,
                    (i)Nomino
                        mfano Raisi,Nchi,Msumbiji,Chisano,Ghana

                     (ii)Kivumishi
                          mfano(a) ushujaa,ustawi,
                                     (b)Watoto wake
                                     (c)Wanafunzi wote

                      (iii)Kiunganishi
                            mfano kwa,na, kama.

                      (iv)Vitenzi
                            mfano kufundishia,fundisha.

                       (v)Kielezi
                            mfano vizuri mno,kesho na baadae
Mbali na tungo neno lugha ya Kiswahili pia hujengwa na tungo kirai,aina hii ya tungo imeweza kujadiliwa na wataalamu mbalimbali


Massamba,Kihore na Hokororo (2012;74) wanasema aina hii ya tungo hujidhihrisha katika kiwango cha kirai.Katika kiwango hiki miundo ya tungo huhusisha maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalumu unazingatia uhusiano uliopo baina ya neno kuu na maneno mengine.   

Kamusi teule ya Kiswahili (2014;311) tungo kirai hutumika katika sarufi kuelezea kipashio cha kimuundo ambacho huweza kuwa neno moja au zaidi linalotokea nomino,kielezi,kiarifa

Kamusi kuu ya Kiswahili (2015;463) tungo kirai ni kipashio cha kimuundo kinachoundwa kwa neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.

Kwa ujumla tungo kirai ni kipashio cha kimuundo ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu lakini hutoa taarifa fulani.

Katika tungo kirai tunaona Massamba na wenzake anasema tungo virai zina maumbo na miundo mbalimbali kulingana na  virai vilivyomo katika lugha inayohusika,Katika lugha ya Kiswahili kuna aina mbalimbali za virai lakini vifuatavyo ni aina ya  virai kutoka kaka makala elekezi
Kirai nomimo,ni aina ya kirai ambalo neno kuu ni nomino
mfano (i) Afrika
                       (ii)Wasomi wabobezi
                       (iii),Kiswahili kinafunzwa.

  Kirai kielezi ni aina ya kirai ambalo neno kuu ni kielezi
mfano (i)Sasa tutizame kesho na baadae
                        (ii)Anafundisha mara chache                                                                                                                                                                                                                                           
                        (iii)Lugha moja hufa kila baada ya siku kumi na nne
                         (iv)Kuogezeka kwa kasi                                                                                                    
                                                                                                                                                         Kirai kivumishi ni aina ya kirai ambalo neno kuu ni kivumishi
             mfano (i)Wanafunzi wote
                        (ii)Mjadala mkali kuhusu kutumia kiingereza au kufundishia ukupamba    
                             moto kati ya 1965 mpaka mwanzo wa 1980

Kirai kitenzi  ni aina ya kirai ambayo neno kuu ni kitenzi
             mfano (i) Anafundisha
                        (ii)pendekezo
                        (ii)kufundisha 

Tungo kishazi ni aina ya tungo imeweza kufasiliwa na wataalamu mbalimbali

Kamusi Teule ya Kiswahili (2014;314) tungo kishazi hutumika katika sarufi kuelezea kundi la maneno yanayojumusha kundi la nomino na kundi kitenzi,kiima na kiarifu,kishazi huru na tegemezi,kishazi sharti,beba,chopekwa,ambatani na ongezi.

Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004;124) tungo kishazi ni kifungu cha maneno yasiyo kamilisha maana.

Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015;469) kishazi ni tungo yenye kiima na kiariafu ambayo imo ndani ya tungo kuu.

Massamba,Kihore na Hokororo (2012;77) wanasema tungo kishazi ni matokeo ya kuweka pamoja miundo miwili au zaidi yenye kirai nomino na kirai kitenzi ndani ya tungo sentensi.Fasili hii na maana kwamba tungo kishazi ni kubwa kuliko tungo kirai,lakini ni ndogo kuliko tungo sentensi.

Kwa jumla tungo kishazi ni neno au kifungu cha maneno yanayotoa taarifa kamili au isiyo kamili.

Kwa kawaida tungo kishazi hujidhihirisha katika muktadha wa sentensi ambamo huwa zinabebwa.Utaratibu wa miundo hii ni kwamba tungo kishazi mbili au zaidi huwa hubebwa na sentensi moja.Massamba na wenzake wanasema kuna aina tatu za tungo kishazi,aina hizo ni kama zifuatazo

Tungo kishazi kirejeshi ambacho kwa kawaida hubebwa na kirai nomino
mfano (i)Miundo mbinu iliyowekwa ilikuwa ya gharama kubwa
                       (ii)Mmeona hizo lugha zinazotumika (AU) na (SADC) ukilinganisha na
                             hizo za (EU) kuna nini kwetu.?

Tungo kishazi kielezi ambacho kwa kawaida hubebwa na kirai kielezi
mfano (i)Hawa wakawa wanasisitiza umuhimu wa watoto kujifunza katika lugha
                           yao ya asili ambayo wanaielewa vizuri

Tungo kishazi ambatani ambazo kwa kawaida huunganishwa ni viunganishi
mfano(i). Kuhusu Kiswahili,matumizi yake yamekuwa yakipanuka tena kwa kasi
                            kubwa ikiwa ni pamoja na msamiati na istilahi zake kuongezeka,Nyanja
                            za matumiz yake kupanuka,idadi ya wazungumzaji wake kuongezeka…
                        (ii)Swali lingine muhimu Je katika dunia inayobadilishwa kasi na sayansi                                                                                     
                              na teknolojia Kiswahili kitakuwepo 2050 au kitakuwa kimevia na                                                                                                                                                                                                                                                                 

Tungo sentensi ni aina ya tungo ambayo imeweza kufasiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo,

Kamusi teule ya Kiswahili (2014;559) tungo sentensi ni neno au fungu la  maneno linalojitokeza ama lenye maana kamilifu na ambalo huwa na mtenda,kitendo na mtendwa.

Kamusi kuu ya Kiswahili (2015;918) tungo sentensi ni tungo yenye neno moja au zaidi ambayo hutoa taarifa kamili,swali au amri na ambayo ina muundo wan a karifu ndan yake.

Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2014;251) tungo sentensi ni fungu la maneno au neno linalowakilisha nafsi,kitenzi wakati na kinachotendwa na linapasha habari kamili.

Massamba,Kihore na Hokororo (2012;197) wanasema tungo sentensi ni tungo ambayo mahusiano ya viambajengo vyake yamejikita katika kiwango cha sentensi,Wanaendelea kwa kusema tungo sentensi  ni za aina nyingi kutegemea aina ya sentensi zinazohusika.



.

Kwa ujumla tungo sentensi ni kipashio kimuundo ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu na hutoa taarifa kamili.

Massamba,Kihore na Hokororo wanasema kuna aina tatu za tungo sentensi nazo ni

Sentensi sahili ni muundo wa tungo sentensi naohusisha kirai  kirai nomio,kirai kitenzi, na yenye maana kamili iliyokusudiwa,kiini cha sentensi sahihi ni kirai kitenzi ambacho kwa kawaida huweza kutokea peke yake au kuandamana na vipashio vingine vya sentensi kama kirai nomino,kirai kivumishi,kirai kielezi.
mfano (i) Shirika la kazi duniani.
                       (ii)Mawasiliano ya lugha huwa nyenzo kuu katika kufanikisha shughuli za
                            binadamu,kiuchumi,kisiasa,kijamii,kiutamaduni,kifasihi,kiteknolojia na
                             kisayansi,kielimu nk

Sentensi ambatani ni sentensi  ambazo huwa ni sentensi mbili au zaidi zilizo huru ambazo uunganishwa pamoja kwa viunganishi.
                 mfano Miundombinu iliyowekwa ilikuwa ya gharama kubwa lakini serikali ya
                             wakati huo ilidhamilia,ikapanga na kutekeleza ili kusimika Kiswahili
                              lugha ya taifa.

Sentensi changamani ni tungo sentensi ambayo inaundwa na kishazi tegemezi na kishazi huru
                   mfano (i)Lugha isiyotumika au kutumiwa hatima yake hutoweka/hufa
                              (ii)Mioyo ikainuliwa wakaielekeza majuu….na bondeni…
                               (iii)Wakati mjadala huu unaendelea fungo anayeitwa UTANDAWAZI                   akaingia uvunguni.

                                           
Hivyo,Tungo za Kiswahili zimeweza kufafanuliwa na wataalamu mbalimbali ambao kila mtaalamu kwa mawazo yao wameweza kutoa michango yao mbalimbali kuhusu tungo za Kiswahili.Katika lugha ya Kiswahili tungo ndogo ni tungo neno na tungo kubwa ni tungo sentensi.Tukingalia katika makala elekezi iliyowasilishwa na prof, A. D. Kiwara ameweza kutumia aina za tungo japokuwa amejikita katika lugha ya mazungumzo lakini ameweza kutumia tungo za Kiswahili kuanzia kiwango kidogo cha tungo yaani tungo neno mpaka kiwango kikubwa tungo sentensi







                                          

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      

                                                                                                                                                                                                    MAREJELEO
 BAKITA (2015) Kamusi Kuu ya Kiswahili.Longhorn.Dar es salaam.

Kiwira A.D (2017) Ukuaji wa Kiswahili na ustawi wa jamii ya wazungumzaji wake.
(CHAUKIDU) Dar es saalam.

 Massamba na wenzake (2012) Sarufi ya Miundo ya Kiswahili Sanifu. ( SAMIKISA)
Sekondari na vyuo.Dar es saalam.

 Ndalu,A.E,Babusa,H n Mirikau,S.A (2014)  Kamusi Teule ya Kiswahili.Nairobi,Kampal
  a ,Dar es salaam,Kigali.

  TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu.Chuo kikuu cha Dar es salaam.Dar es
Powered by Blogger.